Sitta atoboa siri nzito za Bunge la A. Mashariki, Mbunge katuuza

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
WAZIRI wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, ametoboa siri nzito, akidai kuwa mmoja wa wabunge wa jumuia hiyo, kutoka hapa nchini alitia saini mkataba wa mazingira ambao ni hatari kwa taifa, kiasi cha kumlazimu yeye kukimbilia kwa Rais Jakaya Kikwete kumzuia asiukubali.

Bila kumtaja mbunge huyo, Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo, alidai kuwa mbunge huyo wa Afrika Mashariki alikubali kusaini muswada wa sheria ya mazingira (Transboundary Equal System), unaozitaka nchi wanachama kulifanya suala la mazingira lisimamiwe na jumuiya jambo ambalo ni hatari kwa taifa.

Sitta alitoboa jambo hilo jana jijini Dar es Salaam katika semina elekezi kwa wabunge hao, na kudai kuwa baadhi ya nchi wanachama wanacheza mchezo mchafu, ambao usipoangaliwa kwa makini unaweza kuleta matatizo hapa nchini.

“Ukisema suala la mazingira lisimamiwe na jumuia ina maana suala la ardhi ni lazima liingizwe katika jumuia yetu jambo ambalo linaweza kusababisha athari katika nchi,” alisema.

Waziri Sitta alisema kutokana na kutishwa kwa hatua ya mbunge huyo imemlazimu kuwasiliana na kumshauri Rais Kikwete ili asikubali kuupokea na kuusaini.

Aliwaonya wabunge wateule wa Bunge la Afrika Mashariki kuwa makini katika maamuzi mbalimbali yanayohusu taifa kutokana na baadhi ya nchi za jumuiya hiyo kutumia ujanja hasa katika suala la ardhi.

Aliitaja nchi moja (jina linahifadhiwa) kuwa inajaribu kwa kila njia kuhakikisha ardhi inaingizwa katika jumuia kutokana na Tanzania kuwa na ardhi kubwa kuliko nchi nyingine za jumuiya hiyo.

Hata hivyo Sitta aliwataka wabunge hao kuhakikisha wanaweka mbele vipaumbele vya taifa ikiwa ni pamoja na kilimo cha uzalishaji ili kuifanya Tanzania kuwa ghala la chakula na biashara kwa nchi za Afrika Mashariki.

“Kuna mchezo unaoendelea ambapo wenzetu (anawataja) wananunua mahindi yetu na kuyasindika huku wakiyaweka katika mifuko ya sembe na kwenda kuyauza nchi ya Sudan Kusini.”

“Niwaombe wafanyabiashara wa hapa nchini wajaribu kuweka kinu cha kusindika mazao maana masoko yapo mengi ya uhakika,” alisisitiza.

Naye, Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda, alisema kuwa kwa sasa watakuwa na kamati maalumu ya kushughulikia masuala ya Afrika Mashariki kutokana na kuweka ushirikiano baina ya ofisi yake na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki baada ya kuunda kikosi kazi ili kuangalia namna ya kuimarisha uhusiano na wabunge wa EALA.

“Ushirikiano huo utaondoa baadhi ya kasoro zilizojitokeza za kukosa taarifa za mwaka zinazofanywa katika Bunge hilo, kutokuwepo kwa nyaraka za majadiliano,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa EALA, Adam Kimbisa, alisema kuwa watajitahidi kuangalia lipi halali na haramu huku wakitumia akili zao kuepuka kutumiwa na baadhi ya nchi katika Bunge hilo.

My concern;
Naona wanunge hawa wanafuata posho na kuuza sura kinachozungumzwa na kuchangiwa hawakijui mwisho wa siku wanaanguka sahihi
 
pamoja na mapungufu yake Sita ni mtu makini sana,na ni kiongozi....

Izi ishu Jumuiya ya East afrca ningekuwa na uwezo ningezitupilia mbali.
 
Vizuri sana aanzie kwa Makongoro Nyerere anayetaka kusaini Mkataba wa kukubali Ardhi ya Tanzania iwe pamoja na East Afrika kwahiyo Wananchi wa East Africa wanaweza kununua Ardhi Tanganyika

Ni lazima asimamishwe huyo kama wangejua asingepewa Kura kabisa
 
Mimi niliangalia Bungeni siku ile ya Uchaguzi wa Wabunge wa EALA. Wote waliojieleza kuomba kura hakuna hata mmoja aliyeonyesha kuwa ANA UWEZO WA KUTUWAKILISHA KWENYE BUNGE HILO. Wote ni wababaishaji tu na hasa toka Chama hichi cha Magamba. Hivi kama mtu hawezi kujieleza kwa Kiingereza fasaha unategemea ATAZUNGUMZA AU KUCHANGIA NINI AKIFIKA HUKO EALA? EXPECT ALL THESE GUYS TO STAY DUMB FOR 5 YEARS!Watu wasubiri madudu toka EALA katika miaka 5 ijayo. Hakuna kitu pale!
 
Acha fitina zako, Makongoro Nyerere alisema hayo lini..?°
 
Hawa Wabunge wetu katika EALA inatakiwa wajibu maswali yafuatayo:
(1) Watanzania tunataka nini kutoka Jumuia?
(2) Kwa nini Jumuia ya mwanzo ilivunjika mwaka 1977?
(3) Je Watanzania wako tayari kiasi gani kuingia katika Jumuia hiki?

(4) Ni mambo yapi yawe chini ya EAC? Haya mambo lazima yafanyiwe kura ya maoni (referendum).
 
Jana alisisitizia sana suala la ardhi,,,,hataki waafrika wenzetu wapewe ardhi lakini WAZUNGU WANAWAPA NA WAARABU WA DUBAI,,,,si wehu huu
 
nadhani wanatakitwa wapewe kitchen party ya usalama wa taifa kabisa ndio wende huko siuo wanafikila kuuza sura tu
 
Vizuri sana aanzie kwa Makongoro Nyerere anayetaka kusaini Mkataba wa kukubali Ardhi ya Tanzania iwe pamoja na East Afrika kwahiyo Wananchi wa East Africa wanaweza kununua Ardhi Tanganyika

Ni lazima asimamishwe huyo kama wangejua asingepewa Kura kabisa

mkuu hebu msikilize makongoro nyerere kisha uniambie kama umemuelewa au la juu ya swala la ardhi
gonga link hii hapa chini

CHARLES MAKONGORO NYERERE (BUNGENI) - YouTube
 
pamoja na mapungufu yake Sita ni mtu makini sana,na ni kiongozi....

Izi ishu Jumuiya ya East afrca ningekuwa na uwezo ningezitupilia mbali.


hana umakini ni mbeya na anapenda sifa....hana lolote jizi tu nalo..huyu si ndo alipeleka marisiti ya 3m eti kanunua mavidonge namanga pharmacy..ovyooooo
 
Jamani, si mliona aina ya wagombea wenyewe....yule wa TLP na wengine wa vyama vingine vya kisiasa....wengi wao sijui kama wanajua wanachoomba kwenda kukifanya
 
Transboundary Equal System ama Eco system? Hivi Mbunge Mmoja akisaini ndio mkabata unakuwa halali na kuifunganisha Tanzania?

Kuna mtu alishatuambia humu kwamba Wabunge wa nchi zingine wanalipwa na serikali zao on top of what they get from EAC. Akasema wanaweza kuzitumia kuwarubuni wabunge toka Tanzania! Inaonekana huyo Mbunge alirubuniwa kwa hongo.
 
Vizuri sana aanzie kwa Makongoro Nyerere anayetaka kusaini Mkataba wa kukubali Ardhi ya Tanzania iwe pamoja na East Afrika kwahiyo Wananchi wa East Africa wanaweza kununua Ardhi Tanganyika

Ni lazima asimamishwe huyo kama wangejua asingepewa Kura kabisa


Suala la aridhi yetu haliwezi kuamuliwa na sahihi za watu tisa, siku wakijichanganya wakasaini mkataba kama huo ndo watatujua.
 
Suala la aridhi yetu haliwezi kuamuliwa na sahihi za watu tisa, siku wakijichanganya wakasaini mkataba kama huo ndo watatujua.

sasa hawa walioigawa ardhi kwa makaburu tumewafanyaje???Like a faza like a sun
 
hana umakini ni mbeya na anapenda sifa....hana lolote jizi tu nalo..huyu si ndo alipeleka marisiti ya 3m eti kanunua mavidonge namanga pharmacy..ovyooooo

si bora sita ananunua vidonge na risiti mnaziona na kodi vimelipiwa. Kuliko wanaoenda kupima mafua india kwa mipesa kibao ya walipa kodi.!
 
Back
Top Bottom