Sitta: Kuilipa Downs ni kuhujumu uchumi

Kisendi

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
699
178
WAZIRI mpya wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri, amesema hatua yoyote ya kulipa fidia ya Sh 185 bilioni kwa kampuni ya Dowans, ni kuhujumu uchumi wa nchi.

Sitta, ambaye aliongoza Bunge la Tisa lililotikisa nchi kwa kuibua kashfa za ufisadi, pia amesema kuna kila dalili za genge linalohujumu nchi kuandaa mpango wa kutafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.

Sitta alikuwa akitoa maoni yake baada ya kuulizwa na Mwananchi kuhusu hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuhishi wa Kibiashara (ICC) iliyolitaka Shirika la Umeme (Tanesco) kuilipa Dowans Sh185 bilioni kutokana na kuvunja mkataba bila ya kufuata taratibu.

Tanesco ilivunja mkataba huo wa kuzalisha umeme mwaka 2008, ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya kuisha, ikieleza kuwa mkataba huo ulikiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma. Tanesco imesema itazungumzia suala hilo baada ya hukumu hiyo kusajiliwa nchini.

Hukumu hiyo imeamsha mjadala mkubwa uliokuwa umepoa kuhusu kampuni ya Dowans ambayo ilirithi mkataba uliobainika kuwa wa kifisadi wa Richmond Development LLC ambayo ilitakiwa izalishe umeme wa dharura wakati kulipotokea tatizo kubwa la umeme mwaka 2006.
Jana Sitta alizidi kuukoleza mjadala huo aliposema: "Kuna kila dalili ya genge la watu wenye fedha chafu kujaribu kuandaa mpango wa kuihujumu nchi."
"Hakuna uhalali wowote wa kuilipa Dowans kiasi hicho cha fedha, si haki hata kidogo.
"Kuilipa Dowans Sh185 bilioni ni kuhujumu uchumi wa nchi, na kuna kila dalili ni genge lilelile ambalo sasa linatafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi wa 2015."
Sitta, ambaye aliweka bayana dhamira yake ya kuendelea kupambana na ufisadi mara baada ya kuapishwa kuwa waziri, aliendelea kusema: "Ni genge ambalo halina huruma na nchi na umasikini wa Watanzania... na kama likiachwa lijiimarishe, Watanzania wasubiri matatizo makubwa zaidi huko mbele.
"Genge hili limekuwa likiwafanya Watanzania kuwa ni wajinga wasioweza kufikiri. Ni kwa sababu limeshika nchi, linafikiri siku zote litafanya mambo ya hovyo na kuangaliwa... sijui linawatafuta nini Watanzania wazalendo?"
Mbunge huyo wa Urambo Mashariki ambaye wakati akiwa spika Bunge lilijadili kwa kina kashfa ya Richmond iliyokuwa na matokeo ya kihistoria baada ya Edward Lowassa kulazimika kuachia uwaziri mkuu na kufuatiwa na mawaziri wengine wawili, alisema kinachofanyika sasa ni genge hilo kujiandalia mazingira ya kujikusanyia mabilioni ya fedha chafu za uchaguzi wa 2015.
Pamoja na Tanesco kuvunja mkataba na Dowans mwaka 2008, shirika hilo la umma liliibuka na mapendekezo ya kununua genereta za kampuni hiyo zinazoendeshwa kwa gesi, mapendekezo ambayo Bunge la Sitta liliyakataa kwa maelezo kuwa yanakiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma.
Msimamo huo wa Bunge ulimfanya mkurugenzi wa zamani wa Tanesco, Dk Idris Rashid kukubali kwa shingo upande akilaumu wanasiasa kwa kukwamisha masuala ya kitaalamu na kunawa mikono kwamba asilaumiwe kwa matatizo ya baadaye ya umeme.


Wakati nchi ikiwa imeingia kwenye tatizo jingine kubwa la umeme linalokaribiana na la mwaka 2006, ICC ilitoa hukumu ambayo imeamsha mjadala huo na Sitta alisema jana kuwa Tanesco isilaumiwe kwa uamuzi huo akielekeza lawama zake kwa genge hilo ambalo hakutaja walio ndani.
"Nitashiriki kikamilifu kuhakikisha maslahi ya taifa yanalindwa na hakuna mianya yoyote ambayo genge hili inaweza kuitumia kuhujumu nchi," alisema Sitta, ambaye ni mmoja wa wanasiasa wazoefu walio kwenye baraza jipya la mawaziri.


"Hili nataka uninukuu vizuri, kwamba sasa ni dhahiri kuna mkono wa ambao kila dalili unaonyesha ni genge linalotaka kufanya hujuma. Linachotaka kufanya ni mchezo mchafu ambao sisi serikalini tutajitahidi kuuzuia."
Alifafanua kwamba watu hawapaswi kuitwisha mzigo Tanesco kwani uamuzi uliangal;ia kwa kina maslahi ya taifa kuliko baadhi wanavyojaribu kupotosha.


Sitta alisema huu ni wakati wa kuhakikisha genge hilo halifanyi hujuma zake kwa nchi.
Sitta pia alidai kuwa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi nchini wamekuwa wakikwepa kufungua kesi zao kwenye mahakama za ndani kwa hofu ya kuumbuka.
Dowans ilifungua kesi hiyo kwenye mahakama hiyo ya ICC ambayo makao yake makuu yako Paris, Ufaransa.
Source: Mwananchi
 
Watanzania sasa tumechoka, Uchaguzi umeisha umeme sasa mgawo, wafanyabiashara wote wanauza jenereta zao sasa. Kurudisha hela zao, Pia watz tumepewe nini au huu mwenge??? MBONA TUNAUMIA SANA, SASA MAFUTA YUPO JUU, GAS JUU, KILA KITU SHIDA TU, MIFOLENI MAJI MGAWO?? DUHHHHHHHHHHhhh, Hawa watu mbona wanatuyumbisha sana TZ??
 
Hivi kwa nini kila baada ya uchaguzi mkuu kwa mfano 2005 na 2010 tatizo la mgawo wa umeme linatokea,hapa pana jambo si bure?
 
Kweli, Nyuki dume. Huu mgawo kuna jambo, NGELEJA ANATUCHEKEA TU kuwa mgawo utakuwa historia wakati unashika kasi kila kukicha. Mvua zikinyesha maji yanapotea, me maoni yangu hakuna haja ya kuwa na waziri wa nishati maana sioni kama kweli anahtajika, Dr Magufuli apewe na nishati nini??
 
Katika jambno ambalo Sitta unatakiwa kutobwatuka ni hili. Wewe ulikuwa mmoja wa wanaojua hukumu hii kuwa itatokea na hata wakati kesi zinazsikilizwa na kutolewa rufaa mbalimbali. Hii ni ya nne, na kipindi chote hicho ukiwa bungeni hukusema kuwa serikali imeshashindwa mara tatu na ungeweza kuwatumia makamanda wako, lakini kwa kuwa ulikuwa na nia ya kusaka urais na kisha uspika na ulipobwagwa ukaanza kulalama kutaka serikali iendelee kukulipia nyumbna unayoishi na wala hukuzungumzia suala hili. Kwa kuwa Sitta na wewe ni sawa na hao unaowataja kuwa mnahujumu uchumi wetu sasa kwa kukufundisha tu kaa kimya sisi na CDM tutakapochukua nchi tutarejesha hadi kombo la mwisho
 
Mzee wangu Sitta hapo mm binafsi naona umekurupuka,
wakati tunalipa 152mil. za richmond mbona ulikuwa kimya????
au kwa sbb za kunyimwa kale kacheo ndo unamalizia hasira zako kwa hili?
Kwa kweli hii nchi ni kama tunaongozwa na wenda wazi mu.........
 
Katika jambno ambalo Sitta unatakiwa kutobwatuka ni hili. Wewe ulikuwa mmoja wa wanaojua hukumu hii kuwa itatokea na hata wakati kesi zinazsikilizwa na kutolewa rufaa mbalimbali. Hii ni ya nne, na kipindi chote hicho ukiwa bungeni hukusema kuwa serikali imeshashindwa mara tatu na ungeweza kuwatumia makamanda wako, lakini kwa kuwa ulikuwa na nia ya kusaka urais na kisha uspika na ulipobwagwa ukaanza kulalama kutaka serikali iendelee kukulipia nyumbna unayoishi na wala hukuzungumzia suala hili. Kwa kuwa Sitta na wewe ni sawa na hao unaowataja kuwa mnahujumu uchumi wetu sasa kwa kukufundisha tu kaa kimya sisi na CDM tutakapochukua nchi tutarejesha hadi kombo la mwisho

hili nalo neno, namshangaa huyu huyu mzee anavyotofautiana na wazee wenzie kama akina bomani ambao wanakiri kuwa hili ni swala la kuangalia kwa makini. Inasikitisha kuona kuwa mhe. Sita ambaye ndiye alikuwa mwenyeji wa richmond wakati akiwa kituo cha uwekezaji anajadiri mambo ya kisheria kisiasa. Kwa kweli huyu mzee ni mptpshaji as if anatafuta sympathy ya wananchi na wakati huohuo wananchi wawachukie watu furani. Kama yeye ni royal citizen na kwa kuwa yeye ni lawyer aende akakate rufaa ili atetee maslahi ya taifa.
 
Hivi tunakwenda kumlipa nani?? to my understanding hakuna mtazania aliyejitokeza na kusema adharani kwamba yeye ndo mweye Downs !!! na je kwenye hiyo ICC TANESCO alisimama na nani, maana nafikiri ni vyema tukajua je tunawalipa watanzania wenzetu au watu wa sampli gani? Isitoshe sinema ilochezwa tangu Richmond mpaka leo serikali haiwajui wamiliki?? watawala na watu wanaokula nao wafike mahali waone aibu !! wajue itafika sehemu watu hawatavumilia, huu ujinga maana hiyo hela TANESCO ataipata wapi kama siyo kutupandishia ankra za umeme watanzania wanyonge na maskini!! haya mambo yatabackfire wasichojua watawala wanokula na hawa wahuni ni kwamba huyo Don wa genge lao akiona sasa ametosheka atachukua passport ya TZ ataitupa ****** na atachukua ile ya Iran atati mkononi huyo anaondoka zake , sasa ninyi wenzetu mtakimbilia wapi ?? Jamani na kusoma historia zote hizo watu hawajui kwamba falme za kidharimu kuna siku zinadondoshwa kutoka madarakani au mnafikiri TZ ni kisiwa, na zikidondoshwa watu kwa hasira hawabakizi hata mtoto mchanga anayekuwa ananyonya , mtende lakini muwe na woga mjue hamtakaa milele wacha kuwatia vidole vya macho watanzania tena vidole vyenyewe mnavipaka pilipili kwanza!!
Mungu Ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom