Sitosahau siku niliyoshuhudia rafiki yangu akiuwawa na Kiboko.

Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,897
2,000
Salaam wana-Gret thinkers,
Ni muda mwingine tunakutana katika simulizi za kweli zilizotokea katika maisha yetu ya kila siku,Nimeileta leo ili kupishana na sikukuu...karibu..
Mwanzo.
Naitwa Musa nimzaliwa kijiji fulani karibia na Natta, Wilayani Serengeti Mkoani Mara,ni kijana ninae jishughulisha na kilimo,uwindaji na uvuvi katika mito mbalimbali hapa serengeti....
Ilikuwa ni Alhamisi moja, Mwaka 2013 katika shughuli yetu ya uvuvi mimi na rafiki zangu watatu tulishuka na kuelekea mtoni (Rubana)...mto huu unatenganisha makazi ya watu (kijiji chetu) na mbuga ya serengeti, ilikuwa jioni tulienda kutupa nyavu (mitego ya samaki) katika mto huo...tulifika mtoni tukavua nguo tukaingia mtoni kutega na baada ya kumaliza tukatoka mtoni tukavaa mavazi yetu na kurudi nyumbani kujitayarisha kwa kesho yake(ijumaa) kuja kuvua samaki...
Siku ya tukio:- Asubuhi na mapema (Alfajiri) mimi na rafiki zangu tukiwa na baiskeli yetu tuliwahi mtoni, tulivyofika tukavua mavazi yetu kama kawaida kabla ya kuingia majini, Rafiki yangu John(siyo jina lake la kweli) alivua nguo haraka zaidi yetu na kuingia mtoni haraka zaidi yetu kuwahi nyavu zake zilizokuwa kwenye kina kirefu cha maji, basi aliingia hadi alipotega na kuanza kuvuta nyavu huku akijisifu kuwa leo wavu mzito inaonesha kapata wengi...
Ghafla, ikasikika sauti ya muungurumo kutokea majini wote tulishtuka na kutulia tuli, hata sisi tuliokuwa tunataka kuingia mtoni tukasita, kumbe kwenye kile kina kirefu ndani ya maji kulikuwa na kiboko (Hippopotamus) na John alikuwa amemshtua, basi akatoa kichwa chake taratibu na uso kwa uso wakaonana na John,John alishtuka na kuanza kupiga maji kurudi nyuma kutoka mtoni ilo lilikuwa kosa kwani kiboko alirudi ndani ya maji na alipokuja kuibuka tena(maana alikuwa amemzidi speed na kumshika) aling'ata katikati ya miguu (sehemu za siri za John) na kuibuka nazo ila john alikua mzima na akapiga kelele za maumivu na kuomba msaada, sisi wakati huo tayari tulikua juu ya miti (karibu na mto) tukishuhudia tukio hilo bila msaada...
John alikuwa anapiga kelele na kutapa tapa juu ya maji huku kichwa na mikono vikionekana zaidi na hilo lilikuwa kosa jingine tena kubwa zaidi kwani kiboko alicharuka na kumfata tena John safari hii kwa mdomo wake mkubwa na meno yake makali alilenga kichwa baada ya kukipata sawa sawa alikipasua katikati ubongo na damu vyote vikachafua maji ya eneo lile nguvu ziliniishia mara baada ya kuona tukio lile almanusra nianguke kutoka mtini nilishukuru tawi kubwa lililokuwa karibu yangu nililolishika kwa nguvu pale nilipoweweseka...
Basi mara baada ya kiboko kuona jamaa ametulia kwa haraka alitoka mtoni na kuivaa baiskeli tuliyokuwa tumeipaki kwenye njia ya kuingilia mtoni na kuitawanyisha vipande viwili kwa kuing'ata na meno yake kisha kuikanyaga na kuelekea kichakani pembeni ya ule mto huku akiunguruma kwa hasira,sisi tuliokuwa juu ya mti tulitulia tuli mpaka pale alipoacha kupiga kelele ndani ya kile kichaka, ndipo tukapeana ishara za kushuka chini ya miti tukachukua nguo zetu taratibu na kutoka nduki kurudi kijijini mwili wa john tukiuacha mtoni ukiwa ndani ya maji maana maji hayakuwa yakitiririka kwa kasi pale mtoni.........
Inaendelea....
 

Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,897
2,000
Muendelezo:-
Tulipofika kijijini kijijini tukawaita ndugu na marafiki zetu tukapiga simu kambi ya askar wa wanyama pori wakaja kijijin tukaelekea mtoni ilikuwa imeishafika saa moja asubuhi inaelekea saa mbili, tulipofika mtoni kiboko alianza tena kuunguruma baada ya kusikia muungurumo wa gari la askari, Askar kwa taadhari kubwa wakautoa mwili mtoni kuupakia ndani ya gari kisha gari kuondoka. Askari wakabakia na siraha zao kupambana na kiboko,Mpambano ulianza mida ile ya saa mbili, askari kwa kutumia bunduki zao walikuwa wanamshambulia kiboko huku yeye akijihami kwa vitisho na kubadilisha maeneo akitoka kichakani anarudi mtoni akiona risasi zinamzidia alitoka mtoni na kurudi vichakani...
Ilipofika mida ya saa sita kiboko akazidiwa na kuuwawa,baadae ikaja gari ya askari na kumpakia kisha nyama kupelekwa msibani (kwa John), Marehemu alizikwa siku hiyo hiyo maana mwili ulikuwa umeharibika vibaya sana, Marehemu aliacha mke na mtoto mmoja wa miezi miwili....
MWISHO

Imesimuliwa na Musa na kuandikwa na Kijukuu cha hitler Adolph hitler jr
 

Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,897
2,000
Sitosahau siku niliyoshuhudia rafiki yangu akiuwawa na Tembo nitairudia january kwa maboresho maana ya awali ilileta mushker kwa viongozi wa jf...Asante
- Peace92
 

py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,469
2,000

Wanaume wa mikoani bure kabisa yani mpo wawili mnapanda juu ya mti mnashindwa kumsaidia rafiki yenu,mtizame huyu dogo anawashindeni jeshi la mtu mmoja
 

KING 360

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
2,999
2,000
Mwanaume mzima unamuogopa kiboko ww mtu anakunyang'anya demu wako kwa kiwembe
 

Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,897
2,000

Wanaume wa mikoani bure kabisa yani mpo wawili mnapanda juu ya mti mnashindwa kumsaidia rafiki yenu,mtizame huyu dogo anawashindeni jeshi la mtu mmoja
Mkuu hivi kweli unamfahamu kiboko au unadhani ni ng'ombe huyo au nyumbu....Huyo ni zaidi ya nyati(mbogo) kwa ukali....acha kabisa...
 

Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,897
2,000
Mwanaume mzima unamuogopa kiboko ww mtu anakunyang'anya demu wako kwa kiwembe
Kiboko ni mbaya rafiki unaongea tu...hujawai kutana nae uso kwa uso tena akiwa amekasirika......angalia taarifa channel e wapo kwenye kundi la wanyama hatari wanaongoza kwa kuua binaadam Afrika... Simba cha mtoto eti...
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
17,474
2,000
Mh hivi unaanzaje kuzama mtoni hujui hata kuna nini huko ndani!!!!

Tangu nionage muvie ya anaconda kwenye maji mule. hunidumbukizi katika maji ambayo chini sioni.mimi sio samaki naishi bila hata maji.
 

Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,897
2,000
Mh hivi unaanzaje kuzama mtoni hujui hata kuna nini huko ndani!!!!

Tangu nionage muvie ya anaconda kwenye maji mule. hunidumbukizi katika maji ambayo chini sioni.mimi sio samaki naishi bila hata maji.
Maisha ndugu yangu....halafu unafahamu ukiuzoea mtu utauchukulia poa tu kila siku....ukizingatia hakikuwa kipindi cha mvua
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom