Mtoto nae anakua anamtafuta baba yake halali biological,ndo utajua nini maana ya Dunia tambala bovuMkuu mashaka ni upuuzi tu.
Unatakiwa uwe na uhakika kama kweli mkeo kachepuka na kama umehakikisha kachepuka kosa ni la mke sio mtoto.
Mtoto hana kosa mwenye kosa ni mke, ataondoka mke atabaki mtoto, haiwezekani mke nikose na mtoto nikose
Kama mtu mzima unahangaika na kwenda kupima DNA ujue kama mke wako wa ndoa kachepuka au laa basi utu uzima huo ni ovyoHuu uzi utoto ni mwingi kuliko uhalisia. Infact nahisi wengi mnaochangia hapa wala hamjaoa na hata huyo mtoto wa kusingiziwa hamna.
Watu wa Mara wanasema kila mtoto aliyeletwa ndani ya nyumba Mali ya baba
Mkuu toa location ya unakoishi wewe na mkeo naweza fanya ziara yenye mafanikio kwenu na kwangu pia
Aisee kuvumilia mke kuchepuka ukweli mchungu hata mimi siwezi kuvumilia kweli tena nasemaKwa hiyo unafikiri huyu mtoa mada ni mtoto mdogo? Ndo hayo unamwacha mkeo kisa kachepuka tuwe wavumilivu
Ngoja mke Na mtoto wakue ndo utaelewa kwamba Hujui unachosemaNikizaa na mke wangu ukaleta pua yako kuwa mtoto ni wako ukitegemea ntamfukuza au kukuachia mtoto unajidanganya, mtoto sikupi na mke akileta ujinga namtimua,
Yaani mimba nitunze mimi mtoto uje uchukue wewe?
Sheria inasemaje kuhusu hili wakuu??
Unaweza kataa kata kata kua mtoto sio wao na je hao wenye mtoto wakaja kudai mtoto, kisheria imekaaje hii.
Huenda watu wanaogopa hilo kua unaweza kulea mwisho wa siku ikaamuliwa kua mtoto si wako.
Haina haja ya kupima , mwanamke umemkuta si bikra sasa DNA ya nn , apo ni kutafuta Kabuli au majengo ya selikali
Wakati huo mke wake wake na mchizi bado anaendelea kuishi naye au alitimuliwa baada ya kumzaa huyo mtoto?Kuna jamaa maeneo ya pale magomeni DSM mke wake alizaa mtoto muarabu na yeye ni mswahili,jamaa akasema huyu ni mwanangu na haendi popote,bahati nzuri wakati ule hakuna ambae alikuja kudai kama ni mwanae yule mtoto,jamaa akaendelea kulea mpaka wakahamia kigoma mtoto anazidi kukua na uarabu unazidi jamaa akasema huyu ni mwanangu.
Baadae mtoto kakua familia ya waarabu ikaenda mpaka kigoma kuomba msamaha na kusema yule mtoto ni wao na kweli mtoto kafanana na wale jamaa,mzee kagoma hasa na hakutoa mtoto.
Kwa hiyo mkuu ni maamuzi tu haya mambo
Jamaa aliishi naye yule mwanamkeWakati huo mke wake wake na mchizi bado anaendelea kuishi naye au alitimuliwa baada ya kumzaa huyo mtoto?
Mkuu yule jamaa nimeulizia bado yupo na mkewe na mwanawe yule yule,hajamuacha mkewe.Wakati huo mke wake wake na mchizi bado anaendelea kuishi naye au alitimuliwa baada ya kumzaa huyo mtoto?
Mimi nitalea.Staki mambo ya DNANi upuuzi wa hali ya juu sana kwenda kupima D.N.A kwa kigezo cha kutaka kuhakikisha eti kama mtoto ni wako a sio wako.
Watu wanatafuta watoto kwenye ndoa zao wewe unapata unajifanya kwenda kufanya DNA kutaka uhakika.
Tulipopata mtoto wife akaniuliza kimasihara kwamba mtoto hajachukua sura zetu? Nikamuambia maadamu ulihakikisha unamzaa basi huyo ni wetu na mimi ndio baba yake.
Ingelikuwa watoto lazima wafanane na wazazi wao basi dunia nzima wpte tungekuwa na sura ya ADAM na hawa mana ndio binadamu wa mwanzo(kwa mujibu wa imani kadhaa).
Alafu uzuri ni kuwa hata kwa Mungu haupati dhambi ukijimilikisha mtoto kama huyo,yani kila upande unanipa sapoti.
Mimi mtu akipanda ndizi kwenye shamba langu sina haja ya kutafuta nani kapanda,zikiota nitakula na siulizi kitu chochote.
Kama mtu kaja kuweka laki moja yake kwenye mfuko wa suruali yangu alafu akaondoka mimi natumia hizo pesa na wala siulizi chochote.
Na kwa mtoto hivyo hivyo mtu kajipendekeza kupachika mimba kwa mkeo wewe mhodhi mtoto anakuwa wako daima.
Mtoto ni mali ya wazazi kama mungu amejaalia mtoto amezaliwa kwenye ndoa yenu usimuache komaa nae mpaka akue hata kama sio wako kibaiolojia ila ukimlea kimapenzi atakuita baba na atakuwa na mapenzi ya kweli kama baba yake mzazi tu.
Kinachowaweka karibu baba na mtoto sio uhusiano wa kibaoolojia bali ni ukaribu katika malezi yao,hivyo hata kama sio mwanao biologically lakini kimalezi atakuwa mwanao na mtaishi kwa upendo na yeye atajua hivyo.
NB : endapo unaishi na mtu hujamuoa alafu mnapiga washkaji kibao na demu akapata mimba hapo naweza kuona umuhimu wa DNA kwa sababu mali haina mtu maalumu hivyo DNA itatoa majibu nani mwenye mtoto.