Sitta ajiingiza BoT
::Aitetea CCM dhidi ya ufisadi wa mabilioni
::Asema wahukumiwe waliokula, na si chama
::Aapa Bunge kutokuwa uwanja wa vibomu
na nathaniel limu, singida
SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, amesema ufisadi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni suala la mtu binafsi na kamwe lisitafsiriwe kuwa ni la Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Sitta ambaye ni mlezi wa CCM Mkoa wa Singida na Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), ametoa kauli hiyo wakati wa matembezi ya mshikamano na maadhimisho ya miaka 31 ya uhai wa chama hicho.
Akihutubia wananchi katika ukumbi wa CCM mjini Singida, alisema wapo viongozi wa upinzani ambao wanalihusisha suala la ufisadi BoT na chama tawala.
Alisema suala hilo lingekuwa sera ya CCM, isingekuwa rahisi kwa Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua ya haraka kwa watu wanaotuhumiwa kuhusika katika ufisadi huo.
Kutokana na hali hiyo, alisema wananchi hawana haja ya kuwa na wasiwasi kwa kuwa serikali ya awamu ya nne itaendelea kuwachukulia hatua sitahili watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo, bila kujali itikadi za vyama au nyadhifa zao.
Alisisitiza kuwa hatua hizo zitachukuliwa kulingana na taratibu, kanuni na sheria za nchi, na si kwa kufuata baadhi ya watu wanaotaka Bunge ligeuzwe kuwa sehemu ya kujibu alichoita vi-bomu au tuhuma zisizokuwa na miguu wala kichwa.
Alisema baadhi ya viongozi wa upinzani hutafuta umaarufu bandia bungeni.
Alisema lengo ni kuhakikisha kuwa kila suala linashughulikiwa kwa kutoa haki kwa kila upande, na si kuwakandamiza baadhi ya wasio na uwezo wa kwenda kujitetea bungeni.