Sitta: Nitahama CCM wananchi wakitaka nichukue 'nafasi nyingine'

kibunda

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
403
52
Inaonekana sasa Sitta anampango wa kukihama CCM. Gazeti za leo la Tanzania daima limemkariri akisema kuwa hivi sasa hana mpango wa kuhama CCM: Kwa maneno yake: “Kwa sasa sina mpango huo wa kuhama, labda wananchi watake nichukue nafasi nyingine,” alisema Sitta.

Hivyo 'nafasi nyingine' anayoisema yamkini ni URAIS. Kwa kauli hii. Ni dhahiri huyu jamaa atahama chama. Hivi sasa anapima upepo tu.
 
Tanzania Daima ni gazeti la Chadema hilo kwahiyo inawezekana walimwelewa vibaya. Alichomaanisha Sitta ni kuwa hawezi kuhama CCM labda akiahidiwa nafasi nyingine na chama kingine.
 
Hakuna mlango wa kutokea ukishaingia CCM..

Salma, kwa Sitta anaweza kutoka. Tangu muda mrefu ana moto sana wa kupata urais lakini kwa hali ilivyo ndani ya chama chake hivi sasa hawawezi kumpa nafasi. Sasa, kama ataendelea kutaka kutekeleza malengo yake ya kuwa rais basi lazima tu ahame chama.

Vinginevyo labla vita hii inavyoendelea ndani ya CCM ya kuvuana magamba kundi lake ndiyo lishinde kitu ambacho ni kigumu kama ilivyo ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.

Si tumeona juzi kule Igunga kundi lote la wanaharakati ndani ya chama liliwekwa kando. Sijui watashinda vipi? Lakini ufahama kabisa kwa ujasiri wa Sitta anaweza kuhama, ama kuanzisha chama chake kama alivyofanya kwa CCJ.
 
kuna memba mmoja humu jamvini alipata kusema kuwa mh sita ni malaya wa siasa ndio naanza kuamini kwa mbaaaali..
 
Sitta tayari ameshajitengenezea mazingira ya kuhama CCM and the most likely destination ni CDM.
Hivyo angalieni CDM msije kula matapishi yenu kama CCM na Rostamu walivyofanya huko Igunga.
Sitta amejiapiza kama Lusinde alivyojiapiza kwamba CCM ikishindwa Igunga atakunywa sumu. Sitta
amesema kwamba ataendelea kupinga malipo ya downs kwa nguvu zake zote.

Sasa imagine kama baraza la mawaziri likaridhia kuilipa downs which is most likely decision kwa sababu ndiyo
mkakati wa EL, RA from the word go. Je Sitta ataendelea kupinga malipo ya Downs?

Remember collective responsibility, ubashiri wangu ni kwamba Sitta ataendelea kupinga, hivyo aidha atafukuzwa
na JK, lakini kama ni smart unlike Mrema atajiuzuru uwaziri na kupinga malipo Downs. Mwisho wake atafukuzwa CCM
na hapo ndipo atakapoangukia CDM kwa ahadi ya kugombea urais 2015, Kama Mrema na Chavda na NCCR-Mageuzi 1995.

Swali la kujiuliza Je ni nani CCM ataweza kupambana na Sitta wa CDM 2015? Be the juror yourself! Najua CCM hawataki
kusikia kabisa kitu hiki, kwani watalazimika kumsimamisha Magufuli ambaye sio changuo la JK na Ridhwani.
 
Kama tz daima ni gazeti la chadema, wewe ni gazeti la chama gani? Mbona na wewe unatoa uelewa wako hapa?
Tanzania Daima ni gazeti la Chadema hilo kwahiyo inawezekana walimwelewa vibaya. Alichomaanisha Sitta ni kuwa hawezi kuhama CCM labda akiahidiwa nafasi nyingine na chama kingine.
 
Ninanchonpendea Sita ni kusema bila kuogopa,hawa akina Sita ndio wale vijana machachali wa mwanzoni kusomea sheria chuo kikuu ,wanasheria hao kama akina marehemu Kolimba,Warioba ni tofauti na wanasheria wa kizazi hiki cha wanasheria wapenda njuruku ambao wako tayari hata kuuza nchi na kuwapa mateso wananchi wao kwa kuandika hiyo mikata ya kiufisadi.Sita ni jembe ndugu yuko bold kuliko hao wanafiki wengi ambao kazi yao ni kusifia hata mapungufu,tuseme ukweli Sita utamulinganisha na Wassira au yule muuza nyumba Magufuli au huyo sijui anyedai vichenji Membe.Ninani katika baraza la mawaziri mwenye ubavu wa kuikosea serikali ya kikwete naye akiwa humo humo kama si Sita pekee,hao wengine wapo kwa ajili ya kuangalia matumbo yao ,aheri ya Sita anasema hiki ni kijiko na sio sepetu,je mtu kama wassira ana jeuri hiyo(nimumtaja sana wassira sababu yeye ndio veterani katika hiyo kabineti kaanzia enzi za Kambarage ,akaenda upinzani NJAA ilipomzidi akarudi CCM ameufyata mkia ,sasa mtu kama huyu utamtegemea aiseme serikali atakula wapi)
 
