makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Zile tuhuma za Mhe. Sitta,Mhe. Mwakyembe na Nnape za kutaka kuasisi chama kipya cha CCJ_Chama Cha Jamii zimejidhirisha juzi kuwa ni kweli baada ya waheshimiwa hawa kwenda Mbeya kupiga domo na kudhihirisha wazi kuwa hawa jamaa ndiyo Waanzilishi wa CCJ.
Kwa mtu yeyote makini akiangalia ile orodha ya watu walikouwepo kwenye yale maandamano/mikutano na kile kilichozungumzwa na waheshimiwa hawa moja kwa moja inaonyesha kuwa hawa ni WAASISI WA CCJ pasi na shaka yoyote.
Sitta anaposema wale waliosababisha ukosefu wa UMEME wawajibishwe anaonekana kupingana waziwazi na Waziri Ngeleja na kwa maana hiyo ni kupingana na Serikali iliyoko Madarakani ambayo yeye ni Waziri. Hapa Sitta amekiuka kanuni ya Uwajibikaji wa pamoja. Kwanza Sitta anatakiwa kujua kuwa yeye ni sehemu ya tatizo la umeme kwa vile yeye akiwa Spika aliruhusu kuundwa kwa Kamati ya Bunge iliyoibua swala zima la Richmond na hatimaye kupelekea kujiuzulu kwa Lowassa.
Mitambo hii hii ya Richmond ambayo Kamati ya Bunge ya Sitta ikiongozwa na Mhe. Mwakyembe ilisema haifai na hata baada ya ushauri wa kina Zitto na TANESCO kuwa mitambo hiyo inunuliwe na TANESCO ili kuliokoa Taifa LISSINGIE GIZANI. Leo wamekuja Wamarekani wa Symbion na kuthibitisha kuwa mitambo hiyo una ubora wa hali ya juu.
Sasa nchi imo gizani tayari. Je,huyu Sitta na Mwakyembe hawaoni kuwa wao ni sehemu ya tatizo la nchi kuingia gizani na wanatakiwa waachie ngazi?