Sitta: Hakuna wa kunifunga mdomo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Hakuna wa kunifunga mdomo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohammed Shossi, Jan 20, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Wednesday, 19 January 2011 21:53 0diggsdigg

  Ramadhan Semtawa
  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amekoleza moto wa sakata la kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans, akisema kamwe hawezi kufungwa mdomo kupinga malipo ya Sh94 bilioni kwa kampuni hiyo.Kauli ya Sitta imekuwa wakati kukiwa na taarifa kwamba waziri huyo pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe wamebanwa na Ikulu wakitakiwa wasizungumzie tena suala hilo.

  Hata hivyo, akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana Sitta alisema, "Naomba wananchi wafahamu, siwezi kufungwa mdomo kuhusu kupinga malipo kwa kampuni ya kitapeli ya Dowans."

  Sitta ambaye msimamo wake umeibua mjadala mzito nchini na hata ndani ya baraza la mawaziri, alisema hajawahi kutishwa wala kufungwa mdomo kuhusu msimamo wake.

  Kauli hiyo ya Sitta imekuja siku moja tangu gazeti moja la kila siku (siyo Mwananchi) kuripoti kwamba Rais Jakaya Kikwete amemfunga mdomo, uamuzi uliodaiwa kufikiwa juzi katika kikao cha Baraza la Mawaziri, kilichofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.

  Habari hizo zilidai kuwa Sitta na Dk Mwakyembe walikuwa na wakati mgumu kutetea hoja ya kutaka Serikali isiilipe Dowans na kwamba hata Rais alisema hafurahishwi na hukumu ya malipo hayo, hivyo kikao hicho kuwaamuru mawaziri hao kutozungumzia tena suala hilo hadharani.

  Lakini jana Sitta alisema: "Nitaendelea kupinga malipo ya Dowans. Sijawahi kuitwa popote wala na mtu yeyote na kuambiwa nisizungumze suala hilo, hivyo wananchi wasifikiri nimebadili msimamo".

  Aliongeza: "Taarifa zinazosambaa ni za kupikwa tu, zisije zikawapotosha wananchi wakidhani nimewasaliti katika hili, narudia tena sijafungwa mdomo."

  Mbunge huyo wa Urambo Mashariki ambaye aliliongoza Bunge la Tisa katika vita dhidi ya ufisadi, alifafanua kwamba si suala la Dowans tu bali ataendelea kupinga mambo yote machafu kuhusu nchi.

  Aliweka bayana kwamba nchi inahitaji viongozi wenye uwezo wa kusimamia vema maslahi ya taifa bila hofu ili kulinda haki za wananchi na kuboresha maisha yao.

  Sitta alinukuliwa akihoji kile kinachoitwa kukiuka dhana ya uwajibakaji wa pamoja na kuweka bayana, kama dhana hiyo ingekuwa inaheshimika basi uamuzi wa kuilipa au kutoilipa Dowans ungefanywa kwa pamoja.

  Alisema haiwezekani dhana ya uwajibikaji wa pamoja ifanyike bila kushirikisha wengine halafu mwisho itolewe taarifa ya uwajibakaji wa pamoja.

  "Halafu kuna watu wanazungumzia nimekiuka dhana ya uwajibikaji wa pamoja, uwajibikaji wa pamoja ni lazima uamuzi ushirikishe wengine si mmoja kuamua halafu ifahamike ni uwajibakaji wa pamoja," aliongeza.

  Sitta pia amekuwa akihoji kasi ya malipo hayo kwa kampuni ya Dowans wakati nchi ina madeni mengine kama ya Benki ya Dunia na IMF, lakini bado hayajalipwa kwa kasi kama hiyo.

  "Lakini, hii haraka ya kuilipa Dowans ni ya nini? Nchi hii ina madeni ya muda mrefu kama yale ya Benki ya Dunia na IMF, lakini hakuna uharaka wa kulipa kama huu sasa kasi hii inatoka wapi?" alihoji.

  Alisema nchi ina matatizo mengi ikiwemo ya kiuchumi, hivyo haingii akilini kuona Watanzania wanalipa kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa kampuni ya kitapeli.

  Tayari msimamo wa Sitta ulimfanya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, kutoa vitisho kwa mawaziri wenzake akiwataka wakae kimya na kuacha kuzungumzia sakata hilo vinginevyo wajiondoe kwenye Serikali.

