Sitta Azima Maswali BUNGENI: Richmond & BoT Zimsubiri Yeye Atoke Marekani!!

ALAANIWE SITTA
Huyu mtu ni adui wa taifa. Anatumia kila njia kukatisha tamaa juhudi za kupigana na ufisadi. Hivyo hivyo alichelewsha hoja za Dr. Slaa kuhusu BOT scandals mpaka mpiganaji wa watu akaamua ku-withidrawal NA kuingia msituni, matunda yake tumeyaona. Anachotaka ni kuchelewesha kujadiliwa ili aahirishe akijua kabisa Watz kusahau sisi ni mabingwa. Kwa kweli naandika muda huu mbaya nikiwa na machungu sana..hivi hatuna kiongozi mwenye uzalendo hata chembe? Usanii serikalini mpaka bungeni!!! ZITTO na wenzako msikate tamaa, tutapigwa mabomu ya machozi wote, muuumbueni hyuo mzee fisadi, baradhuli na fidhuli mkubwa. TAMWA, TGNP na wengineo mko wapi mama Makinda nadhalilishwa..Mama Kijo tafadhali usichoke kutetea haki..hata kama ni wa CCM bado ni Mtz an mama mwenzio ambaye kadhalilishwa na huyo baradhuli.

ALAANIWE SITTA.
 
mimi najiuliza, kwanini spika hataki naibu wake asimamie masuala "nyeti"? anaogopa nini?

binafsi sijawahi kusikia mama makinda akihusishwa na ufisadi. japokuwa nafahamu mwaka 1995 alikuwa mstari wa mbele katika kuwapigia debe muungwana na pm sidhani kwa sasa kama yupo karibu na mtandao.

aidha nimewahi kuelezwa kwamba huyu mama anakerwa sana na uchafu/ufisadi unaoendelea na huenda hili ndilo lililomsukuma mh. six kumuonya "asikurupuke" kusimamia masuala nyeti. nadhani mh. six anafahamu fika msimamo wa naibu wake na kwamba asipotumia ubabe naibu wake anaweza ruhusu hayo masuala "nyeti" yakazungumzwa na akirudi atakuta uchafu wote hadharani na akawa ameshindwa kuwalinda wale anaotaka kuwalinda. ni maoni yangu tuu
 
.............aidha nimewahi kuelezwa kwamba huyu mama anakerwa sana na uchafu/ufisadi unaoendelea na huenda hili ndilo lililomsukuma mh. six kumuonya "asikurupuke" kusimamia masuala nyeti. nadhani mh. six anafahamu fika msimamo wa naibu wake na kwamba asipotumia ubabe naibu wake anaweza ruhusu hayo masuala "nyeti" yakazungumzwa na akirudi atakuta uchafu wote hadharani na akawa ameshindwa kuwalinda wale anaotaka kuwalinda. ni maoni yangu tuu

...kafara....huo ndio ukweli wenyewe
 
Sitta azuia hoja ya EPA, Richmond

na Peter Nyanje, Dodoma
Tanzania Daima

HATIMA ya hoja kuu mbili zinazoonekana kugusa hisia za watu mbalimbali, ile ya Kashfa ya ubadhirifu wa fedha zilizotengwa katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (Bot) na inayohusu utata katika mkataba wa kuzalisha umeme kati ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kampuni binafsi ya Richmond Development zinaendelea kubakia kitendawili ndani ya Bunge.
Kitendawili hicho kimetokana na kauli iliyotolewa bungeni jana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta, ambaye alitangaza kusitisha mjadala wa hoja hizo kwa muda kutokana na yeye kuwa nje ya nchi kikazi kwa siku kadhaa wiki ijayo.

Katika tangazo lake hilo la jana, Sitta, alisema alikuwa akitarajia kusafiri Jumatatu ijayo kwenda Marekani kwa mwaliko rasmi wa Baraza la Wawakilishi la nchi hiyo na atarejea nchini Alhamisi ya wiki hiyo hiyo ijayo.

“Sikutaka Naibu Spika (Anne Makinda) akurupuke na kuvamia masuala haya nyeti, itabidi yasubiri mpaka pale nitakaporejea… tunayo wiki nzima ya kuyaangalia haya,” alisema.

Dalili za kupigwa danadana kwa suala la EPA kwa mfano zimeanza kuonekana mapema bungeni jana, wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

Mwelekeo huo ulianza baada ya Spika kuzuia kujibiwa kwa swali la nyongeza la Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed (Wawi-CUF) aliyetaka maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo kuhusu kujadiliwa kwa suala la EPA bungeni.

Aliposimama kuuliza swali la nyongeza, Hamad Rashid alisema kuwa Kanuni za Bunge, zinaipa mamlaka taasisi hiyo ambayo ni mhimili wa dola, kujadili jambo lolote linalochunguzwa na taasisi nyingine yoyote nchini ukiacha mahakama.

Hata hivyo, kabla Naibu Waziri hajasimama kujibu, Spika alisimama na akatoa maelezo kuwa, alishatoa maelezo awali kuwa majadiliano na serikali kuhusu suala hilo la EPA yanaendelea na atalitaarifu Bunge hatima ya majadiliano hayo.

Majibu hayo ya Spika yalisababisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema) kusimama kwa lengo la kuuliza swali la nyongeza, juhudi ambazo hata hivyo zilizimwa kwa mara nyingine tena na Sitta, aliyemzuia kwa kusema maelezo aliyoyatoa yameizima hoja hiyo kuendelea kuhojiwa.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa, mapema wiki hii, Spika aliliambia Bunge kuwa, ndani ya wiki hii angetoa taarifa kuhusu matokeo ya mashauriano kati ya ofisi yake na serikali kuhusiana na suala la kuwasilishwa bungeni kwa ripoti kamili iliyoandaliwa na kampuni ya kimataifa ya ukaguzi wa hesabu ya Ernst & Young kuhusu EPA.

Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili nje ya Bunge baada ya kipindi cha maswali na majibu, Zitto alisema kuwa lengo lake la kusimama halikuwa kuulizia masuala ya EPA.

“Inaonekana mzimu wa EPA umetuvaa, kila kitu wao wanaona kama EPA… mimi sikutaka kuulizia kuhusu EPA, hoja yangu ilikuwa ni kuwa Naibu Waziri hakujibu swali lililoulizwa.

“Swali liliuliza kuhusu Debt Conversion Scheme, hizi ni fedha zilizoliwa na wafanyabiashara waliouziwa madeni, hilo ndilo lililoulizwa, lakini waziri alikwepa kulijibu hilo,” alisema Zitto.

Katika swali hilo lililoulizwa na Hamad Rashid kwa niaba ya Dk. Willibrod Slaa (Karatu-Chadema), mbunge huyo alitaka kujua ni watu gani walichukua fedha kupitia mpango huo wa kubadilisha madeni.

Aidha, pamoja na kutaka kujua majina ya watu hao, Dk. Slaa alitaka kufahamishwa kiasi cha fedha kilicholipwa na watu hao hadi Desemba mwaka jana, na iwapo hawajalipa, serikali imewachukulia hatua gani?

Katika majibu yake, Mkullo alisema kuwa hakuna mpango kama huo uliotajwa na Dk. Slaa na kuwa, kama serikali ilivyotoa maelezo bungeni Januari 29, mwaka huu, suala hilo (akimaanisha EPA) linashughulikiwa kulingana na maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete, hivyo ni vema wabunge wakasubiri matokeo yake.

Kikao hiki cha Bunge ndicho ambacho kimepangwa kujadili Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza zabuni iliyozaa mkataba kati ya Tanesco na Richmond ambao ulizua utata mkubwa tangu mwanzoni mwa mwaka jana.

Kutokana na hilo, Bunge lililazimika kuunda kamati teule iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Harisson Mwakyembe, ambayo ilipewa kazi ya kubainisha Kampuni ya Richmond ni ya nani na ina uwezo kiasi gani wa kufanya kazi, kutathimini mchakato wa upatikanaji wa zabuni wa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakiki uhalali wa mkataba kati ya kampuni hiyo na Tanesco.

Kazi nyingine ya kamati hiyo ambayo ilielezwa wazi kwamba ripoti yake ingewekwa wazi katika kikao cha sasa cha Bunge, ilikuwa ni kubainisha uwezo wa Kampuni ya Richmond wa kutoa huduma ya umeme, kupitia taarifa ya Mamlaka ya Zabuni (PPRA) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) na kutolea maoni na kutathimini vitu vingine vyovyote vinavyohusu suala hilo.

Uamuzi wa Bunge kuunda kamati hiyo ulitotokana na pendekezo la Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Biashara, inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli, William Shellukindo (CCM), la kutaka kuundwa kwake kutokana na kuwapo kwa shaka kwenye mkataba huo jambo ambalo alisema lisingepaswa kufumbiwa macho wala kupuuzwa.

Kwa upande wa Kashfa ya EPA, Bunge lilikuwa likitarajia kupatiwa ripoti kamili ya kampuni ya ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young ambayo iligundua upotevu wa shilingi bilioni 133 katika kipindi cha kati ya mwaka 2005/2006.

Ugunduzi huo ulitokana na uamuzi wa serikali uliotangazwa wakati wa Bunge la Bajeti katikati ya mwaka jana baada ya kutokea kwa hoja nzito za wabunge waliofikia hatua ya kutaka kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza madai ya ubadhirifu ndani ya Benki Kuu.

Wiki iliyopita, wabunge kadhaa walimtaka Spika kuitaka serikali kuwasilisha bungeni ripoti nzima ya Ernst & Young ili kutoa fursa kwa Bunge kuipitia na kuijadili kama walivyoahidiwa na serikali Agosti mwaka jana.

Kugundulika kwa Kashfa ya EPA, kulisababisha Rais Kikwete alazimike kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, Daudi Ballali na akatangaza kuanza rasmi kwa uchunguzi kuhusu suala hilo, ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu kwa wale wote watakaobainika kuhusika katika ubadhirifu huo.
 
This is why I stated that there is a need to dissolve the parliament and the cabinet and create a transitional government for 36 months.

Mbunge kauliza, kajibiwa upupu, kakaa kimya badala ya kuuliza swali la nyongeza kama hivi ifuatavyo:


Huku kuogopana ndiko kunafanya ufisadi ushamiri!

Duh! ukisoma majibu yao wanayoyatoa ya ubabaishaji yasiyokuwa na kichwa wala miguu unatamani kulia. Wanaificha ripoti ya ukaguzi kwa sababu imebadilishwa sana, hivyo wanajua wakiitoa hadharani watu watataka wapate uhakika kutoka Ernst & Young kama hiyo ripoti ndiyo iliyoandikwa na wao. Ernst & Young wakiikana ripoti hiyo kwamba siyo yao basi hiyo itakuwa ni forgery na anayehusika kufanya forgery wenyewe wanaita 'mchakato' hiyo ni lazima aende lupango.
 
Kumuita mwanadamu mwenzake kwamba anakurupuka mbele ya Bunge na Taifa it must be serious . Sitta ni mtu wa kukurupuka aliye na sutra ya kishetani. Hana soni wala haya . Utaweza kumuona hata usoni alivyo .
 
Huyu Mzee ni wa Ovyo sana,na anaongoza kwa usanii.anafanya Bunge kuwa Mali yake utazania alizaliwa kuwa Spika.Kunahaja hata wananchi kupiga kura kumchagua spika.

Hivi kwnaiani tusiwaponde mawe??<sheria za dini zinasemaje??>>

Huyu ndiye mtu wa viwango na kasi ya kupenda safariza nje huku akitembea na ofisi kwenye brief case.Yaani ni upuuzi per ssay na wa kiwango cha juu.

ndio maana hata karamagi alisafiri na mihuri mpaka london kusaini mikataba ya Nuzwagi.Ndio staili ya uongopzi wa awamu ya nne.

Mamvi kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni anshindwa hata kutoia muungozo??Bora na bwana zero sumaye.
 
Live toka hapa Dodoma . Sitta kwa mara nyingine amezima issue ya kutaka hoja iende Bungeni kwa kusema anashauriana na Serikali na anatatoa majibu baadaye . Hii ni baada ya wapinzani kuanza kuibana serikali na Zitto akiwa anakaribia kusimama kumwaga mambo basi Spika akasema basi inatosha atalisemea baadaye .So sasa ni matangazo maana kesha ua sooo. Hili ndilo Bunge letu la watukufu wetu wale .

iri naro harina hata miapari. sasa uritakaga yamupitege. renyewe si ririsemaga ririkwendaga kufataga mugao wa mipesa wariyoombaga ribunge ra mimerekani. sasa muritakaga warishamburiye na renyewe hariko. siririfanyaga ustawarabu kutakaga rishamburiwege uku renyewe riko mbere. sikuerewi unararamikaga rijambo ripi.
 
Nafikiri hapo Speaker Six huenda anamnyanyasa Mheshimiwa Makinda kijinsia! Ni kuwa ni kwa sababu ni mwanamke au vipi? Au yeye ana akili zaidi kuliko watu wote humo bungeni? Isije ikawa ana majibu ya kila mjadala unaoendelea hapo bungeni kwa hiyo anataka kupindisha hizo debates.

Kwa nini anafikiri asipokuwepo mambo ya kitaifa hayawezi kuendelea! Lazima ajue yeye yupo hapo kwa ridhaa ya Watanzania tu, cheo ni dhamana na asikitumie kwa manufaa yake.

Hapo hakuna cha STANDARD wala nini.. Standard tunayoijua sisi ni katiba ya nchi na taratibu za bunge sasa asifanye bunge kama ni mambo yake binafsi ya kifamilia.

