Sitta: Elimu na Afya bure inawezekana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Elimu na Afya bure inawezekana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Sep 1, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Saturday, 01 September 2012 09:03

  Edwin Mjwahuzi, Kagera
  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema Serikali kutoa huduma ya Elimu na Afya bure inawezekana ikiwa tu mianya ya rushwa na ufisadi itadhibitiwa ipasavyo na wananchi wataweza kunufaika na rasilimali zilizopo nchini.

  Sitta alisema ni lazima turudi kwenye misingi ya uadilifu, kujali wanyonge, kukataa rushwa na kukataa ufisadi wa aina yoyote ndipo tutaweza kukusanya na kuinua uchumi wa kutosha na kulipana mishahara mizuri, kumlipa pensheni mzee na kutoa huduma hizo bure.

  Aliyasema hayo alipokaribishwa katika mkutano wa akinamama wajane kutoka wilayani Karagwe na Kyelwa mkoani Kagera na kuwashirikisha wazee wa Wilaya hizo uliofanyika katika ukumbi uliopo katika ofisi za CCM wilayani Karagwe.

  Sitta alisema itakuwa ndoto za kupata huduma hizo bure kama nchi haitafanikiwa kuziba mianya yote ya rushwa na wananchi wataendelea kupiga kelele wakitaka kupatiwa huduma hizo bila ya mafanikio.

  “Ningependa kuwaambia wananchi, najua karibu wote tunataka utoaji wa huduma ya afya, elimu ya kuanzi msingi mpaka elimu ya juu kuwa bure, ndugu zangu katika hali ambayo hata huduma ya afya ya kawaida haipatikani ni mtihani mkubwa kwa kutoa elimu ya bure,” alisema.

  Aliongeza, “Hatuwezi kuwa na nchi ina kila kitu, tunayo makaa ya mawe, maziwa, mito, bahari, madini, gesi, mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjaro na tuna hekta za kilimo zaidi ya milioni 88, tunataka Watanzania muamke na muache kushabikia rushwa ndogo ndogo tuingie katika utamaduni unaotuwezesha kujenga heshima ya nchi yetu kwa kujali uongozi ulionyooka na wenye uhadilifu.”

  Sitta alisema wananchi wasiwe na ndoto ya maisha bora kwa kila mtanzania ikiwa rushwa na ufisadi utaendelea kutawala na kufumbiwa macho.

  "Ndugu zangu hatuwezi kupata maisha bora kama kiwango cha rushwa, ufisadi na dhuluma kikiwa hivi hivi tunavyokiona hivi sasa, kwa sababu Serikali ilileta utoaji pembejeo kwa kutumia vocha sasa tutaendelea vipi kama vocha zenyewe zinachakachuliwa?" alihoji.

  “Iwapo tutadhibiti mianya ya ufisadi na rushwa, nchi yetu itainuka na kuweza kuwasaidia wazee wetu, wajane, watoto yatima kwa kuwapatia huduma nyingi nzuri, ilimpadi tu ufisadi unatakiwa kupigwa vita kuanzia chini huku,” alisema Sitta.

  Sitta pia aliwaomba wajane hao na wazee kupita kila mahali na kuwashaui wananchi wao wakiwemo na wana CCM kuwa makini wa watu wanaojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa na kiserikali wasije wakafanya makosa kuwaweka watu wenye nia mbaya na nchi hii kwa kujali matumbo yao na familia zao.

  “Sasa hivi hata kule bungeni mnaona baadhi ya mawaziri, anatokea mtu amekuwa waziri ndani ya miaka 2 au chini ya hapo unasikia kanunua nyumba Mikocheni ya mabilioni, haiwezekani na wala haingii akilini hakuwa waziri wa wananchi huyu ameingia kuchuma tu,” alisema.

  Waziri Sitta amemaliza juzi ziara ya kiserikali ya siku tano mkoani humo alipokuwa akiangalia miradi mbalimbali inayohusiana na muingiliano wa uchumi na kijamii kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
   
 2. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mbona kwenye kampeni za 2010 urambo hakuyasema.Hakuna mwanaCCM yeyote anayeaminika kwa sasa.kazi yao kudandia ajenda za wapinzani tu.aende zake
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  If I remember correctly, wakati wa campaign 2010 Sitta alikebehi ahadi ya CHADEMA ya kutoa elimu bure akidai kuwa haiwezekani. Sasa 3 years later anafanya u-turn! Kwa nini huyu mzee anabadilika kila kukicha?
   
 4. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Swala siyo kusema kana inawezekana au haiwezekani, kinachohitajika ni kuonyesha kwa vitendo jinsi inavyowezekana.
   
 5. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,784
  Likes Received: 6,115
  Trophy Points: 280
  Huwa hawa magamba wananishangaza sana. Yeye ni WAZIRI KAMILI anayeingia ndani ya Baraza la Mawaziri (BLM) ambalo Mwenyekiti wa vikao hivyo ni Rais, Amiri Jeshi Mkuu, na Mwajiri namba moja Tanzania. Sasa hayo mambo badala ya kwenda kuyalalamikia huko Kagera kwani asiyazungumze ndani ya BLM ambalo ndicho chombo cha juu na cha mwisho cha kumshauri Rais na kufanya implementation mara moja?

  Hebu aache unafiki na stori zake zisizo na mashiko, asitake kutafuta umaarufu kupitia sera za wapinzani. Huyu mzee kimsingi huwa haeleweki msimamo wake; anataka nini na hataki nini.
   
 6. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Mnafiki sana huyu mzee. Tena Mnafiki sana huyu.
   
 7. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,784
  Likes Received: 6,115
  Trophy Points: 280
  Yaani huyu ni wa kuogopa kama ukoma. Mwanasiasa thabiti lazima awe na hoja za kuzisimamia na hata ikibidi kuzifia na sio hawa wasoma upepo na wezi wa sera mradi kulinda matumbo yao. Hili zee ni linafiki halina mfano. Mara mia afadhali fisadi papa mwenye msimamo unaoeleweka (hata kama ni wa kifisadi kwani jamii itajua namna ya 'kudili' naye) kuliko anayejidai msafi ilhali hana msimamo.
   
 8. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  aisee huyu jamaa ni bonge la mnafki kupindukia, waliposema wapinzania mambo haya alikebei, sasa akisema yeye, inawezekana! kwa kuwa yeye ni nani? jamaa simzimikii kabisa. nawapa pole waliyo poteza muda wao kusikiliza pumba za huyu mnafki
   
 9. Eliza wa Tegeta

  Eliza wa Tegeta JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu bwana ni problem iliyokamilika, a complete set odf problems.
   
 10. Eliza wa Tegeta

  Eliza wa Tegeta JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu bwana ni problem iliyokamilika, a complete set of problems.
   
 11. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  kama inawezekana aanze na kwao Urambo nadhani kikwente ataiga mfano kutoka kwake
   
 12. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Kumbuka kwamba wakati huo Makamba alikuwa amepiga marufuku wagombea wa CCM kushiriki midahalo lakini Sitta akaomba apewe mdahalo na Dr. Slaa awaumbue CHADEMA na sera yao ya elimu bure. Kumbuka Sitta alitumia maneno kwamba Dr. Slaa ni saizi yangu.

  Mwambieni JF ni database ya kila analotamka humu nchini.
   
 13. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Kumbuka kwamba wakati huo Makamba alikuwa amepiga marufuku wagombea wa CCM kushiriki midahalo lakini Sitta akaomba apewe mdahalo na Dr. Slaa awaumbue CHADEMA na sera yao ya elimu bure. Kumbuka Sitta alitumia maneno kwamba Dr. Slaa ni saizi yangu.

  Mwambieni JF ni database ya kila linalotamkwa humu nchini.
   
 14. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,784
  Likes Received: 6,115
  Trophy Points: 280
  Eliza umenena vizuri sana. Yaani huyu ni "complete package" ya matatizo; humo humo kuna unafiki, uongo, kutojiamini, umamluki, kukosa msimamo, makundi, viufisadi, jizi la sera, huku akijidai kuwa upande wa wanyonge. Yaani hii package iko full.
   
 15. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0

  kwani hilo ndio amelijua leo?
   
 16. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,784
  Likes Received: 6,115
  Trophy Points: 280

  Ha ha ha ha ha! Halafu leo anarudia matapishi yale yale! Watanzania tuwe makini sana na huyu mtu anayeitwa Sitta. By far better Anne mwenye msimamo unaoeleweka kuliko huyu jamaa asiyeeleweka.
   
 17. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu FJM, sijawahi kuamini kauli na matendo ya Sitta tangu akiwa Spika na hata sasa akiwa Waziri.
   
 18. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Ni zaidi ya mnafiki ni serikali gani anayoongelea na amekuwa kwenye hiyo serikali kwa muda gani?
   
 19. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Naweza kusema bila shaka kwamba, inawezekana kwa sasa akawa ndio mtu mnafiki katika ukanda huu wa maziwa makuu kwa watu wote wenye umri kama wake.
  One upon a time I had alot of expectations out of him, kumbe it was empty expectation.
   
 20. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr. Slaa amemuweka vizuri kabisa kuwa huyu ni mnafiki. Naacha kumsikiliza. kumbe ndo maana hata JK alimuita mpinzani alipoongea na JB
   
Loading...