Sitta ampa changamoto Makinda

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Sitta ampa changamoto Makinda Send to a friend Saturday, 13 November 2010 00:30 0diggsdigg

anamakindampya.jpg
Spika mpya wa Bunge, Anna Makinda akiongozwa na Askari wa bunge kuingia bungeni mjini Dodoma jana baada ya kuchaguliwa na wabunge wengi kushika wadhifa huo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Habel Chidawali na Boniface Meena, Dodoma
BAADA ya wabunge kumchagua kwa kishindo Anna Makinda kuwa Spika wa Bunge la kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyekuwa Spika wa Bunge la tisa, Samuel Sitta amemtaka kuwa makini kwa kuhakikisha kwamba, chombo hicho cha kutunga sheria hakipotezi mwelekeo kutoka mahali kilipofikia kidemokrasia.

Makinda ambaye ni mbunge wa Njombe Kusini, alichaguliwa jana kwa kura 265 ambazo ni sawa na asilimia 74.2 ya kura zote zilizopigwa (327), huku mpinzani wake Mabere Marando akiambuliwa 53 (asilimia 16.2) na kura tisa ziliharibika.

Baada ya matokeo hayo, Spika Makinda aliwashukuru wabunge kwa kumchagua kwa kura nyingi ambazo alisema anaamini zimeonyesha kuwa wabunge wengi wamemkubali. Aliahidi kuwa atafanya kazi ya uspika kwa kuzingatia misingi na kanuni za bunge.

“Nitajitahidi kuzielewa kanuni za bunge pamoja na ninyi waheshimiwa wabunge, hivyo naomba mzisome na kuzielewa vema sheria za Bunge letu tukufu ili kusiwe na mgongano wa kimaslahi,” alisema Makinda.

Spika huyo alisema atajitahidi kulifanya bunge liwe moja, bora, imara na liwe la watu wote kwa kuanzisha utaratibu wa vipindi katika vyombo vya habari ikiwemo radio ambavyo vitawawezesha wananchi kuzielewa kanuni za Bunge.

Aliwaonya wabunge kwamba hatakiwi kupeleka ndani ya bungeni hoja zenye maslahi binafsi au kwa kutumiwa na mtu au vikundi vya watu na kusisitiza kuwa wapeleke bungeni hoja zinazotoka katika majimboni yao.

"Kitakachozingatiwa humu bungeni ni sheria, kanuni na taratibu hatuwezi kuingiza bungeni mambo yanayobeba maslahi ya watu fulani au vikundi, hivyo msome na mzielewe kanuni za Bunge," alisisistiza.

Akitoa mchango wake kuhusiana na kuchaguliwa kwa Makinda, Sitta ambaye alijizolea umaarufu kwa kuliongoza Bunge lililopata umaarufu kutokana na kuruhusu mijadala ya wazi, alimtaka spika huyo kutoyumbishwa katika kipindi chote cha uongozi wake.

Alibainisha kuwa hivi sasa wananchi wameelevu zaidi kwani wanafuatilia kwa umakini masuala ya Bunge, hivyo wanahitaji kuona vitu vizuri na haki ikitendeka ndani ya chombo hichi. Alishauri kuwa viwango na msimamo waliokuwa wameufikia katika Bunge la Tisa unafaa kuendelezwa.

Sitta alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nje ya Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Alisema hana shaka na uwezo wa Makinda, lakini alibainisha kuwa Bunge la Kumi lina changamoto kubwa kuliko mabunge yote yaliyotangulia katika historia ya Tanzania.

“Mimi nadhani ataweza kumudu vema kazi hiyo, ila ninamtahadharisha kuwa asiwe na msimamo wa kuyumbishwa na wala asiwe na upendeleo na ikibidi, afuate nyayo zangu naamini kuwa bunge litakuwa na heshima kubwa,” alisema Sitta.

Mbunge huyo wa Urambo Mashariki alisema Bunge la Kumi lina wasomi wengi ambao wengi wao ni vijana na hivyo ni bunge bora kuliko yaliyotangulia.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo litakuwa na mijadala mizito yenye changamoto nyingi linalomlazimu Makinda kuwa makini zaidi katika majukumu yake.
Akizungnza kwenye ukumbi wa Spika baada ya kuanza rasmi kazi hiyo, Makinda alisema hatatumia nafasi hiyo kumsafisha mtu yeyote anayetaka kugombea urais kama watu wanavyodai.

Pia alisema kuwa hajawekwa kwenye uspika na mafisadi, ila alisimama mwenyewe kwa kuwa aliamua kugombea nafasi hiyo.

"Kuwa spika ni ratiba ya maisha yangu, ni kitu ambacho nilikuwa nakifikiria na mimi ni mtu wa kufuata taratibu. Kwanza sijui kama kuna mafisadi kwa kuwa fisadi ni mwanaume anayeiba mke wa mtu," alisema Makinda.

Kuhusu uendeshaji wake wa bunge alisema kuwa hatakubaliana na hoja za kukomoana bali atahitaji hoja zilizofanyiwa utafiti ili maamuzi yanapotolewa yaweze kuleta tija.

Alisema siasa si za kuzua maneno tu lazima hoja ziwe za kitafiti na ni lazima wabunge wawe na uwezo wa kuibua mambo ili kazi iwe nzito.

"Nasikitika kuwa bunge lililopita lilikuwa na hoja nzito moja tu ya Richmond, zilitakiwa ziwe zaidi ya kumi kama hizo ili bunge liwe na nguvu zaidi,"alisema Spika huyo ambaye katika bunge lililopita alikuwa Naibu Spika akimsaidia Sitta.

Makinda alisema katika bunge hili atatoa kipaumbele kwa huduma za wabunge na wafanyakazi wa bunge kuwa bora zaidi na kutoa elimu kwa wabunge iliwaweze kuzielewa kanuni vizuri
 
Sitta ampa changamoto Makinda Send to a friend Saturday, 13 November 2010 00:30 0diggsdigg

.......Akizungumza kwenye ukumbi wa Spika baada ya kuanza rasmi kazi hiyo, Makinda alisema hatatumia nafasi hiyo kumsafisha mtu yeyote anayetaka kugombea urais kama watu wanavyodai.

Pia alisema kuwa hajawekwa kwenye uspika na mafisadi, ila alisimama mwenyewe kwa kuwa aliamua kugombea nafasi hiyo.

"Kuwa spika ni ratiba ya maisha yangu, ni kitu ambacho nilikuwa nakifikiria na mimi ni mtu wa kufuata taratibu. Kwanza sijui kama kuna mafisadi kwa kuwa fisadi ni mwanaume anayeiba mke wa mtu,"
alisema Makinda.Makinda alisema katika bunge hili atatoa kipaumbele kwa huduma za wabunge na wafanyakazi wa bunge kuwa bora zaidi na kutoa elimu kwa wabunge iliwaweze kuzielewa kanuni vizuri

Yale waliyokuwa wakisema ya Spika Mwanamke ndio yameanza hivyoo...

Anyway Hongera Spika Makinda:smile-big:
 
"Aliwaonya wabunge kwamba hatakiwi kupeleka ndani ya bungeni hoja zenye maslahi binafsi au kwa kutumiwa na mtu au vikundi vya watu na kusisitiza kuwa wapeleke bungeni hoja zinazotoka katika majimboni yao."

NAFIKIRI KWA KUWA BUNGE NI NATIONAL ASSEMBLY WABUNGE HAWAPASWI KUWA LIMITED KWA MASWALA YA MAJIMBONI PEKEE(KUWA LOCALIZED).KULAZIMIZA WABUNGE WAKOMAE TUU NA MASUALA HAYO YA MIFUKO MAJIMBONI KUTAVURUGA MAJUKUMU YAO MENGINE KWA TAIFA.HAPA WASIWASI WANGU NI KWA MFANO:

1. SUALA KAMA SAKATA LA RICHMOND HALINA JIMBO HATA MOJA LAKINI ATHARI ZAKE NI KWA TAIFA ZIMA. SOTE TUNAFAHAMU UMUHIMU WA NISHATI KTK UCHUMI KWA SEKTA MBALIBALI NA TAIFA KWA UJUMLA. TOKEA MAJUMBANI, MASHULENI,KTK VITUO VYA AFYA SHULE, VIWANDA NA TAASISI ANUAI AMBAZO ZINA MCHANGO MUHIMU KTK KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA WOTE .

2. SUALA LA WAWEKEZAJI KUTIRIRISHA MAJI TAKA YENYE SUMU TOKA MGODINI KWENYE MITO HUKO TARIME IJAPOKUWA LAWEZA KUONEKANA NI LA HUKO TU LINAMGUSA KILA MTANZANIA MOJA KWA MOJA AU LA. KWA KUWA TAIFA LETU NI MOJA LEO IMETOKEA MARA SIKU NYINGINE YAWEZA KUWA NJOMBE. NI MUHIMU KTK SUALA KAMA HILI WABUNGE WOTE WASHIRIKIANE KUHAKIKISHA SERIKALI INA TIMIZA WAJIBU WAKE WA KULINDA USALAMA WA RAIA KWA HALI NA MALI, KWA KUJALI MSLAHI YA RAIA NA SI VINGINEVYO.


WITO: WABUNGE WATUMIE VIZURI WKT WALIONAO. WAPIME MAMBO NA KUTOA UZITO STAHIKI KWA KILA CHANGAMOTO INAYOLIKABILI TAIFA HILI.
KUWAFANYA WABUNGE LOCALIZED WKT TUNATARAJI WAWE NATIONAL, LEARNING GLOBALY NI HATARI.

"Kitakachozingatiwa humu bungeni ni sheria, kanuni na taratibu hatuwezi kuingiza bungeni mambo yanayobeba maslahi ya watu fulani au vikundi, hivyo msome na mzielewe kanuni za Bunge," alisisistiza."

KATIBA YA NCHI NDIYO SHERIA MAMA YA NHCI HII, NDIYO INAYOLIPA BUNGE MAMLAKA YA UTENDAJI WAKE KUWA HURU KAMA MUHIMILI WA DOLA. KANUNI YEYOTE ILE IMBAYO INA ELEZA VINGINEVYO NI BATILI KWA MUJIBU WA KATIBA. MATUMAINI NI KUWA KANUNI ZIMETUNGWA KURAHISISHA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA BUNGE(4 SIMPLICITY'S SAKE) CAUTION "SIMPLICITY AND ELEGENCE ARE USEFUL CONCEPTS BUT BAD PRACTICE" WAHESHIMIWA WASISITE KUHOJI PINDI KANUNI ZINAPOTOA TAFSIRI NYINGINE TOFAUTI NA KATIBA, WAKUMBUKE(WOTE INCLUDING MAKINDA) WAMEAPA KUILINDA NA KUITETEA KATIBA.

Akitoa mchango wake kuhusiana na kuchaguliwa kwa Makinda, Sitta ambaye alijizolea umaarufu kwa kuliongoza Bunge lililopata umaarufu kutokana na kuruhusu mijadala ya wazi, alimtaka spika huyo kutoyumbishwa katika kipindi chote cha uongozi wake.
NANI WA KUMYUMBISHA NA KWA AJILI YA NINI? KWA MASLAHI YA NANI? NA KWA MUJIBU WA SHERIA IPI?
TAFAKARI!
"Alibainisha kuwa hivi sasa wananchi wameelevu zaidi kwani wanafuatilia kwa umakini masuala ya Bunge, hivyo wanahitaji kuona vitu vizuri na haki ikitendeka ndani ya chombo hichi. Alishauri kuwa viwango na msimamo waliokuwa wameufikia katika Bunge la Tisa unafaa kuendelezwa".

VIWANGO!!!
 
Back
Top Bottom