Sitokaa niwasamehe wazazi wangu kwa kunikatalia kumuoa binti niliyempenda kisa tofauti zetu za Dini

Mi wala nisingesikiliza la nani wala nani, ilimradi familia yangu na mama watoto inaenda fresh, hata wazazi walie wacheke walalamike mie waaaala, mi ndo naishi na mama watoto wao watazamaji tu
 
Ninavyo fahamu mimi; Biblia imekataza kabisa mkristo kuoa mtu asiye kuwa mkristo labda kama abadili dini kwanza awe mkristo ndio aolewe

Sijui kwa nini uwalaumu wazazi wako kiasi hicho wakati ulikuwa UNAENDA KINYUME na Biblia unayo iamini pamoja na kuwa, wazazi wanaweza kuwa na sababu zao za ziada (kama wazazi).

Kumbuka; Wazazi wana nafasi kubwa sana hapa Duniani na kama umeweza kuwasikiliza na kuacha kumuoa huyo bint; nakuomba kama kaka yako uwasamehe!
Mkuu biblia inakataza kusema uongo , kuzini , kutamani n.k
Mbona yote hayo watu wanafanya na hawatengwi na ukoo
Lakini hili la kuoa jamaa ndio atengwe??

Au hadi biblia ina double standard??
 
Mkuu kam Ilham ana mdogo wake fanya unipe namba PM nahisi atanifaa kwa ndoa.
Pili tutakuwa tunadumisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar wakati huu ambao kuna changamoto kibao za muungano..
 
Wazazi nao lakini wakati mwingi huwa ni wajibu wao kumwelekeza mtoto wao,
pia wanatakiwa kumsikiliza mtoto wao na kumwelekeza vizuri pole sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom