Sitta, Makame tangazeni uchaguzi Biharamulo kabla ya Mei 15 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta, Makame tangazeni uchaguzi Biharamulo kabla ya Mei 15

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serayamajimbo, May 11, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  May 11, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tayari Kabuye ameshazikwa, Mungu amlaze mahali pema. Sasa nini kinasubiri kutangaza jimbo kuwa wazi? Leo ni tarehe 11 na Tume ya uchaguzi iliwahi kusema huko nyuma kuwa ikifika tarehe 15 Mei kama hakuna kiti kilichotangazwa kuwa wazi ndio hivyo tena hakuna uchaguzi mwingine wa marudio wa ubunge mpaka uchaguzi mkuu 2010. Je, CCM mnaogopa ya Tarime na Busanda ndio maana mmeamua kushirikiana na Sitta na Makame kuweka mpira kwapani?

  Serayamajimbo
   
 2. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,223
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Hilo ndo basi tena hadi 2010. lazima kusoma upepo wa busanda unavyokwenda isije ikawa another loose tp CCM. Ni jambo jema hilo jimbo likisubiri 2010. upinzani sasa needs a break, wasije wakajikuta hawana hela za 2010.

  Cha msingi ni kuhakikisha ifikapo hiyo 2010, hakuna jimbo mbunge wa CCM kupita bila kupingwa kama ilivyotokea kwenye baadhi ya majimbo 2005. Hata kama ni kwa kushindwa lakini upinzani uwepo tu.
   
 3. M

  Mwakaleli Member

  #3
  May 11, 2009
  Joined: Sep 23, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninachoelewa mimi ni kwamba Kabuye hakuwa mbunge baada ya mshindani wake pwana Choya kumpeleka mahakani kuwa alitumia lugha ya matusi na mahakama ikaamua bwana Choya apewe ubunge. Lakini Marehemu Kabuye alikata rufaa ambayo mpaka mauti yanamkuta ilikuwa haijaamuliwa. tuendelee na mjadala sasa, karibuni
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  watu wanawaza uchaguzi kazi hawafanyi......kama kule busanda nafikiri coster 4 zinajaa viongozi wa ccm walioko kule....
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135


  Hapa umesema kweli. Bora kuwe na upinzani hata wakishindwa ili mradi wame pingwa.
   
 6. C

  CHANGA Member

  #6
  May 12, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Tayari Sita ameandika barua kutangaza kuwa Jimbo liko wazi kwenda kwa Makame. Sasa ni makame kutangaza tarehe ya uchaguzi tu
   
 7. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2009
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,611
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Kazi ipo mwaka huu
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280
  Makame atasema hana hela!!! Economy crunch!!!!!!!!!!!!! Si mnawajua SISIEM???
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...