Sitta avusha mipaka moto wa ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta avusha mipaka moto wa ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Sep 30, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  MADA ya rushwa na ufisadi ambayo imekuwa ikivuma nchini kwa muda sasa itakuwa miongoni mwa agenda ya za Mkutano wa 55 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA) unaoendelea mjini Arusha.

  Rais wa CPA, Bw. Samwel Sitta ambaye amekuwa kinara wa mapambano dhidi ya ufisadi nchini, aliyasema hayo jana wakati akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu mada zitakazojadiliwa katika mkutano huo utakaofunguliwa na Rais Jakaya Kikwete.

  Bw. Sitta aliuelezea mkutano huo utakaotumia sh bilioni tatu kuwa ni wa mafanikio makubwa, ukijumuisha wabunge kutoka nchi mbalimbali duniani, 800 wakiwa tayari wamewasili mjini Arusha.

  Rais Kikwete atawasili mjini humo kesho akitokea Washngton DC, Marekani alikokwenda kwa ajili ya uzinduzi wa ubalozi mpya wa Tanzania nchini humo na kuhudhuri Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

  "Katika mkutano huu maspika 38 na manaibu spika 17 wataudhuria huku kaulimbiu ikiwa ni "Kukabiliana na Changamoto mbalimbali wakati ujao," alisema.

  Mada nyingine zitakazojadiliwa katika mkutano huo kuwa ni Jinsi mtindo wa serikali za mseto zinavyoviza demokrasia, Nchi zifanye nini kukabili mtikisiko wa uchumi duniani na Jukumu la wabunge kupambana na uhalifu wa kisiasa.

  "Ufisadi na rushwa vitajadiliwa katika mkutano huo kwa sababu inawezekana mtikisiko wa uchumi unaweza ukatokana na rushwa na kwamba ndio maana wabunge wa Tanzania wamekuwa wakichukia sana rushwa," alisema Sitta.

  Kwa mujibu wa Sitta, kwa mwaka jana Tanzania ilipoteza karibu dola bilioni 20 zilizotokana na mikataba mibovu na ufisadi na kwamba mikataba hiyo isipothibitiwa vizazi vijavyo vitapata shida ya kulipa madeni wakati waliokuwa wanafaidi wamefariki dunia.

  Bw. Sitta alitaja mada nyingine zitakazojadiliwa kuwa ni mabadiliko ya hali ya hewa inayotokana na vitendo vya uchafuzi wa mazingira unaotokana na wanadamu pamoja na kutazama sababu zipi zinazoleta migongano ndani ya jamii kama vile vita katika nchi za Afrika zinazosababisha vifo vya watu wasiokuwa na hatia.

  "Mada zote hizi zitajadiliwa mara baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano huu Oktoba 2 hadi mwisho wa mkutano huu na Oktoba 3 utawatembeza wajumbe wetu katika maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii kama vile Mlima Kilimanjaro na wale wenye uwezo watapanda mita 1000 wengine watakwenda mbuga za wanyama Ngorongoro,Serengeti, Tarangire na Zanzibar."alisema.

  Bw. Sitta alisema kuwa pamoja na Tanzania kuuandaa mkutano huo kwa gharama kubwa ya sh. Bilioni 3, fedha hizo zote zitarejea kutokana na kila mshiriki kulipia gharama ya mkutano huo.

  Wakati huo huo Bw. Sitta alisema kuwa nchi ya Rwanda iliomba kushirikishwa katika Jumuiya hiyo, ambapo ombi lao litajadiliwa katika kamati ya sekretarieti leo na kwamba ana imani kuwa ombi lao litakubaliwa.
   
 2. Ndanda to Lomwe

  Ndanda to Lomwe Member

  #2
  Sep 30, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chanja mbuga mzee wa kasi na viwango,tuko nyuma yako.Tunakusubiri November bungeni,lazima serikali ilete majibu ya hoja za wabunge usirudi nyuma.
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mzee wa viwango na speed tunakutakia kila la kheri katika kufanikisha mkutano wa jumuiya ya madola ila kumbuka tu kuwa baada ya hapo kazi ya RICHMONDULI inakungoja bungeni!! Pia kuna angalizo hili; USIMUAMINI makamba anaweza akakuchoma kisu cha mgongoni!!!
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  tutaona madhara ya kutikiswa na ccm kule dodoma ............akiwa strong hakika tutamuunga mkono,................
   
Loading...