Sitta azuia kuwanyanyasa wafanyabiashara mpakani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta azuia kuwanyanyasa wafanyabiashara mpakani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 29, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tuesday, 28 August 2012 21:24

  [​IMG]Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akizungumza na wananchi na wafanyabiashara ndogo waliopo katika mpaka wa Tanzania na Uganda eneo la Mtukula, wilayani Missenyi juzi, akiwa katika ziara yake ya kiserikali mkoani Kagera. Picha na Edwin Mjwahuzi

  Edwin Mjwahuzi, Bukoba
  WAZIRIi wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amepiga marufuku vitendo vya unyanyasaji kwa wafanyabiashara ndogo ndogo wakiwamo mama lishe katika mpaka wa Mtukula unaotenganisha nchi ya Tanzania na Uganda.

  Sitta alitoa amri hiyo baada ya mmoja wa wafanyabiashara katika eneo hilo, Sauda Athumani kudai kuwa wananyanyaswa na mzabuni wa ukusanyaji ushuru wa Halmashauri ya Wilaya ya Misenye.

  Sitta alisema, jamani nawaomba nyinyi viongozi na watumishi na wachukuaji ushuru acheni kuwanyanyasa wafanyabiashara hawa, badala yake kaeni na kupanga ni jinsi gani ya kuwawezesha kufanya biashara zao katika mazingira mazuri.

  “Halmashauri inapaswa kuweka mpango madhubuti utakaowawezesha wafanyabiashara kujenga vibanda vya muda kwa ajili ya shughuli zao, hususan upikaji na uuzaji chakula,” alisema.

  Sitta alitembelea mpaka huo ulipo mkoani Kagera akiwa katika ziara ya siku tano kuangalia miradi mbalimbali inayohusiana na muingiliano wa uchumi na kijamii kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
  Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu, Fabian Massawe ameeleza changamoto zinazokabili mkoa wake katika maeneo ya mipaka kati yaTanzania nchi jirani ambazo ni wananchama wa Jumuiya hiyo (EAC).

  Kanali Massawe alisema mkoa huo unahitaji Sh 400 milioni ili kukabiliana na changamoto zote za mipaka ya Tanzania na nchi ya Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya kwa upande wa Ziwa Victoria.

  Aliyasema hayo juzi wakati akitoa taarifa ya mkoa wake wa Waziri Sitta ambaye yupo ziarani mkoani humo.
  Alisema mpaka uliopo kati ya Tanzania kwa upande mmoja na Rwanda, Uganda na Burundi wenye urefu wa Kilomita 552.6, umekuwa ni sehemu inayopendwa kutumiwa na wahamiaji haramu kuvuka na kuingia nchini.

  “Mheshimiwa Waziri eneo hili ambalo kwa sehemu kubwa ni msitu, linahitaji ushiriki wa taasisi zinazounda Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ili kufanikisha jitihada za kukabiliana na changamoto”.

  Kanali Massawe alisema takwimu zinaonyesha kuwapo kwa wahamiaji haramu 35,000 mkoani humo wanaokaribishwa na wenyeji na kushirikiana katika shughuli za uzalisha mali ikiwamo kuchunga mifugo, uvuvi na kilimo.

  Alisema nchi inapozidi kupata ongezeko la wahamiaji haramu panaweza kuibuka kwa machafuko kama inavyotokea hivi sasa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

  Akijibu taarifa hiyo Waziri Sitta alisema anashangazwa na taarifa za kuhitajika kwa Sh400 milioni wakati Serikali ilishaidhinisha zitolewe.
   
Loading...