Sitishwi na uzushi - Nape Nnauye

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]WEDNESDAY, 31 AUGUST 2011 20:03 NEWSROOM uhuru publications


anape%20leo.jpg










NA MWANDISHI WETU UHURU PUBLICATIONS

KATIBU wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema hajawahi kufanya mawasiliano na ofisa usalama yeyote ili kuandaa mgombea urais wa mwaka 2015.

Amesema uzushi huo haumtishi na ataendelea kutetea maslahi ya CCM. Nape amesema habari zilizoripotiwa na gazeti moja la kila wiki zikidai anamuandaa mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2015, hazina ukweli na zina lengo la kuwapotosha wananchi. Gazeti hilo lililoripoti ÔSiri za Nape njeÕ limetakiwa kutoa uthibitisho wa mawasiliano hayo. Nape amesema atawajibika iwapo itathibitika ni kweli.

Kuna siasa za uongo na uzushi zimekuwa zikiendelea kwa lengo la kuharibu dhana nzima ya kujivua gamba ndani ya CCM,alisema. Nape alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi na wanachama wa CCM kuendelea kuwa na mshikamano na kupuuza maneno ya uzushi. Alisema Chama bado kiko imara na kinaendelea na harakati za kujijenga upya na kuwa karibu na wananchi. Gazeti hilo limedai Nape amekuwa akifanya mawasiliano na ofisa usalama Lucy Mwandosya.
Hata hivyo, taarifa za uhakika zinasema Lucy, ambaye ni mke wa Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, si ofisa usalama na hivi sasa anamuuguza mumewe nchini India.
Alisema habari hiyo ni mkakati wa uendelezaji siasa chafu dhidi yake, zenye lengo la kumfunga mdomo ili ashindwe kupigania maslahi ya CCM.
Kada huyo wa CCM alisema suala la kuandaa mgombea si kazi yake, bali ya Chama na kwamba, hajatumwa kufanya kazi hiyo kama ilivyopotoshwa.
ÒNitaendelea kutetea maslahi ya Chama, hizi siasa za uzushi kamwe hazinitishi. Hakuna vita ya kutafuta mgombe urais ndani ya CCM na muda ukifika Chama kina taratibu zake,Ó alisema.

LAST UPDATED ( WEDNESDAY, 31 AUGUST 2011 20:27 )
 
Nape ni victim wa dhana halisi ya ukweli na uwazi na kwa vyovyote vile ataandamwa na 'kashfa' nyingi kwa sababu tu ya msimamo wake, hasa dhidi ya vitendo ambavyo vimeipotezea haiba CCM. Mwanzoni walisema anapotosha dhana ya kujivua gamba na kwamba hakutumwa hivyo na Mwenyekiti. Pale Mwenyekiti alipomtetea wakagundua kwamba si mropokaji na sasa wamempachika kundi ambalo hata hivyo halipo. Hata hivyo kuna dhambi gani kwa yeye kumuunga mkono yeyote kati ya wale wenye nia ya kugombea uongozi wakati tunafahamu kwamba wale wanaozua huo uvumi nao wana wagombea wanaowandaa? Nape endelea kukaza buti, umeshawakamata pabaya.
 
Hao CCM wanajiandaa na kikao cha NEC cha vuta ni vute, piga ni kupige huku kila upande ukidai Rais yupo nao! Rais wetu kiboko, juzi kama nimesikia jamaa mmoja wa kwa EL akitamba kuwa Rais yupo upande wao na mwisho wa siku watu watashangaa kama walivyoshangaa Mkapa akimkana SAS na kumpigia kampeni Kikwete!

Hawa CCJ nao wanapiga jaramba kifua mbele kuwa Rais yupo nao na ndio kawapa maagizo ya kuvua gamba! Rais yeye mwenyewe mimi sijawai kumsikia kwenye Umma kwa kauli yake binafsi kujuwa lipi ni lipi! Njoja tusubiri Kikao ndio dakika 90 zao.
 
Miaka 50 ya uhuru bado tuna watu waropokaji,na wanoshindwa kufikiri kama Nape kweli hii ni ajabu. VIJANA WA CHADEMA MUDA NDIO HUU POPOTE TULIPO TUWEKE MIKAKATI YA KUIKOMBOA toka kwa watu kama hawa.
 
Nape ni mnafiki tu, wakati wa kuvua gamba, alisema nini juu ya rostam, lowassa na chenge?????????????????????????, yeye ni kijana wa uongo na unafiki,, kama bibilia inasema SHETANI NI BABA WA....................
 
Acheni kupoteza muda kumuongelea huyo looser .Mbona mnampa kichwa sana huyu kiongozi wa CCJ na CCM ?Hana lolote tuongelee hoja za maana.
 
Nape hunajipya hayoyote ndio uliyataka ukiingia kwenyesiasa za maji taka na wewe lazima uwe taka
 
nape ni victim wa dhana halisi ya ukweli na uwazi na kwa vyovyote vile ataandamwa na 'kashfa' nyingi kwa sababu tu ya msimamo wake, hasa dhidi ya vitendo ambavyo vimeipotezea haiba ccm. Mwanzoni walisema anapotosha dhana ya kujivua gamba na kwamba hakutumwa hivyo na mwenyekiti. Pale mwenyekiti alipomtetea wakagundua kwamba si mropokaji na sasa wamempachika kundi ambalo hata hivyo halipo. Hata hivyo kuna dhambi gani kwa yeye kumuunga mkono yeyote kati ya wale wenye nia ya kugombea uongozi wakati tunafahamu kwamba wale wanaozua huo uvumi nao wana wagombea wanaowandaa? Nape endelea kukaza buti, umeshawakamata pabaya.

ukitaka kujua nape ni kigeugeu na hana msimamo kabisa sikiliza anavyolamaba matapishi yake igunga kumhusu rosata azizi
 
Back
Top Bottom