nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
[h=2][/h]WEDNESDAY, 31 AUGUST 2011 20:03 NEWSROOM uhuru publications
NA MWANDISHI WETU UHURU PUBLICATIONS
KATIBU wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema hajawahi kufanya mawasiliano na ofisa usalama yeyote ili kuandaa mgombea urais wa mwaka 2015.
Amesema uzushi huo haumtishi na ataendelea kutetea maslahi ya CCM. Nape amesema habari zilizoripotiwa na gazeti moja la kila wiki zikidai anamuandaa mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2015, hazina ukweli na zina lengo la kuwapotosha wananchi. Gazeti hilo lililoripoti ÔSiri za Nape njeÕ limetakiwa kutoa uthibitisho wa mawasiliano hayo. Nape amesema atawajibika iwapo itathibitika ni kweli.
Kuna siasa za uongo na uzushi zimekuwa zikiendelea kwa lengo la kuharibu dhana nzima ya kujivua gamba ndani ya CCM,alisema. Nape alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi na wanachama wa CCM kuendelea kuwa na mshikamano na kupuuza maneno ya uzushi. Alisema Chama bado kiko imara na kinaendelea na harakati za kujijenga upya na kuwa karibu na wananchi. Gazeti hilo limedai Nape amekuwa akifanya mawasiliano na ofisa usalama Lucy Mwandosya.
Hata hivyo, taarifa za uhakika zinasema Lucy, ambaye ni mke wa Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, si ofisa usalama na hivi sasa anamuuguza mumewe nchini India.
Alisema habari hiyo ni mkakati wa uendelezaji siasa chafu dhidi yake, zenye lengo la kumfunga mdomo ili ashindwe kupigania maslahi ya CCM.
Kada huyo wa CCM alisema suala la kuandaa mgombea si kazi yake, bali ya Chama na kwamba, hajatumwa kufanya kazi hiyo kama ilivyopotoshwa.
ÒNitaendelea kutetea maslahi ya Chama, hizi siasa za uzushi kamwe hazinitishi. Hakuna vita ya kutafuta mgombe urais ndani ya CCM na muda ukifika Chama kina taratibu zake,Ó alisema.
LAST UPDATED ( WEDNESDAY, 31 AUGUST 2011 20:27 )