Sitta ajiingiza BoT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta ajiingiza BoT

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by August, Jan 30, 2008.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2008
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  Sitta ajiingiza BoT
  ::Aitetea CCM dhidi ya ufisadi wa mabilioni
  ::Asema wahukumiwe waliokula, na si chama
  ::Aapa Bunge kutokuwa uwanja wa ‘vibomu’

  na nathaniel limu, singida

  SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, amesema ufisadi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni suala la mtu binafsi na kamwe lisitafsiriwe kuwa ni la Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Sitta ambaye ni mlezi wa CCM Mkoa wa Singida na Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), ametoa kauli hiyo wakati wa matembezi ya mshikamano na maadhimisho ya miaka 31 ya uhai wa chama hicho.

  Akihutubia wananchi katika ukumbi wa CCM mjini Singida, alisema wapo viongozi wa upinzani ambao wanalihusisha suala la ufisadi BoT na chama tawala.

  Alisema suala hilo lingekuwa sera ya CCM, isingekuwa rahisi kwa Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua ya haraka kwa watu wanaotuhumiwa kuhusika katika ufisadi huo.

  Kutokana na hali hiyo, alisema wananchi hawana haja ya kuwa na wasiwasi kwa kuwa serikali ya awamu ya nne itaendelea kuwachukulia hatua sitahili watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo, bila kujali itikadi za vyama au nyadhifa zao.

  Alisisitiza kuwa hatua hizo zitachukuliwa kulingana na taratibu, kanuni na sheria za nchi, na si kwa kufuata baadhi ya watu wanaotaka Bunge ligeuzwe kuwa sehemu ya kujibu alichoita “vi-bomu” au tuhuma zisizokuwa na miguu wala kichwa.

  Alisema baadhi ya viongozi wa upinzani hutafuta umaarufu bandia bungeni.

  Alisema lengo ni kuhakikisha kuwa kila suala linashughulikiwa kwa kutoa haki kwa kila upande, na si kuwakandamiza baadhi ya wasio na uwezo wa kwenda kujitetea bungeni.
   
 2. C

  Chuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  August..tunashkuru kwa taarifa...next time ni vyema kuwapunguzia kazi Ma-Mods...tuweke link sehem husika. Pia unavyoweka news weka source kama wewe ndio source onyesha ktk statement zako...
   
 3. K

  Koba JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  hivi hili lizee lina maana gani linaposema tuhuma zisizo na kichwa wala miguu na bunge sio sehemu ya vibomu,hili lizee lifisadi naona limejisahau na linafikiri lenyewe ni lifalme,bila kuiondoa mijizee kama hii tutaendelea kuwa maskini maana linafikiri Bunge ni nyumba yake binafsi..jinga sana hili(sorry kwa lugha mbovu lakini linaudhi sana)
   
 4. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2008
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,224
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Nampa pole sana Mzee Sitta, kwa kutetea sisiemu.
  Watendaji wa sirikali wakifanya mema, sisiemu juu! Wakivurunda, sisiemu haihusiki! Tumweleweje?
  Vioja kwa kwenda mbele.
   
 5. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wekeni kumbukumbu hayo maneno yake iko siku atayakana kama alivyokana skendo aliyoipeleka bungeni Dr. Slaa. Time will Tell ngoja Balali azungumze
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Sitta ana kichwa cha panzi . Yaani panzi anaweza kuwa anataka kuelekea Morogoro mizigo anapakia gari za Mombasa na yeye anapanda la Mtwara . Ndiyo Sitta .
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Sijui kuhusu mengine aliyosema Spika, lakini kwa haya juu ninamuunga mkono kuwa si CCm yote iliyokula hela hizo.
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Koba, nilikuwa nipo kwenye "not so good mood", lakini loooh, lugha uliyotumia imenifanya nimecheka saaaana. You can really work with words. Lugha uliyotumia sidhani kama ina matatizo yoyote, you have made my night!
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  ES un ataka kusemaje ?
  Unawezake kumtofautisha Rais JK akiwa Ziarani na Uenyekiti wake wa CCM . Chama ni ni nani na wali iba kwenye BOT wametumia nguvu gani ? Serikali iliyo madaraka ambayo imeiba ni ya Chama kipi . Unataka kusemaje hasa ? Hebu niweke sawa mzee wangu
   
 10. m

  mtambo Senior Member

  #10
  Jan 30, 2008
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 112
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyerere alikufa na CCM yake. Hawa wasanii ilibidi waunde chama chao na wakiite "Chama Cha Wasanii" tujue moja maana yanayotokea na yanayosemwa na hao wanajiita wana chama tawala mbona yanatisha?.

  Zee zima mvi mpaka kope za macho bado linaongea utumbo ambao hata mtoto wa miaka mitatu hawezi kuongea hivyo. Hao vigogo walichota mapesa yetu BOT ni kutoka chama gani?. Meremeta na Deep Green ni kampuni za nani kama si CCM?. Mizee kama hii inajiona miungu watu lakini muda wao umefika ni kuwachapa bakora za migogo mpaka warudishe mapesa yetu.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Jan 30, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,429
  Trophy Points: 280
  Mkuu waliooza CCM ni wengi mno! kiasi ambacho ni vigumu mno kuchagua yupi ni fisadi na yupi ni mwadilifu hata hao wachache waadilifu wamekaa kimya kabisa katika kuupigia kelele ufisadi basi na wao tunawaweka katika kundi hilo la mafisadi.
   
 12. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #12
  Jan 30, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu ES,

  Madhambi ya viongozi wakuu wa chama hata siku moja hayawezi kutenganishwa na chama.

  Nitakubali akisema hawawezi kuhukumiwa wanachama lakini kama viongozi wa chama wanavuruga ni lazima chama kilaumiwe. Pia ni chama hicho hicho ambacho kinatakiwa kuwa cha kwanza kuwachukulia hatua na kujisafisha.

  Watu kama Sitta inatakiwa wafike mahali na wakubali kulipa bunge makali ili kuweza kupambana na haya maovu ambayo kila siku yanajitokeza kwenye nchi zetu.
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Jan 30, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu Bubu,

  Unajua kuwa ninaheshimu sana hoja zako maana huwa zimetulia, na ninafahamu kuwa una one important skill ya siasa yaaani unaweza kusikiliza, mimi ni mwanachama wa CCM tena hai, lakini sijaiba hela ya serikali wala ya chama,

  Ninasema kuwa ni haki ya wananchi kukasirishwa na yanayoendelea kuhusiana na viongozi wabovu wachache, kama ripoti ya BOT inavyowasema, na kama ripoti ya Dr. Slaaa inavyowataja kwa majina pia, sasa hao wachukuliwe hatua za kisheria,

  Lakini kutuita wanachama wote wa CCM, wezi au mafisadi politically na katika any civilization, ni lugha nzito sana mkuu, maana Kenya sio wa-Kikuyu wote walioiba uchaguzi mkuu!
   
 14. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #14
  Jan 30, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  FME,

  Pmaoja na kujitetea kote, Leo hii jambo jema lolote litaitwa la CCM hata kama limefanywa na makamba peke yake. mfano muafaka wa maalimu sefu na Mangula uliitwa wa CCm na CUF.

  Iweje baya ni la wachache na zuri ni wengi? Tuachane na maswala ya Kenya tutakimbia mada
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Jan 30, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Bowbow,
  Naungana nawe ktk hili kwani tatizo limeanza na viongozi wa CCM wenyewe wanapotangaza mazuri kuwa ni ya CCM.
  Hata hilo la Amani na utulivu hupewa wao credits na sio wananchi wote.
  Mzee Es mzee wangu samahani leo hii tunatumia msemo wa Myahudi kuwa rafiki ya adui yako siku zote ni adui yako! nje ya hapo ni kujidanganya wenyewe kama wanavyofanya waarabu.
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Jan 30, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu Bow Wow,

  Heshima mbele, hivi kuna muafaka ulifanikiwa kati ya CUF na CCM?

  Mkuu nimekusikia maelezo yako, lakini bado hayatoshelezi kuwaita wana-CCM wote sisi ni mafisadi, kama vile ambavyo sio wananchi wote wa bongo walioipigia kura CCM, maana kama maana yake ni hiyo mnayoisema, basi wananchi wote bongo tuliiichagua CCM na kwa hiyo wananchi wote wa Tanzania ni mafisadi, au?
   
 17. K

  Kalamu JF-Expert Member

  #17
  Jan 30, 2008
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 874
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mungu awape nini wapinzani?

  Hizi ndio 'talking points' wanazotakiwa kuzikusanya na kuzifanyia kazi ipasavyo. Kazi ya wapinzani kuwaeleza wananchi wakiwa na vielelezo vilivyo wazi kama hivi inaweza kuwa rahisi sana kueleweka.

  Keep going Mr Sita, you are doing a commendable job indeed.
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Jan 30, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,429
  Trophy Points: 280
  Watu wenye msimamo kama wako ndani ya CCM ni wachache mno! Nakuvulia kofia kwa kuweka mbele maslahi ya Tanzania kabla ya yale ya CCM lakini kundi lenu ni kama tone moja la maji katika bahari. Hao wasio mafisadi wako wapi waikomboe CCM toka mikononi mwa mafisadi, wako wapi wawakemee viongozi wanaowakumbatia na kuwalinda mafisadi. Kama ndani ya CCM kungekuwa na watu wengi wenye msimamo kama wako, basi CCM ingekuwa safi kabisa mafisadi wangeiogopa CCM. Lakini ukweli ni kwamba mafisadi wote miaka ya karibuni wamekuwa wakikimbilia CCM ili na wao wakafanishe ufisadi wao na wewe unalijua hili. Samaki mmoja akioza....:)
   
 19. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #19
  Jan 30, 2008
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mkuu ES, Heshima yako mzee. Kweli najua sio wanachama wto ni mafisadi bali mko wachache safi ila nao wako kimya kabisa.

  Mnenikumbusha kila jambo jema basi CCM wanatakaga kujisiafia kuwa ni kazi yao hata kama linamhusu mtu binafsi.

  Nakumbuka Richard (ambaye sijui hata kama ana kadi ya chama) baada ya kushinda mashindano ya ngono (BBA). CCM na mijinguo yao ya kijani walijazana Airport kumpokea na Kiongozi wa CCM akasema nimatunda ya malezi mazuri ya CCM.

  Sasa linapokuja hili swala la ufisadi ambalo lina wagusa viongozi wakubwa tuu ndani ya chama wao wanasema ni mambo binafsi na hayahusiani na chama. Hizi si ndio double standard jamani? Nadhani mzee Sitta chama kingewawajibisha na ikiwezekana hata kiwanyang'anye kadi za uanachama na sio kuongea mambo ambayo naona ndio hayana kichwa wala miguu.
   
 20. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #20
  Jan 30, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Heshima mbele mzee, unasahau kuwa ukichafuka mguu wako huwezi kusema sio mimi, ni mguu wangu. Viungo vya mwili wako ni sehemu ya mwili wako. Same as watu walioingia kwenye nyadhifa za serikali kwa tikiti ya CCM, au walichota mapesa BOT kwa kutumia jina la deep green bado CCM inahusishwa moja kwa moja, hapo hawawezi kukwepa kwa njia yoyote, we should never lose track of that!
   
Loading...