Sitosahau niliponusurika kuchomwa moto tulipoenda kuiba mimi na rafiki zangu

jooohs

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
2,066
8,593
Katika haya maisha sisi kama binadamu tunapitia changamoto nyingi sana ,zipo changamoto za magonjwa ,umasikini, ukosefu wa ajira ukosefu wa pesa ,mapenzi nk.
Kila mtu ukikaanae na kumsikiliza atakwambia changamoto inayo msumbua au iliyowahi kukutananayo. Kunachangamoto zinazotatuka na nyingine ambazo ambazo haziwezi kutatuka.

Lakini katika maisha yangu changamoto iliyowahi nitesa sana tena katika umri mdogo sana ni umasikini pamoja na ugonjwa uliokuwa unamsumbua mama yangu.

Ikumbukwe mimi katika familia yangu ndio nilikuwa kijana mkubwa japo kuna kaka zangu wakubwa upande wa mama wa kambo japo mahisiano yalikuwa mabaya sana.

Mwaka 2003 ni mwaka ambao nilianza elimu yangu ya.msingi katika mkoa fulani huko kanda ya ziwa .Na katika huo mwaka baba yangu aliondoka kwanda kutafuta maisha nje ya nchi (kenya ) , lakini mpaka naandika hapa muda huu hajawahi rudi na hatujui yuko wapi .

Sasa majukumu yote ya familia alibakinayo mama baada ya juhudi za kumtafuta baba kushindikana. Tatizo lilipo kuja kuanzia bibi yangu kizaa baba akachochea maneno eti mama amemtoa baba kafara ili achukue nyumba, .Kilichofanyika tulifukuzwa kwenye nyumba mimi dada yangu na mdogo wangu wa kiume pamoja na mama.
Nakumbuka siku hiyo bamdogo alikuja akasema hiyo nyumba tuhame maana ameshamuuzia mtu.

Hatukuwa na jinsi ikabidi tuhamie kwenye kiwanja chetu kingine japo kilikuwa na migogoro kiko barabarani ilibidi mama akodishe mtu akafyatua matofali ya udogo tukajenga nyumba ya majani moja na jiko mimi nikawa nalala jikoni.
Baada ya hapo maisha yaliendelea kawaida kwani mama alikuwa anafanya biashara ya kuuza viazi vitamu. Analangua na kuuza sokoni nikasoma kwa kuungaunga mpaka nikamaliza darasa la saba .

Nimesoma shule ya msingi bila viatu kwa miaka mingi ,kaptura nilikuwa nayo imechanika makalion ya kuanzia la kwanza nimemaliza nayo darasa la 5 ilifikamahala mwalimu akitaka kunichapa ananiambia wewe nyanyuka maana makalio yote yalikuwa wazi.

Matatizo yalikuja kuanza baada ya mama kupata mimba nyingine ambae ni mdogo wangu wa mwisho maana alipojifungua alikuwa hawezi kutembea mguu mmoja ulikuwa unamsumbua mtaji wote tukamalizia hospital tatizo lilizidi kuwa kubwa tukajaribu kuomba msaada kwa bamdogo walikata kuwa hawana pesa japo kwa upande wao miasha yalikuwa yamewanyookea.

Ilibidi jumuiya ya kanisani waingilie kati wakachanga pesa wakamtoa mama hospitalini japo alikuwa hawezi kutembea,alishindwa kufanya biashara na wakati huo. Selection za form 1 zilikuwa zimetoka nilienda na rafiki zangu kuchukua form.Asee kuangalia gharama sijui pesa ya dawati inafika kama laki moja na hapo home hatuna hata mia ndani.

Kuna mwalimu alikuwa anatufundisha primary ikabidi mama aongeenae ndio akasema ninaweza kwenda kuongea na mkuu wa shule akanipa barua nikaenda kwa afisa elimu labda nitasaidiwa ilibidi ni fanye hivyo zunguka kwa mwenyekiti,katani kwa afisa elimu nikapata kibali cha kusoma bila kulipa ada .

Dada yangu alikuwa amefeli elimu ya msingi yuko nyumbani ikabidi aendee kufanya kazi za ndani dar kuna mama alisema mwanae ni nesi anahitaji mfanyakazi .Tukabaki mimi na wadogo zangu wawili wa kiume mmoja alikuwa darasa 3 mwingine mchanga.

Mambo yakawa magumu.maana mama yuko ndani hajiwezi mimi naenda kusoma ,naondoka asubuhi narudi saa kumi kulingana na umbali nikirudi home hakuna msosi yani mdogo wangu anasoma primary akirudi njaa, hakuna kitu ndani nikiangalia kuna mdogo angu mwingine mchanga nachoka kabisa.

Ilibidi nifunge safari nikaenda kwa bamdogo kumueleza hali halisi akanambia nenda nyumbani kesho nitakuja kuwaona nilifurahi sana nikamwabia mama lakin hakuweza kutusaidia
hata mia .

Kuna yule jamaa aliezaa na.mama mdogo wangu wa mwisho yeye alifariki kabla hata ya mama kujifungua alifia bar akiwa amelewa vibaya tulikuja pata habari kuwa mke wake halali na mama mkwewe waliseti mipango wakamuwekea sumu ili ajekufia nyumbani wamtie mama hatiani ila bahati ya mungu akapita bar.

Baada ya msoto kuzidi ikabidi nianze utoro shule. Kiangazi kikapiga nakumbuka 2010 kiangazi kikapiga vibaya mama pamoja na igonjwa wake alikuwa anaenda kutembea anachuma mboga mchanganyiko akikutana na mchicha,kunde,mgagani vyote anachemsha tunapiga msosi lakini kutokana na kiangazi hata izo mboga zikakosekana kabisa .

Ilifika mahala ikawa ikifika usiku mimi na mdogo wangu tunaenda kuvamia mashamba ya watu wenye visima tuchuma mchicha tena hovyo hovyo ila ruhusa tunaenda kupika hata saa 8 usiku tunakula.

Nikaanza utoro shuleni kwani sikuona umuhimu wa shule nikirudi nyumban hakuna chakula kuna siku tulikuwa tumepigwa njaa kali toka asubuh hatuna hatasenti.mama kila kona anadaiwa tukashitukia mia mbili inadondoka kutoka juu hilo jambo mpaka leo huwa nikikaa nafikiria nani aliyeirusha.

Ilibidi nianze utoro shuleni maana sikuona tena umihimu wa shule kivile nikajiunga kufyatua matofali ya kuchoma nakumbuka tofali moja mtu unalipwa shilingi 30 nikawa najitahidi nafyatua matofali 100 kwa siku nalipwa 3000 nikawa naendelea hivyo hivyo nikipata pesa naenda nanunua mahindi nasaga napeleka nyumbani. Shida ikaanza unaweza fyatua boss akija kukagua kazi anakwambia matofali umefuatua vibaya nakukata hela, au kama unataka kazi ukifyatua matofali 100 inapidi uongeze mengine 30 ya fidia daa mambo yakawa magumu

Nikatoka hapo nakumbuka nikajiunga kwa wanaochota mchanga mtoni asee asikwambie ile kazi yaani unaingia mtoni maji yanatiririka unachota mchanga ukiinua koleo mchanga wote umepelekwa na maji mtafanya hivyo mkifikisha wakujaza gari mnapewa 10000 hapo mko kama watu wa 5 mnagawana 2000 kesho tena mnaendele shule nikawa naenda mara chache sana.

Shida ilikuja kuanzia kwa jamaa alikuwa jirani yetu jina sito weza kumtaja (juma) yeye alikuwa hajaenda shule kabisa sasa nikamfata nikamwabia kama atakuwa na mchongo wa kibarua chochote anishitie akasema poah ,haikupita hata siku jioni niliporudi nyumbani mama akaniambia juma alikuwa anakutafuta nikasema sawa usiku huo huo nikaenda akaniambia kuna chuma lake amepewa lakini ni zito sana kesho asubuhi mapema nimsaidia kubeba tukiliuza atanigawia pesa nikasema sawa ,ilipofika.

kesho yake tikaanza safari ilikuwa mbali sana karibu na mlima fulani tulipofika ilikuwa ni eneo kama garage hivi inafensi kubwa jamaa akaniambia nisubir barabarani kazama mule akalitoa tena kwa kuliviringisha asee lilikuwa zito hatari tulilibeba wawili tukatembea kama kilomita mbili.nanusu tukaliuza kwenye mzani wa vyuma chakavu jamaa akanipatia mgao 4000 yeye akabaki na 5000 nakumbuka nilifurahi sana.

Nilipita nikanunua tisheti ya buku pesa iliyobaki nikafanya shopping nikamgawia na mama 1000 pia .nakumbuka hiyo wiki niienda shuleni kwani kidogo hali ilikuwa inaruhusu.

SIKU ya mkosi ikafika nakumbuka iikuwa inaelekea siku kuu ya pasaka huyo juma akanifata akaniambia kuna dili nataka tuchonge sikuwa na wasiwasi nikaenda nikamkuta yuko na jamaa mwingine anaitwa manu, kufika wakaniambia kuna mama huwa anafuga kuku wa mayai na kienyeji sasa tutegee ulemuda ambao anaondoka kusambaza huwa anabaki mfanyakazi tunaruka ukuta tunachukua kila mtu jogoo tutapiga pesa hata 10000 kila mmoja siku fikiria vizuri lakini nilikuwa nawaza pesa nikakubali.

Siku ikafika kweli yule mama aliondoka na kigari kidogo kwenye mida ya saa 4 maana tulifika mapema sema tulikuwa tunajifanya kupiga story kwa ndani kidogo, yule mama aivyoondokaa ikabidi jama wakaanza kuruka ukuta mimi nikawa wamwisho roho ikasita lakini nilikuwa nimebaki mwenyewe ikabidi niruke kumbe banda lilikuwa nyuma kidogo eee jama hawakujali wakenda kufungua kuku zikapiga kelele halafu kulikuwa na watu wengine sii mfanyakazi pekee nikasikia sauti mwizi mwizi ee bwana eeee. Nilijaribu kuruka ukuta mara ya kwanza ikashindikana, mara ya pili nikaruka nikafanikiwa nikaanza kukimbia.

Lakini jinsi nilivyokuwa nakimbia ndivyo sauti ziliendelea akili yangu ikawa inanituma pita kwenye vichochoro lakini kila napopita nasikia yule pale.mwizi wa kuku. Asee katika siku za maisha yangu ile siku nilichanganyikiwa nikawa nnajisemeamoyoni mimi sii mwizi nani atanielewa wale jamaa zangu sijui walikimbilia wapi nilijitahidi kukimbia nikasema lazima nikimbilie kanisani maana kanisa la sda lilikuwa karibu.

Daa jamani ile kukimbila kanisani ndio nilijikoroga ,kanisa lilikuwa la wasabato lilikuwa limezungushiwa fensi ya michongoma ilibidi nipite hivyo hivyo nikaingia mpaka ndani nakumbuka nilikuta kama kikao flani hivi cha waimba kwaya niliingia nikaenda kwenye korido nikazama chini ya meza ilikuwa imepambwa na vitambaa.

Wakati nikomule nikaanza kulia leo nakufa wazo la mama likaniijia nikachanganyikiwa mama atabaki na nanini nililia sana. kila nikikumbuka siku ile naenda kukaa mahali mwenyewe nalia, yani nilijiona wathamani sana hata bila ya pesa maana nilijua mama yangu wadogo zangu wananihitaji bado halafu mm ndio naenda kufa mungu nisaidie.

Hazikupita hata dakika tano nikasikia watu wamejaa nje ya kanisa wanasema atoke atoke tutapasua vioo kelele zikazidi ndipo nikasikia mtu amefunua kile kitambaa alikuwa sijui ni pasta akasema toka watu wanaleta fujoo jaman yaaninilihisi kufaa mwili wote ulikuwa umepigwa ganzi kama nataka kukojoa lakini sina mkojo.

Baadae vijana kama watano wakaingia kanisani kunichukua wengine wanafimbo, panga mawe daa mama mmoja akaning'angania jamani musipige huyu mtoto ni mdogo sana kunajamaa akasema muachie yule mama alipigwa banzi moja mpaka akaniachia wakanitoa kwa kipigo mabuti, mikanda lakini muda huwo nikawa tu nawaza mama yangu jee akifika hapa atajisikiaje jee nikiuwawa hapa itakuwaje yani moyo wangu ulikuwa unauma sana zaidi ya vile vipigo walivyokuwa wananipatia.

Nakumbuka walinishika miguu na mikono wakanigeuza kifudi fudi ases sijawahi pigwa vilee mpaka leo nina alama mgongoni yani walinichakaza aswaa baadae jamaa mmoja akasema huyu ni wakuchoma moto tumen boda alete mafuta asee nikasema mungu leo ndio mwisho wangu niokoe baada ya kusema hivyo kumbe kunaraia huwa wanaogopa nikaona wengine wanatawanyiaka wakina mama pia ,daa sijui nguvu zile nilitoa wapi ikabidi nisimame nikaanza kukimbia lakini bado watu waliendlea kunipiga wangine wananipigana mawe .

Nikaona hapa nikimbie kuelekea kwa mwenyekiti maana hilo kanisa ni karibu sana na kwa mwenyekiti, hapo mwili nimetapakaa damu kichwani tisheti walikuwa wamenichania, nilipata upenyo nikakimbilia kwenye kichochoro nikazidi kukimbia

Nakumbuka nilizama kwenye fensi ya michongoama ambayo ilikuwa mingi nikatokezea kwenye nyimba za mtaa mwingine siku kata tamaa maana watu wengi walishindwa kuvuka ikabidi wazunguke barabarani sikupoteza muda nikakimbia hadi kwa mwenyekiti nikaingia ndani uvunguni japo yeye mwenyewe hakuwepo ila nashukuru alikuwa anavijana wengi wakubwa anaoishinao ndio walio saidia maana waligoma watu kuingia baada ya muda mwenyekiti alikuja nikawekwa pale hadi saa12 nashukuru askari hawakuja, wakanipatia sweta lenye kofia nikaenda nyumbani.

Mama alilia sana siku hiyo yaani nilichafua jina mtaa mzima.
Kitu nilichokuja gundua kuwa nilikuwa na umuhimu sana kwenye familia yangu kuliko pesa nilizokuwa nasumbukia nashukuru mungu niliendelea kupambana kwenye masomo namtaani pia mwaka huu nimemliza chuo na degree yangu actuarial science na maisha yanaenda vizuri. Jamaa mmoja tuliekuwa naekwenye tukio mwaka 2016 alihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la ubakaji Butimba.
 
Binadamu tuna matatizo sana, unaweza ukafikiria kuwa wewe una shida kumbe kuna watu wanazaidi ya shida.

Kuna wakati mwingine unaweza ukamuona mtu hata pesa ya kula hana,na hali mwingine unakunywa savanna zaidi ya saba bar na kula kitimoti za kutosha, huwa nafikiria sana na kujiuliza,ndo mana sijawahi kuombwa msaada na mtu mwenye uhitaji nikampuuzia, hii dunia iacha tu kama ilivyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom