Sitta awashukia maadui wake: Amwita mmoja "Mhalifu sugu"!

Hivi wao wafanyakazi wa ofisi ya Bunge wao nao ni wanasiasa?.

Wao hawashiriki kumpigia kura Spika wa Bunge bali ni wabunge kwa niaba ya wananchi ambao ndio wanampigia kura mtu wanaependa awe spika miongoni mwao.

Hii ni ishara ya jeuri ya hao watumishi kwa kuwa wao wanakula na wanashiba kwa hio sidhani kama wana uwezo wa kuwasemea wabunge na wananchi kwamba kazi ya spika Samwel Sitta inawaridhisha.

Nina imani na baadhi ya wabunge ambao wanaombea Samwel Sitta ajiuzuru kiti hicho na kumpisha mtu mwingine wenye nia ya kuwa spika wa bunge.

Samwel Sitta ameshindwa kusimamia heshima ya bunge ambayo ni demokrasia kamili, kwa maana kwamba hoja mbalimbali zenye lengo la kukosoa maovu zinazingatiwa.

Pili Samwel Sitta ameshindwa kusimamia mambo muhimu ambayo yanahusu maslahi ya taifa kama vile usalama wa wabunge wawapo bungeni katika vikao vyao kwa kitendo kilichotokea cha kugundulika kwa unga katika viti vya bunge.

Kwa mtazamo wangu kwa watu kama Samwel Sitta ambae baada ya kumwona katika recent comments zake dhidi ya "various accusations" ninamwona kwamba ni "an obstacle to cleaning up the political system" ambayo mpaka sasa inatushinda tangu enzi hizoo.

Mimi kama raia sina cha kufanya ila ninawaomba wale wabunge woote ambao ni decent katika kufikiri future ya watoto wa taifa la kesho, kuhakikisha kwamba kunakuwa na motion ya kutokuwa na imani na Samwel Sitta na imfanye ajiuzuru na achaguliwe spika mwingine ambae ni "very understanding".

Bunge letu linahitaji mabadiliko na hasa katika wakati huu ambao hata nchi ya Rwanda tu wanakuja juu kwa kasi.

Many out there will not believe we are serious about the changes that are necessary as long as Samwel Sitta is in the chair, and that is the terrible situation we are in.
 
Last edited:
Halafu kuna wanaodhani kwamba katiba mpya itamaliza kabisa matatizo tuliyonayo. CCM haiheshimu katiba yao wenyewe je wataweza kuheshimu katiba ya nchi hata kama tukiwa na katiba mpya!? Angalia hawa mafisadi ndani ya CCM walivyoendelea kukumbatiwa ndani ya chama hicho akina Mkapa, RA, Chenge, Mramba, Msabaha, Lowassa, Karamagi na wengineo wengi.

Kama CCM ingeamua kufuata yaliyomo ndani ya katiba yao kuhusu watu kama hawa basi wote wangeshafukuzwa CCM siku nyingi sana lakini bado wanapeta tu! Kwa hiyo hata kama tutapata katiba mpya CCM wanaweza kabisa kutoiheshimu na kufanya wanavyotaka ili wabaki madarakani miaka nenda miaka rudi. Nchi yetu jamani ina matatizo makubwa sana.

Kwahiyo tatizo haswa la nchi yetu ni muundo na mwenendo wa CCM, Ubabe wake, uwongo wake, usanii wake, uchonganishi wake, kufanya vitu vya kisirisiri, vifichoficho, agenda zisizowajali wananchi, kudhani siasa pekee ndiyi huleta maendeleo kwenye nchi nk. HILI NDIYO TATIZO!
 
Tatizo ni beyond wabunge wa CCM! Tatizo ni wananchi watakaowapigia tena kura hao wabunge (akiwemo spika) na kuwarudisha bungeni

Tatizo si wananchi, tatizo ni Katiba ambayo haitoi nafasi ya kuwa na tume huru ya uchaguzi, wabunge wa CCM na CCM kwa ujumla hawachaguliwi na wananchi bali wanatangazwa na tume ya uchaguzi kuwa ni washindi regardless matokeo halisi ya kura.

Tunaposema wananchi wanaichagua CCM tunawapa CCM legitimacy ya kuendeleza michezo yao michafu. Kama itapatikana tume huru, wabunge wa CCM hawatazidi hata nusu.
 
Last edited:
Hivi wao wafanyakazi wa ofisi ya Bunge wao nao ni wanasiasa?.

Wao hawashiriki kumpigia kura Spika wa Bunge bali ni wabunge kwa niaba ya wananchi ambao ndio wanampigia kura mtu wanaependa awe spika miongoni mwao.

Hii ni ishara ya jeuri ya hao watumishi kwa kuwa wao wanakula na wanashiba kwa hio sidhani kama wana uwezo wa kuwasemea wabunge na wananchi kwamba kazi ya spika Samwel Sitta inawaridhisha.

Hili nalo ni tatizo jingine kubwa. Huu ni ufisadi kwa staili nyingine, labda tuseme wa fikra. Wao kuwa wafanyakazi wabunge wanaona kama wanastahili kujiamria nani awe spika au wapo sehemu ambayo haipaswi kuguswa. Tatizo nadhani ni mfumo wetu ulivyo ndio maana hata watu wanaofanya kazi sehemu moja au kitengo fulani cha serikali wanajiona ni bora kuliko wenzao, na sijui wanajipima hilo kutokana na nini?

Wabunge wanajiona ni untouchables! Mawaziri ndio usiseme kabisa, kauli zao zinatupa mwanga wanaogelea kwenye madaraka makubwa. Mtakumbuka kuna waziri mmoja alimwambia Dk. Slaa atafute hoja nyingine kwa sababu anahoji kuhusu ufisadi na meremeta na vitu kama hivyo? Huku kwa maoni yangu ni kulewa madaraka!

Kuna viongozi wanazibinafsisha taasisi za umma, ndiyo maana hawataki kupingwa kwa lolote wanalosema hata kama ni makosa, na watafanya kila lililo ndani ya uwezo wao kumuangamiza anayewapinga.
 
Tatizo si wananchi, tatizo ni Katiba ambayo haitoi nafasi ya kuwa na tume huru ya uchaguzi, wabunge wa CCM na CCM kwa ujumla hawachaguliwi na wananchi bali wanatangazwa na tume ya uchaguzi kuwa ni washindi regardless matokeo halisi ya kura.

Tunaposema wananchi wanaichagua CCM tunawapa CCM regitimacy ya kuendeleza michezo yao michafu. Kama itapatikana tume huru, wabunge wa CCM hawatazidi hata nusu.

nakubalina na wewe hapo kabisa lakini hili ni moja tu ya matatizo ya haki mengi ambayo chama tawala inatunyima regardless of the party name ata kama ingekua chama gani (si CCM) kiko madarakani. kwa sheria zilizopo bila ya vyombo huru vya ku-montor fairness in our society itakua ni vigumu sana kushutumu wengine katika jamii, nahili ni moja la tatizo kubwa kwenye jamii yeyote si tzania tu bali popote pale.

siasa si mbinu moja wala njia moja tu ni nyingi ndio maana kwenye democrasia ya kweli kuna vyama vingi with different view points all aim to solve their social issues in trying to achieve whole hapiness even though absolute fairness isnot guarantee but politics is always about debating what you think its right and ways of solving problems no man should have absolute views of what is right for allo uf us just because he has priveledge in a certain place either a forum, political party or position in a society unless its a heirachy society with strong class structures but anywhere that permits social mobility people should be allowed to challenge what they think wont serve best in society. no view is hundred percent that is why people debate to shy away from it i think it cowardness.
 
Last edited by a moderator:
TUNA IMANI NA MHE. SPIKA, KATIBU WA BUNGE – WATUMISHI WA BUNGE

Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge wameeleza kuwa wana imani na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ambaye wamemuelezea kuwa ni mtu makini asiyetetereka katika kutetea hadhi ya Bunge na Taifa kwa ujumla.

Akisoma risala kwa niaba ya watumishi wa ofisi hiyo katika sherehe ya wafanyakazi baada ya kumaliza Mkutano wa 16 wa Bunge, Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge, Bwana Angumbwike Ng'wavi alisema kuwa wamesikitishwa na baadhi ya habari zinazozagaa kuwa eti Mheshimiwa Spika anawagawa watumishi wa Bunge, ''tunafahamu kuna kundi la watu linalokereka na uhuru wa taasisi ya Bunge unavyokuwa na namna Bunge linavyofanya kazi zake kutokana na sasa Bunge kuwa mstari wa mbele kupambana na uovu uliopo katika jamii yetu. Mtu yeyote anayetetea haki na kupambana na uovu mtu huyo siku zote atakuwa na uadui kutoka kwa wale wanaonufaika na uovu huo'' alisema Bwana Ng'wavi.

Aidha, Bwana Ng'wavi alieleleza kuwa mtu mwema kupakwa matope kwa lengo la kumkatisha tamaa siyo kitu cha kushangaza katika ulimwengu huu kwani hata vitabu vitakatifu vinaeleza kuwa Mitume wa Mungu pamoja na mema yote waliyoyatenda bado walipigwa vita na wanadamu. Wengine waliteswa na hata kuuawa.

'' Wafanyakazi wa Bunge tuna imani na Mheshimiwa Spika na tunapenda kutoa wito kwa Spika kuwa aendelee na ujasiri huo katika vita dhidi ya ufisadi kwani baadaye historia itaonyesha ni nani hasa alikuwa mkweli na mtetezi wa nchi hii na wananchi wake. Kuna mwanafalsa moja aliwahi kusema, kwa lugha ya Kiingereza "If want your name to continue living even after your death do something worth writing or write something worth reading" Kwatafsiri isiyo rasmi mwanafalsafa huyu anasema ukitaka jina lako liendelee kuwa hai hata baada ya kifo chako fanya jambo linalostahili kuandikwa au andika kitu kinachostahiliki kusomwa'' ilisema sehemu ya risala hiyo.

Wakizungumzia kuhusu madai kuwa Katibu wa Bunge wa sasa, hana sifa za kushikilia nafasi hiyo, Wafanyakazi hao walisema kuwa wanashangazwa na madai hayo kwa kuwa katibu wa sasa ni mtaalam aliebobea katika masuala ya Bunge na uendeshaji wake, '' Bahati mbaya wanaoeneza hayo hawajafanya utafiti wa kutosha, kwani kama wangefanya utafiti wa kutosha wangegundua kuwa Dk. Thomas Kashililah ana uzoefu wa masuala ya Bunge kwa zaidi ya miaka ishirini akiwa ameshika nyadhifa mbali mbali ikiwemo Ukurugenzi wa Idara nyeti ya MipangO naTeknolojia ya Mawasiliano, Ofisa wa Bajeti, Katibu Mezani, Katibu wa Kamati za Bunge na Afisa Mfawidhi wa Ofisi Ndogo ya Bunge jijini Dar es salaam'' ilisema sehemu ya risala hiyo.
Wafanyakazi hao walisema kuwa Dkt. Kashililah ambae ni daktari wa falsafa ana sifa za kutosha na zimepita sifa za msingi anazopaswa kuwa nazo Katibu wa Bunge na wametoa wito kuwa asikatishwe tamaa na maneno hayo ya uzushi bali aendelee kuchapa kazi na kwa kushirikiana na Mhe. Spika aboreshe mazingira ya kazi na vitendea kazi.

Hivi karibuni kumekuwa na juhudi zinazofanywa na watu wasiopenda jitihada zinazofanywa na taasisi nyeti ya Bunge kwa kujaribu kuwachafua viongozi wa juu wa taasisi ya Bunge kupitia magazeti na mitandao ambapo Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge limelaani na kusema kuwa sio sahihi hata kidogo.

Imetumwa na Said Yakubu

kama alikuwa na sifa zilizopita kwanini alikubali nafasi hiyo?ukiwa una sifa za udereva ukipewa ukondakta utakubali?

PhD watu wengi wanazo, DR.Emmanuel Nchimbi au DR.KAMALA au DR.Mary Nagu hizo PhD zao zinaweza kushindana na Zitto Kabwe?
hawa wanamsema Thomas Kashilillah yupi? huyu ambaye anatoa ajira bungeni kwa ukristu na kupendelea vihiyo toka Nyegezi.
 
Nina imani na baadhi ya wabunge ambao wanaombea Samwel Sitta ajiuzuru kiti hicho na kumpisha mtu mwingine wenye nia ya kuwa spika wa bunge.

Pili Samwel Sitta ameshindwa kusimamia mambo muhimu ambayo yanahusu maslahi ya taifa kama vile usalama wa wabunge wawapo bungeni katika vikao vyao kwa kitendo kilichotokea cha kugundulika kwa unga katika viti vya bunge.

Mimi kama raia sina cha kufanya ila ninawaomba wale wabunge woote ambao ni decent katika kufikiri future ya watoto wa taifa la kesho, kuhakikisha kwamba kunakuwa na motion ya kutokuwa na imani na Samwel Sitta na imfanye ajiuzuru na achaguliwe spika mwingine ambae ni "very understanding".

1.Wabunge wepi unaoongelea, hawa hawa wa bunge hili? Waliopo ni wachache idadi yao kutosha kuleta mabadiriliko hayo bungeni.

2. Ni mbunge yupi unayefikiria atakalia kiti kile na kuhakikisha analinda maslahi ya taifa na si ya serikali, atahakikisha hoja zote za kifisadi zinachambuliwa kwa uhuru,kikamilifu na kuhakikisha uwajibishwaji wa wahusika wote? Ni wabunge wepi na wangapi watakaompigia kura?

3.Mnaomshutumu Spika Sitta, dhamila za roho zenu ni nyeupe kwamba tatizo ni yeye kama Sitta, kwamba anaweza akachaguliwa mwingine akatekeleza wajibu wake na kulinda maslahi ya nchi katika mfumo huu huu uliopo na kwenye aina ya wabunge walio wengi tulio nao?
 
kweli Tatizo ni CCM?

Zambia, Kenya na Malawi kwa zaidi ya miaka 10 sasa wanaongozwa na upinzani..are they better off than Tz?

Hivi Chiluba hakuwa mpinzani??

Tatizo ni sisi Watz wenyewe--tuache kureduce our problems to CCM only!
 
Hii peke yake haionyeshi kwamba Spika Sitta hana tuhuma za kujibu.Siku hizi Watanzania tuna tabia za kusafishana,na hizi zina weza kuwa harakati za aina hiyo hiyo.Time will tell kama Sitta kweli ni Mr.Clean kama yeye mwenyewe anavyo dai.
tuna imani na mhe. Spika, katibu wa bunge – watumishi wa bunge

wafanyakazi wa ofisi ya bunge wameeleza kuwa wana imani na spika wa bunge, samuel sitta, ambaye wamemuelezea kuwa ni mtu makini asiyetetereka katika kutetea hadhi ya bunge na taifa kwa ujumla.

akisoma risala kwa niaba ya watumishi wa ofisi hiyo katika sherehe ya wafanyakazi baada ya kumaliza mkutano wa 16 wa bunge, katibu wa baraza la wafanyakazi wa ofisi ya bunge, bwana angumbwike ng’wavi alisema kuwa wamesikitishwa na baadhi ya habari zinazozagaa kuwa eti mheshimiwa spika anawagawa watumishi wa bunge, ‘’tunafahamu kuna kundi la watu linalokereka na uhuru wa taasisi ya bunge unavyokuwa na namna bunge linavyofanya kazi zake kutokana na sasa bunge kuwa mstari wa mbele kupambana na uovu uliopo katika jamii yetu. Mtu yeyote anayetetea haki na kupambana na uovu mtu huyo siku zote atakuwa na uadui kutoka kwa wale wanaonufaika na uovu huo’’ alisema bwana ng’wavi.

aidha, bwana ng’wavi alieleleza kuwa mtu mwema kupakwa matope kwa lengo la kumkatisha tamaa siyo kitu cha kushangaza katika ulimwengu huu kwani hata vitabu vitakatifu vinaeleza kuwa mitume wa mungu pamoja na mema yote waliyoyatenda bado walipigwa vita na wanadamu. Wengine waliteswa na hata kuuawa.

‘’ wafanyakazi wa bunge tuna imani na mheshimiwa spika na tunapenda kutoa wito kwa spika kuwa aendelee na ujasiri huo katika vita dhidi ya ufisadi kwani baadaye historia itaonyesha ni nani hasa alikuwa mkweli na mtetezi wa nchi hii na wananchi wake. Kuna mwanafalsa moja aliwahi kusema, kwa lugha ya kiingereza “if want your name to continue living even after your death do something worth writing or write something worth reading” kwatafsiri isiyo rasmi mwanafalsafa huyu anasema ukitaka jina lako liendelee kuwa hai hata baada ya kifo chako fanya jambo linalostahili kuandikwa au andika kitu kinachostahiliki kusomwa’’ ilisema sehemu ya risala hiyo.

wakizungumzia kuhusu madai kuwa katibu wa bunge wa sasa, hana sifa za kushikilia nafasi hiyo, wafanyakazi hao walisema kuwa wanashangazwa na madai hayo kwa kuwa katibu wa sasa ni mtaalam aliebobea katika masuala ya bunge na uendeshaji wake, ‘’ bahati mbaya wanaoeneza hayo hawajafanya utafiti wa kutosha, kwani kama wangefanya utafiti wa kutosha wangegundua kuwa dk. Thomas kashililah ana uzoefu wa masuala ya bunge kwa zaidi ya miaka ishirini akiwa ameshika nyadhifa mbali mbali ikiwemo ukurugenzi wa idara nyeti ya mipango nateknolojia ya mawasiliano, ofisa wa bajeti, katibu mezani, katibu wa kamati za bunge na afisa mfawidhi wa ofisi ndogo ya bunge jijini dar es salaam’’ ilisema sehemu ya risala hiyo.

wafanyakazi hao walisema kuwa dkt. Kashililah ambae ni daktari wa falsafa ana sifa za kutosha na zimepita sifa za msingi anazopaswa kuwa nazo katibu wa bunge na wametoa wito kuwa asikatishwe tamaa na maneno hayo ya uzushi bali aendelee kuchapa kazi na kwa kushirikiana na mhe. Spika aboreshe mazingira ya kazi na vitendea kazi.

hivi karibuni kumekuwa na juhudi zinazofanywa na watu wasiopenda jitihada zinazofanywa na taasisi nyeti ya bunge kwa kujaribu kuwachafua viongozi wa juu wa taasisi ya bunge kupitia magazeti na mitandao ambapo baraza la wafanyakazi wa ofisi ya bunge limelaani na kusema kuwa sio sahihi hata kidogo.

imetumwa na said yakubu
 
Mapambano ya ufisadi kila kukicha yanaingia doa mbadhilifu anapo patikana wanatokea wapambe kwa nguvu zote wanamsafisha. Hapa mwamuzi wa mwisho ni mwananchi mlala hoi anaye wachagua hawa majamaa mimi na wewe naamini hatuta panga foleni kupiga kura.
 
huyu ambaye anatoa ajira bungeni kwa ukristu na kupendelea vihiyo toka Nyegezi.
mkuu unaboa bana kila mahali unachoomekea udini. Kwa hiyo wewe unaungana na wanaosema Muungwana anagawa vyeo kwa kuangalia ile alama nyeusi usoni??
 
Kiongozi wa taasisi au asasi ya UMMA ambaye ni FISADI ndiye anayekubalika kwa wafanyakazi wa chini yake na atadumu sana na kutetewa kwa nguvu kwelikweli! Hiyo ndio Tanzania tunayoijenga kwa sasa. Haihitaji akili nyingi kujua kwa nini hali iko hivyo.
 
Unajua, huyu Spika ni mjanja sana kupita kiasi. Yuko kama kinyonga. Leo anaipendelea serikali na kuwabana wabunge na kesho inawapendelea wabunge na kuibana serikali. Yeye ana kundi la wabunge wake maalum wakiwemo akina Selelii, Ole Sendeka, mpendazoe, Ana kilango, Mwakyembe, etc ambao utaona kila inapotokea hoja ya kuibamiza serikali basi huwapa nafasi ya kwanza wazungumze. Inaonyesha huwa wana vikao vyao vya pembeni kupanga mikakati dhidi ya serikali.

Zinapotokea hoja za wapinzani, ili kujipendekeza kwa CCM, huwa anawanyanyasa na kuwadhalilisha kama vile alivyofanya kwa kufukuza Cheyo nje ya Bunge bila sababu ya msingi.

Sasa basi, kwa kuwa serikali inajua mchezo anoucheza, yenyewe inasubiri tu wakati muafaka wa kum hold by the balls. Huu ufisadi unaozungumziwa juu yake hata CAG amekwisha uweka katika maandishi katika audit yake ya ofisi ya Bunge. Nadhani mtakumbuka kuwa Cheyo alikwisha lisema hilo. Kwa hiyo ukiona Spika siku hizi anaifagilia serikali ujue ni mbinu ya kupoza kombora hilo. Na serikali nayo inampoza kwa kumpa kila anachokiomba kama vile extra ulinzi n.k.

Kwa kuwa muda wa Bunge umebaki mdogo kabla ya uchaguzi ujuo naona this time Spika atapona. Na hizi mbinu ya kuwa manuovre wafanyakazi ni moja ya mbinu zake za ku survive, lakini kipindi kijacho huenda mambo yatakamwiya magumu.

The bottom line ni kuwa Spika anataka sana Urais hasa 2015. Lakini kutokana na ukinyonga wake, sidhani atafanikiwa, kwani by that time watu wengi watakuwa wamemjua kuwa ni mtu wa aina gani.
 
Mh!, ama kweli siasa ni sihasa. Hebu tupe report ya CAG inayomuweka wazi Sitta.

Hili la Sitta kuwa mjanja nakubaliana na wewe, hata kama ungekuwa wewe ungekuwa kwenye position yake. Nafasi yake kama spika ni kubwa sana hivyo sometimes anatakiwa sio tu kuwa, bali kuonekana anatetea chama chake na serikali yake. Yaani issue ya partisan huwezi kuikwepa. Ila kuna watu miongoni mwa chama chake hawamtaki kwa kuwa hakuwalinda katika kashfa zao kujadiliwa japo nguvu kubwa zilitumika na watu hao hao kumuweka.
 
Tatizo si wananchi, tatizo ni Katiba ambayo haitoi nafasi ya kuwa na tume huru ya uchaguzi, wabunge wa CCM na CCM kwa ujumla hawachaguliwi na wananchi bali wanatangazwa na tume ya uchaguzi kuwa ni washindi regardless matokeo halisi ya kura.

Tunaposema wananchi wanaichagua CCM tunawapa CCM legitimacy ya kuendeleza michezo yao michafu. Kama itapatikana tume huru, wabunge wa CCM hawatazidi hata nusu.

Specifically ni kipengele gani cha katiba unachokizungumzia....
 
Watanzania hatuna imani kabisa na Spika maana maamuzi yake mengi ni kuikingia kifua Serikali Bungeni kila inapokuwa katika hali ngumu. Amefanya hivyo kwenye mijadala mbali mbali ikiwemo ya Vitambulisho vya Taifa, Richmond, Meremeta n.k. Na huu usanii wa "Tuna imani na Spika na Katibu wa Bunge" nani kautunga!? Spika, Katibu wa Bunge au wote ili kuteea ulaji wao!? Kweli nchi yetu kuna usanii wa hali ya juu.

Hahahaaaa! wana JF mnatuchanganya! akiwabana mafisadi mnasema hatendi haki, akifanya hivi mnasema natetea serikali sasa mnataka lipi? Au na wewe unafanya TANZANIA DAIMA ambapo mmeamua kuwatetea fisadis.
 
Spika huyu huyu kashafanya blunders nyingi hapo bungeni.mnaweza kurejea barua ya Mheshimiwa Adam Malima kumpinga spika ipo humu humu JF.

Mh.Shelukindo ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya bunge ameshangazwa kuona mhasibu mkuu wa bunge hana sifa za uhasibu ikiwemo CPA.

SHERIA ya uhasibu inasema kila mahala penye shilingi milioni 20 mhasibu wake awe na elimu ya uhasibu ngazi ya CPA.bunge lina mabilioni ya mapesa anayeshikilia mapesa hayo hana sifa za uhasibu.umakini wa spika uko wapi?

Katibu wa bunge Thomas Kashilillah akishirikiana na Raphael Nombo wameajiri watu wasio na sifa za kuajiriwa.TENA WOTE ni wahitimu wa chuo kimoja,intake moja.

mkuu Kanda 2, wanadai eti wana sifa maana ni wakereketwa na makada wa chama ccm
 
Back
Top Bottom