Elections 2010 Sitta: Kutoka Uspika hadi Uwaziri; safari ya anguko inakaribia

kutoka kuwa mhimili mmoja wapo wa serikali mpaka kupewa kawizara...nadhani angekataa alafu angepaisha zaidi sauti yake bungeni na angegombea urais 2015................lkn kwa kuwa kwake cheo ni cheo tu hata km ni kuwa kiongozi wa waokota makopo basi..
 
Hapo kwishnehi.....waulizeni CHENGE,MSABAHA,KAMALA hii wizara nuksi sana miaka mitano tu watu watatu wamekufa kisiasa
 
Mi naona kama kafungwa vile. Kwa kuunganishwa ndani ya serikali atasema nini tena.
 
Ni kumpoza maumivu tu ila kwa mwendo wa siasa nchini sasa hivi hawataweza...hawajui kuwa sitta was a soldier there is an army!!!!!!
 
Hakustahili kuwa kwenye baraza!

Sikio la kufa halisikii dawa. Mwanzo nilimwambia hasichukue fomu ya Uspika, hakusikia; baada ya kutemwa kwa style ya kumchinjia kobe baharini; nikamwambia tena asikubali kuingia kwenye baraza la mawaziri, hajasikia tena. Sasa asubiri huko kujiita 'chuma cha pua' kutakapokuwa 'mpira wa pua'.
 
MAFISADI wamemfanyia kweli tena Mhe Sitta!!!!

Kwa heshima zote EAC si wizara bali ni Idara mojawapo katika Wizara ya Mambo ya Njee. Kawekwa pale strategically ili:

(1) ASIPATE mwanya wa kushughulika na mambo yatakayomfanya aendelee kuvutia kwetu sisi Wananchi kwa sababu hiyo wizara wala haitugusi, pia

(2) ni kumkomesha huko kwa sababu Idara hiyo ya EAC siku zote haina bajeti, programu wala mashirika ya kusimamia.

(3) Kumfunika mdomo na dhana ya 'Jukumu la Pamoja kwa Baraza la Mawaziri' kusudi akose uwanja mmpana wa kukemea bali kutumikia MAFISADI. Ndio hivyo kapatikana mtego wa pili tena!!!

Anyway, kibendera kitakwepo kwenda kijijini na kaulinzi.
 
Sitta ameshaahidi kuendeleza mapambano na mafisadi hata bila kuwa Spika wa bunge. Hili bila shaka alikusudia kulifanya akiwa mbunge wa kawaida kwa njia ya kuihoji serikali. Lakini sasa kwa kuchaguliwa kuwa Waziri anajikuta mahali pa kuulizwa yeye maswali na kuyajibu.

Serikali iliyopo leo ndiyo ile ile aliyoitikisa jana akionesha kuwa imejaa mafisadi. Sasa ni sehemu ya serikali hiyo. Kuendelea kuitikisa akiwa waziri humo ndani kwa ndani ni sawa na kusukuma gari ukiwa wewe mwenyewe uko ndani yake, unaabiri. Simply impossible.

Sasa kwa dhamiri yake Sitta itafanyaje kama kweli anataka kuitii? Maamuzi mengi ni dhahiri yatapingana na dhamiri yake, naye atalazimika kuyatetea, mfano ni bei ya bati iliyokubalika EAC. Option ni moja tu, KUJIUZULU uwaziri na kurudi bungeni kama muuliza maswali. Ushujaa huo ataumudu?
 
Hilo nalo neno
 
huyu mzee walimmaliza siku ile ile walipomkata jina lake kugombea Uspika, sasa hivi Yeye na Mwakyembe kwisha kazi - hawana meno tena, acha mzee wa watu ale na yeye za mwisho mwisho kabla ya kurudi kwao Urambo kustaafu kwa amani.

Huwezi kushambulia genge la wanyanganyi wakati na wewe umo humo humo.
 
Good Question but.....! Kila mtu anapenda ulaji, Sitta wamempa ulaji unadhani ataukataa? Ataukubali labda afikiri kuleta mageuzi akiwa humo humo ndani kwa kushawishi mabadiliko fulani fulani ya utendaji lakini kutema keki iliyo mdomoni mh!!! itakuwa ngumu kidogo.
 
WanaJF,
Kwa maoni yangu binafsi, kukubali kwa Sitta Wizara ya EA ni kukubali kuhongwa na kunyamazishwa kwa yale aliyofanyiwa. Iwapo kweli atakubali nitakuwa nimethibitisha yale ambayo siku zote nimeyasema kuwa " Hana Uti wa Mgongo". Kuna siku ukweli utawekwa hadharani. Lakini akikubali na akawauza Watanzania kwa ajili ya maslahi yake binafsi, basi ninamtakia Heri sana....

MAFISADI wamemfanyia kweli tena Mhe Sitta!!!!

Kwa heshima zote EAC si wizara bali ni Idara mojawapo katika Wizara ya Mambo ya Njee. Kawekwa pale strategically ili:

(1) ASIPATE mwanya wa kushughulika na mambo yatakayomfanya aendelee kuvutia kwetu sisi Wananchi kwa sababu hiyo wizara wala haitugusi, pia

(2) ni kumkomesha huko kwa sababu Idara hiyo ya EAC siku zote haina bajeti, programu wala mashirika ya kusimamia.

(3) Kumfunika mdomo na dhana ya 'Jukumu la Pamoja kwa Baraza la Mawaziri' kusudi akose uwanja mmpana wa kukemea bali kutumikia MAFISADI. Ndio hivyo kapatikana mtego wa pili tena!!!

Anyway, kibendera kitakwepo kwenda kijijini na kaulinzi.
 
Hii wizara ya kushughulikia mambo ya Afrika Mashariki ni upuuzi mtupu na kupeena tuu vyote, kwanini iyo shughuli isiwe chini ya wizara ya mambo ya nje? Hatuwezi kuanzisha wizara kwa kila jambo. Je tuanzishe wizara ya Globalization? Wizara ya kushughulikia uhusiano na Ulaya, wizara ya kushughulikia uhusiano na Amerika... Hii ni kuwaumiza wapiga kura maana hiyo wizara ya uhusiano wa Afrika Mashariki kazi yake nini? Ina Katibu, Naibu, Waziri na wafanyakazi kibao. Kama pana balozi wa Tanzania Afrika Mashariki je wizara ya nini?
 
Kutoka kiongozi wa mhimili wa pili wa dola (bunge) hadi kuongoza wizara isiyojulikana ya Afrika Mashariki naweza kusema isiyo na hadhi kwake kwa vile huwezi kuilinganisha na wizara kama ya Katiba na Sheria.

Sitta amepewa nafasi hiyo ili kumpoza kutokana na machungu aliyopata baada ya jina lake kukatwa kwa makusudi kwenye kinyang'anyiro cha uspika kwa madai kwamba safari hii ni zamu ya wanawake kuongoza mhimili huo wa dola.

Sitta amewekwa hapo kama pazia kwa nia ya kumfunga mdomo ili asitumie nafasi yake kama mbunge huru kuichachafya serikali kama alivyokuwa akiruhusu mijadala ya aina hiyo wakati alipokuwa spika katika Bunge lililopita.

SS ajifunze kwa waliomtangulia kuongoza wizara hiyo kama Dk. Ibrahim Msabaha na Deodorous Kamala kuwa hawakusikika na mwisho wa siku si kuwa walianguka kisiasa tu bali walishindwa kwenye majimbo yao pia.

Nampa miaka miwili tutakuwa tumemsahau kwenye nyanja za siasa.
 
Jamani Sitta kelele zake zilikuwaa kulindaa tumbo lake kupitia rasilimali za umma kwani cheo kwake ndo neema..ni vizuri kumwona spika aliyepita akiwajibika kwenye uwaziri....

jk kawategaa wabayaa wake ili mradi kumlaumu sasa hawawezi tenaa..magufuli vs mwakyembe.....waooooooooo..
 
Back
Top Bottom