Sitompongeza Kagasheki kwa hili, linadhihirisha uozo Serikalini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitompongeza Kagasheki kwa hili, linadhihirisha uozo Serikalini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mjomba wa taifa, Aug 15, 2012.

 1. Mjomba wa taifa

  Mjomba wa taifa JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 232
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  NI juzi tu toka Waziri wa Maliasili na Utalii kutangaza kuwafukuza kazi viongozi waandamizi katika wizara yake upande wa wanyama pori kwa sakata la kutorosha wanyama na ndege nje ya nchi.

  Ni wazi kuwa katika taratibu za kusafirisha wanyama nje ya nchi ni idara nyingi zinahusika kuhakikisha taratibu zinafuatwa ikiwa ni pamoja na mamlaka ya uwanja wa ndege, askari wa doria barabarani mpaka kufika uwanja wa ndege,Usalama wa Taifa n.k
  Hivyo basi bila kuwajibishwa kwa mfumo mzima hakuna maana ya kutoa pongezi bali itakuwa ni ujinga kutoa pongezi kwa kitu kidogo kama hizo hali ya kuwa upo upuuzi mkubwa na hakuna anaewajibika ktk Serikali. Hizo idara nyingine zipo wapi kutoa ripoti zao? Mbona hatuambiwi yule mkuu wa Wilaya na OCD waliokwenda kuchimba dhahabu ktk hifadhi ya Taifa kule Serengeti wameishia wapi.

  Kama mamlaka zimeshindwa kuona utoroshaji wa Wanyama wakubwa kama Twiga inakuwaje kwa vitu vidogo kama vipande vya Almas, Dhahabu, kete za Cocain?

  Cha muhimu hapa watu wawajibike kwa kuachia ngazi kwa uzembe uliofanyika na unaoendelea kufanyika katika Serikali yote kwani serikali yote ime-paralyze and is now a fragile state. Hakuna kuchekeana hapa huku tunazidi kuumizwa na washenzi wachache.
   
 2. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Full kulindana big fish will always swallow small fish !
   
 3. P

  Paul S.S Verified User

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Angalau ameplay part yake. Ulitaka akamfukuze na OCD na wengine asio na mamlaka nao?
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Aliye karibu Kagasheki amueleze kwamba Mziki tunaotaka kuucheza na kuwapokea Wanyama wetu KIA.
   
 5. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,277
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Well said,me nilitegemea kwamba huu msala utaondoka na watu wengi.Ukiangalia trend nzima kiongozi hapo mpaka uhamiaji wamo.
   
 6. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  We need our Animals back.
   
 7. P

  Paul S.S Verified User

  #7
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Na hutaki wahusika wawajibishwe.................mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake mkuu, wale ndio kagasheki anamamlaka nao kisheria
  Inatakiwa tukomae na wengine waige mfano wake badala ya kuponda kwakuwa wengine wazembe
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,453
  Likes Received: 5,703
  Trophy Points: 280
  wakuu mimi naomba niwe kinyume na kaka aliyetangulia hapo juu.Nampongeza kwa hili ila hawa jamaa Twiga hawakupitia angani walipitia Airport.

  Sasa Mwakyembe tuambie na wewe wafanyakazi wa KADCO waliyokuwepo siku hiyo kwa nini bado wanaendelea na kazi?

  Kulikuwa na walinzi na hao wamefanywaje?
   
 9. peri

  peri JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Umenena vyema mkuu.
   
 10. C

  Careboy wamuntere Senior Member

  #10
  Aug 15, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaweza kuwa right lakini chanzo cha yote ni huko wanyama pori, na kagasheki kwa mamlaka yake ameonyesha uthubutu wa kweli na hivyo anastahili pongezi 100%, kuhusu sekta zingine nazo zina taratibu zake za kuwajibishana pale inapothibitika beyond reasonable doubt, haya siyo masuala ya kukurupuka kuchukua maamuzi kwani yanagusa maslahi ya nchi na hatua za kuchukua lazima ziwe stahiki, makini na za haki, na sio kuleta masifa. na utawala makini makini ni ule unaochukua sastainable action na sio zima moto, na hichi kinachoendelea ni sustainable na wala sio zima moto ndo maana unaona simba mwenda pole anakula nyama taratibuuuuuuuuu, bila kwenda pole ni vigumu kubaini mtandao mzima. sema hujui uongozi ukoje, na unafikiri ni kunyonga tu ukisikia watu wameongea kumbe it is a process towards achievement of the goal.
   
 11. d

  decruca JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hawa waliofukuzwa kazi wakifikishwa mahakamani basi chain yote itakuwa wazi, lkn kama ndio bac mwisho wa adhabu, watakuwa ndio mbuzi wa kafara kwa sakata zima.
   
 12. O

  Omugurusi Member

  #12
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sababu za kumpongeza Alhaji Kagasheki ni kuwa yeye kafanya kazi yake na hakuishia hapo katika taarifa yake kaeleza kuwa kawasiliana na CITES na Serikali ya Qatar. Nahisi anataka Qatar warudishe wanyama wetu. Sasa waliobaki akina Zoka, Waziri Nchimbi na Waziri Mwakyembe nao wafanye kazi yao kama wana ushahidi. Mwisho wa yote tinataka wanyama wetu 136 aina 14 tofauti warudishwe. Nina uhakika wameishazaa (maana toka Novemba 2010 ni kipindi kirefu), watoto waliozaliwa wabaki nao sisi tupate chetu. HAYA NDIYO MAMBO YA KUJADILI. :A S cry:
   
 13. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Ninafikiri tunachopaswa kukifanya kama watanzania wenye uchungu na nchi yetu ni kuuondoa uongozi mzima uliopo madarakani sasa hivi. Tuanze upya with a clean slate. Wenzetu wa nchi zingine humu humu Afrika wameweza kufanya mabadiliko na kwa kweli wanapiga hatua.

  Tatizo la Tanzania ninavyoona mimi ni kuwa na chama kimoja madarakani kwa zaidi ya miaka 50. Pamoja na kwamba kilianza TANU, baadaye kikabadili jina kilipoungana na ASP na kuunda CCM, bado mfumo wa kiutawala umekuwa ni ule ule. Viongozi ni wale wale. Kwa maana hiyo hatujawahi kufanya mabadiliko ya kimsingi. Hata tulipoanzisha katiba ya vyama vingi, bado mtazamo wa watu walio wengi hasa walio kwenye madaraka ni ule ule wa chama kimoja. Kwa sababu hii hawajali wananchi wanataka nini, wanafikiri bado enzi za 'Chama kimeshika hatamu' kama ilivyokuwa kwenye serikali ya chama kimoja. Ndiyo sababu hata vyama vya upinzani wanavikwamisha na kuviona kama ni vyama vya wasaliti, hata kuthubutu kutamka ya kuwa CCM itatawala milele. Wanajiona ya kwamba ni wao tu wanaoweza kuwa madarakani Tanzania, kama nchi zenye mfumo wa kifalme au kisultani.

  Ndiyo sababu viongozi wanakuwa juu ya wananchi, badala ya wananchi kuwa ndio mabosi wa viongozi, na kuwadhibiti pale wanapokosea. Kwa kuwa wameoza wote, hatuna jinsi ya kujisafisha bila kwanza kuwaondoa wote. Halafu tutachagua wale tunaoona wanafaa tunaweza kuwapa madaraka yanayostahili. La sivyo watatolewa kafara mmoja au wawili, lakini meli bado itaendelea kuzama. Serikali nzima haina dira, kuanzia JK na kushuka chini, wote waondoke kwanza, ndipo tutakapopona!
   
 14. a

  adolay JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,027
  Trophy Points: 280
  Huyu anathubu big up waziri.

  Anatimuwa kulingana na mipaka ya madaraka yake.

  Ni wazi hawezi kumtimuwa rais au wazi mkuu, he has done the job, well done kagasheki ila endelea isiwe nguvu ya peps.
   
Loading...