Sitta Bungeni alazimika kutoa maelezo ya ziara yake

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Bunge limeanza sasa na Sitta asema kwa nini amevunja safari ya Marekani .Kasema alialikwa chakula huko kwa mujibu wa taratibu za US.

Pia ameomba radhi kwa kumtumia neno Kukurupuka na yeye anadhani anachonganishwa .
Spika asema pia semina baada ya kuvurugika imechangia yeye kuvunja safari .

Kasema ana Imani na Naibu Spika na amerudi kwa sababu yeye ndiye Spika na anajali utawala bora .

Amerejea kwa ajili ya hoja ya Richmond.Ni swala zito na yeye karudi kuwapo .

Sasa Richmonduli inawekwa mezani .
 
rroo na iri naro rinawaigi kweri na miapari ya kudakiaga. siwaiongerea hiyo miapari kwenye ripunge. ri tvt sirinaaparishaga hiyo miapari raifu.
 
Vuta subira mkuu . Wameanza na maswali na majibu lakini Sitta lasema leo ngoma mezani.Katamka mwenyewe .Nami nangoja .Soma vyema utaona nimem quote akisema kwamba leo ni jambo zito liko mezani nami niko hapa .
 
Vuta subira mkuu . Wameanza na maswali na majibu lakini Sitta lasema leo ngoma mezani.Katamka mwenyewe .Nami nangoja .Soma vyema utaona nimem quote akisema kwamba leo ni jambo zito liko mezani nami niko hapa .

Sawa mkuu, sasa hata mi nasikiliza.....Lets hope utakuwa mjadala mzito kama alivyosema 6.
 
Mungu ibariki tanzania,wasiifanyie edditing hiyo report ije kama ilivyo
 
Tunasubiri habari zaidi. Kulikoni hili la RICHMONDULI lionekane ndiyo la utawala bora. Naogopa kama kutakuwa na editing ya hiyo ripoti
 
Dili hilo linakuja sasa naona Mwakyembe amejikita kusoma na watu nikiwemo mimi tuko makini kusikiliza .Kazi hiyo
 
Wakati Mwakyembe anasoma ripoti naona Kingunge kashika kichwa baada ya kusikia barua kuandikwa Jumapili siku ya mapumziko na Wizara.
 
Inaelekea watamtema Msabaha maana kila kitu ni yeye na wizara yake.

Mwakyembe anamtetea Lowassa, usanii tayari.
 
kazi ipo nasikia PM kakosa raha kabisa na wabunge wengi wameshika tama kusikiliza kwa makini...
 
Richmond ulikuwa mradi wa Lowassa na Rostam, kulingana na Msabaha na Balozi Kazaura. Lakini walisema hayo nje ya kiapo.
 
Lowasa kabadilika rangu kabisa . Ngasongwa hoi kashika tama.Leo Malecela na Kingunge hawajalala Bungeni inaonyesha ukali wa jambo hili .
 
Balozi Kazaura katika ripoti yake ndio kakandamiza kwa kusema richmonduli ni mradi wa Big brother na EL
 
Tanzania bwana! Jamaa anasoma report kubwa namna hiyo bila hata glass ya maji? Mtu anaweza kuanguka hivi hivi.
 
Tanzania bwana! Jamaa anasoma report kubwa namna hiyo bila hata glass ya maji? Mtu anaweza kuanguka hivi hivi.

Kazi ni kubwa maana hata jasho ndani jumba lile la kiyoyozi lakini anafuta majasho kama hana akili nzuri .Tunaendelea kusikiliza .Naona Karamagi akili yako haifanyi kazi ghafla .
 
Mwakyembe anamwaga mapendekezo ili ngome watu wagawane sasa.
 
Mwakyembe anamwaga mapendekezo ili ngome watu wagawane sasa.

Lunyungu,

Tupe summary ya ripoti hususan walio husika, tutajie majina yao na uhusika wao. Mengine tuta yajua baadae tafadhali mkuu maana hata kazi sasa hazifanyiki tunachungulia chungulia huku nachelea nisije nikamwaga ugali wa watoto hapa....
 
Back
Top Bottom