Sitta: Marais watatu hapana, CCM iache kichwa ngumu iridhie serikali tatu

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
a.JPG

  • "Mimi nilipomsikiliza Jaji Warioba safari hii, jinsi alivyojenga hoja ya serikali tatu, nimeona kuna hoja za msingi sana zipo kwa sababu kuna mambo makubwa na ya msingi yameshafanyika. Huwezi kupitisha Katiba inayosema miswada inayopitishwa bungeni isifanye kazi Zanzibar hadi Baraza la Wawakilishi likae na kuridhia, ukishafika hapo, basi serikali tatu haziepukiki," alisisitiza Sitta.

WAKATI Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amewasilisha rasimu ya pili ya mabadiliko ya Katiba kwa Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta, amesema Tanzania haiwezi kuongozwa na marais watatu.
Sitta alisema anakubaliana na mawazo ya tume ya Warioba ya kuwa na serikali tatu, lakini hakubali Rais wa Zanzibar na Tanganyika nao waitwe marais kama yule wa Muungano.

Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema kuwa ili serikali tatu zifanye kazi kwa kuheshimiana, kuwekeana mipaka, rais wa Tanganyika na wa Zanzibar, wapewe majina na hadhi nyingine ili Tanzania iwe na rais mmoja tu wa Muungano.
"Niliposikia maoni na ufafanuzi wa kina jinsi serikali tatu zitakavyokuwa, nimekubaliana na mawazo ya tume kwamba tuwe na serikali tatu. Lakini kwa maoni yangu tuwe na amiri jeshi mkuu mmoja tu ambaye ni Rais wa Muungano, maana hatuwezi kuwa na marais watatu kwenye nchi mmoja," alisisitiza. Waziri huyo mwandamizi wa Serikali ya Rais Kikwete, alitolea mfano wa Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC) kwamba rasimu yake imependekeza kuwa na rais mmoja tu na si marais sita wanaounda shirikisho hilo.

Pia alipendekeza jina la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania libadilishwe na badala yake liitwe Shirikisho la nchi za Tanzania.
Akizungumzia msimamo wa Chama chake Cha Mapinduzi (CCM), kupinga serikali tatu na kutaka muundo wa serikali mbili uendelee, Sitta alisema kuwa CCM isibaki kuwa kichwa ngumu kupinga serikali tatu.

Alisema CCM inakosea kung'ang'ania serikali mbili wakati Katiba ya Zanzibar ndiyo iliamua serikali mbili, hivyo serikali ya tatu kwa sasa haiepukiki.
Akitolea mfano, alisema Katiba ya Zanzibar inataka miswaada yote inayopitishwa na Bunge la Jamhuri iridhiwe kwanza na Baraza la Wawakilishi, jambo ambalo alisema si sahihi. Alisema Katiba ya Zanzibar imefanya mambo mengi kuihalalisha Zanzibar kuwa nchi kamili na imefanya mambo hayo bila ridhaa ya Tanzania Bara.

Alisema ili kubaki na serikali mbili, lazima Zanzibar ikubali kuifumua Katiba yake inayotoa mamlaka kamili kwa rais wa visiwa hivyo, jambo ambalo alisema Wazanzibari hawawezi kulikubali.
"Mimi nilipomsikiliza Jaji Warioba safari hii, jinsi alivyojenga hoja ya serikali tatu, nimeona kuna hoja za msingi sana zipo kwa sababu kuna mambo makubwa na ya msingi yameshafanyika. Huwezi kupitisha Katiba inayosema miswada inayopitishwa bungeni isifanye kazi Zanzibar hadi Baraza la Wawakilishi likae na kuridhia, ukishafika hapo, basi serikali tatu haziepukiki," alisisitiza Sitta.

Sitta alisema tume ya Warioba imefanya kazi kubwa na nzuri kwani rasimu ya pili imekwenda mbali kuangalia vitu kama zawadi za viongozi, jambo ambalo zamani viongozi waliona ni haki yao kupata zawadi za aina hiyo bila kujali kwamba hiyo ni rushwa.
Kwa mujibu wa Sitta, kuna mambo ya msingi ya kuendelea kujadili nje na ndani ya CCM nayo ni namna ya kuiendesha Serikali ya Muungano kwani kwa maoni ya tume, serikali hiyo itakuwa ikichangiwa zaidi na Tanganyika, jambo ambalo linaweza kuibua manung'uniko ya upande mmoja wa Muungano.

Aliwataka Wana CCM na wadau wengine kuifanyia kazi kauli ya Rais Kikwete aliyokaririwa mara kuwa vyama visipojali masilahi ya taifa katika mchakato wa Katiba, Katiba mpya itakwama na Watanzania watalazimika kuendelea kutumia katiba ya sasa.
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
Samweli Sitta ana mtazamo wa kitaifa zaidi katika kuangalia sura kamili ya rasimu ya katiba ilivyoandaliwa na Tume kuwa imekaa vema kwa misingi ya kuangalia kuondoa migongano iliyopo sasa na katiba ya Tanzania visiwani. Haoni shida kuwashushia shutuma wanachama wenzake wa CCM na msimamo wa chama kwa jumla kwa kuwaasa kuacha kichwa ngumu kwa kuwa ving'ang'anizi wa serikali mbili. Naona kati ya viongozi waandamizi ndani ya CCM na serikali Sitta kichwa chake kimetulia.
 
Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,873
1,500
Mtazunguka sana lakini tatizo linafahamika na CCM hawataki kuli face, kwasababu wamewalea sana Wazanzibari.

Mworobani wa haya yote ILIKUWA SERIKALI MOJA, AMRI JESHI MMOJA.

Lakini kwakuwa Watanganyika tunawaogopa Wazanzibari mtapendekeza hata SERIKALI 20 lakini hamata waridhisha kamwe Wazanzibari, chokochoko zitaendelea na one day Muungano utavunjika tu.
 
IPECACUANHA

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
3,143
2,000
He was once said to be a person with Two tongues meaning what comes out of his mouth should not be taken as what he believes. What you are seeing coming out of him is a "jerky" movement after being left out.....
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
He was once said to be a person with Two tongues meaning what comes out of his mouth should not be taken as what he believes. What you are seeing coming out of him is a "jerky" movement after being left out.....

Jadili hoja yake ya kuamini kwamba serikali tatu ni sehemu ya kupunguza matatizo ya Muungano kuliko ilivyo sasa serikali mbili. Nakubaliana naye kwamba kuwa na marais watatu katika nchi mmoja haijengi mangiki, labda tungekuwa na jina tofauti kwa watakaoongoza serikali ya Tanganyika na serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Labda uwazi wa Sitta kwamba CCM iache kichwa nguvu kuridhia serikali tatu ndo kianchowaumiza zaidi nahisi, lakini ukweli ndio huu wataalamu katika masuala ya sheria na uongozi ambao wapo ndani ya jopo la Tume ya katiba wameangalia kwa undani na kuoanisha maoni ya wananchi na taasisi mbalimbali.
 
Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,574
2,000
Samweli Sitta ana mtazamo wa kitaifa zaidi katika kuangalia sura kamili ya rasimu ya katiba ilivyoandaliwa na Tume kuwa imekaa vema kwa misingi ya kuangalia kuondoa migongano iliyopo sasa na katiba ya Tanzania visiwani. Haoni shida kuwashushia shutuma wanachama wenzake wa CCM na msimamo wa chama kwa jumla kwa kuwaasa kuacha kichwa ngumu kwa kuwa ving'ang'anizi wa serikali mbili. Naona kati ya viongozi waandamizi ndani ya CCM na serikali Sitta kichwa chake kimetulia.

Nakubaliana na Sitta kwenye hili la Marais watatu. Ilahili la yeye kusema amekuwa convinced na Warioba ........... yeye kama kiongoziwa serikali kwa miaka mingi tena akiwa na vyeo nyeti kama Uspika, Uwaziri wakatiba n.k. alitakiwa kuziona hizo kasoro siku nyingi.Anavyoibuka leo na kusema hivi inaonyesha ni jinsi gani propaganda za CCMzilivyoliharibu Taifa na ni aina gani ya viongozitulionao...................... they do not have independent mind rather theycannot speak their minds openly!!
 
mrelbattawy

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
564
195
Ivi ndugu zetu wa Tanganyika na Samuel SiTTA., bado katika nafsi zenu hamtaki kukubali kwanini kama Zanzibar ni nchi?

1. Unaposema Rais awe mmoja wa Muungano wengine kutoka Tanganyika na Zanzibar wawe wakuu wa Mikoa kwa mtazamo wa kawaida nani atakubali hiyo rai kutoka Zanzibar? hata Dr Shein haikubali.,

2. Na jengine kwanini miswada isipite Baraza la Wawakili kujadiliwa ndio iwe shehira kwa Zanzibar., manaake huyu Sitta alikusudia kuimaliza kabisa kabisa Zanzibar., yaani alitaka Wazanzibar wamezwe kuliko kumezwa

Si mtu mzuri Sitta., ana nia mbaya sana Wazanzibar., wacha makaratasi ya Rasimu ya kwanza kabla kuunda tume yachanwe chanwe mbele yake hadi jasho likamtoka.
 
georgeallen

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
3,755
1,225
Jadili hoja yake ya kuamini kwamba serikali tatu ni sehemu ya kupunguza matatizo ya Muungano kuliko ilivyo sasa serikali mbili. Nakubaliana naye kwamba kuwa na marais watatu katika nchi mmoja haijengi mangiki, labda tungekuwa na jina tofauti kwa watakaoongoza serikali ya Tanganyika na serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Labda uwazi wa Sitta kwamba CCM iache kichwa nguvu kuridhia serikali tatu ndo kianchowaumiza zaidi nahisi, lakini ukweli ndio huu wataalamu katika masuala ya sheria na uongozi ambao wapo ndani ya jopo la Tume ya katiba wameangalia kwa undani na kuoanisha maoni ya wananchi na taasisi mbalimbali.
[/QUOTE

Labda tuwe na ushirikiano kama wa ulaya (EU) . kila nchi iwe na kila kitu rais, jeshi, polisi etc Raisi wa muungano awepo tu kama ilivyo kwa emmanuel Barrosso
 
mharakati

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,273
1,225
sitta amekua mtu wa kimantiki zaidi ndani ya uongozi huku akichukua utaifa zaidi kitu kisichokubalika ndani ya CCM na imeshamgharimu (uspika) na bila M/kiti kua anamuheshimu mzee sitta nafikiri hata uanachama asingekua nao achilia mbali uwaziri wake
 
Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Mwanasiasa mahili ni yule anayekuwa na nguzo ya kisiasa. Huwezi kutumia hoja za mwanasiasa asiye na nguzo kisiasa kutaka kuhalalisha hoja kwa vile tu ameongea jambo ambalo linapaka mafuta mawazo na fikra zako.

Huyu mwanasiasa anaposema CCM ni kichwa ngumu anasahau kuwa hata yeye pia ni kichwa ngumu kwa sababu bado ni CCM na kikubwa kabisa ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM. Hata wakati Zanzibar inafanya mchakato katika Katiba yao, hakuweza hata kupiga kelele za kisiasa kuhusiana na madudu waliyoweka ambayo yanagongana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano (1977).

Mh. Sitta anatumia unafiki wake kuchota na kuingiza wananchi katika harakati zake za kisiasa kwa kujiondoa katika sarakasi za CCM ambazo zimezaa katiba ya Zanzibar inayopingana na Katiba ya JMT (1977).

Siasa za matukio na fuata upepo wa kisiasa haziwezi kumsaidia katika harakati zake kwa sababu anafanya wananchi washindwe kuuelewa msimamo wake wa kesho achilia mbali kesho kutwa.

Mwarobaini wa kero za Muungano ni kura ya maoni peke yake ili kupata political legitimacy na siyo political cherry picking. Serikali tatu, nne, tano au sita haziwezi kuondoa kero sugu za muungano ambazo zinachagizwa na ubinafsi wa Wazanzibari.

Hawa ndiyo wanasiasa wa Tanzania.
 
FDR.Jr

JF-Expert Member
Jun 17, 2008
1,356
1,500
Kauli hii ya Samwel Sitta imeniumiza moyo sana , hivyo Mheshimiwa Samwel Sitta, wana Jf na wana CCM wenzangu "Nini maoni yenu juu ya yale yaliyotangulia kusemwa na Tundu Lissu 2011-13 kuwa ujio wa katiba mpya ya Zanzibar ni uhaini na kuvunja Muungano???"

  • "Mimi nilipomsikiliza Jaji Warioba safari hii, jinsi alivyojenga hoja ya serikali tatu, nimeona kuna hoja za msingi sana zipo kwa sababu kuna mambo makubwa na ya msingi yameshafanyika. Huwezi kupitisha Katiba inayosema miswada inayopitishwa bungeni isifanye kazi Zanzibar hadi Baraza la Wawakilishi likae na kuridhia, ukishafika hapo, basi serikali tatu haziepukiki," alisisitiza Sitta.

WAKATI Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amewasilisha rasimu ya pili ya mabadiliko ya Katiba kwa Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta, amesema Tanzania haiwezi kuongozwa na marais watatu.
Sitta alisema anakubaliana na mawazo ya tume ya Warioba ya kuwa na serikali tatu, lakini hakubali Rais wa Zanzibar na Tanganyika nao waitwe marais kama yule wa Muungano.

Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema kuwa ili serikali tatu zifanye kazi kwa kuheshimiana, kuwekeana mipaka, rais wa Tanganyika na wa Zanzibar, wapewe majina na hadhi nyingine ili Tanzania iwe na rais mmoja tu wa Muungano.
"Niliposikia maoni na ufafanuzi wa kina jinsi serikali tatu zitakavyokuwa, nimekubaliana na mawazo ya tume kwamba tuwe na serikali tatu. Lakini kwa maoni yangu tuwe na amiri jeshi mkuu mmoja tu ambaye ni Rais wa Muungano, maana hatuwezi kuwa na marais watatu kwenye nchi mmoja," alisisitiza. Waziri huyo mwandamizi wa Serikali ya Rais Kikwete, alitolea mfano wa Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC) kwamba rasimu yake imependekeza kuwa na rais mmoja tu na si marais sita wanaounda shirikisho hilo.

Pia alipendekeza jina la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania libadilishwe na badala yake liitwe Shirikisho la nchi za Tanzania.
Akizungumzia msimamo wa Chama chake Cha Mapinduzi (CCM), kupinga serikali tatu na kutaka muundo wa serikali mbili uendelee, Sitta alisema kuwa CCM isibaki kuwa kichwa ngumu kupinga serikali tatu.

Alisema CCM inakosea kung'ang'ania serikali mbili wakati Katiba ya Zanzibar ndiyo iliamua serikali mbili, hivyo serikali ya tatu kwa sasa haiepukiki.
Akitolea mfano, alisema Katiba ya Zanzibar inataka miswaada yote inayopitishwa na Bunge la Jamhuri iridhiwe kwanza na Baraza la Wawakilishi, jambo ambalo alisema si sahihi. Alisema Katiba ya Zanzibar imefanya mambo mengi kuihalalisha Zanzibar kuwa nchi kamili na imefanya mambo hayo bila ridhaa ya Tanzania Bara.

Alisema ili kubaki na serikali mbili, lazima Zanzibar ikubali kuifumua Katiba yake inayotoa mamlaka kamili kwa rais wa visiwa hivyo, jambo ambalo alisema Wazanzibari hawawezi kulikubali.
"Mimi nilipomsikiliza Jaji Warioba safari hii, jinsi alivyojenga hoja ya serikali tatu, nimeona kuna hoja za msingi sana zipo kwa sababu kuna mambo makubwa na ya msingi yameshafanyika. Huwezi kupitisha Katiba inayosema miswada inayopitishwa bungeni isifanye kazi Zanzibar hadi Baraza la Wawakilishi likae na kuridhia, ukishafika hapo, basi serikali tatu haziepukiki," alisisitiza Sitta.

