Elections 2010 Sitta kujitoa CCM na kujiunga CHADEMA?

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Kuna tetesi kutoka kwa washkaji kutoka kanda ya kati kuwa kitendo cha 6 kuchakachuliwa uspika kimemuuma sana, habari zinasema kuwa anadai kuwa alichokuwa ameambiwa na EL kuwa hatakuwa Spika wa bunge la 10 limetimia.
Source hizo zinadai kuwa kwa sasa 6 yupo tayari kujiondoa chamani, na hatimaye uchaguzi wa jimbo la urambo kufanywa upya, ambapo yeye atagombea kupitia CHADEMA.
Kinachoendelea kule mjengoni ni kwamba 6 anampigia upatu Marando awe Spika wa bunge.
 
mh sidhani maana ninavyojua wanasiasa wengi hawana moyo huo TZ haswa ndani ya CCM! labda kule Kenya ambapo ni Raila tu anaweza unazi huo!
 
Kuna tetesi kutoka kwa washkaji kutoka kanda ya kati kuwa kitendo cha 6 kuchakachuliwa uspika kimemuuma sana, habari zinasema kuwa anadai kuwa alichokuwa ameambiwa na EL kuwa hatakuwa Spika wa bunge la 10 limetimia.
Source hizo zinadai kuwa kwa sasa 6 yupo tayari kujiondoa chamani, na hatimaye uchaguzi wa jimbo la urambo kufanywa upya, ambapo yeye atagombea kupitia CHADEMA.
Kinachoendelea kule mjengoni ni kwamba 6 anampigia upatu Marando awe Spika wa bunge.

If Mr Six can dare to do so will be our politician of the century in Tanzania. I would love to see something like that happens. But with the way we have been brought up (all Tanzanians with our soft hearts) that will never happen.

Anyway I stay connected.

Njimba.
 
Hana ubavu huo, si walitaka kumnyan'ganya kadi akawalamba miguu.Na yeye alilitumia bunge kupata umaarufu, hizo ndio cost zake, wajanja wenzake wamemuwahi, asubiri huruma za JK kwenye uteuzi
 
Natamani sasa itokee japo ni vigumu kutokea kwa mbunge kufanya jambo la uzalendo badala ya kung'ang'ania maslahi. Hizi ni tetesi ambazo zinaweza kuwa kweli ama la!!
 
Kwenye nafasi za uteuzi sidhani kama anaweza kuwa jasiri kama alivyokuwa spika. Akinyanyua mdomo kibano atakachopata bora mbwa mwizi!!! Nafuu kwake nikujiondoa chamani, japo ni ngumu, ni heri Ngamia kupenya katika tundu la Sindano kuliko Sitta kuuachia ulaji wa jimbo.
 
Natamani sasa itokee japo ni vigumu kutokea kwa mbunge kufanya jambo la uzalendo badala ya kung'ang'ania maslahi. Hizi ni tetesi ambazo zinaweza kuwa kweli ama la!!
idea yako kama umekuwepo kwenye serikali ya moyo wangu
 
Yote uliongea hayana mwelekeo lakini hili ni kweli na hayuko pekee yake.......

Kinachoendelea kule mjengoni ni kwamba 6 anampigia upatu Marando awe Spika wa bunge.
 
Kwa kufuata falsfa ya kuwa "ikiwa huwezi kushindana nao, ungana nao", mimi naona bado ni mapema kwa 6 kuihama CCM, atakuwa na faida kubwa zaidi kwa upinzani ikiwa ataendelea kuwa mpinzani ndani ya chama chake. Hilo litawauma CCM, na kwa kuwa ni wajukuu wa "haambiliki", watamtoa, na hilo litauthibitishia umma kuwa ama kweli CCM ina wenyewe (mafisadi). Sasa hapo ndio atoke na kugongomelea msumari mwa mwisho katika jeneza la CCM. Unadhani atatoka peke yake? La, hapana, ataondoka na wale wote walio na uchungu na nchi hii.
 
Kuna tetesi kutoka kwa washkaji kutoka kanda ya kati kuwa kitendo cha 6 kuchakachuliwa uspika kimemuuma sana, habari zinasema kuwa anadai kuwa alichokuwa ameambiwa na EL kuwa hatakuwa Spika wa bunge la 10 limetimia.
Source hizo zinadai kuwa kwa sasa 6 yupo tayari kujiondoa chamani, na hatimaye uchaguzi wa jimbo la urambo kufanywa upya, ambapo yeye atagombea kupitia CHADEMA.
Kinachoendelea kule mjengoni ni kwamba 6 anampigia upatu Marando awe Spika wa bunge.
Kama magazeti ya kibongo ukisoma kwa pupa umeliwa....
 
Hawezi kuhama kwa sababu ya kuukosa uspika,vinginevyo atajishusha hadhi,kwamba ni mroho wa madaraka.
 
Nakumbuka Hekaya za Abunuwasi!

kicheko.jpeg
 
Hawezi kuhama kwa sababu ya kuukosa uspika,vinginevyo atajishusha hadhi,kwamba ni mroho wa madaraka.
Nina habari kuwa jana aliitwa Ikulu Dodoma akakataa kwenda na vilevile leo hakushiriki katika kikao cha wabunge wa CCM kumchagua mgombea wa CCM. Kazi ipo.
 
Back
Top Bottom