Sitta tayari ameshajitengenezea mazingira ya kuhama CCM and the most likely destination ni CDM.
Hivyo angalieni CDM msije kula matapishi yenu kama CCM na Rostamu walivyofanya huko Igunga.
Sitta amejiapiza kama Lusinde alivyojiapiza kwamba CCM ikishindwa Igunga atakunywa sumu. Sitta
amesema kwamba ataendelea kupinga malipo ya downs kwa nguvu zake zote.

Sasa imagine kama baraza la mawaziri likaridhia kuilipa downs which is most likely decision kwa sababu ndiyo
mkakati wa EL, RA from the word go. Je Sitta ataendelea kupinga malipo ya Downs?

Remember collective responsibility, ubashiri wangu ni kwamba Sitta ataendelea kupinga, hivyo aidha atafukuzwa
na JK, lakini kama ni smart unlike Mrema atajiuzuru uwaziri na kupinga malipo Downs. Mwisho wake atafukuzwa CCM
na hapo ndipo atakapoangukia CDM kwa ahadi ya kugombea urais 2015, Kama Mrema na Chavda na NCCR-Mageuzi 1995.

Swali la kujiuliza Je ni nani CCM ataweza kupambana na Sitta wa CDM 2015? Be the juror yourself! Najua CCM hawataki
kusikia kabisa kitu hiki, kwani watalazimika kumsimamisha Magufuli ambaye sio changuo la JK na Ridhwani.

huyu sidhani!
 
Tanzania Daima ni gazeti la Chadema hilo kwahiyo inawezekana walimwelewa vibaya. Alichomaanisha Sitta ni kuwa hawezi kuhama CCM labda akiahidiwa nafasi nyingine na chama kingine.
Mbona sioni tofauti ya kilichonukuliwa na gazeti na hii tafsiri yako? Au wewe ndio hukuelewa? Halafu unatudanganya eti Tanzania Daima ni la Chadema!!!! Uelewa wako mdogo sana. Hivi mlevi akikwambia njia unayoenda ina simba utampuuza kwa sababu ni mlevi? Tofautisha Tz Daima na Uhuru bwana!!
 
mwenzie keshalishwa sumu, yeye anaanza kuongea hovyo au wamemwanzia kichwani.
 
Sitta anaweza kazi sema umri kidogo umekwenda..inabidi ailie timing 2013 hapo baada ya uozo huu wa serikali ya CCM kuendelea ili upepo usiishe ifikapo 2015. akitoka sasa hivi JK atafukuza magamba kweli na kuweka mtu mwingine ambaye wananchi kidogo wanamfikiria na hapo Sitta atakua kama Mrema maskini..timing is all that matters.
 
Sitta tayari ameshajitengenezea mazingira ya kuhama CCM and the most likely destination ni CDM.
Hivyo angalieni CDM msije kula matapishi yenu kama CCM na Rostamu walivyofanya huko Igunga.
Sitta amejiapiza kama Lusinde alivyojiapiza kwamba CCM ikishindwa Igunga atakunywa sumu. Sitta
amesema kwamba ataendelea kupinga malipo ya downs kwa nguvu zake zote.

Sasa imagine kama baraza la mawaziri likaridhia kuilipa downs which is most likely decision kwa sababu ndiyo
mkakati wa EL, RA from the word go. Je Sitta ataendelea kupinga malipo ya Downs?

Remember collective responsibility, ubashiri wangu ni kwamba Sitta ataendelea kupinga, hivyo aidha atafukuzwa
na JK, lakini kama ni smart unlike Mrema atajiuzuru uwaziri na kupinga malipo Downs. Mwisho wake atafukuzwa CCM
na hapo ndipo atakapoangukia CDM kwa ahadi ya kugombea urais 2015, Kama Mrema na Chavda na NCCR-Mageuzi 1995.

Swali la kujiuliza Je ni nani CCM ataweza kupambana na Sitta wa CDM 2015? Be the juror yourself! Najua CCM hawataki
kusikia kabisa kitu hiki, kwani watalazimika kumsimamisha Magufuli ambaye sio changuo la JK na Ridhwani.

ridhwani, hebu sema tena nadhani umekosea kuandika. Huyo kimburu ni nani ktk nchii?!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom