Sitosahau: Nilipokea muujiza kwa njia ya Njozi

Buhaya Empire

Senior Member
Aug 3, 2016
116
299
Habari,

Leo nimeona nishee na ninyi kisa ambacho kwangu ni tukio muhimu sanaa kwa namna zote katika maisha yangu.

Nilipokuwa na umri mdogo nilikuwa na tatizo moja sugu na la kusikitisha sana, tatizo la kukojoa kitandani kila nnapolala usiku.

Pamoja na kwamba nilikuwa mdogo lakini kwakweli nilikuwa nafadhaika sana.

Niliendelea na tabia hiyo ya kukera niliyoshindwa kuidhibiti mpaka nilipofikisha umri wa miaka 14, inasikitisha sana.

Nilipokuwa katika miaka 14 sikumbuki siku wala tarehe ila nakumbuka katika usiku mmoja nilipata njozi, ilikuwa hivi: wakati nilipokuwa nimelala huku tukiwa tumezima taa mimi na mjomba wangu anayenizidi miaka miwili katika vitanda tofauti, alikuja mtu mmoja katika ndoto ambaye sikumbuki alikuwa jinsia gani na wala sikunbuki alivaa mavazi gani.. Alipofika katika kitanda changu akaniuliza swali moja tu "unataka nikufanyie nini?".

Ajabu na kweli ni kwamba bila kumumunya maneno wala kusita nilitoa Jibu moja pia "Nakojoa kitandani.." basi yule mtu sikumbuki namna alivoyondoka na wala hakunijibu na njozi ikaishia hapo.

Amini usiamini toka siku hiyo mpaka leo hii ni miaka 13 imepita, sijawahi kukojoa kitandani hata kwa bahati mbaya!

Nashukuru sana kwa nilichokiota lakini mpaka leo sielewi nini maana yake mambo haya.

Kwa wale msiyoamini katika njozi mnapaswa kuutafakari upya msimamo wenu.

Kwa kheri.
 
Wewe una maono
Jitahidi kuwa karibu na Mungu
Utafanikiwa mengi na utakuwa ukiomba kitu Mungu atakujibu,tena wewe umeongea na Mungu kwenye lugha ya waziwazi ambayo umeielewa
Mungu azidi kuwa pamoja nawe,mpokee bwana Yesu kama bado hujampokea,utaona ukuu wake ùlivyo mzuri na wa ajabu
 
Habari,

Leo nimeona nishee na ninyi kisa ambacho kwangu ni tukio muhimu sanaa kwa namna zote katika maisha yangu.

Nilipokuwa na umri mdogo nilikuwa na tatizo moja sugu na la kusikitisha sana, tatizo la kukojoa kitandani kila nnapolala usiku.

Pamoja na kwamba nilikuwa mdogo lakini kwakweli nilikuwa nafadhaika sana.

Niliendelea na tabia hiyo ya kukera niliyoshindwa kuidhibiti mpaka nilipofikisha umri wa miaka 14, inasikitisha sana.

Nilipokuwa katika miaka 14 sikumbuki siku wala tarehe ila nakumbuka katika usiku mmoja nilipata njozi, ilikuwa hivi: wakati nilipokuwa nimelala huku tukiwa tumezima taa mimi na mjomba wangu anayenizidi miaka miwili katika vitanda tofauti, alikuja mtu mmoja katika ndoto ambaye sikumbuki alikuwa jinsia gani na wala sikunbuki alivaa mavazi gani.. Alipofika katika kitanda changu akaniuliza swali moja tu "unataka nikufanyie nini?".

Ajabu na kweli ni kwamba bila kumumunya maneno wala kusita nilitoa Jibu moja pia "Nakojoa kitandani.." basi yule mtu sikumbuki namna alivoyondoka na wala hakunijibu na njozi ikaishia hapo.

Amini usiamini toka siku hiyo mpaka leo hii ni miaka 13 imepita, sijawahi kukojoa kitandani hata kwa bahati mbaya!

Nashukuru sana kwa nilichokiota lakini mpaka leo sielewi nini maana yake mambo haya.

Kwa wale msiyoamini katika njozi mnapaswa kuutafakari upya msimamo wenu.

Kwa kheri.
dini gani wewe?
 
Back
Top Bottom