Toka lini bungeni kuna mambo makubwa na madogo? Kumbe kuna mambo mengine speaker hayatilii maanani hapo kwenye vikao
 
Hapa ndipo utakapojua kuwa hatuna taasisi. Hivi inakuwaje kiumbe mmoja anapoondoka masuala "nyetu" hayana ruhusa ya kujadiliwa mpaka atakaporudi safari?
 
Huyu Mzee ni wa Ovyo sana,na anaongoza kwa usanii.anafanya Bunge kuwa Mali yake utazania alizaliwa kuwa Spika.Kunahaja hata wananchi kupiga kura kumchagua spika.

Hivi kwnaiani tusiwaponde mawe??<sheria za dini zinasemaje??>>

Huyu ndiye mtu wa viwango na kasi ya kupenda safariza nje huku akitembea na ofisi kwenye brief case.Yaani ni upuuzi per ssay na wa kiwango cha juu.

ndio maana hata karamagi alisafiri na mihuri mpaka london kusaini mikataba ya Nuzwagi.Ndio staili ya uongopzi wa awamu ya nne.

Mamvi kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni anshindwa hata kutoia muungozo??Bora na bwana zero sumaye.


Gembe, Heshima kwako.
Nakubaliana nawe kwamba sasa bunge kwa fikra za Six ni "Samwel Sitta Briefcase Office Organisation" simply I mean his NGO

Kwa wale mliosoma kiatabu cha Shabaan Robert "Kusadikika" Six hana tofauti kabisa na Waziri Mkuu Majivuno. Huyu mtu katika kipindi kile, pamoja na kuwa elimu ilikwisha gunduliwa, yeye alifikiri na aliamini kuwa nvi ndiyo kipimo cha hekima na maarifa. Ukimsikiliza Six katika hoja zake siku zote anapojitetea kwa maamuzi anayotoa bila kuzingatia kanunu, husema "....kwa hekima zangu..", "...kwa busara zangu..."

Duh! kama kweli server ya busara na hekima kwa maamuzi nyeti ya Wadanganyika kajaaliwa Six, basi kuna kila haja kwa wale wenye imani ya mitume kuanza kuiombea Danganyika kwa jina la Six.
 
jamani mzee wetu ana chembechembe za udikteta. waulizeni wafanya kazi wa TIC enzi zake jinsia alivyokuwa anaongoza pale.
 
"" na akitaka kuwaweza ni pale ambapo atakaporudi na kuamua kuwa mambo haya ni mazito na muda hautoshi kwa mjadala kwa hivyo anaamua kwa "busara zake" (sasa hivi busara ziko kisheria na kiutaratibu) hadi mkutano wa Aprili.

""Hapo ndipo Watanzani watatambua embe ni tunda, na nyanya ni kiungio!""

i like dat Mwanakijiji!!!!ur correct hilo ndilo analorudi nalo ndugu yangu na mjadala mpaka april,,uko kwenye ""CHAMA MKUU"" natumaini wale vibopa wa chama cha mafissadi wanalijua hili kwamba akirudi anakuja kusema nini!!!!
""KILA MWENYE PUMZI NA AMSIFU BWANA"
 
Tusipokikataa Chama Cha Mafisadi tutaendelea kuwa tumepinduliwa hivi hivi. Hivi kweli tunavyopelekwa kwa jeuri namna hii bado wadanganyika hawashituki kabisa! Hili zee Sitta limekaa kwenye madaraka mda mrefu lina jeuri kama akina Mramba(anayetulisha nyasi).

WANANCHI AMKENIIIIIIIII, CCM ITATUMALIZAAAA...UUUWIIII..
 
Tzpride Keleeeeeuwiiiiiiiiiiiiiii
Hujui Tumeshapinduliwaaaaaa Na Hawa Mafisadi Sasa Hivi Wameshaanzaa Kutulallia Tusubiri Watatufanya Nini????
 
Na Richmond nayo ina utata upi wakati kaye ilisha kamilika na ni yeye kutupatia taarifa tu ama bado anahitaji muda kutumia Busara zake ? JK kama ni safio act kama si safi unatuzuga basi CCM yangu inakufa hivi hivi .
 
Hivi Sitta anaitunishia misuli serikali au wabunge? Je wabunge wanaogopa nini wakati hana ubavu wa kuwafukuza kazi? Unganeni MPs, go beyond your party politics and show Tanzanians that you can change things and we will put you in the books of history of this country for ever. Remove this dictator from power. Uwezo, nia na sababu mnavyo. Do it now!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom