Sitta: DOWANS iliirithi Richmond isiyotambuliwa kisheria; Aapa kamwe hatakubali serikali kuilipa!

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779
[h=3]
[/h]

*Aapa kamwe hatakubali serikali kuilipa Dowans
*Asema iliirithi Richmond isiyotambuliwa kisheria
*Wanaharakati watangaza siku 10 za maandamano
*Yaelezwa TANESCO kukata rufaa changa la macho

Na Waandishi Wetu

SIKU chache baada ya Mahakama Kuu kusajili tuzo ya malipo ya sh. bilioni 94 ambazo
Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) linapaswa kuilipa kampuni ya Dowans, Waziri wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Samuel Sitta amesema katu hawezi kukubaliana na malipo hayo kwa kampuni ambayo ni haramu nchini.

Bw. Sitta ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipinga serikali kuilipa kampuni hiyo, alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha Keki ya Taifa kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Mlimani, mada ikiwa ni miaka 50 ya maendeleo na changamoto ya uadilifu.

Alisema miongoni mwa sababu zinazomfanya kuonesha msimamo huo ni kwa sababu kampuni hiyo ni haramu kwa kuwa ilirithishwa mikoba na kampuni ya Richmond, ambayo haitambuliwi na Sheria ya Manunuzi nchini pamoja wala Mamla ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Akizungumzia kuwamo ndani ya serikali anayoikosoa, alisema, "Baadhi ya mambo tumeyaepusha yasijirudie kiuzembe kwa sababu tupo na tunayafuatilia kwa karibu, kama tusingekuwa serikalini na kuonesha misimamo yetu bila kujali tupo ndani kuna mambo yasingepata suluhisho, ndiyo maana wengine tunasema hakuna haja hata kidogo ya kuilipa hata senti moja kampuni haramu ya Dowans

Hivyo, tuvute subira kwa kuwa serikali ipo katika hatua ya kukata rufaa ya tuzo hiyo, mambo huenda yakawa mazuri na kama hayatakuwa mazuri tutafahamu la kufanya wakati huo," alisema Bw. Sitta.

Aliongeza kuwa jambo la kushangaza kampuni hiyo ya Dowans wakati ikiendelea kufuatilia tuzo hiyo, imeiuza mitambo yake kwa kampuni ya Symbion kwa gharama kubwa zaidi, na suala hilo haliwezi kufumbiwa macho akiwa miongoni mwa wanaharakati wanaopinga ulipaji wa fedha hizo.

"Dowans wameuza mitambo yao kwa kampuni ya kuzalisha umeme ya Symbion mara dufu zaidi, kiasi cha dola milioni 120, hivyo hatuwezi kuwafumbia macho watu waovu kwa kuwa ndani ya sheria zetu hamna sehemu inayoruhusu kuwepo kampuni haramu kama hii," alisema Bw. Sitta.

Alisema Richmond ni utaratibu wa kijanja na ndio maana hawakufuata taratibu zozote, na kwamba vigezo ambavyo waliviweka TANESCO vya mzabuni vilikuwa 24 lakini vilipunguzwa hadi kubakia vinne ili kuipitisha.

“Dowans ni biashara ya kipumbavu…nawashangaa hata hao wanaotulaumu sisi kuwa ndio tumeifikisha nchi katika hatua hiyo ya kutakiwa kulipa deni hilo, Dowans ni wizi na kila Mtanzania anapaswa kulaani ushenzi huo badala ya kushangilia,” alisema.

Alisema kuwa Tanzania iliingia mkataba na Kampuni ya Richmond ili ifue na kuzalisha umeme lakini cha ajabu humo humo kukafanyika wizi na mkataba huo hewa wakarithishwa Dowans.

"Dowans hatukuwapa mkataba bali walirithi uharamu wa kampuni hewa, hivyo hatuwezi kubebesha wananchi matatizo ya uharamu halafu tukashangilia kuibiwa,” alisema.

"Dowans ni wajanja, wamecheza mchezo katika makaratasi, kitu ambacho ukikaa chini na kukichunguza kwa makini utagundua kuwa tumelipa mamilioni ya fedha bila ya sababu za msingi," alisema.

Mabadiliko ndani ya CCM

Bw. Sitta alisema iwapo itafikia mahali na kugundua kwamba yale ambayo yanapangwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hususani kufanya mabadiliko ya haraka ili kuokoa jahazi, kwa upande wake atafanya maamuzi ambayo anaona ni sahihi kwa manufaa ya Watanzania.

"Tangu Oktoba 5, 1960 mimi nilikuwa mwanachama rasmi wa Chama cha TANU hadi kuwa CCM mwaka 1977, ninatambua mengi ambayo tulikuwa tunafanya enzi za TANU kwa sasa hayatekelezeki kwa manufaa ya Watanzania na ilifika mahali nikaanza kuandamwa sana, kutokana na misimamo yangu, ndiyo maana ikifika mahali nikiona hamna mabadiliko CCM, kwa upande wangu ninaweza kuchukua maamuzi.

"Ukizingatia kipindi hicho chote utagundua ndani ya chama nina zaidi ya miaka 50, hivyo wale wanaoona nijiuzulu madaraka, ikifikia hatua ya kufanya hivyo nitajuzulu lakini bado, ninatambua ndani ya CCM kuna watu wenye uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko iwapo tutafunga mikanda na kudhamiria kuwatetea Watanzania kisawa sawa," aliongeza.

Uchaguzi Igunga

Akitoa tathimini yake juu ya uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Igunga, alisema ushindi ambao CCM iliupata siyo jambo la kujivunia, bali inapaswa kujipanga sawa sawa kwa kuwa matokeo hayo yaliashiria taa ya njano.

"Kura zetu jimbo la Igunga si jambo la kujivunia hasa ukizingatia kwamba zaidi ya asilimia 55 ya kura ndiyo ushindi wetu huku CHADEMA kikichukua nafasi ya pili kwa zaidi ya asilimia 40, hiyo ni ishara ya taa ya njano ambayo inapaswa kufanyiwa kazi haraka na viongozi wa chama chetu kabla mambo hayajawa mengine," alisema.

Wanaharakati kuandamana

Msimamo wa Bw. Sitta unaungwa mkono na wanaharakati ambao wameamua kupinga malipo hayo barabarani, kwa watu kuandamana kwa amani
nchi nzima, na wamewataka Watanzania kutumia ibada za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili wiki hii kuomba ujasiri wa kutetea nchi yao.

Katika maandamano hayo, waandamanaji wametakiwa kutumia muda wa siku kumi kuvaa vitambaa vyeusi mikononi na bendera za taifa shingoni au kichwani, ikiwa ni ishara ya kutokukubaliana na ufisadi
unaofanyika nchini na kuishinikiza serikali kutolipa fedha hizo.

Wanaharakati hao wanadai kuwa hiyo ndiyo njia pekee ambayo Watanzania wanaopinga harufu ya ufisadi inayodaiwa kuzunguka sakata hilo, wamebakiwa nayo, kwani kwa mujibu wa mkataba wa kampuni tata ya Richmond na TANESCO, uliorithiwa na Dowans, hukumu
iliyotolewa na Mahakama Kuu mapema mwezi huu na kusajili tuzo hiyo, ilikuwa ndiyo fursa ya mwisho kwa utaratibu wa kimahakama.

Kifungu cha 14 cha hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) kinaeleza bayana namna pande hizo mbili zilivyokubaliana kuwa maamuzi ya msuluhishi huyo yatakuwa ni ya mwisho na yanapaswa kuheshimiwa na pande zote mbili, hivyo hakuna upande utaweza kukata rufaa mara baada ya mahakama kuu kutoa uamuzi wa kusajili tuzo hiyo.

Maandamano hayo yameitishwa nchi nzima Oktoba 14, ambayo huwa ni siku ya maombolezo ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye baada ya kufariki dunia alizikwa baada ya siku 10. Hivyo muda huo ndiyo utakaotumika kupinga Dowans na ufisadi mwingine wa mali za umma nchini.

Wanaharakati hao ni Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), HakiElimu, Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Agenda Participation 2000, SIKIKA Tanzania na HDT.

"Jambo hili limetusikitisha sana kwa kuwa serikali kama mlinzi wa rasilimali za umma ametusaliti au ameshirikiana na wezi kuiba au kutumia vibaya rasilimali za umma. Pia hali hii inaonesha dhahiri kuwa kuna viongozi wa serikali wanaonufaika na watakaogawana rasilimali hii. Tokea mwanzo umma haukushiriki katika kujua kuwa TANESCO imeshtakiwa kwa kuingia katika mikataba mibaya.

"Pia linadhihirisha kuwa serikali imedhamiria kulipa tuzo ya Dowans. Hii inatupa maswali maswali mengi; Je, Dowans ni nani mpaka serikali inamlinda hivyo? Je, malipo hayo analipwa nani? Na yanatoka katika kipengele kipi cha bajeti ya serikali? Ni hatua gani imechukuliwa dhidi ya waliotuingiza katika mkataba huu?" alihoji Bw. Irenei Kiria, Mkurugenzi Mtendaji wa SIKIKA alipokuwa akitoa tamko hilo kwa niaba ya wenzake.

"Tunatoa wito kwa Watanzania wote tuadhimishe kifo cha Baba wa Taifa, kwa kuvaa nguo nyeusi, siku ya maombolezo kuanzia Oktoba 14 hadi 23 alipozikwa, tukikumbuka msimamo wake wa kupinga ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za taifa...wananchi wote
ambao ndiyo walipa kodi ambao hawajapendezwa na mlolongo huu na ufisadi mwingine wajiandae, wawe na uthubutu na kujitokeza kwa wingi kusimamia haki zao," aliongeza Bw. Kiria.

"Uamuzi wa TANESCO kwenda mahakamani kukata rufaa ni danganya toto tu...tunapigwa changa la macho hapa walishakubaliana kuwa hawatashtakiana katika mahakama yoyote Tanzania na imeelezwa pia katika hukumu ya ICC kuwa hakuna upande utakata rufaa juu ya maamuzi hayo baada ya mahakama kuu kukubali tuzo. Kwa hiyo hapo tumefika mwisho hatutarajii uamuzi tofauti.

"Maamuzi sasa ni kwa wananchi. Katiba iko chini ya wananchi maana katika nchi za kidemokrasia wananchi ndiyo wanatunga katiba. Katiba inatasfiriwa katika sheria, sheria katika kanuni na kanuni katika miongozo mbalimbali. Kifungu cha 27 cha katiba yetu pamoja na ubovu wake, kinatoa mamlaka kwa wananchi kulinda rasilimali za nchi. Hivyo tunawaomba Watanzania kutumia wiki hiyo kupinga suala hili na ufisadi mwingine nchini," alisema Bw. Marcos Albany kutoka LHRC.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TAMWA, Bi. Ananilea Nkya alisema kuwa alisema kuwa yako makundi mbalimbali ya kijamii nchini yanaidai serikali, akitolea mifano ya walimu na wastaafu wa Afrika Mashariki, lakini serikali haijawahi kuonekana kuharakisha kuwalipa kama inavyofanyika kwa Dowans. Akaongeza kuwa Watanzania wanalodai kubwa la kuboreshewa maisha yao, lakini hawajawahi kutimiziwa na serikali.

Tanesco yakata rufaa

Wakati malipo ya Dowans yakipingwa kila kona, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupitia kwa mawakili mawake leo inatarajiwa kuwasilisha ombi la kukata rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaa kupinga uamuzi wa kuilipa sh. bilioni 94 kampuni ya kufufua umeme ya Dowans Tanzania.

Akizungumza kwa waandishi wa habari kwa njia ya simu, mmoja wa mawakili hao, Dkt. Hawa Sinare alisema kwa sasa wapo katika hatua za mwisho kukamilisha hati ya ombi hilo.

Septemba 28, mwaka huu Mahakama Kuu ilitoa uamuzi wa kusajiliwa kwa tuzo ya kampuni ya Dowas inayoitaka TANESCO kulipa mabilioni hayo ya fedha.

Uwamuzi huo ulitolewa mahakamani hapo na Jaji Emilian Mushi wa mahakama hiyo baada ya kusikiliza na kujilizisha na hoja za pande zote mbili na kuweka wazi kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kutengua makubaliano ya mkataba waliojiwekea kati ya Dowans na Tanesco.

Miongoni mwa makubaliano hayo ni kuwa masuala yote ya kisheria yatasuluhishwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na uamuzi utakaotolewa na mahakama hiyo utakuwa wa mwisho.

Habari hii imeandikwa na Godfrey Ismaily, Gladness Mbona, Stella Aron, Tumaini Makene na Rehema Mohamed.
 
mikatabafeki

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
12,790
4,621
hapa ni sawa na kufukuzana na uperpo tu mana mkulu ndo atoa agizo mahakama itoe hayo maamuzi
 
Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,615
Yote tisa, swali moja tu kwa Sitta -Mbona mmeitambua Symbion walirithi wengine wa mitambo ile ile yenye historia ya Richmond??
 
bigboi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
920
1,665
Jamani haya maandamano yanaanza lini! Tunaazia wapi ! Tunakutana wapi! Wengine tushapinda sasa hivi tushachoka huu mziki wa dowans sasa ni too much alafu kama noma na iwe noma poa tu kuishi bahati kufa lazima
 
Mbogela

JF-Expert Member
Jan 28, 2008
1,379
247
6 ni mchumia tumbo km walivyo magamba wote, katika maazimio 23 ya bunge lake ya richmond hakusimamia utekelezaji wa hata 1 kibaya zaidi aliposikia wanataka kuchukua kadi yao akavaa joho lenye bendera ya JMT akaongoza bunge kuyazika maazimio yot.
Leo atasemaje dowans wasilipwe? Akitaka tumuamini basi ajaribu kujitenga nao, aachie uwaziri awape kadi yao
 
Daniel Anderson

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
872
140
Do once. Do once.
Mlamba asali halambi kidole kimoja.
Wakalamba tena baada ya EPA kupitia KAGODA. Wakaongeza kwa kulamba dayaMOND ili wawe veri RICH.
Waliponogewa wakaamua kuongeza idadi ya vidole vyao kwenye buyu la asali.
Sasa wakasema DO ONCE more plz.
Imewapalia wakakohoa kwa nguvu mpaka WADANGANYIKA wakasikia.
Hawa walevi kugundua kibuyu chao kimefujwa na haya majizi machache wameamua kusambaa kuyasaka mezi haya porini, nyumbani, vijiweni na kwokote yatakapopatikana. Kaya hii haikaliki tena. Mpaka machumiatumbo yatakapofurushwa.
Hayata kula wala kunywa kwa moto wa wadanganyika wa siku 10 utakaoyachoma kweli kweli.
 
Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,127
Yote tisa, swali moja tu kwa Sitta -Mbona mmeitambua Symbion walirithi wengine wa mitambo ile ile yenye historia ya Richmond??

Mkandara ,

Unakijua kisa cha mbwa kuitwa Jibwa?? Ndio Dowans na Symbion, Sitta anapigia kelele Dowans (mbwa) lakini Symbion (Jibwa) wana matatizo kama ya Dowans ila kimya. Ndio maana mie huyu jamaa nishasema siku nyingi mnafiki na hizi kelele za kutaka achaguliwe urais 2015. Zungushaneni ila mjue Deni la Dowans linakuwa na ijapokuwa sifurahii kulipwa kwa kampuni ya kisanii katika dili hii ya kitapeli ila kwenye vifungu vya kisheria tushaumizwa na hivyo malipo yao ni halali. Tumalizane nao tuwageukie Symbion ambao hadi leo hatujaona umeme wao ijapokuwa tunawalipa mamilioni kwa siku. Kweli watanzania sisi aliyetuloga kafa!!!!
 
mzee wa njaa

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
1,366
222
Nahisi tunachezewa shere hapa................wote ni wale wale...Mwaka 1980 Sitta alikuwa waziri wa ujenzi yaani mpaka leo yuko Madarakani anaongea nini sasa kama si upuuzi tu.
 
WATANABE

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
1,092
466
Mnafiki mkubwa huyu kama ajijua yota haya kwanini aliufunga mjadala wa Richmond/Dowans bungeni alipotishiwa kunyang'anywa kadi ya CCM. Kama alikuwa jasiri kweli alitakiwa kuwakabidhi kadi yake kwa ridhaa yake na sio kuufunga kinyemela mjadal ule. Sitta ni sehemu ya tatizo hili.
 
Ta Muganyizi

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
5,360
2,720
hata kama lakini 6 nafuu. Wasirra anaweza sema haya. Hebu tuwe objective kidogo. Huyu anathubutu kusema, wengine sio watanzania walioko ccm wabubnge zaidi ya 200? ccm hai. Wote waseme basi . Awe manafiki au mkweli lakini walau kajitoa mhanga. Tusiwe biased bana.
 
Mkuu naona hujaelewa madhara ya Sitta kwenye hili ukilinganisha na Wasirra. wasirra ni mpwayukaji kwa wtau wenye uelewa wala huna haja ya kubabaika na anachosema, Sitta alikuwa Spika wa Bunge akauzima mjadala wakati kupitia ule Mjadala kulikuwa na azimio la kuishataki Richmond Mahakamani na ikibidi mali zake zitaifishwe, leo hii tungkuwa tunaongelea Richmond na dada yake Dowans kuilipa serikali na wanachi wa Tanzania na si vinginevyo. Kulikuwa na maazimio ya wote waliohusika wawajibishwe, Mkuu wa TAKUKURU Hosea anapeta mpaka leo, Mwanyika akastafu kwa hiari na kulipwa pensheni na mfao kibao, Manumba, vivyo hivyo. Badala ya kulipwa na kuitafisha maliza Richmond sisi ndio tunatkiw akulipa, aliyesababisha uzembe huu ni nani? Ni Samweli Sitta kwa kuuzima mjadala bila yale maazimio kutekelezwa. Huyu ni Adui namba moja wa Sekta ya Umeme Tanzania.
 
Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,615
Swali hilo limeelekezwa kwa asiyestahili.
Alaaa vipi hastahili wakati mada hii inajieleza kasema nini? mada hii haiwahusu wengine isipokuwa yeye kama kichwa kinavyojieleza..Wananchi sisi hatuwataki Dowans, Richmond na hata hao Symbion kwa sababu lengo lilikuwa kutuingiza mjini hivyo hawawezi kufanikiwa kwa kubadilisha au kupitia majina mengine kwa hizo Megawatts 100...Anachokifanya Sitta ni kucheza siasa ili kujiweka ktk nafasi nzuri ya kugombea Urais 2015 lakini kama alivyosema mwanaharakati mmoja hapo juu, huwezi sukuma gari ukiwa umekaa ndani!
 
Mzee Kipara

Member
Jan 3, 2011
83
42
Mkuu naona hujaelewa madhara ya Sitta kwenye hili ukilinganisha na Wasirra. wasirra ni mpwayukaji kwa wtau wenye uelewa wala huna haja ya kubabaika na anachosema, Sitta alikuwa Spika wa Bunge akauzima mjadala wakati kupitia ule Mjadala kulikuwa na azimio la kuishataki Richmond Mahakamani na ikibidi mali zake zitaifishwe, leo hii tungkuwa tunaongelea Richmond na dada yake Dowans kuilipa serikali na wanachi wa Tanzania na si vinginevyo. Kulikuwa na maazimio ya wote waliohusika wawajibishwe, Mkuu wa TAKUKURU Hosea anapeta mpaka leo, Mwanyika akastafu kwa hiari na kulipwa pensheni na mfao kibao, Manumba, vivyo hivyo. Badala ya kulipwa na kuitafisha maliza Richmond sisi ndio tunatkiw akulipa, aliyesababisha uzembe huu ni nani? Ni Samweli Sitta kwa kuuzima mjadala bila yale maazimio kutekelezwa. Huyu ni Adui namba moja wa Sekta ya Umeme Tanzania.

Nashindwa kuelewa mnapomtupia Sita lawama za kashfa ya dowans ilihali watu waliosign huo mkataba wapo, watu waliolaghai mpaka hatimae richmond/dowans wakaweza kutuibia wapo, watu wanaonufaika na wizi wa richmond/dowans wapo, na hamna anayewasema. At least Sita aliruhusu mjadala wa richmond hadi kufikia Lowasa kujiuzuru, unafikiri ingekuwa anna makinda au msekwa hata hiyo richmond ingejadiliwa? Au mmeshasahau kwamba hawa wenye dowans ndo walicheza sinema mpaka sita akakosa uspika kwa sababu ya alivyowafanyia akiwa spika na uoga wa ambayo angefanya kama angeendelea kuwa spika?

Kweli sita kuna maamuzi aliyafanya ambayo hata mimi sikuyafurahia, lakini cha muhimu ni kuwa sasa hivi anaendesha kampeni ya kupinga tusiibiwe na dowans, kumpinga ni kusapoti huu wizi na mimi siwaelewi kabisa mnaposema sita akae kimya. Watanzania mna matatizo gani, mtu anawatetea mnampinga, well, hata kama anaganga njaa au anajitafutia jina kwa ajili ya 2015, cha muhimu si ni kwamba anatetea pesa za walipa kodi watanzania? Hakuna ubaya wowote kwa mtu kutetea maslahi ya nchi ili kujijengea jina, au ninyi mnapenda wagombea wanaosimama kwa kuuza sura tu bila kuwa na rekodi ya kusimamia maslahi ya taifa.

Na hili swala la kwamba lazima atoke ccm ndo mumsikilize mimi sioni mantiki yake, kwani nani alishatoka ccm akasikilizwa na watanzania, wote waliotoka wanaishia kufilisika kisiasa (Mrema, Mpandazoe etc). Sisemi kwamba kuhamia upinzani ni vibaya, lakini tuheshimu utashi wa mtu kuwa katika chama fulani na tuangalie zaidi matendo yake katika kuitetea tanzania.

Mwisho kabisa nasema hili deni lisilipwe, tufanye maandamano tufanye lolote lile lakini tutaonekana hamnazo kama tutawapa ml 111 watu ambao wameshatuibia vyakutosha tayari.
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
931
Mkandara ,

Unakijua kisa cha mbwa kuitwa Jibwa?? Ndio Dowans na Symbion, Sitta anapigia kelele Dowans (mbwa) lakini Symbion (Jibwa) wana matatizo kama ya Dowans ila kimya. Ndio maana mie huyu jamaa nishasema siku nyingi mnafiki na hizi kelele za kutaka achaguliwe urais 2015. Zungushaneni ila mjue Deni la Dowans linakuwa na ijapokuwa sifurahii kulipwa kwa kampuni ya kisanii katika dili hii ya kitapeli ila kwenye vifungu vya kisheria tushaumizwa na hivyo malipo yao ni halali. Tumalizane nao tuwageukie Symbion ambao hadi leo hatujaona umeme wao ijapokuwa tunawalipa mamilioni kwa siku. Kweli watanzania sisi aliyetuloga kafa!!!!

Nchi hii ina watu ambao wamelogwa kutetea ufisadi..na kuishi kwa illusion

Symbion hutasikia kwa mdomo wa mtanzania you know why it is an american company...

Wacha kizazi kingine kitazinduka tu..
 
Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,615
Nashindwa kuelewa mnapomtupia Sita lawama za kashfa ya dowans ilihali watu waliosign huo mkataba wapo, watu waliolaghai mpaka hatimae richmond/dowans wakaweza kutuibia wapo, watu wanaonufaika na wizi wa richmond/dowans wapo, na hamna anayewasema. At least Sita aliruhusu mjadala wa richmond hadi kufikia Lowasa kujiuzuru, unafikiri ingekuwa anna makinda au msekwa hata hiyo richmond ingejadiliwa? Au mmeshasahau kwamba hawa wenye dowans ndo walicheza sinema mpaka sita akakosa uspika kwa sababu ya alivyowafanyia akiwa spika na uoga wa ambayo angefanya kama angeendelea kuwa spika?

Kweli sita kuna maamuzi aliyafanya ambayo hata mimi sikuyafurahia, lakini cha muhimu ni kuwa sasa hivi anaendesha kampeni ya kupinga tusiibiwe na dowans, kumpinga ni kusapoti huu wizi na mimi siwaelewi kabisa mnaposema sita akae kimya. Watanzania mna matatizo gani, mtu anawatetea mnampinga, well, hata kama anaganga njaa au anajitafutia jina kwa ajili ya 2015, cha muhimu si ni kwamba anatetea pesa za walipa kodi watanzania? Hakuna ubaya wowote kwa mtu kutetea maslahi ya nchi ili kujijengea jina, au ninyi mnapenda wagombea wanaosimama kwa kuuza sura tu bila kuwa na rekodi ya kusimamia maslahi ya taifa.

Na hili swala la kwamba lazima atoke ccm ndo mumsikilize mimi sioni mantiki yake, kwani nani alishatoka ccm akasikilizwa na watanzania, wote waliotoka wanaishia kufilisika kisiasa (Mrema, Mpandazoe etc). Sisemi kwamba kuhamia upinzani ni vibaya, lakini tuheshimu utashi wa mtu kuwa katika chama fulani na tuangalie zaidi matendo yake katika kuitetea tanzania.

Mwisho kabisa nasema hili deni lisilipwe, tufanye maandamano tufanye lolote lile lakini tutaonekana hamnazo kama tutawapa ml 111 watu ambao wameshatuibia vyakutosha tayari.
Acha tabia ya usahaulifu, Kamati ya Mwakyembe ilikuwa ni kamati ya rais sii ya bunge hivyo Sitta alilazimika kuweka mjadala baada ya rais kuruhusu swala hilo liende bungeni na hadi kujiuzulu kwa Lowassa kama waziri mkuu. Sitta alikataa katakata swala la Richmond lisijadiliwe hata baada ya Lowassa kujiuzulu hakuruhusu swala hilo liendelee kuzungumziwa wakati ushahidi wote walikuwa nao bungeni.

Mimi nilishindwa kuelewa kwa nini wananchi na Bunge walitaka rais ndiye awawajibishe Lowassa na Rostam hali kesha wapeni greenlight ya kufanya uchunguzi na hata kukubali kujiziulu kwa Lawassa ktk mhimili wake (serikali). Hivi kweli ilikuwa kazi ya rais kufungua mashtaka hali bungeni hajapatikana na makosa? Swala la Richmond lilifia bungeni chini ya uongozi wa Sitta, Jk alishaifanya kazi yake toka upande wake.

Sitta angesema ushahidi ulokusanywa unatosha kuwawajibisha watuhumiwa na kumwambia Lowassa kama mbunge anapaswa kujieleza bungeni dhidi ya tuhuma hizo. Lowassa alijiuzulu kama Waziri mkuu, mhimili wa serikali na sii kama mbunge mhimili ambao Sitta alikuwa mwenye mamlaka yote ya kuwaita wahusika na tungepata ufumbuzi na pengine hata tusingewaona hawa Lowassa na Rostam wakisimama tena kugombea Ubunge mwaka 2010.. Sitta was the man behind kila liloshindikana bungeni na hata tukaletewa Dowans na leo tumefungashiwa Symbion...
 
Mbogela

JF-Expert Member
Jan 28, 2008
1,379
247
Nashindwa kuelewa mnapomtupia Sita lawama za kashfa ya dowans ilihali watu waliosign huo mkataba wapo, watu waliolaghai mpaka hatimae richmond/dowans wakaweza kutuibia wapo, watu wanaonufaika na wizi wa richmond/dowans wapo, na hamna anayewasema. At least Sita aliruhusu mjadala wa richmond hadi kufikia Lowasa kujiuzuru, unafikiri ingekuwa anna makinda au msekwa hata hiyo richmond ingejadiliwa? Au mmeshasahau kwamba hawa wenye dowans ndo walicheza sinema mpaka sita akakosa uspika kwa sababu ya alivyowafanyia akiwa spika na uoga wa ambayo angefanya kama angeendelea kuwa spika?

Mwisho kabisa nasema hili deni lisilipwe, tufanye maandamano tufanye lolote lile lakini tutaonekana hamnazo kama tutawapa ml 111 watu ambao wameshatuibia vyakutosha tayari.

katika sakata la Richmond/Dowans wapo makundi matatu au manneya watu wanaostahili kupewa lawama.
1. Ni wamiliki wa dowans, Hawa ni wezi na majambazi yaliyotengeneza deal na kuwapiga mchanga wa macho watanzania. Hawa wanastahili kushtakiwa kwa sheria zetu za Uhujumu uchumi ya mwaka 1982. Lakini je wanafahamika??? Kuwafahamu hao unahitaji kupata mtu wa pili wa kumlaumu
3. waliosaini Mikataba. Hawa ni watendaji wetu wa serikali wakiongoza na mwanasheria mkuu wetu wa serikali Johnson Mwanyika, Hawa walisaini mikataba na mwenie Idrisa (CEO TANESCO) hali wakijua wanakaa meza moja na matapeli, wezi, majambazi na mijitu kupe. Hawa wanawajua walioingia nao mkataba, na wanajua ni nani aliwashawishi kuwatambua Richmond, na wanamjua aliyewalazimisha kusaini hiyo Mikataba lakini wapo kimya. Je Kuna mtu mwingine anaweza kutusaidia kujua majizi hayo????
3. Mwakyembe et al. Mwakyembe na Mwenzake Stella Manyanya and Co: walipewa jukumu la kutafuta ukweli na kuuwakilisha Bungeni na kwa umma wa watanzania. Kwa ujumla hawa jamaa walifanya kazi nzuri sana ya kubaini Ukweli, na pia walitoa mapendekezo yaliyokuwa ni mazuri pia. LAKINI hawa wanastahili lawama kutoka umma wa watanzania kutokana na kwenda kinyume na hadidu za rejea za kutafuta na ueleza ukweli wote kuhusiana na sakata la Richmond. Kilichotokea na kuwa Bw. Mwakyembe na Timu yake waliwakilisha ukweli Nusu na nusu kuuacha. Wao walitumia busara yao kuwa kama wangetoa ukweli mtupu nchi ingeingia mtatizoni. Sijui walipata wapi busara hii, Nchi ingeingia katika matatizo yepi? Kikundi cha majizi Vs wenye Nchi ni matatizo?? walipaswa kutuambia ukweli mtupu. Hata hivyo waliwakilisha taarifa yao Bungeni, ambalo boss wake alikuwa huyo Samwel 6. Sasa huyu alikuwa na wajibu wake wa kufanya ambao haukuufanya kwa makini na anakuwa mtu wetu wa tatu wa kubeba lawama.
4 Samweli Sitta: Yeye akiwa spika na kiongozi wa shughuri zote za bunge alipaswa kujiridhisha kuwa kamati ya Mwakyembe imefaya kazi kwa kiwango kilichotegemewa, mbili imekusanya taarifa zote zilizotakiwa na tatu imewakilisha taarifa zote. Sitta bila shaka alijiridhisha kuwa Mwakyembe na wenzie walifanya kazi yao vizuri na walikuwa na taarifa zote muhimu, Kwa vile yeye tatizo lake lilikuwa ni nafasi ya Uwaziri Mkuu since 2005 basi akaamua kwa busara zake mwenyewe naye kuelekeza nguvu kwenye kumbana waziri mkuu na mawaziri waandamizi, na kuacha maazimio mengine 22 yanaelea hewani. Sitta alifanya kosa la msingi la kujiridhisha kuwa kwa kujiuzuru kwa Lowassa tayari tatizo la Richmond lilikuwa solved. Sitta alipaswa kuhakikisha anafanya kazi yake mpaka mwisho. Alipaswa kuibana kamati ya Mwakyembe itoe aarifa yote kama ilivyokuwa imekusanya, Pia alipaswa kuhakikisha serikali inatekeleza maazimio yote. Pale iliposhindwa kutekeleza angechukua kasi zaidi ya kuhakikisha Pinda naye anajiuzuru kwa kushindwa kutekeleza maazimio ya bunge na maelekezo ya bunge kwa serikali.

Hata hivyo Samweli 6 Akaenda mbali zaidi na hata kusimama BOLD kwenye vyombo vya habari kulitetea bunge na yeye mwenyewe kuwa wamefanya kazi yao kwa kiwango cha uafanisi and according to the Tanzanian expectation.

Kama Mjadala wa Richmond ungekuwa umekwisha tungekuwa hatuna la kusema juu ya Sitta lakini shida inakuja kwasababu bado kuna impurities nyingi zinaendelea kuelea kwenye siasa na maendeleo ya tanzania. Na impurities hizi ni Richmond/Dowans.
Huyu Sitta alikuwa na nafasi nzuri sana wakati ule, sasa hawezi kuanza kujiapisha kuwa isilipwe, wakati alipokuwa ameshika mpini na Richmodn imeshika makali hakutumia nafasi hiyo. Na wakati ule Sitta alikuwa anabembeleza apewe nafasi ya uspika tena. Sitta ni kigeu geu wala hayupo kwa maslahi ya taifa ila yupo kw amaslahi yake binafsi. Kama Sitta angekuwa kw amaslahi ya taifa zaidi angeweza kuona mwaka 2006 October kuwa Ajenda ya Buzwagi ilikuwa kwa manufaa ya taifa. lakini kwa vile alikuwa kwa maslahi yake binafsi na chama Chake kuuzima mjadala wa buzwagi na hata kumfukuza Mh. Zitto Kabwe, leo nchi hii inaingia hasara kubwa sana kutokana na migodi ya madini. Sitta huyu huyu leo anajidai kutetea VG Cent vya dowans alishindwa kuona mamilioni yanayopotea kutokana na maswada wa kifisadi ulikuwa umesainiwa na Karamagi kwenye Guest House London.
 
nguluvisonzo

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
515
68
Yote tisa, swali moja tu kwa Sitta -Mbona mmeitambua Symbion walirithi wengine wa mitambo ile ile yenye historia ya Richmond??

Symbion haijarithi mikataba imenunua mitambo,ni vitu viwili tofauti kati ya RICHMOND NA DOWANS,elewa ndugu yangu hapo hakuna kurithi mikataba ya dowans,tatizo lilikuwa DOWANS ilirithi mikataba na ambayo wanatumia kuibana TANESCO ndio maana tunasema mikataba na hukumu iliyotolewa ni haramu,ndio ambacho 6 naye anapinga
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom