Sitta asoma alama za nyakati,atangaza kustaafu siasa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta asoma alama za nyakati,atangaza kustaafu siasa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Oct 1, 2010.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Thursday, 30 September 2010 19:54

  [​IMG]

  Aliyekuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta

  Ibrahim Bakari, Urambo

  SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta amesema wakati umefika kwa yeye kustaafu siasa. Sitta, ambaye alisifika kwa kuliongoza Bunge lililohoji na kuibua kashfa mbalimbali dhidi ya serikali, anaungana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambaye pia alitangaza kuwa ataachana na siasa ifikapo mwaka 2015.

  Sitta alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Soka wa Urambo mjini Tabora, ikiwa ni muda mfupi kabla ya kumkaribishwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete
  kuzungumza na wananchi.

  "Mimi ndiye Samuel Sitta chuma cha pua; nataka kustaafu siasa, lakini kwa kura za kutosha... kura za kishindo, lakini nisingependa kupata kura nyingi, zisizidi za rais," alisema Sitta bila kueleza sababu za kuchukua uamuzi huofafanua zaidi kinachomfanya kutaka kufanya hivyo.

  Sitta, 68, anayetetea kiti chake cha ubunge wa Jimbo la Urambo Mashariki alishika kiti hicho cha uspika kwa mara ya kwanza mwaka 2005.

  Akizungumza kwenye mkutano huo uliofurika mashabiki wa CCM, Sitta alimtaka Kikwete atakapoingia madarakani, lalamiko lake la kwanza ni ikulu kuhakikisha jimbo la Urambo Mashariki linakuwa la kwanza kupata maji.
  Sitta, ambaye mwaka 2015 atakuwa na umri wa miaka 73, amekuwa kwenye utumishi wa umma kwa muda mrefu kuanzia miaka ya themanini, akiwa amefanya kazi mbalimbali kuanzia katibu wa mkoa wa CCM hadi mjumbe wa halmashauri kuu, na pia amewashi kuwa waziri na pia kuwa mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (IPC).

  Akizungumzia tumbaku mkoani humo, Sitta alisema kuwa serikali imesimama kikamilifu kuhakikisha bei ya zao hilo inasimama, na kusema mwaka 2005 kilo moja ya tumbaku ilinunuliwa kwa Sh850 lakini sasa inauzwa hadi Sh4,000.

  Sitta alisema kwa kuwa mkoa wa Tabora ni maarufu kwa kilimo cha tumbaku, msimu ujao watakapopatiwa pembejeo na zana za kilimo, wanaweza kuzalisha tumbaku kilo milioni 24 zinazoweza kuingizia taifa Sh84bilioni.
  Hata hivyo, alilalamikia ukosefu wa wakunga na wataalamu wa afya na dawa katika hospitali, zahanati na vituo vya afya, walimu, maabara za kisasa na barabara.

  Naye Kikwete aliwasifu wancnhi wa Urambo kwa kujitokeza.
  "Ningekuta watu wachache ningekonda, lakini mmejaa; sasa nimenenepa," alisema "Kama Rais, nitahakikisha napambana na wote wanaogoma kupangiwa kazi.

  "Wanaomba kusoma wakitokea Urambo, tunawakubalia tukiamini kuwa watarudi Urambo; wanapomaliza, tunawapangia kazi wanakataa, sasa tutaangalia uwezekano wa kuwabana."

  Kikwete alisema pia kuwa kazi kubwa iliyopo na ambayo ni changamoto kwa serikali ni kuhakikisha kuwa vyote vinakamilishwa kwa wakati ikiwemo ujenzi wa barabara, upatikanaji wa maji kwa kuangalia misaada ya serikali ya Japan na wahisani wengi.

  "Hivi sasa naumiza kichwa, nasaka wahisani wa kutujengea barabara ya Manyoni-Kigoma ya kilomita 700, hii ni kubwa kweli. Wahisani tutakaowapata, tutawapa vipande lakini hadi vikamilike katika kiwango cha lami," alisema Kikwete aliyewataka wananchi wa Urambo kutomwangusha Sitta.
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Yale mawazo yake ya kugombea uraisi nndo yamepotea duu. lakini kweli Majimboni saizi vijana wameingia huko hutaki kutoka kwa Heshima, unalazimiswa kama mzee wangu MALECELA
   
 3. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,994
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Wamejifunza mengi kutoka Bumbuli na kwingineko.Zile zama za kijana hawezi kumwondoa mzee zimepitwa.Ni heri kusfaafu kuliko fedheha.
   
 4. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Simwamini!! Kama ni kwili angeachia mwaka huu.......!! Anataka kura za huruma huyu!!!!
   
 5. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Angeachia sasa kama wenzake wale wa Sumbawanga - kingeeleweka.
   
Loading...