Sitta: Nitasema ukweli daima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Nitasema ukweli daima

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jul 23, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Sitta: Nitasema ukweli daima
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 22 July 2011 20:16 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Ramadhan Semtawa
  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta, amesema ataendelea kusema ukweli daima kwa wananchi kuhusu kasoro ndani ya CCM na serikali akiamini kuwa huo ndiyo uwajibakaji.

  Kauli hiyo ya Sitta, inakuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, kumtuhumu kuwa anataka kuigawa CCM na kuibomoa serikali.Guninita alitoa kauli hizo juzi alipokuwa akizungumza katika mkutano wa wanachama wa CCM wa Tawi la Mbezi, uliojadili matatizo ya chama chao.

  Katika mazungumzo yake Mwenyekiti huyo alimwelezea waziri huyo,kuwa ni mtu hatari mwenye malengo ya kikitumbukiza chama shimoni.Hata hivyo akizungumzia jijini Dar es Salaam jana na baadhi ya vyombo vya habari, Sitta alisema kuna wafuasi wa mafisadi ndani ya CCM, wanaohofu ukweli kwa kchelea kufahamika wa maovu yao.

  Sitta alisema serikali makini lazima ikiri upungufu unaotokana na makosa yake."Nilichokisema Mbeya ni kuambia Watanzania ukweli. Na nitaendelea kuwaambia ukweli," alisisitiza spika huyo mstaafu.

  Alisema serikali makini haiwezi kudanganya wananchi wake na kusisitiza kuwa watanzania wa leo ni watu wenye akili na hawawezi kuwambiwa habari nzuri kuhusu umeme wakati umeme ni tatizo.

  "Siwezi kuishi katika uongo. Naamini katika ukweli na nitaendelea kusema ukweli. Sasa hivi utamdanganya Mtanzania gani, kuna vijana zaidi ya 100,000 wako katika vyuo vikuu leo uende kwa wananchi ukawadanganye, ebo," alise ma Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki.


  Alisema ni ukweli usiopingika kwamba miundombinu mingi ya umeme ilijengwa tangu serikali ya awamu ya kwanza chini Hayati Mwalimu Julius Nyerere, na kwamba kuwaeleza wananchi upungufu na kasoro za kiutendaji wa serikali katika kuwekeza umeme si tatizo.

  "Yaani mtu anataka leo uende ukadanganye wananchi. Kwanza unapoeleza wananchi ukweli wa mapungufu ya kiutendaji unaijengea heshima serikali. Serikalia makini ni ile inayokiri mapungufu kwa wananchi na kuwaambia inataka kufanya nini kama nilivyofanya kule Mbeya," alisisitiza.

  "Kule Mbeya niliueleza ule umati ukweli kuhusu mapungufu yetu serikalini na wananchi walituelewa. Kuna mapungufu tumeyakiri na tunajipanga kuyapatia ufumbuzi. Umeme ni tatizo kubwa huwezi kueleza uongo kwa Watanzania wakakuelewa, waambie wananchi ukweli watakuelewa,"alisema.Alisema miaka ya nyuma kulifanyika utafiti kuhusu uzalishaji umeme katika maporomoko ya maji ya Stiglers, mradi ambao ungeweza kuzalisha megawati zaidi ya 2,000, lakini hadi sasa haujaendelezwa.

  "Sasa haya ndiyo mapungufu yetu, lakini wanatokea baadhi ya watu wenye upeo mdogo ndani ya CCM wanaoendekeza siasa za ufuasi, wanakaa na kuzungumza mambo ya hovyo," alisisitiza.

  Akiwa Mbeya, Sitta alisema tatizo la umeme linatokana na mapungufu mbalimbali ya serikali ikiwamo mikataba mibovu na kutaka wahusika washughulikiwe huku serikali ikijipanga kutatua matatizo hayo.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  [h=4]Comments [/h]


  0 #4 Mwanaweja 2011-07-23 02:18 ulicho kiongea sitta ni kweli maporomoko ya maji ya Stiglers documents zipo wakwenye mafile tu ndio maana hatuendelei mimi siamini kama kweli kuwekeza kwenye umeme wa maji kunatatizo bali ni uvivu wa viongozi wetu kutekeleza maelekezo ya wataalamu hasa inapokuwa wanasiasa wanabadilisha kuwa mtaji wakupata kura na kuendelea kutuibia kwa ajili ya manufaa yao na amini hayo maporomoko yanatosha kabisa ni kuamua tu tujiwekeze hapo yote tunayo yaona leo yatatizo la umeme yataisha.
  Quote

  -1 #3 magamba 2011-07-23 02:14 Yaani hamuoni kuwa mnajitumbukiza shimoni wenyewe.
  Quote

  0 #2 amos epimack nyanda 2011-07-23 02:11 Hili ni jambo la msingi sana: ukweli huweka huru! Ufisadi na ufedhuli ni mambo mabaya, huharibu mahusiano. Dhambi hula vibaya na [NENO BAYA]liza.Mheshimiwa Sitta endelea kuwashauri wote wenye mamlaka na dhamana ya kuwatumikia wananchi kuwa waadilifu.
  Quote

  0 #1 John Guninita 2011-07-23 01:42 Halafu nakumbuka nilikuparura siku moja JK akakutetea,sasa tuone na hili kama atakutetea.Akikutetea naenda zangu KAFU kwani shingkumi beigani bwana.Ni kweli mimi ni mfuasi mzuri wa wale watuhumiwa wenu,kwa hiyo mkiwatosa wote mi ntakula wapi jamani.Ila wewe 6 ni mkali sana naogopa ukiukwa ujk 2015 utatufunga kwa hiyo lazima tujipange kukushughulikia
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  tatizo la Guninita ni shule ni sifuri na yashangaza kifuu kama huyu bado naye annaminika kuwa kiongozi...huu ni uthibitisho nchi hii inaendeshwa na vipofu........................Guninita anajua nini juu ya matatizo ya umeme kwa mfano?
   
 4. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Shida ya kupeana vyeo for convience na mfumo wa kuwajibika kwa viogozi badala ya wananchi ni tatizo kubwa kwa CCM na serikali yake. I tell you kuna viongozi wakiongea unatamani hata kulia..they are completely disconnected na wananchi...imagine Sita ameongea ukweli kuhusu mapungufu ya Serikali this fool Gunia I mean Guninita anaibuka na kuzungumzia kukitumbukiza shimoni chama you see na kama ni for sake ya wananchi na kitumbukie tu..The fact is CCM dayz are numbered. Mijitu useless yenye kujifikiria matumbo yao siku zote ndio huishia kuvuruga utulivu wa nchi...ona kinachoendelea Malawi.
   
 5. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bado simuamini Sita..anaonekana ana ajenda ya Siri..huwezi kukata tawi la mti ulilokalia???..Ni mawili ama uwe CCJ...ama uwe CCM lakini undumulakuwili baba utakuua..
   
 6. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Bora Guninita mara 100 kuliko 6 mnafiki: FYI nchi huendeshwa na baraza la mawaziri ambalo 6 ni mmojawapo, vema angetueleza yeye ameshauri nini kwenye baraza na kimefanyika nini, otherwise anataka kuwachochea wananchi dhidi ya gvt anayoiongoza yeye. Najua anataka gvt ya kikwete ianguke ili ccj itawale. Hafai.
   
 7. u

  ureni JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Jamani mimi sita mambo yake nimefuatilia toka alipokua spika mimi naamini huyu jamaa yuko positive kabisa na nchii hii,na anaroho safi ya kutetea watanzania,kitu nilichokiona anabanwa sana na kuchafuliwa na mafisadi,sitta tumpe nafasi ya urais next msimu am sure mabadiliko mtayaona,kitu kingine nilichokiona kwake nimtu ambaye ni ngumu kumnunua ili atete mambo ya uongo,huyu sitta nampa big up ni kiongozi mzuri lakini tatizo amebanwa na mafisadi tusimchukie kabisa tumpe support.
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,291
  Likes Received: 19,446
  Trophy Points: 280
  John Guninita 2011-07-23 01:42 Halafu nakumbuka nilikuparura siku moja JK akakutetea,sasa tuone na hili kama atakutetea.Akikutetea naenda zangu KAFU kwani shingkumi beigani bwana.Ni kweli mimi ni mfuasi mzuri wa wale watuhumiwa wenu,kwa hiyo mkiwatosa wote mi ntakula wapi jamani.Ila wewe 6 ni mkali sana naogopa ukiukwa ujk 2015 utatufunga kwa hiyo lazima tujipange kukushughulikia
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,291
  Likes Received: 19,446
  Trophy Points: 280
  leh..makubwa
   
 10. c

  carefree JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  six hana lolote hafai urai wala urahisi kwanza kwa umri wake kungekuwa na chama cha kutetea haki za wazee kingeshaiburuza serikali kwa cort kujibu kwa nini huyu mzee anachoshwa wkt umri wake wa kumzika ulishapita .
  Sita mnafiki na umaskini wa taifa hili analipiwa kodi 12 m per month , anasema wanaopinga posho zinazonufaisha wachache ni wanafiki , alizima ghafla mjadala wa richmond alipokuwa spika baada ya kuelezwa ukiendelea atang'olewa akahofia kukosa mafao yake .
  Ur like grandpa 2 me lkn mambo yako siiiiyo
   
 11. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Siamini kama mtanzania yeyote anaweza kutoa kauli hizi isipokuwa sita mwenyewe.
   
Loading...