Sitosahau nilikiona cha moto urithi wa mali za babu

SEHEMU YA 34

ILIPOISHIA
Nikaenda nyuma ya gari na kulitoa lile shepe.
“Njoo hapa” akaniambia akiwa amesimama mahali fulani kando ya lile gari.
Nilipofika karibu yake akaniambia.
“Chimba mahali hapa”
Alinionesha pale aliposimama kisha akaondoka na kusimama kando yake.
Nikaanza kupachimba mahali hapo kwa kutumia lile shepe. Bahati nzuri mchanga ulikuwa laini, sikutumia nguvu nyingi. Niliendelea kuchimba mpaka shimo likafikia urefu wa wastani wa futi mbili.
“Nichimbe hadi wapi?”
“Bado. Endelea kuchimba” Maimun akaniambia.
Nikaendelea kuchimba. Mwili wangu ukaanza kutoka jasho. Nikaacha kuchimba na kuvua shati.
“Lete nikushikie” Maimun akaniambia.
Nikampa lile shati na kuendelea kuchimba.
SASA ENDELEA
Niliendelea kuchimba lile shimo mpaka likanifikia usawa wa kifua. Nilikuwa nikimwaga mchanga juu ya shimo hilo. Ghafla nikaona ninapiga kitu kama mwamba au jiwe lililokuwa chini ya ardhi.
“Sijui nimepiga nini hapa?” nikamuuliza Maimun kwa mshituko.
“Huo ni mwamba, upige tena” Maimun akaniambia.
Nikaupiga tena kwa shepe.
“Piga tena”
Nikaupiga kwa mara ya tatu. Ule mwamba ukapasuka.
“Umepasuka” nikamwambia Maimun.
“Hebu washa kitochi cha simu yako umulike hapo palipopasuka” Maimun akaniambia.
Nikajipapasa mfukoni na kutoa simu yangu. Niliwasha kitochi nikamulika pale chini.
Mama yangu! Niliona vipande vya madini yanayomeremeta vikiwa vimetawanyika!
“Nini hii?” nikamuuliza Maimun kwa mshituko.
“Kwani umeona nini?”
“Sijui ni madini haya. Huu mwaba ulikuwa na madini!”
“Ndiyo ni madini”
“Sijui ni madini ya aina gani?”
“Ni Tanzanite, ni yale aliyokuwa akiuza babu yako”
“Niyachukue”
“Ndiyo yachukue”
Nikainama haraka na kuyachukua yale madini.
Vilikuwa vipande saba vya madini.
“Huu ni utajiri hasa! Nikajiambia kimoyomoyo kisha nikamshukuru Mungu.
“Mungu anipe nini tena!”
Yakiwa mikononi mwangu madini hayo yalikuwa yakiakisi rangi mbali mbali za dunia. Zile rangi zilikuwa kama zinazunguka. Ilikuwa ni furaha hata kuyatazama.
“Ni vipande vingapi?” Maimun akaniuliza.
“Viko saba”
“Haya sasa toka kwenye hili shimo”
“Ngoja niendelee kuupiga huu mwamba”
“Hapana, usirudie tena. Toka kwenye shimo” Maimun akanionya.
Nikayatia yale madini mifukoni mwangu kisha nikalitoa lile shepe na kuliweka juu ya shimo hilo.
“Lete mkono wako nikutoe” Maimun akaniambia.
Nikampa mkono wangu Maimun, akaushika na kunivuta. Mara moja
nikjioan niko juu ya lile shimo.
“Anza kulifukia haraka haraka”
Nikalichukua shepe hilo na kufukia lile shimo.
“Tutakuja lini tena kuchimba?” nikamuuliza Maimun kwa tamaa huku nikiendelea kufukia shimo hilo.
“Baada ya miezi sita”
“Ah kwanini! Mbona mbali sana?”
“Ndiyo masharti yake. Haya madini yanakaliwa na majini. Huwezi kuja kienyeji tu na kuyachimba na hata ukija hutoyaona. Masharti yake ndiyo haya ninayokupa. Kila baada ya miezi sita tunakuja kuchimba tena”
“Sawa”
Niliendelea kulifukia lile shimo mpaka nikaliweka sawa.
“Watu wengine hawatakuja kufukua?” nikamuuliza Maimun.
“Ni nani atakayethubutu?”
“Wanaweza kutokea watu wakaja kufukua”
“Hawatapata kitu chochote. Chukua shati lako tuondoke”
Nililichukua lile shati alilokuwa amelishika Maimun nikalivaa.
“Twenzetu” akaniambia.
Nililiweka shepe nyuma ya gari.
“Utaendesha wewe?” Maimun akaniambia.
“Sawa” nikamjibu haraka haraka na kwenda kufungua mlango wa gari wa upande wa dereva.
Maimun alifungua mlango wa upande wa pili wa dereva na kujipakia.
“Washa gari tuondoke. Muda umekwenda sana”
Nikaliwsha gari na kuliondoa. Nilipokuja na Maimun mahali hapo nilikuwa nimefadhaika lakini wakati tunaondoka moyo wangu ulikuwa na furaha iliyopita kiasi.
“Hivi babu yangu ulikuwa unakuja naye hapa hapa kuchimba haya madini?”
“Ninajua mimi kama tulikuwa tunakuja hapa au mahali pengine”
“Hutaki kuniiambia”
“Si lazima kila kitu ukijue kwa sasa Kasim”
“Sawa mke wangu”
Nikabaki kimya mpaka tulipotokea pale mahali ambapo majambazi walitaka kulipora gari langu. Yule mtu aliyenata huku mkono wake mmoja ukipiga ngumi kwenye hewa alikuwa bado amenata vile vile na yule aliyeaguka alikuwa bado yuko chini. Lile gari lao pia lilikuwa pale pale.
“Kumbe hawa watu bado wapo?”nikamuuliza Maimun.
“Si uwaache tu. Majambazi wanakuhusu nini?”
“Nilikuwa nasema tu”
“Sema maneno yenye maana. Achana
na watu hao”
“Inaonekana walikuudhi sana”
 
SEHEMU YA 35

ILIPOISHIA
Maimun hakunijibu chochote na mimi nikanyamaza. Mawazo yalikuwa yakipita akilini mwangu
Niliwaza si muda mrefu nitakuwa mmoja
wa matajiri wakubwa hapa nchini. Nitakuwa ninazungka kwa ndege katika nchi mbalimbali kama alivyokuwa babu yangu.
Huku nikiliendesha gari kwa mbwembwe, nilijiambia fedha itakaponikubali sawasawa, nitamshawishi Maimun ninunue jumba jingine la kifahari eneo la Masaki ambalo nilikuwa niikitamani sana kuishi.
Pia nilitaka ninunue gari jingine la gharama kutoka Ulaya. Ikiwezekana magari mawili la Maimun na la kwangu.
Tulipofika nyumbani Maimun aliniambia niyatoe yale madini. Nikayatoa mifukoni.
Aliyashika shika na kuyaangalia kisha aliniambia.
“Kuwa makini sana, wewe bado ni kijana mdogo. Nakuomba uwe msikivu. Ujue kuwa ukifanya papara utakwenda na maji”
“Kwanini?”
“Si lazima kila kitu nikwambie, unapaswa kutumia akili yako. Mimi sitaki uwe mtu wa papara”
SASA ENDELEA
“Kwani umenionaje mke wangu?” nikamuuliza Maimun baada ya kutomuelewa.
“Nimekuona una papara. Jicho limekutoka kwenye haya madini. Unajiona tayari umeshakuwa tajiri. Nataka nikukumbushe kuwa hii mali yote ni yangu mimi. Wewe ninakupa uimiliki tu, wakati wowote utakapovunja masharti yangu nninaichukua mwenyewe”
“Sitavunja masharti yako, wewe acha tu niimiliki. Kila mara unapenda kunituhumu lakini mimi sina tatizo”
“Sasa sikiliza. Tafuta wanunuzi wa haya madini hapa hapa nchini. Sitaki uende nje ya nchi kama alivyokuwa babu yako. Na pia huwezi kuyauza madini yote kwa pamoja. Uza moja moja”
“Kwanini hutaki niende nikayauze nchi za nje wakati huko nitapata bei nzuri kuliko ya hapa?” nikamuuliza.
“Uhitajji kupata pesa nyingi. Pesa yoyote utakayopata itakutosha kwa sababu kila baada ya miezi sita utapata madini mingine, una wasiwasi gani?”
“Mimi nilitaka niende nje lakini kama unataka tuyauze hapa hapa, sawa”
“Wewe unajua jiwe moja litakupatia kiasi gani?”
Pesa nyingi sana. Naweza hata kujenga jumba moja la ghorofa”
“Sasa kiherehere chako ni cha nini?”
Nikacheka kidogo kisha nikamwambia.
“Sina kiherehere. Sasa nitakwenda kuyauza lini haya madini?’
“Ni wewe tu”
Basi kesho nitaanza kufanya utafiti wa wateja”
“Sawa”
Naam, hivyo ndiyo nilivyoanza kutajirika. Nilifanikiwa kuviuza vipande vyote saba. Nikapata kiasi kikubwa cha pesa. Maimun aliniambia pesa hizo nisiziweke benki, niziache pale pale nyumbani atazilinda mwenyewe.
Badala ya sanduku moja la pesa tulilokuwa nalo kabatini, tukawa na masanduku mawili. Kila baada ya miezi sita nilienda na Maimun kuchimba madini mengine ambayo niliyauza. Nikapata utajiri mkubwa.
Maimun aliniruhusu ninunue nyumba jingine Masaki. Nikanunua jumba la kifahari ambalo alikuwa akiishi mzungu mmoja. Nililinunua kwa bilioni tatu.
Nikaagiza magari mawili kutoka
Uingereza aina ya Benz. Moja nilitaka nimpe Maimun lakini akaniambia hataki kuwa na gari la peke yake ila tuyatumie yote mawili kwa pamoja.
Pia nilifungua miradi mbali mbali ya kibiashara. Nikawa mmoja wa watu maarufu katika jiji la Dar na pia nikawa mmoja wa matijiri wakubwa Afrika.
Baada ya kuishi na Maimun kwa miaka
mitatu aliniambia yale madini yamekwisha, kwa hiyo tutumie fedha tulizonazo na kwamba atakapoona inafaa atanionesha mahali pengine pa kuchimba madini mengine ya Tanzanite.
Siku za mwanzo mwanzo nilizoanza kuishi na Maimun nilikuwa nikimuogopa lakini kidogo dogo nikaanza kumzoea na kumuona wa kawaida. Ilifikia mahali nilikuwa ninabishana naye kupinga maamuzi yake na kumwambia kwamba mimi ndiye mume, kwa hiyo anapaswa kunisikiliza mimi.
“Nimekupa mali sasa imekulewesha”
alikuwa akiniambia baada ya kuona sitaki kumsikiliza.
“Sio hivyo Maimun, amri zako nyingine zinanikera”
“Mimi najua kinachokupa kiburi ni huu utajiri lakini ujue kwamba ninaweza kuufyeka kwa siku moja tu”
“Hapana, usifanye hivyo Maimun. Nipe uhuru wa kushauriana na wewe. Kwanini ninapokushauri kitu unatishia kuchukua mali yako?”
“Ni kwa sababu ninataka unitii mimi”
“Basi yaishe. Naogopa kurudi katika umasikini”
Hivyo ndivyo nilivyokuwa ninaishi na Maimun. Alikuwa na wivu mwingi pamoja na kufuatilia mambo yangu kwa karibu. Wakati mwingine nilikuwa nachukia.
Kwa maisha ya nyumbani, Maimun alikuwa mke wa kweli aliyenionesha upendo na alinipa mamlaka ya kuimiliki nyumba vile ninavyotaka mimi. Wakati mwingine nilimtolea ukali, Maimun akaniomba msamaha kwa kuwa nilikuwa mume wake.
Jamani huu ndio mkasa wa urithi wa babu yangu. Nilikiona cha moto lakini mwishoni nikaja kupata mke wa kijini na kupata utajiri ambao sikuutarajia.
Kilichokuwa kinanipa uchungu ni kuwa Maimun alipata ujauzito wangu mara tatu lakini alikwenda kujifungulia kwao. Wale watoto alikuwa akiwaleta nyumbani usiku. Inapofika alfajiri anawarudisha kwao.
Nilipomuuliza ni kwanini anafanya hivyo aliniambia anataka watoto hao wawe majini kama yeye. Hakutaka wazoeane na watu na kwamba watoto hao hawataenda shule ila watasomea huko
huko ujinini.
“Watakapokuwa wakubwa watakuja kukusaidia, watakuwa kama binaadamu na utaweza kuwatuma popote” Maimun aliniambia.
Mtoto wangu wa kwanza niliyemzaa na Maimun, hivi sasa ana miaka saba. Wa pili ana miaka minne na wa tatu bado ni mchanga. Nilikuwa kiona jinsi anavyonyonyeshwa na mama yake ifikapo usiku anapokuja naye nyumbani pamoja na wale watoto wengine.
Sijui nitakapokufa Maimun atakwenda kwa nani kwani sikuwa na mrithi. Huenda atakwenda kwa mtu mwingine atakayemchunuka.
Hadi hii leo niko na Maimun huko nyumbani kwangu Masaki lakini wageni ni marufuku nyumbani kwangu.
MWISHO
 
SEHEMU YA 12


ILIPOISHIA
Vile vile nilitaka kujua jinsi yule msichana anavyohusika na mali za babu yangu. Amejuaje kama mali za babu yangu zimepotea?
Au ana maelezo gani ambayo anataka kunipa kuhusu mali hizo na ameyapata wapi?
Suala la mali lilinipa shauku lakini suala la mauaji lilinitia hofu. Ilibidi nigwaye na nifikiri vya kutosha kabla ya kuamua kwenda huko Mwananyamala.
Baada ya kuwaza kwa muda mrefu nilitoka pale nyumbani, nikaenda
kwenye mkahawa uliokuwa jirani. Niliagiza chakula nikala huku nikiwaza.
Nilipomaliza kula niliitoka. Siku ile kulikuwa na mechi kati ya Simba na Yanga. Nikaenda uwanja wa taifa. Nilikuwa mpenzi wa mpira wa miguu na shabiki wa moja ya timu hizo.
Niliangalia mpira hadi saa kumi na mbili jioni. Sikupata furaha kwa vile timu zilitoka sare bila kufungana. Nikarudi nyumbani.
Mpaka muda huo nilikuwa nimepuuza kwenda Mwananyamala kumuulizia
Sharif Nasri.
Asubuhi ya siku ya pili yake yule msichana akanipigia simu.
“Mbona hukwenda kule nilikokuelekeza?” akaniuliza.
“Nitakwenda leo”
“Ni muhimu. Tafadhali usipuuze”
SASA ENDELEA
Baada ya kunywa chai niliona niende huko Mwananyamala alikonielekeza huyo msichana ili nikapate taarifa zake. Nilitarajia si tu ningeweza kugundua
msichana huyo alikuwa nani pia ningeweza kujua sababu ya kuwaua wale watu.
Hata hivyo wakati nikienda huko Mwananyamala nilikuwa nikijua fika kwamba yule msichana alikuwa mtu wa hatari.
Lakini kubwa zaidi lililonisukuma niende, ni vile alivyoniambia kuwa alikuwa na
tarifa ya malli za babu yangu ambazo mpaka muda ule zilikuwa ni kitendawili nilichoshindwa kukitegua.
Kadhalika mauaji yale ya watu wanne ambao walikuwa wakidaiwa na babu yangu yalizidi kunipa shauku ya kutaka kumjua vyema msichana huyo ambaye mpaka muda ule nilikuwa nikiamini kwamba ndiye aliyewaua.
Nilipofika Mwananyamala niliutafuta mtaa niioelekezwa hadi nikaupata.
Nikaitafuta nyumba yenye namba aliyonitajia yule msichana. Nilipoiona nilijisikia kuanza kupata hofu nikajiambia kuwa nami leo naenda kufa.
Sikujua ni kwanini nilipata hofu. Lakini nilihisi nilipata hofu kwa sababu nilipagundua mahali ambapo ningepata taarifa za yule msichana ambazo zilikuwa zikiumiza kichwa changu.
Mbele ya ile nyumba nilikuta mzee aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha uvivu akivuta mtemba.
Alikuwa mzee mrefu na mwembamba aliyekuwa na ndevu nyingi nyeupe. Alikuwa amevaa shati jeupe na suruali nyeupe. Kichwani alikuwa amevaa kofia ya darize.
Jinsi nilivyomsoma kutokana na mavazi yake na sura yake, alikuwa mswahili wa pwani aliyekuwa amechanganya na ushirazi. Umri wa mzee huyo haukuwa chini ya miaka sabini na mitano ingawa bado alionekana kuwa na nguvu za kutosha.
Nilisimamisha gari karibu na baraza ya nyumba hiyo nikaizima moto na kutoa gea zote na kuvuta hand break na kushuka.
Vile nilivyomuuona mswahili nikamtolea salaam.
“Asalaam alaykum”
“Waalayka salaam” aliniitikia. Ingawa alikuwa mwembamba, sauti yake ilikuwa nzito inayokwaruza.
“Habari za hapa?” niliendelea kumsalimia nikiwa nimesimama mbele yake.
“Nzuri. Karibu” akanikaribisha huku akinitazama kwa macho ya udadisi.
Macho yake yalikuwa madogo yaliyokuwa na kope nyeupe.
“Samahani mzee wangu, kulikuwa na mtu ninamuulizia. Aliniambia ninaweza kumpata hapa”
“Ni nani?”
“Anaitwa Ummy Sharif Nasri”
Mzee nilipomtajia jina hilo alishituka akautoa mtemba wake midomoni kisha akaniuliza tena huku akiwa amenikazia macho.
“Unasema nani?”
“Ummy Sharif Nasri”
Mzee aliendelea kunikazia macho.
“Wewe unatokea wapi?”
“Natokea hapa hapa Dar”
“Unamfahamuje Ummy?”
“Sikuwa nikimfahamu tangu zamani ila
jana nilipigiwa simu na msichana aliyejitambulisha kwa jina hilo akaniambia nikutane naye kwa sababu ana taarifa za mali za marehemu babu yangu”
“Alikwambia anaitwa Ummy Sharifu Nasri?”
“Ndiyo”
“Alikuelekeza uje kwenye nnyumba hii?”
“Ndiyo”
“Uliwahi kumuona yeye mwenyewe?”
“Nilimuona jana”
“Una hakika kwamba ulimuona Ummy?”
“Ndiyo nnilimuonna”
“Nikikuonesha picha yake unaweza kumtambua”
“Ndiyo nitamtambua”
“Hebu subiri”
Mzee alionesha wazi nilimchanganya akili. Aliinuka kwennye kiti akaingia
ndani.
Sikujua ni kwanini alitaharuki. Baada ya muda kidogo alitoka akiwa ameshika kitabu cha picha.
“Hebu sogea hapa karibu” akanniambia huku akifungua karasa za kile kitabu.
“Hebu angalia hii picha. Msichana uliyemuona ndiye huyo?”
Mzee alinionesha picha moja ya ukubwa wa bahasha ya barua. Ilikuwa ikumuonesha yule msichana akitabasamu.
“Ndiye huyu?” Mzee akaniuliza.
“Ndiye yeye”
“Mtazame vizuri”
“Nimemtazama vizuri, ndiye yeye Ummy Sharif Nasri”
“Unaponiambia hivyo unanichanganya…!”
ITAENDELEA
Daah story kali sana!
 
Sawa msalimie shemela na kitoto cha shilawadu kama ataƙileta usiku huu
 

Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom