Sitegemei Show za Dar - Izzo Bizness

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,485
54,855
Msanii kutoka 'Green City' akiwakilisha kundi la The Amaizing, Izzo Bizness amedai hawezi kulala njaa kusubiri simu za promota kwa ajili ya show kwani kipaji anacho ndio maana anajiongeza zaidi mikoani.
izzo%20bz.jpg

Msanii Izzo Bizness

Izzo amefunguka hayo baada ya maswali mengi kuzuka kwa nini hana 'show' nyingi Dar Es salaam kama mikoani, na kueleza kwamba muziki ni biashara yake hivyo hataweza kubweteka huku biashara yake inaharibika..

"Sikai kutegemea mpaka Promota anipigie simu kuhusu show maana hapo kuna kuna kuanza mazungumzo na kushushana bei, ila natengeneza mwenyewe najijua mikoa flani ndani ya Tanzania nakubalika nachukua opportunity hiyo kutengeneza show hizo peke yangu na mwisho wa siku maisha yanaendelea. Haipendezi msanii kama mimi nianze kupiga vizinga hadi vya vocha , Hata prof. Jay aliwahi kusema kama kipaji unacho kwa nini ufe na njaa, na ndivyo nifanyavyo mimi ", Izzo alifafanua

Aidha Izzo ameongeza kwamba pamoja na changamoto kama kundi la The Amaizing wanazokumbana nazo amewataka wasanii waimbaji wajipange sana kwani ujio wa Abella Music lazima uwatingishe kwenye game.

abella%20izo.jpg


"Kwa sasa The Amaizing tuna changamoto ukizingatia Abella ni mgeni ndo anaanza kutengeneza mashabiki kwa hiyo na uhakika akishapata kile anachohitaji atakuwa moto balaa na nitoe angalizo kwa waimbaji siyo kwa kuwa-disrespect hapana ila ujio wa Abella lazima uwasumbue hivyo wajipnge sana", Izzo aliongeza.

Chanzo: EATV
 
Jamaa tangu awe kwenye kundi naona kama uwezo wake umeshuka vile!
Hivi huyu mwanamke ni mpenzi wake au wapo kibiashara tu?
 
Mahaba kwenye muziki hayajawahi kumuacha msanii salama, huyo demu anampoteza bila yeye kujua
 
Jamaa kinacho mbeba ni muonekano anajua kutupia but kimuziki kwa kweli hamna kitu nyimbo zake zote hazieleweki ukiacha Riz1,bora hata ya HarmoRapa.
 
ZILIPENDWA IZZO JISHUGHULISHE NA KILIMO MAANA MBEYA ARDHI INA RUTUBA
 
Sioni cha maana anachofanya kwenye muziki. Huyu jamaa afanye shughuli zingine maana shule ameenda si haba, labda kama alisoma kwa kukariri. Kipaji cha muziki hana kama anavyojiona yeye. Naamini ana uwezo wa kufanya mambo mengine vizuri zaidi. Ni moja ya "macelebrity"wanaojielewa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom