Sitosahau siku ambayo tulifika Mbeya saa saba mchana. Njia nzima nilitubu dhambi zangu

Kwahiyo ni kweli hilo bus lilifika Mbeya hii hii yenye milima ya kitonga + kona kona za morogoro SAA 7???, akii nilidhani mleta Uzi anatupa chai. Au ilikua helicopter huwenda mmesahau ,si bus

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana hakuna chai kiongozi, tena kuna bus lingine zainab hata halikutembea siku njingi sijui liliamia road IPI. Wakati ule kweli Mungu alikuwa na wanadamu, ingekuwa ndiyo kwa ajali hizi. Watu wengi sana wangekuwa wameshatangulizwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi mwaka 2017 mwezi wa 11 nilitoka Dar saa 7 na dk kadhaa asubuhi pale rqngi 3 mbagala nilifika Songea saa mbili kasoro dk 4kupitia lindi ni safari ya Km 1024 ,,,,,Gari super feo DLM dereva alikua mwarabu mwarabu aliyekuwa anaendesha superfeo ya Dar-Mtwara....nakumbuka hiyo siku tulipofika Lindi abiria wakaanza kupiga kelele maana tulikua tunakimbizana na ya Mbinga,jamaa qlipunguza spidi mpka 40 abiria tukapiga tena kelele jamaa akawa huru hapo alipiga kiatu balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya 2000 mwanzo njia ya Songea kama sikosei ni Zainabs au Kiswele ilikula mweleka ikaua watu karibu wote. Miongoni mwa ajali mbaya sana za barabarani kuwahi kutokea iaka ya karibuni
 
story ya uongo hii...! hakuna gari ya kutoka dar 12 asbh ikafika Mbeya 7 mchana..! Hata barabara ingekuwa tambarare ni imenyooka straight na unapita mwenyewe barabarani..!

Hakuna kitu kama hicho
Siyo ya kutunga,, kama basi la hood ilikuwa inaingia Mbeya saa 9:30 mpaka saa 10:00 litashindwa nn hilo,, na kuna imewahi ingia mbeya saa 7:00 mchana na ilikuwa ni Isuzu,,,
Mimi nimesafiri na kampuni ya hood kutoka Mbeya hadi Arusha tunatoka saa 11:00 asubuhi tunafika arusha saa 7 mpaka saa 9 usiku,,, lakini Leo hii kutoka Mbeya hadi Arusha ni ni kama masaa 36 wakati zamani ilikuwa masaa 16 mpaka masaa 19..... Njia ya Chalinze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tochi nadhani huwawehusha madreva. Akiwa na uchungu wa 30thou yake aloitoa akipewa ishara kuwa mbele ni shwari huamua kujitoa utu.
Enzi hizo kulikuwa hakuna tochi na ajali zilikuwa za kuhesabu na ni nadra sana bus kula vichwa vyote 65. Walikuwa wanabaki wa kuja kutuambia kilicho tokea. Leo, bus likiamua linakula vichwa vyote 65 na mikanda mmevaa.
Mwendo kasi sio ajali bali ajali huletwa na mengine ka vile kafara
 
Siyo ya kutunga,, kama basi la hood ilikuwa inaingia Mbeya saa 9:30 mpaka saa 10:00 litashindwa nn hilo,, na kuna imewahi ingia mbeya saa 7:00 mchana na ilikuwa ni Isuzu,,,
Mimi nimesafiri na kampuni ya hood kutoka Mbeya hadi Arusha tunatoka saa 11:00 asubuhi tunafika arusha saa 7 mpaka saa 9 usiku,,, lakini Leo hii kutoka Mbeya hadi Arusha ni ni kama masaa 36 wakati zamani ilikuwa masaa 16 mpaka masaa 19..... Njia ya Chalinze

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hiyo hood uliyopanda ilichelewa maana Hood ilikuwa inaingia saa 3 ama 4
 
Samahani,mataa ya ubungo yaliwekwa mwaka gani?
Miaka ya 90. Sikumbuki vizuri ilikuwa Bus gani kati ya Matema au Safina. Tulitoka Dar saa 12 asubuhi kwa mara ya kwanza naelekea Mbeya.

Tulitoka na hilo Bus tukavuka mataa tukaitafuta kimara mbezi tukakamata barabara sasa ya Mkoani huko mbele.Hapo ndo nilianza kuona milango ya mbinguni ikifunguka na kufunga.

Sikuwahi kuona Dereva anapiga mti/mpini kama yule jamaa.Gari ilikuwa inakimbia sijapata kuona duniani. Abiria tulikuwa tunaogopa hata kukohoa au kupiga chafya kwa wasiwasi kuwa unaweza mtingisha dereva ukasababisha ajali.

Dereva alikuwa anapiga mkono/mpini balaaa njia nzima nikawa nasali nikitubu dhambi zangu zote na kuomba msamaha maana sikuwa na hakika kama tungefika salama. Nilikumbuka mapambio mbalimbali na nyimbo za kuelezea Ukuu wa Mungu.

Yeye dereva alikuwa kimya akihesabu tu gear zake kama vile anasoma Rozari au Tasbihi na wakati mwingine akibadilishana maneno mawili matatu na konda.

Alipiga mpini kiroho mbaya/ile kinyama sana. Saa saba na robo anaanza kupangua gia kaingia town tupo Mbeya.Aisee siwezi sahau safari ile nilikuwa naona mbingu zinafunguka na kufunga. Nawakumbuka ndugu na jamaa zangu huku machozi ya kitoka ila tulifika.

Ghafla tuliona gari ya Polisi imetuunganishia mitaa fulani hivi kumechangamka.Dereva hakusimama akaendelea kupiga mpini mpaka tumefika stand ....

Tulikuja shtuka tumefika stand watu wamejaaa hawaamini.Nadhani jamaa aliweka historia haikuwahi kutokea hapo nyuma. Tumefika stand bus imesimama akazipangua gia mpaka zero akaiacha gari inanguruma yeye kaegamia usukani. Baada ya dakika kadhaa Polisi wakafika. Wakamfuata dereva mbele wakamwambia ashuke wakamtia pingu. Wakaondoka naye.

Nakumbuka mimi nilifika nyumbani kwa wenyeji wangu wanatenga meza wale chakula cha mchana.lile bus ilikuwa lielekee Kyela alienda nalo dereva mwingine yule jamaa walimweka ndani.

Najiuliza yule dereva aliendelea na upigaji ule wa mpini? Na je kwa sasa yupo wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom