Sitta ‘amshushua’ waziri mwenzake kutokana na kukwepa kujibu swali la Mbunge Zitto Kabwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta ‘amshushua’ waziri mwenzake kutokana na kukwepa kujibu swali la Mbunge Zitto Kabwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 17, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145  na Tamali Vullu, Dodoma
  WAZIRI wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amemuumbua Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga, kutokana na kukwepa kujibu swali la mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA).


  Sitta ambaye jana alikuwa Kaimu Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, alilazimika kuingilia kati kutoa majibu ya ufafanuzi baada ya Naibu Waziri huyo kutomridhisha muuliza swali.


  Katika swali lake, Zitto alihoji inakuwaje kampuni ya simu za mikononi ya Tigo kuendeshwa kwa asilimia 100 na wawekezaji wa nje wakati sheria hairuhusu na kusema kuwa hisa za serikali zilizokuwapo awali ziliuzwa kinyemela.

  “Kabla ya hapo Watanzania walikuwa na hisa, lakini ziliuzwa kinyemela mwaka 2005 siku chache baada ya Rais kuapishwa.


  “Kwa nini serikali imeruhusu kampuni ya Tigo kuendelea kufanya kazi wakati imekiuka sheria kwa kumilikiwa asilimia 100 na wageni na kwa nini kampuni za simu haziorodheshwi kwenye soko la hisa na hazilipi kodi?” alihoji Zitto.


  Akijibu swali hilo, Naibu Waziri, Kitwanga, alimtaka Zitto kuisoma upya sheria ya EPOCA na kanuni zake.


  Alisema kampuni zote haziwezi kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa kuwa kuna taratibu zake.


  Hatua hiyo ilimwinua Waziri Sitta, ambaye alisema ni muhimu serikali kufanya mambo kwa uwazi, ili kuondoa malalamiko kwa wananchi.


  “Haya mambo yanayosemwa na wenzetu yawezekana ndani yake kuna ukweli. Ni muhimu serikali kufanya mambo kwa uwazi,” alisema.


  Alisema kutokana na hali hiyo, suala la kampuni ya simu za mikononi ya Tigo kuendeshwa kwa asilimia 100 na wawekezaji wa nje, serikali italifuatilia na kutoa taarifa.


  Awali katika swali lake la msingi, mbunge wa Mpanda Mjini, Saidi Arfi (CHADEMA), alihoji inakuwaje Tigo imilikiwe na watu wa nje kwa asilimia 100.


  Alihoji kwa nini hisa za kampuni ya Zain hazikupelekwa DSE na kuuzwa kwa Watanzania na badala yake zikauzwa kwa kampuni ya Airtel kinyume na sheria inayotaka hisa hizo ziuzwe kupitia soko la hisa.


  Akijibu swali hilo, Kitwanga alisema hisa za serikali asilimia 40 katika kampuni ya Zain Tanzania ambayo sasa inaitwa Airtel hazijabadilika.


  Alisema kampuni ya Bharti haikununua hisa za serikali bali ilinunua hisa za kampuni mama ya Celtel Tanzania BV ambayo ni mwanahisa mwenza wa serikali katika Zain.


  Hata hivyo, alisema wakati utakapowadia kwa serikaili ya Tanzania kuuza hisa zake kwa wananchi, utaratibu utawekwa kulingana na sheria, kanuni na taratibu zilizopo ili kuwapatia fursa wananchi kununua hisa hizo au hata nyingine zitakazokuwapo.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Uvivu wa baadhi ya Mawaziri; na kama hivyo Mimi ni JK Kikwete hauna Uwaziri tena hasa katika saula nyeti la hisa
   
 3. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Zitto naye huyu dogo huwa ni kichwa sana´
  kwa hili hongera sana kaka.
  SOLIDARITY FOREVER
  TOLERANCE GIVES POWER.
   
 4. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  anajipendekeza tu huyo, si alisema wapinzani wamekaa kinafikinafiki
   
 5. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Naibu Hata mimi nilimuona huyo Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga yaani aliboa mbaya in short I am not sure kama alikua anajua anajibu nini yaani tunaibiwa yeye anakazana anatetea mpaka povu linamtoka mdomoni
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tatizo la Zitto akiikomalia sana iyo issue jamaa wa Tigo wakija muweka sawa kimyaaaaaaaaaaaaa
  Mfano ni issue ya madini chaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 7. Gwandalized

  Gwandalized JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  in zitto we Trust
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hayo unayosema ni kweli ; sasa tutaona kama atafuatilia ile issue ya kiwanja ambacho Mkullo aliuza kwa METL kinyemela bila kufuata utaratibu kwani yeye ndio aliibua suala hilo na CAG amedhihilisha kuwa ni kweli Mkullo aliuza kiwanja bila kufuata utaratibu!! METL wakimlambisha asali kidogo hutamsikia akipiga kelele tena kuhusu suala la kiwanja hicho.
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  You and your wife!
   
 10. Judi wa Kishua

  Judi wa Kishua JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 525
  Trophy Points: 180
  all tanzanians..
   
 11. b

  bakenyile Member

  #11
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  toghocho Sitta hawezi kujipendekeza ila wewe na wenzio wengi mmekosa fadhira kwa huyu shujaa, ndio maana saa ya kuikomboa nchi ilipo fika wote mlinunuliwa mkawa mnapiga maandishi tu hapa ya kinafiki. Watanzania wazalendo ebu tujiulize kwenye issue ya Richmond ni kitu gani tulicho kifanya kuonyesha kuwa tunaunga mkono kupambana na lile suala? Hakuna aliyeenda barabarani hata kuonyesha kwamba wameibiwa badala yake mkawa wa kwanza kukebehi. Acheni kuzungumzia vyama tuwe wazalendo tuzungumzie utanzania. Mtu akifanya kitu kwa masilahi y
  a nchi hatakama ametokea CCM mpe haki yake kwakuwa wote lengo ni kuona Tanzania yenye maendeleo vyama ni njia tu ya kupitia.
   
 12. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo sina la kusema tena.
   
 13. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  sasa mbona mkuu unatukosea adabu hivyo...?!
  Inakuwaje una-generalize mambo mkuu?
  Hiyo ni dhambi mbaya sana na unapaswa utubu kabla ya bwana wa mabwana hajarudi.
   
 14. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Yaan Kama ingewezeka Pinda andelee kusafiri ili Sitta ashikilie hicho kiti uwa anawapa kubwa sana hawa wavivu wa kufikiri.
  Lile swali alilouliza Kamanda mbowe kuhusu mawazi kutumia nafasi zao kuwatisha wananchi kwenye kampeni ungesikia mambo zake.
   
 15. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #15
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  serikali ya TANZANIA inachekesha sana,hivi hawaoni mifano ya nchi nyingine?

  1.China Mobile Limited (simplified Chinese: 中国移动通信; traditional Chinese: 中國移動通信; pinyin: Zhōngguó Yídòng Tōngxìn) is a Chinese state-owned telecommunication company that provides mobile voice and multimedia services[SUP]][/SUP] through its nationwide mobile telecommunications network–the largest of its kind, worldwide. The company also wins global pride of place as the largest mobile telecommunications company by market capitalization. It is listed on both the NYSE and the Hong Kong stock exchange.As of January 2012, China Mobile is the world's largest mobile phone operator with about 655 million subscribers.

  2.China Unicom was founded as a Government-owned corporation, established on July 19, 1994, by the Ministry of Information Industry and approved by theState Council.


  hivi hii nchi inamiliki kitu gani sasa?

  wanyama wanakwenda,madini yanakwenda,ardhi hiyoo,bandari hiyoo,viwanda kwisha

  uchumi wetu utakuaje kama serikali haimiliki njia kuu za uchumi?
   
 16. broken ages

  broken ages Senior Member

  #16
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 160
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Swali lianakuwa gumu kujibu kwa sababu jibu halikuandaliwa WAla haikutegemewa kugundulika wakati waliposaini mkataba ndipo Ulipofanyika ujanjaujanja wa watu wachache kufaidi kwa kusaini mikataba isiyokuwa na manufaa kwa watanzania wote kuwaona wenzao ndani ya nch ni mbumbumbu wasioelewa si rahisi kugundua ya kuwa jasho Lao linaliwa na wachache waliowapa dhamana ya kuwaongoza.kumbe wanapokujaulizwa maswali ndipo wanapata kigugumizi na hata wakati mwingine kujibu kwa jaziba.
   
Loading...