  Hata hivyo, wakosoaji wamemwelezea Chikawe kama ambaye pia amekiuka taratibu kutokana na kuzungumza suala hilo kwenye vyombo vya habari, badala ya taratibu za kiserikali.

  Tangu Mahakama ya Usuluhishi ya Biashara ya kimataifa (ICC Court) kutoa hukumu ya mwezi Novemba, ikitaka Tanesco ilipe Dowans, Sitta alikuwa waziri wa kwanza kupinga malipo hayo hadharani.

  Hata hivyo, pamoja na Sitta kupinga, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema alikwisha kusema bayana kwamba Serikali haiwezi kukata rufani katika sakata hilo, lazima ilipe faini hiyo.
   
 2. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,161
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Good go ahead, wewe ni mpambanaji japo watu tunaweza kukutafsri tujuavyo. Lakini fanya sehemu yako na wakiendelea jiuzulu uwaachie serikali yao ya kisanii. Endelea tu kaka Samweli

  Hawa jamaa wanacheza na maneno kukidhi haja zao, Kule Arusha walisema Intelijensia, sasa wanakuja na "Uwajibikaji wa pamoja" wakati ni uamuzi wa Jakaya, Fredrick na William pekee. Uwajibikaji wa pamoja unatoka wapi kwenye madudu kama haya ya Dowans. Hakika Samweli na Harison msikubali maana ninyi mnaijua vema Dowans kutoka A mpaka Z na ndio maana hata Edward aliamua kuachia ngazi na Jakaya akakubali kwa kuziba nafasi hiyo kwa uteuzi wa Mizengo
   
 3. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Napingana na hapo kwenye bold nyekundu mkuu, wanajf wengi wanaamini kuwa watu kama Samwel Sitta, Harrison Mwakyembe and company wapo in a wrong place "ccm" kwakuwa wapo against CCM mnapokuwa jumuia kubwa mfano wa chama sio wote watakao kuwa na muono mmoja kila mtu anamtazamo wake nadhani hata hapa JF tunashuhudia Zitto akisakamwa kwa kuwa na maono tofauti na kina Slaa na watu wanapendekeza ahame chama eti kwa kuwa mawazo yake ni tofauti na wengine ndani ya chama na kusahau dhana ya "demokrasia" Elimu ya urai bado sana miongoni mwa jamii ya kitanzania.
   
 4. Don Alaba

  Don Alaba Senior Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 158
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  DSC01394.JPG
  Ukweli mtupu!!!!!!!!!!!!
   
 5. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ila nadhani mzee 6 kuna kitu anakitafuta kutoka kwa jk,kama si kufukuzwa uwaziri,basi kuna kitu kingine,maaana kakomaaa kweli kweli kuwa hato badili msimamo wake wa kupinga dowans,na gazeti la RA rai wameaanza kazi waliyo ambiwa na boss wao(RA)kuwa ripoti ya mwakyembe nanukuu"yadhibitika ripoti ya mwakyembe ilijaa maelezo mengi ya hadaa"mwisho wa kunukuu.kuan mchezo mchafu unafanywa sasa hivi ili kuweza kuwachafua 6 na mwakyembe.
   
 6. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #6
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Wadau wa siasa wakubali wakatae hakuna wakati ambao kumekuwa na uhuru wa kutoa maoni kama wakati wa Jakaya,
   
 7. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #7
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Msisahau haya magazeti yapo kibiashara kwahiyo lazima wakati mwingine waandishi wawe innovative ili kuatract hadhira.
   
 8. coby

  coby JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Na ndio maana jana wamemchokoza leo kayatoa tuliyokua tunayataka. Lengo TZ daima jana lilikua kujua mzee 6 bado ana uleule msimamo au keshachakachuliwa. Thanx 6 kwa kuendelea kukomalia hii ishu
   
 9. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mr. 6, tuko pamoja na usikubali kufungwa mdomo! Waambie pia wapambanaji wenzako-hakuna kufungwa mdomo mpaka tujue fedha za dowans analipwa nani na kwa nini???????hapo ndo tutakuwa na uwajibikaji wa sote (pamoja) yaani serikali na wananchi-siyo chikawe na mawaziri wake.
   
 10. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Pambana mzee 6, umma upo nyuma yako.
   
 11. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tanzania daima wameanza kutumika kutoa habari za ajabu.
   
 12. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mzee Six tuko pamoja nawe. Achana na hao wadhalimu, njoo kwetu sisi wana wa nchi tukupe kazi kubwa zaidi.
   
Loading...