Sitta: Nipo tayari kwa hukumu yoyote CCM


Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
13
Points
0
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 13 0
Mwananchi Exuper Kachenje
18/2/2010


  • ASEMA MARIDHIANO HAYAONDOI IMANI YAKE KATIKA KUPAMBANA NA UFISADI
SPIKA wa Bunge Samuel Sitta amesema yupo tayari kwa hukumu yoyote itakayotolewa na chama chake CCM, iwapo msimamo wake wa kupinga ufisadi, rushwa na maovu ndani ya chama hicho, utaonekana ni tatizo.

Sitta alitoa msimamo huo jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili ambapo pia alibainisha kuwa hatua zilizochukuliwa na CCM kupitia kamati maalumu ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwenye kikao cha Nec, itasaidia kupunguza uhasama ndani ya chama hicho.

"Nasema uhasama ni suala la moyo wa mtu na la kibinadamu kabisa na mifano ni mingi tu. Lakini, watu wanapokuwa na uhasama, imani inabaki vile vile. Mimi nitaendelea kukemea ufisadi, rushwa na kama hilo ndilo litakuwa ni tatizo kwa CCM, basi nitakuwa tayari kwa hukumu yoyote ya Chama Cha Mapinduzi," alisema Spika Sitta na kuongeza:

"Kama nikikemea ufisadi au nikisema kwamba lazima tuwe wakali zaidi ni tatizo kwa CCM, basi nipo tayari kwa hukumu yoyote, eeh".

Sitta pamoja na baadhi ya wabunge waliojipambanua kama wapambanaji wa ufisadi amekuwa akitajwa na baadhi ya vyombo vya habari waziwazi kuwa na uhasama na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa na Mbunge wa Igunga Rostam Aziz huku ikielezwa kuwa chanzo cha uhasama huo ni kashfa ya Richmond.

Kashfa ya Richmond ndiyo iliyomfanya Lowassa na mawaziri wengine wawili, Nazir Karamagi na Dk Ibrahim Msabaha, kujiuzulu.

Uhasama ulisabisha CCM chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kuunda kamati maalumu ya watu watatu kutafuta chanzo na suluhu ya mgogoro huo.

Kamati hiyo inaongozwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na wajumbe wake ni Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM bara, Pius Msekwa.

"Msimamo wangu dhidi ya ufisadi, maovu na rushwa bado upo palepale, kilichopunguzwa na CCM juzi kupitia Kamati ya Mzee Mwinyi ni uhasama kati yangu, Rostam na Lowassa, si wanatajwa kila siku?

"Tulikosana kisiasa ndani ya chama chetu CCM lakini, hilo la kutupunguzia uhasama haliondoi imani yangu wala msimamo wangu kuhusu kupambana na ufisadi."

Akitolea mfano wa maridhiano ya rais wa Zanzibar, Aman Abeid Karume na katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharrif Hamad, Sitta alisema hao walikuwa mahasimu wamefikia maridhiano lakini, hawakubadili msimamo na imani zao.

"Hivi ndivyo ilivyo kwangu kwamba, hatua hiyo ya kupunguza uhasama haiondoi wala kubadili msimamo wangu dhidi ya mapambano ya rushwa na ufisadi," alisisitiza.

Alisema: "Seif alisikilizana na Karume lakini, hawakubadili imani wala vyama. Mnaweza kukubaliana kuondoa uhasama lakini, imani ikabaki palepale".

Aliongeza: "Hata Ireland, taifa la kikristo lililopigana kwa zaidi ya miaka 30, baadaye waliunda chombo kwa maslahi yao wote mapigano yakaisha. Lakini kila mmoja akabaki na imani yake, Wakatoliki na imani yao, Waprotestanti walibaki na imani yao ingawa wote wanaamini katika Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu."

Aliongeza kuwa ndivyo ilivyo kwake, anaamini kuwa Katiba ya CCM inamruhusu na kumpa nafasi ya kuendelea kukemea rushwa na ufisadi jambo ambalo alisema ataendelea kulitekeleza.

Alibainisha kuwa suala la kupungua uhasama baina yao kama viongozi ndani ya CCM ni la heri, linahitaji muda na vitendo halisi ndiyo sababu hata kamati ya Mzee Mwinyi imeongezewa muda ili kufanyia kazi baadhi ya mambo.

"Hata rais alisema, uhasama ni hatari, ukialikwa katika sherehe, ukitaka kuinuka una hofu kuacha glasi yako mezani, kupunguza uhasama ni heri, lakini hili halibadili imani ya mtu. Kuondoa uhasama inachukua muda, lazima vitendo vya kurejesha imani viwepo: "Hili litachukua muda ndio maana hata Kamati ya Mwinyi imeongezewa muda, uhasama ni suala la kibinadamu kabisa." alisema Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki.
 
Shapu

Shapu

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2008
Messages
2,016
Likes
360
Points
180
Shapu

Shapu

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2008
2,016 360 180
Sie twasikiliza tuu yakhee... maana mambo ni yale yale hamna badiliko kucheza na lugha. Eti uhasama!
 
B

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2009
Messages
1,090
Likes
1,273
Points
280
B

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2009
1,090 1,273 280
Patamu hapa.

Ebu tueleweshane:Uhasama wa Sitta na Lowasa auliletwa na msimamo wa Sitta kukataa ufisadi.Ufisadi bado upo. Sasa uhasama unaishaje maana uliletwa na ufisadi ambao haujaisha?!

Msimamo wa Sitta kuhusu ufisadi unaeleweka. Je msimamo wa Lowasa kuhusu ufisadi ni upi? Msimamo wa CCM kuhusu ufisadi ni upi? CCM anayoisema Sitta kuwa inamruhusu kupinga ufisadi ni ipi hiyo isiyo CCM ya Lowasa?Maswali ni mengi kuliko majibu. Mashaka mengi kuliko matumaini.
 
B

bigilankana

Senior Member
Joined
Dec 15, 2009
Messages
143
Likes
2
Points
0
B

bigilankana

Senior Member
Joined Dec 15, 2009
143 2 0
Patamu hapa.

Ebu tueleweshane:Uhasama wa Sitta na Lowasa auliletwa na msimamo wa Sitta kukataa ufisadi.Ufisadi bado upo. Sasa uhasama unaishaje maana uliletwa na ufisadi ambao haujaisha?!

Msimamo wa Sitta kuhusu ufisadi unaeleweka. Je msimamo wa Lowasa kuhusu ufisadi ni upi? Msimamo wa CCM kuhusu ufisadi ni upi? CCM anayoisema Sitta kuwa inamruhusu kupinga ufisadi ni ipi hiyo isiyo CCM ya Lowasa?Maswali ni mengi kuliko majibu. Mashaka mengi kuliko matumaini.
Kuna busara katika maneno ya Sitta. ni maneno ya mtu mzima. Kakiri uhasama ulikuwapo na wanaondoa uhasama. Lakini imani ya kupambana na Ufisadi haitoki.
 
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
16,231
Likes
351
Points
180
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
16,231 351 180
God, May you grant me with life..plentiful life!...these other minor problems will solve for themselves!
 
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Messages
1,338
Likes
127
Points
160
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2008
1,338 127 160
Which means hapa Six kampa black and white Lowasa kuwa yeye ni fisadi. Haya mambo bado mabichi kabisa, kama wanadhani kuwa moto umepoa, bado kwa sana
 
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
13
Points
0
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 13 0
Chanzo kikuu cha uhasama wala si Richardmonduli ni Uspika Msekwa baada ya kuukosa uspika aliondoka kwa kinyongo akaanza kuwatumia wanamtandao bungeni ionekane six hawezi kazi alipotokea Richardmonduli six akasema hamadi kibindoni Mungu anipe nini na yeye akaanza kumtumia Richardmonduli kuwamaliza wanamtandao hiyo ndiyo sinema lakini steringi mkuu ni Msekwa, EL na RA wanaingia kwenye sinema hii kwa sababu tu ni wahusika wakuu wa Richmond vingevyo bado uhasama ungekuwepo kati ya Msekwa na Sitta.
 
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
13
Points
0
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 13 0
Which means hapa Six kampa black and white Lowasa kuwa yeye ni fisadi. Haya mambo bado mabichi kabisa, kama wanadhani kuwa moto umepoa, bado kwa sana
That is that mara nyingi viongozi walikuwa wakisema kama kuna mtu anamjua fisadi ni nani amtaje sasa wameanza kutajana tena kwa majina tusubiri kuona ngumi bungeni kama Kenya patamu hapo maana Lowassa naye hatavumia atajibu mapigo tu
 
Drifter

Drifter

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2010
Messages
2,063
Likes
778
Points
280
Drifter

Drifter

JF-Expert Member
Joined Jan 4, 2010
2,063 778 280
"Kama nikikemea ufisadi au nikisema kwamba lazima tuwe wakali zaidi ni tatizo kwa CCM, basi nipo tayari kwa hukumu yoyote, eeh". ....
Kauli ya mtu mzima hii. Inaonyesha jinsi siasa za CCM zilivyo ngumu. Inapotokea mtu mkubwa ndani ya chama anaongea kama vile ana mashaka na MSIMAMO HALISI wa chama chake kuhusu ufisadi, basi sie wananchi wa kawaida tujue hakuna cha kutegemea hapo. Na kwa Muungwana hili ni suala la UHASAMA tu ambalo jawabu lake ni upatanisho! These people are playing nasty games with the future of the country.
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
32
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 32 0
Sitta anadanganya.je yuko tayari kufukuzwa chama?
 
M

Mkandara

Verified Member
Joined
Mar 3, 2006
Messages
15,460
Likes
189
Points
160
M

Mkandara

Verified Member
Joined Mar 3, 2006
15,460 189 160
Nimesema siku zote kwamba mtu ama kiongozi yeyote anayekubali kupeana mkono na Shetani basi huyo sii kiongozi..

Mi sielewi ni imani ipi anayozungumzia Mzee Sitta?.. Huyu Lowassa na Rostam hawa kwa pamoja ni muumini wa chama CCM. Wote wako kanisa moja, wana imani moja wanachotofautiana ni vitendo vyao, hivyop Upatanisho pekee ambao unaweza kuleta maana ni pale huyu Sitta atakapo kataa uongozi wa hawa watu ndani ya kanisa lake..

Mfano wake wa Katoliki/Protentant au Karume na Seif hii ni mifano dhaifu sana kwani hawa watu wanatengana kiimani kwanza, tafsiri ya imani zao ktk kumjenga binadamu zinagongana na hawaelewani kiimani. Kwa hiyo tunachoona kwao ni suluhu baina ya imani mbili tofauti kuweka amani baina yao.. Yaani kifupi amini unachoamini nami nitaamini nachoamini usiwalazimishe watu wangu kufuatana imani yako. lakini ktk swala la Sitta, hii ni suluhu ya waumini wenyewe wenye imani moja ambao kati yao kuna wale wanaokiuka maadili ya imani tangulizi. Kupinga kwa Sitta ndani ya imani hiyo hakuwezi kuwasaidia wauumini wala kuwalinda dhidi na vitendo dhalimu vya hawa viongozi.

Hivyo basi suluhu ya mzee Sitta ni ktk kukubali yaishe, wameshinda wao!...ni suluhu inamhusu yeye binafsi au chama (kanisa) na sii kwa maslahi ya upatanisho wa imani mbili tofauti wananchi bali upatanisho wa matendo..in other word, shake hand with a devil, kwani unaweza kumlaani shetani kanisani lakini ukaendeleza ushetani nje ya kanisa!

Lawama zote nazipeleka kwa baba wa Taifa, marehemu mwalimu Nyerere ambaye alirithisha madaraka ya nchi yetu kwa wahuni! Haya nayoyasikia leo ni uhuni mtupu..Na matokeo yote ya Ufisadi na uharamia nchini umetokana na mwalimu mwenyewe kukabidhi nchi yetu watu wasiofaa kabisa kuwa viongozi...Kikwete hawezi kubadilisha kitu na hakuna kiongozi yeyote anayeweza kubadilisha hali hii issipokuwa kiongozi dikteta kama Kagame ambaye aliwaxhalaza bakora kwanza Wahutu na Watusi hadi wakaweka akili, wakanyooka kisha ndio akaweza kuiendeleza nchi... kinyume cha hapo tusahau na haihitaji elimu ya juu sana kuelewa.

Na nasema hivi, haitatokea kiongozi yeyote ambaye ataweza kuirudisha nchi yetu ktk mstari pasipo kuwa Dikteta.. na hakika kura yangu nitampa..

Wakati wa kudanganyana umekwisha!..Iwapo imani ya Sitta ni kuukashifu Ufisadi kanisani wakati akijua fika kwamba kanisa lake mwenyewe linaendesha sala za kumshirikisha shetani sijui atachoweza kukemea ni kitu gani..
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,901
Likes
8,114
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,901 8,114 280
Maneno mazito hayo mzee Mkandara!
 
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,525
Likes
8
Points
135
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,525 8 135
Hongera sana kwa kuona hivyo ndio maana nasema kuwa sera ya ufisadi siyo yao CCM walichukua sera hiyo kwa mbele, Toka EPA, Richmond, na madudu mengine, kweli moyo wangu unauma sana
 
I

Inviolata

Member
Joined
Apr 23, 2009
Messages
71
Likes
1
Points
0
I

Inviolata

Member
Joined Apr 23, 2009
71 1 0
Achana nao hao wapinga Ufisadi uanzishe Chama chako ambacho unaweza kusimamia sera ambazo unaziamini na unaweza kuzitekeleza without being questioned. Ukipiga kelele halafu ukabakia humo ambamo huwezi kufanya maamuzi yoyote makubwa sidhani kama inasaidia sana. These corrupt people need more than kuwapinga kwa maneno. You need to have power to take them out which you dont have. Uspika hautoshi kwa watu kama Rostam wanaonekana ni wazito sana or rather say they are the ones who rule this Country coz they do whatever they want and nobody can dare to touch them.
 
R

Rafikikabisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2009
Messages
252
Likes
36
Points
45
R

Rafikikabisa

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2009
252 36 45
Sitta anadanganya.je yuko tayari kufukuzwa chama?
Sitta amekuwa tayari kukaa na mafisadi anatafuta pa kutokea hili awe nao.

Hayuko tayari kuongoza mapambano ya kungoa mafisadi CCM.

Muda si Mrefu tutaona anawakumbatia na kuwapongeza walivyo na ngozi ngumu.
 
Drifter

Drifter

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2010
Messages
2,063
Likes
778
Points
280
Drifter

Drifter

JF-Expert Member
Joined Jan 4, 2010
2,063 778 280
Sitta na wenzake wanaotaka kuendelea kuwa na nafasi katika uongozi wa kisiasa nchini, wanajua kuwa hivi sasa chombo pekee cha uhakika kusafiria ni CCM tu ambacho kinadhibitiwa na wabaya wao. Hapo ndipo ujanja wao ulipoishia. Labda suala la mgombea binafsi likubaliwe kitu ambacho wenye CCM si wajinga kukiruhusu.
 
Rufiji

Rufiji

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2006
Messages
1,755
Likes
263
Points
180
Rufiji

Rufiji

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2006
1,755 263 180
Mkandara,

Maneno uliyoyazungumza ni makubwa sana, na wenye masikio watakuwa wamesikia. Kinachonisikitisha mimi ni kuwa hali ya Tanzania inazidi kuwa mbaya kila siku . Hawa mafisadi sasa wanacontrol every aspect ya maisha ya mtanzania, na mbaya zaidi wana hela kupita serikali !

Inasikitisha kuona watawala wetu leo awafikirii kabisa ni nchi gani watakayoachia watoto wao, wajukuu zao. Viongozi wetu wamekuwa wahuni , hawavana values kabisa. Hawajali kabisa kuhusu legacy watakayoacha.


Mimi naamini ya kuwa mtu yeyote anayesema ya kuwa anaupinga ufisadi, na ni mwananachama wa CCM ni mnafiki ! Huwezi kupinga ufisadi wakati uko kwenye chama ambacho sio tuu ni source ya ufisadi lakini pia kina embrace ufisadi !
 
Kinyambiss

Kinyambiss

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2007
Messages
1,372
Likes
7
Points
135
Kinyambiss

Kinyambiss

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2007
1,372 7 135
Sitta na Ndoto zake za 2015.. lol.. Anakemea ufisadi kweli lakini Standards and Speed isiwe Double Standards.. Mbona haongelei wale wa BRAZIL wake..lol na Ile barabara ya Dodoma iliyotiwa lami ya 3mm. ikalika mbaya... Hawa wawili wanagombania urais 2015. But wakigombana na kutajana mabaya yao, basi si mbaya as long as we know mioyo yao imekaa wapi kimaukwelii.
 
M

MgonjwaUkimwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
1,309
Likes
562
Points
280
M

MgonjwaUkimwi

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2006
1,309 562 280
Iwapo imani ya Sitta ni kuukashifu Ufisadi kanisani wakati akijua fika kwamba kanisa lake mwenyewe linaendesha sala za kumshirikisha shetani sijui atachoweza kukemea ni kitu gani..
Kwa hiyo mzee Mkandara unataka kutoa suluhisho gani hapa? Nimejaribu kukusoma mara kadhaa bila kuambulia mantiki.

Nijuavyo mimi kanisa ni la watu na wanaoweza kulibadirisha ni waumini wake, wanaoweza kubadirisha imani za kanisa ni waumini wake na sio vinginevyo. Sitta ni miongoni mwa waumini wa kanisa lake (CCM) wanaoweza kuchochea mabadiriko, ni miongoni mwa watu wanaoweza kubadiri imani ya kanisa lake.

Sasa Mkandara sijui ulitaka kushauri kwamba Sitta ajiondoe ccm au aache kukemea mabaya katika chama chake. Si mnasema change has to come from within? If so why are we discouraging those starting internal combustion that may bring about change?
 

Forum statistics

Threads 1,251,233
Members 481,615
Posts 29,763,462