Nikupateje
JF-Expert Member
- Dec 22, 2009
- 1,334
- 988
Huyu Sitta ni opportunist, tunakumbuka alikataa mwanzo Serikali tatu wananchi walioyeipendekeza katika maoni yao. Sasa ameona upepo haugeuzi uelekeo na yeye ameamua kuungana nasi kimwli lakini kiroho kuna kitu analenga. Huyu Mzee wa CCJ amechoka na anatakiwa apumzishwe maana majeraha ya kuukosa uspika au Uwaziri Mkuu bado yanamsumbua.
Tanganyika bila Zanzibar inawezekana!
tatizo si Samwel Sitta, tatizo ni kumbukumbu ndogo ya watu humu JF na kukurupuka bila kufanya research. Sitta tangu limeanza suala la katiba mpya yeye hoja yake ni kutotaka marais watatu.
Haya ni marudi tu ya kauli yake, na kwa sisi tunaokumbuka kauli yake ya kwanza ningeshangaa kama angesema tofauti na alivyosema.