Sitta: Kutoka Uspika hadi Uwaziri; safari ya anguko inakaribia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Kutoka Uspika hadi Uwaziri; safari ya anguko inakaribia

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by skeleton, Nov 21, 2010.

 1. s

  skeleton Member

  #1
  Nov 21, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliyekuwa mpinga ufasadi na spika wa bunge mh. Samuel Sitta kwa mtazamo wangu amejimaliza kabisa kisiasa.

  Nasema hivyo kwani kwa kukubali kubaki na kungojea cheo atakachopewa na JK(nasema anangojea cheo kwani sioni sababu nyingine ambayo ingemfanya abaki CCM baada ya kujeruhiwa hivyo), ni kwamba amekubali kununuliwa na hawezi kupinga ufisadi kwenye chama ambacho ni cha kifisadi. Hii inamaanisha kwamba juhudi zake zote za kupinga ufisadi ni sifuri kama amekubali kumkumbatia JK na pia kwa kukubali kubaki kwenye chama kilichomjeruhi vibaya sana katika kinyang'anyiro cha uspika.

  Yote aliyoyafanya nyuma kwangu mimi yanakuwa hayana maana tena kwani amerudi kundini kwa mafisadi hata kama yeye si fisadi, lakini ndo keshamkumbatia bosi wake ambaye ni fisadi. Kumpinga itakuwa ngumu sana kama atapewa ulaji naJK, na hata akipinga havitakuwa na nguvu akiwa ndani ya chama kwani atakuwa keshawekwa mfukoni kwa kupewa ulaji.

  Mh. Sitta nae anaonyesha nae ana njaa kwani hamna sababu ambayo ingemfanya aendelee kubaki ndani ya CCM kama si njaa na kusubiria kupozwa cheo. Inamaanisha nae anapenda cheo kuliko wananchi aliodai anawapenda sana na anatetea maslahi yake. Sikutegemea kwa mtu mwenye busara kama yeye bado angebaki CCM.

  Kwangu mimi ni kwamba amekwisha vunjwa miguu kabisaa. Na hatakuwa tena na nguvu za kupiga vita ufisadi kama JK atampa ulaji. Na hii ina apply kwa wapinga ufisadi wote walio ndani ya CCM hawatakuwa na nguvu sana ya kupambana na ufisadi kwani sasa hivi vigezo vya CCM ni kwamba kama unataka kuwa mwana CCM mzuri, criteria ya kwanza ni either usipinge ufisadi au uwe neutral.

  Kwa kifupi CCM ni chama chenye viongozi wanao encourage ufisadi na hivyo inakuwa ndio itikadi ya chama na wanachama wake wote! Huwezi kupinga ufisadi vizuri ukiwa ndani ya chama cha wasanii na majangili kama kina Rostam, Lowassa, Makamba, JK n.k. Watakumaliza tu! Hivyo mh. Sitta kabla hujachelewa ondoka CCM! Hujachelewa!
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 25,261
  Likes Received: 7,080
  Trophy Points: 280
  Yaweza kua kweli
   
 3. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,301
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  asante mkuu lakini ungeifanya japo kusomeka hivyo ingewavutia wengi lakini umevingirisha mno kiasi kwamba habari
  yako inachosha kuisoma japo ni funpi
   
 4. m

  mgalatia mbongo Member

  #4
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu ni bonge la mnafiki ambaye mimi naona tayari kashalipia gharama ya unafiki wake.
   
 5. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,301
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  tungo tata....ama tungo tegemezi.....hebu imwage yote
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nawashangaa mnaosema Sitta kajiua kisiasa wakati ametangaza kustaafu siasa 5 years to come na anataka apumzike na familia yake ale pension yake. Any way kitu chochote kinachoonekana kuwafurahisha wanachadema hata kama ni pumba lazima kiletwe hapa. Badilikeni
   
 7. Gobegobe

  Gobegobe JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 245
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mtazamo kwa mtazamo, Skeleton kumbuka kwamba Sitta aliomba ridhaa kwa wana urambo ili aweze kuwawakilisha Bungen kwa kuwa Mbunge wao, kumbe basi mengine ni matokeo tu ya kuwa Mbunge. Ni dhahiri kuwa baada kuupata ubunge alipenda kuwa Spika, lakini CC ikaamua vinginevyo. Sasa, kwa kuukosa uspika ndo sababu ya kuhama chama? Ungewafaa nini uamuzi huo wana urambo ambao walimwamini na kumpa ridhaa ya kuwawakilisha? Unakumbuka falasafa yake ya kwamba kazi ya siasa inahitaji kuwa na ngozi ngumu? Hebu mtafakari tena katika angle hiyo.
   
 8. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35


  Angelistaafu siasa kwa heshima na taadhima na watu wasingemsahau kama angejitoa toka CCM lakini kwa aina hii ya kusubiri apewe cheo cha uwaziri ni kutetea zaidi ulaji wake na si kwa ajili ya wananchi kama anavyodai siku zote.
   
 9. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  KISIKI CHA MPINGO MWANZO MWISHO,,,,,hakuna kujiua kisiasa wala nini
   
 10. m

  mgalatia mbongo Member

  #10
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alikuwa analiongoza bunge muhimili wa dola unao jitegemea . Sasa pamoja na kudhalilishwa kote huko bado ukawe AnsRable kwa Pinda hata kama ni maslahi yake binafsi, hapana, maana si ya wana urambo hatukumtuma akadhalilishwe kiasi hiki, na unyamaze ili ututumikie. Kweli kuna jamaa alishaniambia ukiwa mwanasisa hunatofauti na mbwia unga. Watu wanasema mvi nyingi ni busara, lakini kwa mheshimiwa huyu msemo huu nina wasiwasi tena mkubwa. Busara ya kweli ni ile mtu apewayo na MUNGU.
   
 11. J

  John10 JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama akiondoka CCM basi maisha yake yanaweza kuwa hatarini. Kumbuka kina Malima, Kolimba. CCM ni chama cha FreeMason.

  CCM-FreeMason, wapo tayari kummaliza mtu yoyote kimaisha iwapo mtu huyo, ataleta athari ktk CCM-FreeMason. Nchi yetu ishaliwa na hawa wezi CCM-Mason.
   
 12. m

  mgalatia mbongo Member

  #12
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa ana uhakika gani kuwa huo sio muendelezo wa kummaliza ambao ulishanza?
   
 13. J

  John10 JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Akiwa Neutral, bila ya kukimaliza CCM_FreeMason. Sasa hivi utaona hawa jamaa CCM-FreeMason watakapoanza kuwamaliza waandishi wa habari.

  CCM-FreeMason kazi yao kubwa ni Kuifilisi na kuibia Nchi. Hela zote zinasafirishwa nje ya nchi.
  Kila mwaka tunapata kiongozi ambaye anaanza vizuri kupingana na CCM-FreeMason, lakini ghafla utasikia huyo mtu kabadilika kawa Neutral, au hayupo duniani. Hawa jamaa ni hatari sana kwa nchi.
   
 14. c

  chama JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2010
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hujamaliza kumpa ushauri ahame CCM aende chama gani unachoona kitamfaa, lingekuwa jambo la busara kama ungempa ushauri wa kina kumbuka Sitta ni mtu mzima ambaye amekuwa kwenye medani ya siasa kwa miongo mingi, vita dhidi ya mafiadi si vya Sitta peke yake ni vya watanzania wote.
   
 15. mgen

  mgen JF Bronze Member

  #15
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 13,941
  Likes Received: 1,391
  Trophy Points: 280
  usijali mwanangu mbwa kala mwanaye alishika mpini wa kuleta mabadiliko makubwa TZ lakini he bowed down shauri yake historia itasema
   
 16. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,301
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Binafsi naona pale ndio saizi yake. Watu wanaona hiyo kama si wizara nyeti, lakini mimi naiona ni nyeti kweli kweli. Inahitaji mtu makini na jasiri wa kutetea maslahi nchi kwenye jumuia hiyo. Sitta ni kichwa na ana misimamo. Jamani naomba maoni yenu
   
 17. k

  kibenya JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 373
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  6 Amefutwa machozi lakini macho yake bado mekundu wizara aliyopewa haimrudishii heshima aliyokua nayo kwa kulinda heshima yake angekataa hiyo post
   
 18. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 23,993
  Likes Received: 2,717
  Trophy Points: 280
  hivi kabla hawajatangazwa.....huwa wanaambiwa kwanza?...
   
 19. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Masikiinnnnnnnnnnnnnniiiiiiiiiiiiiiii sitaaaaaaa
   
 20. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #20
  Nov 24, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  CCM wamempa hiyo kwa sababu wananchi wengi sana watakuwa wanalalamikia EAC by 2015 maana tutakuwa tumenyonywa kishenzi na kenya na Uganda sasa wamempa ili watu wamuone hafai katika jamii maana hiyo wizara itakuwa na lawama kinoma baada ya wakenya kuchukua ajira na ardhi sehemu kibao.

  Wakati Kamara ndo kasaini mikataba yote ya EAC yeye anakwenda kutekeleza, kama ni mimi nafumua upya maovu yote ya Kamara

  Peoples power
   
Loading...