Sitosita kukifuta chama chochote cha siasa - Tendwa & Ujio wa chama kipya cha PDM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitosita kukifuta chama chochote cha siasa - Tendwa & Ujio wa chama kipya cha PDM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Babuji, Mar 6, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Mar 6, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MSAJILI wa Vyama Vya Siasa John Tendwa amesema hatosita kukifuta chama chochote cha siasa ambacho kitaonekana kukosa wanachama wanaofikia 2,000 kama sheria ya usajili wa vyama vya siasa inavyotaka.

  Kauli hiyo ya masikitiko kwa baadhi ya vyama aliitoa wakati akizungumza na mwandishi wa Nifahamishe ikiwa ni baada ya kutoa cheti cha usajili wa muda kwa chama kipya cha kisiasa cha Peoples Democratic Movement (PDM) ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  Alisema sheria ya usajili wa vyama vya siasa inamruhusu Msajili kusajili vyama vingi kwa lengo la kukuza demokrasia lakini pia inampa mamlaka kukifuta chama ambacho kinakosa sifa.

  Msajili alisema sheria inakitaka chama kuwa na wanachama wasiopungua 2,000 kutoka mikoa 10 ya Tanzania ambapo nane ni Bara na miliwili kutoka Unguja na Pemba.

  "Nawahakikishia nyie PDM na vyama vingine kuwa kama hamtatimiza masharti ya kuwa na wanachama 2,000 katika mikoa 10 ya Tanzania sitosita kuwafuta," alisema.

  Msajili huyo wa vyama vya siasa nchini alisema kuwa kwa sasa ofisi yake ipo kwenye mchakato wa kutembelea mikoa ili kuangalia uhai wa vyama vya siasa nchini.

   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Uyo msajili keshakatiwa chake asibabaishe watu kuna vyama havina hata ofisi na bado vinausajili ,huyu ni fisadi au tuseme pandikizi mwengine anaetumiwa na Sultani CCM.
   
 3. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #3
  Mar 6, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  PDM - Nasikia ndio chama ambacho wabunge wa CCM wanapambana na ufisadi wataingia. A break away party from CCM.

  Lakini pia kulikuwa na maneno kuwa kina Lowasa wamesponsor kuanzisha chama ambacho aliyekuwa anafuatilia ni Julius Miselya.

  Tusubiri tuone.
   
 4. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  aisee, tusubiri tuone...
   
 5. M

  Mutu JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2009
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama habari ndio hiyo bomba ,ni vema hawa watu wakiwa hawashirikiani kuiba
   
 6. A

  Audax JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bara wajitenge,maana wakishajitenga watakuwa wanatusaidia kupata nyaraka kwa urahisi zaidi!!
   
 7. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Jamanie ebu tusaidieni kidogo: PDM kwa kiswahili kitaitwaje? Isijekuwa wanatengeneza chama cha kupunguza nguvu upinzani badala ya kupunguza nguvu za sultani?
   
 8. 3

  3 kids Member

  #8
  Mar 7, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sijui kama ni kweli lakini ngoja tuone kama ulivyosema......mmmhhhh!!!?????????
   
 9. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nakitakia mafanikio kama zaidi ya chama cha Mrema wa mwaka 1995
   
 10. K

  Kwaminchi Senior Member

  #10
  Mar 7, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nafikiri, sheria inataka chama kiwe na wanachama, at least 2,000 katika at least mikoa 10 pamoja na Unguja na Pemba. Sio ofisi.

  Hata TANU/CCM ilipoanza, ilifanya shughuli zake katika vyumba na nyumba za watu binafsi. Hawakuibuka na ofisi kila mahali.

  Wanaoanza tuwape nafasi ya kukaa, kusimama dede na kutembea. Kila la heri
  Pii-Dii-Emu. Hatujui ni nani atakayetutoa shimoni humu.
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mheshimiwa mbunge this is good news. Kama kweli yanatimia basi nachukulia habari hii kama ni begining of the end. Lakini isije kuwa ndio mafisadi wanataka kutumia trick ya Moi, kunakuwa na vyama vingi ambavyo vyote vinakuwa dhaifu na chama tawala kinaendelea kunufaika. Kwanini Chadema isifanye juhudi za kuwa accomodate wapinga ufisadi kutoka CCM na kuwa force kubwa zaidi?
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama ni wafuasi wa Sultani CCM wameamua kujikata na kuunda chama kingine naona watakuwa hawajafanya la maana sana ,aidha ni kujitafutia balaa na Sultani ,atawakamata mmoja mmoja na kuhakikisha kesi zao zinafuata sera ya kasi mpya ,bora wangeachia ngazi na kupumzika huku wakimpiga madongo madogo madogo Sltani CCM.
   
 13. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Zitto kama hayo unayoyasema yana ukweli !! Maana umesema umesikia ,nilitumai kwa vile upo karibu na jiko ungeliweka za uhakika kabisa na kuwaangazia wana JF.

  Wabunge wa CCM ambao wanapambana na ufisadi wataingia ? Na sio wabunge wanaoshutumiwa na ufisadi wataingia ? a little bt misunderstands !

  Maana hapo inatubidi tutazame uwingi upo wapi kati ya makundi hayo mawili na kwa vyovyote kundi litakalobakia litakuwa na nguvu za nchi kwa vile mihimili yote ya Nchi na hatamu zake watakuwa au zitakua mikononi mwao.

  Cha muhimu kama hao ni wakweli nawanataka kuzusha upinzani mkubwa basi wajiunge na Chama chochote cha upinzani ambacho wanahisi kimetulia na wanaweza kabisa kuwahamisha wapiga kura wao kirahisi ,kuliko kusema wanafungua chama kingine kwa kweli hawataeleweka zaidi ya kuwababaisha wananchi ,hivi ni kweli vyama vyote vilivyopo hawawezi kujiunga navyo ,kama wao ni wanasiasa wa kweli wangewekeza nguvu zao katika vyama viliopo tu ,kufungua chama kingine hakutawafikisha mbali na watasambaratika na kupoteza nguvu ambayo ilitarajiwa kumegeka kutoka kwa wafuasi wa Sultani CCM na kujiunga na chama kingine cha upinzani naona ikiwa hawa wapo luzi wanahitaji kushauriwa kwa haraka kabla hawajasambaratika na kumezwa na hila za Sultani CCM vinginevyo ikiwa watakataa basi wajue hawajabadilisha chochote zaidi ya kutafuta tawi jingine la mafisadi.
   
 14. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaka CCM bado hakuna wapinga ufisadi kwa dhati haswa miongoni mwa hao wabunge wetu. Wengi wanapiga kelele ili kujiwekea mazingira ya kulinda nafasi zao kutoka kwa wapinzani wao ndani ya CCM na wengine wanafanya hivyo ili kulinda nafasi ya CCM katika kiti cha enzi (UTAWALA). Ukweli ni kuwa hii sio taarifa njema kwa wanaoota kuwa na upinzani makini kutokea ndani ya CCM. CHADEMA wawe makini katika kuaccomodate hayo makapi ya CCM. Wana nafasi kubwa ya kujijenga wenyewe kuliko kuingiza vinyamkela vilivyotoka CCM kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vyenye lengo la kulinda MASLAHI YA CHAMA, MASLAHI YA TABAKA TAWALA na MASLAHI BINAFSI.

  omarilyas
   
 15. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wako wafuasi wa Sultani CCM wanaweza kupokeleka kwenye upinzani na wako ambao hawapokeleki kundi hili la waliokuwa hawapokeleki ni hatari kupokelewa aidha ikiwa watapokelewa basi sheria za vyama vingine nafikiri usote kama mwaka ndio unaweza kugombea nafasi katika vyama vyao nafikiri sheria hii ipo upande wa CUF sijui kwa vyama vingine kama ipo ,kwa maana hiyo unakuwa huwezi kutumika katika sehemu za uongozi zaidi ya kuwa mwanachama wa kawaida tofauti na mwanachama mpya ambe alikuwa hayupo chama chochote kile ,huo ndio utaratibu uliopo katika CUF kama sikosei.
   
 16. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Sasa CHADEMA nao si wameshatuonyesha rangi yao halisi katika swala la dowans, japo najizuia kuwashatumu wengineo kama Kitila Mkumbo na mwenyekiti wao. Bora hicho chama kama wana nia njema wajaribu maana waliopo sasa ni ufisadi kwa kwenda mbele.
   
Loading...