Sitta alisema tume ya Warioba imefanya kazi kubwa na nzuri kwani rasimu ya pili imekwenda mbali kuangalia vitu kama zawadi za viongozi, jambo ambalo zamani viongozi waliona ni haki yao kupata zawadi za aina hiyo bila kujali kwamba hiyo ni rushwa.
Kwa mujibu wa Sitta, kuna mambo ya msingi ya kuendelea kujadili nje na ndani ya CCM nayo ni namna ya kuiendesha Serikali ya Muungano kwani kwa maoni ya tume, serikali hiyo itakuwa ikichangiwa zaidi na Tanganyika, jambo ambalo linaweza kuibua manung'uniko ya upande mmoja wa Muungano.

Aliwataka Wana CCM na wadau wengine kuifanyia kazi kauli ya Rais Kikwete aliyokaririwa mara kuwa vyama visipojali masilahi ya taifa katika mchakato wa Katiba, Katiba mpya itakwama na Watanzania watalazimika kuendelea kutumia katiba ya sasa.
 
mharakati

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,273
1,225
Serikali tatu haziepukiki na kama znz wanaogopa kumuita kiongozi wao kitu kingine chochote chini ya Rais kwa kuhisi kuiua znz, sisi tulioiua Tanganyika kwa miaka zaidi ya 50 tunataka Tanganyika yetu iwe na mamalaka swa na znz ndani ya muungano au shirikisho hii...in other words ccm ikae tayari kuvunja muungano Tanganyika haiwezi kuendelea kumezwa na vijitu vichache visivyo na shukhran.....

ironically hao viongozi wa znz ndiyo hao hao wanaomiliki mali nyingi huku Bara na mama zao na baba zao wakiishi huku..Tanganyika will only gain from this eventual break up
 
Anko Sam

JF-Expert Member
Jun 30, 2010
3,206
1,195
Huyu Sitta ni opportunist, tunakumbuka alikataa mwanzo Serikali tatu wananchi walioyeipendekeza katika maoni yao. Sasa ameona upepo haugeuzi uelekeo na yeye ameamua kuungana nasi kimwli lakini kiroho kuna kitu analenga. Huyu Mzee wa CCJ amechoka na anatakiwa apumzishwe maana majeraha ya kuukosa uspika au Uwaziri Mkuu bado yanamsumbua.

Tanganyika bila Zanzibar inawezekana!
 
Nyunyu

JF-Expert Member
Mar 9, 2009
4,357
2,000
Jadili hoja yake ya kuamini kwamba serikali tatu ni sehemu ya kupunguza matatizo ya Muungano kuliko ilivyo sasa serikali mbili. Nakubaliana naye kwamba kuwa na marais watatu katika nchi mmoja haijengi mangiki, labda tungekuwa na jina tofauti kwa watakaoongoza serikali ya Tanganyika na serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Labda uwazi wa Sitta kwamba CCM iache kichwa nguvu kuridhia serikali tatu ndo kianchowaumiza zaidi nahisi, lakini ukweli ndio huu wataalamu katika masuala ya sheria na uongozi ambao wapo ndani ya jopo la Tume ya katiba wameangalia kwa undani na kuoanisha maoni ya wananchi na taasisi mbalimbali.

We may call them Prime Ministers!!!
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,413
2,000
CCM ilinganishe uwezo wa kujenga hoja kati ya 6 na E.L ...mie CCM siipendi ila namkubali sana 6 kwa uwezo wake wa kucheza na siasa ya hoja na si ya kununua watu kama mwenzie
 
MWANAKA

JF-Expert Member
Oct 4, 2013
4,289
2,000
Huyu Sitta ni opportunist, tunakumbuka alikataa mwanzo Serikali tatu wananchi walioyeipendekeza katika maoni yao. Sasa ameona upepo haugeuzi uelekeo na yeye ameamua kuungana nasi kimwli lakini kiroho kuna kitu analenga. Huyu Mzee wa CCJ amechoka na anatakiwa apumzishwe maana majeraha ya kuukosa uspika au Uwaziri Mkuu bado yanamsumbua.

Tanganyika bila Zanzibar inawezekana!

hapana mkuu huyu jamaa yupo sahihi kwa mazingira haya ya sasa
Kama utakumbuka vema ni kweli aliwahi kusema juu ya kuwepo kwa serikali 2 au 1 kwa kigezo kwamba kitendo cha kuweka serikali tatu ni dhahili tunakwenda kuuvunja muungano
Na maadamu wenzetu zanzibar wameng'ang'ania kuwa na mamlaka kamili kwenye serikali yao haitakuwa jambo jema kwa watanganyika kunyimwa serikali yao
Kwa hiyo option zilizopo kwa sasa ni mbili tu either tuwe na serikali moja kwa maana ya jamhuri ya muungano wa tanzania au tuwe na serikali tatu yaani tanganyika zanzibar na muungano na kwakweli kwa hili la serkali tatu ni ukweli usiopingika kwamba muda si mrefu muungano utakuwa kwishney !
 
Kigonsela

Member
Dec 31, 2013
24
0
kwa hiyo mh sitta mwanzoni alipinga serikali 3 bila kuwa na sababu za msingi? kama kiongozi mwandamizi alitakiwa hayaone haya tokea awali, hivyo ya kuwa katiba ya zanzibar ina dosari ndio amejua leo?
 
mpemba mbishi

JF-Expert Member
Nov 27, 2011
1,132
1,195
Mh Sitta najua unaupenda sana muungano lakini ushauri wako kuwa kuwepo na serikali 3 lakini zanzibar na tanganyika kusiwe na rais bali waitwe majina mengine ni kosa kubwa sana ambalo wazanzibar hawatoweza kukusamehe kabisa.
Ukweli wa hali ilivyo nikuwa wazanzibar wengi hawaupendi muungano kwa madai unawakandamiza, hivyo wametafuta njia ya kujikwamua ili angalau wapunguze wanayoyaita madhila ya muungano, hivyo ilionekana njia sahihi ni mamlaka kamili na wakikosa hayo angalau iwe serikali 3.
hivyo kwa ushauri huo nadhani hata hao wa ccm ambao wanaunga mkono serikali 2 kwa hilo watalikataa.
kumbuka warioba alisema waliamua kukubali serikali 3 ili kuulinda muungano, akimaanisha kuwa wazanzibar hawaupendi muungano ila upande wa bara ndio wanaoung'ang'ania.
hivyo basi njia pekee ambayo bara itaendelea kufanya nikuwaridhisha wazanzibar ili usivunjike muungano. swali la kujiuliza kwanini bara ndio inaulinda sana muungano?
hilo jibu lake sitta na wenzake wanalijua.
wakatabahu.....

peche luke

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
365
0
Ivi ndugu zetu wa Tanganyika na Samuel SiTTA., bado katika nafsi zenu hamtaki kukubali kwanini kama Zanzibar ni nchi?

1. Unaposema Rais awe mmoja wa Muungano wengine kutoka Tanganyika na Zanzibar wawe wakuu wa Mikoa kwa mtazamo wa kawaida nani atakubali hiyo rai kutoka Zanzibar? hata Dr Shein haikubali.,

2. Na jengine kwanini miswada isipite Baraza la Wawakili kujadiliwa ndio iwe shehira kwa Zanzibar., manaake huyu Sitta alikusudia kuimaliza kabisa kabisa Zanzibar., yaani alitaka Wazanzibar wamezwe kuliko kumezwa

Si mtu mzuri Sitta., ana nia mbaya sana Wazanzibar., wacha makaratasi ya Rasimu ya kwanza kabla kuunda tume yachanwe chanwe mbele yake hadi jasho likamtoka.

Kwenye kuchukua na kumiliki ardhi ya Tanganyika mnaona sawa na hamuoni kuwa suala hili linatakiwa lipitishwe na blw. Ila linapokuja suala la serikali moja znz inamezwa.Nakuambieni huu ubaguzi wenu una mwisho. Kwa utaratibu huu operesheni kimbunga itadumu sana tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom