Sitta:Chadema waruhusiwa kumkataa JK......................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Gazeti la Majira linatuhabarisha leo ya kuwa Mheshimiwa Spika Mstaafu ambaye ana elimu ya sheria amefafanua kuwa Chadema wanayohaki ya kisheria kumkataa JK...................

Hii inaondoa mashaka ya baadhi ya watu waliokuwa wanafikiri haki hiyo Chadema hawana.................................

Gazeti hilo la majira limeweka kwenye ukurasa wake wa kwanza kichwa cha habari kipana kisemacho "Chadema wanaruhusiwa kumsusia Kikwete" - Sitta
 
Mimi jana niliwambia kwamba chadema hawakukurupuka ni watu makini uwezi kuwalinganisha na cuf walioanza na mdrasat chadema walianzia chekechea.
 
Gazeti la Majira linatuhabarisha leo ya kuwa Mheshimiwa Spika Mstaafu ambaye ana elimu ya sheria amefafanua kuwa Chadema wanayohaki ya kisheria kumkataa JK...................

Hii inaondoa mashaka ya baadhi ya watu waliokuwa wanafikiri haki hiyo Chadema hawana.................................

Gazeti hilo la majira limeweka kwenye ukurasa wake wa kwanza kichwa cha habari kipana kisemacho "Chadema wanaruhusiwa kumsusia Kikwete" - Sitta
Mr. Six you are a clean/right person in the worse part.
 
Yeah, sitta yuko sahihi na ndivyo mwongozo wa nchi (katiba) unavyoeleza, ingawa tunajua fika kuwa maneno yake hayo yanaweza kutafasiriwa isivyo na ndugu zake lakini hata upindishwe vipi siku zote ukweli utabaki kuwa pale pale, tusubiri kusikia bi makinda atasimama upande gani kama ni kumuunga mkono bosi wake wa zamani na kusimamia katiba ama ni kutekeleza matakwa ya waliompeleka
 
ivi kumkubali rais aliyeiba kura kuingia madarakani ni lazima?hivi hawa CCM vipi???hahaaa imewauma mnoooooooooooooooooooo
 
Gazeti gani? Majira mmmhhhh! hata siliamini saaana. Ila leo litauza kwa habari hiyo.

Anyway, Watanzania wengi tunaishi kwa kunyenyekea nyenyekea saana hata pale ambapo tunaonewa tunaona sawa tu. Bado tuko kwenye zama za kuchekeana chekeana kana kwamba bila ya mtu fulani hatuwezi kuishi.

Na hii ni kutokana na kuwa wengi hatujaweza kusimama kidete na kufungua milango yetu kwa kuweza kuishi kutumia vichwa vyetu badala ya kufuata mkumbo kama ilivyo sasa kwa wengi wa watanzania wenzangu.
Inakuwa ngumu sana kumshawishi mtu ambaye hajawahi kupata kashi kashi za maisha na kukutana na matatizo mengi na kuyatatua kwa solutions tofauti tofauti nyingi, kuliko ambaye amekuwa na kuamini kuwa hali aliyonayo ni sawa tu wala hajui cha kufanya, zaidi ya kusubiri wakati kama wa uchaguzi na kuweza kununua hata bati na mifuko ya cement na kujenga chumba kimoja cha kulala.

Its time for a CHANGE!
 
Hofu yangu ni usalama wa Sita.
Kwa kauli hiyo aliyoitoa, hivi
hawa mafisadi watamwacha kweli?
 
Mimi jana niliwambia kwamba chadema hawakukurupuka ni watu makini uwezi kuwalinganisha na cuf walioanza na mdrasat chadema walianzia chekechea.

Tusiingize mambo ya udini katika hoja zetu. Madrasa yanatoa elimu nzuri kabisa ya Kiislamu kama ambavyo Wakristu wanasoma Mafundisho. Mimi elimu yangu ilianzia mafundisho kwa kuwa wazazi wangu waliona "Chekechea kuwa ni kupoteza muda na kwenda kunywa uji." Nilifundishwa kusoma nyumbani. Kwa sasa sikubaliani na mtazamo wao naamini Chekechea nzuri ni kitu kizuri.

Hoja yangu ni kuwa Madrasa na Mafundisho ni elimu nzuri na si kitu cha kubeza. Kama tunapinga msimamo wa mtu tupinge kwa mawazo yenye mantiki na yanayoweza kumshawishi unayemwambia aweze elimika au muweze kuanzisha majadiliano na si kutumia lugha ambayo inazuia mazungumzo na kuamsha chuki kama ya kupinga dini, kabila au rangi ya mtu. Naomba kutoa hoja.
 
Gazeti gani? Majira mmmhhhh! hata siliamini saaana. Ila leo litauza kwa habari hiyo.

Yaani wamaanisha gazeti la Majira wameichakachua habari hii kwa kujitungia na Sitta hakusema hivyo au wamaanisha nini?
 
Sitta usiogope, uwe tayari hata kufa kwa kusema haki, japo wakati mwingine huwa unaachi then unakuja kubana.
 
Huhitaji kuwa genius kutambua kuwa Chadema hawakufanya makosa kususia au kutomtambua Raisi. Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na ni wale waoga tu ambao kama tunavyojua watanzania wengi ndivyo walivyo na pia wanaona kuwa ilikuwa ni makosa kususia, nakumbuka mwaka jana nilimtetea mtoto wa jirani yangu ambaye alikamatwa na polisi na kuwekwa cell bila sababu inayoeleweka na wazazi wake hao walikuwa wanaogopa kwenda kuuulizia kulikoni?, ndipo nilipowalazimisha twende nao mpaka kituoni ambapo nilijibizana nao mpaka wakamtoa!, cha ajabu ni kwamba nilikuwa nawauliza kila mara sababu ya kumuweka ndani hawakunieleza na cha ajabu kingine ni wale wazazi wa huyo kijana kuniomba sana nisijibizane nao ati wasije wakatuweka ndani wote heheheh! Mtanzania kweli hajui haki yake na kunahitajika nguvu ya ziada ku empower jamii! sickening!!

Hongera Sitta tuko pamoja!
 
Sita anafanya vizuri sana kueleza ukweli wa mambo na sio zile siasa za kina chiligati na makamba za ushabiki ambazo zinaendesha CCM.Mimi naamini muda si mrefu ccm wenyewe wataaibika kwani wao wenyewe sasa hivi maelewano si mazuri hasa katika mwelekeo wa chama na nchi,nafikiri wale wakweli watasimamia ukweli wao kwa manufaa ya taifa hili.
 
Nafikiri kuwa Chadema wanaupeo mkubwa wa kufikisha jambo tofauti na CUF wanaopenda kutumia nguvu, hivyo kilichotakiwa ni kufikisha ujumbe kwa jumuiya ya kimataifa kuwa Chadema wanataka nini.
 
Sitta watanzania tupo nyuma yako, tunakubali ukweli na tunalilia siku zote haki itendeke bila kujali itikadi zetu wala vipato vyetu..
Mola na akutie ujasiri.
 
kila mwananchi mwenye mapenzi mema na nchi hii hataona kosa lolote juuu ya chadema kususia hotuba ya rais bali mambumbuna wanaojiita wasomi wa vyeti vya mezani ndio wasiojua matokeo chanya na faida ya watu makini (CHADEMA) kumgomea rais jamani jk sio mungu kuwa ukimpinga utalaaniwa THINK TWICE.
 
Kitendo cha Chadema kususia hotuba ya Kiongozi aliyechaguliwa na NEC iliyoundwa na CCM makusudi kabisa ili kulinda maslahi yao ni cha kishujaa. Watanzania wengi hasa vijana wamefunguka macho, bado vijijini lakini hata hao wa vijijini wamestuka na huo ni mwanzo mzuri. CHADEMA tuookoeni miaka 49, afadhali kabla ya uhuru tulichapwa viboko lakini mashamba ya mikonge, pamba, na reli ilikuwepo, leo miaka 49 ya uhuru vyote vimetoweka imebaki NEC ya kutoa maamuzi bila kupingwa na mahakama yoyote ile. Je hao NEC malipo yao nini? Mungu atawalipa machozi ya wananchi wanaoishi kwenye nyumba za makuti na nyie mpo kwenye mapajero na majumba ya kifahari mungu hamtupimtu wake ipo siku angalieni Saadam Hussein alitawala kimabvu mwisho wake mliuona, akin Mobutu Seseko, Idd Amin, Samuel Doe
 
Back
Top Bottom