Sitashangaa "VOTE OF NO CONFIDENCE" ikapigwa kabla ya 2015...

what if badala ya kupiga kura ya vote of no confindence, wabunge watawashawishi wananchi kuingia street? Hii itamwathiri nani?
 
what if badala ya kupiga kura ya vote of no confindence, wabunge watawashawishi wananchi kuingia street? Hii itamwathiri nani?

Wabunge wapi hao mkuu wenye guts hizo
hawa hawa wa magamba siamini kama wanaweza kufanya hayo
 
Wabunge wapi hao mkuu wenye guts hizo
hawa hawa wa magamba siamini kama wanaweza kufanya hayo

Wabunge wote bila kujali itikadi! Wawapatie wananchi data za kutosha, kisha wao wakae nyuma kwa kuhofia vyama vyao kuwawajibisha...kisha mwendo mdundo! Jamii itaishinikiza serikali kwa mbinu zote ili iheshimu utawara bora
 


Wabunge wote bila kujali itikadi! Wawapatie wananchi data za kutosha, kisha wao wakae nyuma kwa kuhofia vyama vyao kuwawajibisha...kisha mwendo mdundo! Jamii itaishinikiza serikali kwa mbinu zote ili iheshimu utawara bora

Mkuu uonavyo kwa wabunge wengi wa magamba kuna mwenye utashi huo wakati wanalilia posho na mishahara mikubwa zaidi pale
hakuna utashi huo kwa wabunge weutu wanasema mdomoni ila mioyoni hakuna kitu
 
Jamani kwa wale ambao wamekuwa wakifuatilia mienendo ya mabunge ya Tanzania hata ukichukulia mfano wa bunge lililopita tu la tisa utagundua kwamba hata hao wabunge wa CCM nao wanasoma alama za nyakati.

Mtakubaliana na mimi kwamba hivi juzi tu wakati bunge la kumi linaanza hakuna hata mbunge mmoja wa CCM ambaye angemuunga mkono Zitto wakati anatoa hoja ile lakini kwa walioona hii asubuhi watakubaliana na mimi kwamba NOTHING LASTS FOREVER

Naona wamekuja na strategy ya kuwa pre-empty magwanda; inakuwa afadhali kwenye public opinion kuliko kuwa pinga maana wakiwapinga huko mtaani elimu ya uraia imekolezwa na maandamano! Magwanda nao wanatakiwa kuangalia jinsi ya ku counter-attack maana hii issue tangu mwanzo ni bomu limeteguliwa wakaona wamelitegua kwa staili ya kuumiza ma key players na madhara yake ni makubwa kuliko kisiasa maana hao huwa wanafanya kweli haiishi kwenye maneno.

Safari hii wamejaribu strategy ya ku by time nakusoma mchezo vizuri ndiyo maana hawakuruhusu malumbano ya muda mrefu ila kufikia conclusion kwakuwapa credit magamba kwamba waliboresha hoja....Lakini all in all hakutakuwa na afadhali yeyote hali itakuwa mbaya zaidi kuliko hata sasa kwani kila pumzi yenye uhai inatekeleza agizo la mwana wa Mfalme ambaye serikali zote za dunia huwa chini yake! Njia pekee nikukubali kuondoa kizazi hiki kiovu cha mafisadi mbali na hapo Mungu hawezi tulia mpaka hilo litimie jipeni tu moyo muone jinsi lilivyo kweli neno lake kuwa kila goti lazima lipigwe mbele yake na kila ulimi ukiri kuwa yeye ni Bwana!
 


Wabunge wote bila kujali itikadi! Wawapatie wananchi data za kutosha, kisha wao wakae nyuma kwa kuhofia vyama vyao kuwawajibisha...kisha mwendo mdundo! Jamii itaishinikiza serikali kwa mbinu zote ili iheshimu utawara bora

Usiwe na haraka sana mbona ukuta wa jeriko ulidondoka bila yeyote kuugusa? We subiri uone magamba yatakavyo geukiana na kujisambaratisha wenyewe nakutukabidhi utawala wetu bila kuwaomba kufanya hivyo; na ndipo sasa sisi kwa raha zetu tutapanga tuende mwendo na style tuitakayo na si hii ya wachache kula nyama huku wengine wakila nyasi kama walivyotuambia siku za nyuma. Ndege yao iliyopaa imepata hitilafu angani rubani anajitahidi lakini inaoneka injini ya akiba nayo imeharibika na kuna hatari ikashika moto soon!
 
TF uko kama mimi hii kitu siamini na haitotokea
Ngoja niweke hapa kifungu cha katiba uone mlolongo ilivyo mrefu na ambao magamba hawatakubali hata tone


46A]46A. Bunge laweza kumshtaki Rais Sheria Na. 20 ya 1992 ib. 8; 12 ya 1995 ib. 4
(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais–
(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au sheria ya maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba; au
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.
(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu kama–
(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa aliyoyatenda Rais, na ikipendekeza kuwa Kamati Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze mashtaka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;
(b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na kama ikiungwa mkono na Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, atatangaza majina ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.
(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani–
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;
(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar; na
(c) Wabunge saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa uwakilishi baina ya vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni.
(5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya ibara 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashtaka yaliyotolewa dhidi yake.
(6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuundwa, itakaa, ichunguze na kuchambua mashtaka dhidi ya Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
(7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa yake kwa Spika.
(8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
(9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.
(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge lilipopitisha azimio hilo.
(11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na mashtaka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.

Wanajua haya yote..tatizo wamelishwa unga wa ndele..wengi wao wa CCM wameacha akili na utashi wao pale Lumumba na Dodoma makao makuu..wakiingia bungeni wanakua kama mazombi...
 
Hapa ni kuangalia kwenye weak point and its sensitive, then unaanzia hapo vinginevyo tukitakai kucheza kotekote hawa Magamba hatuwawezi kwa sasa. They made the rules for their long term interests.
 
Inawezekana kuna technical error kwenye report ya CAG ama inawezekana mtoa hoja alitumika ili kupoza joto la hoja za umeme na mafuta zilizokuwa zinaibana serikali kipindi kile...., lakini Watanzania wanajua na wanafuatilia kila kinachojiri.
Haiitaji mnajimu kutabiri hatima ya haya matukio.

Wana JF
Hivi CAG anatetea serikali au Wananchi?
CAG wakati wanakakua huwa wana consider maswali ya kipolice au kiusalama kama wanavyo hoji watuhumiwa?
CAG katka sakata la Jairo Je yeye ni police pia ni mahakama? huwa hakuna chombo kingine kinacho iuliza cabinet ya CAG baada ya auditing?
 
Wanajua haya yote..tatizo wamelishwa unga wa ndele..wengi wao wa CCM wameacha akili na utashi wao pale Lumumba na Dodoma makao makuu..wakiingia bungeni wanakua kama mazombi...

Wanajua na wanaijua kabisa katiba na inasema nini kuhusu hilo ila wakishakuwa mle ndani wanakumbuka posho tuu na marupurupu wanayopata hawakumbuki tena kuwa kuna wananchi waliowatuma
 
Wabunge wapi hao mkuu wenye guts hizo
hawa hawa wa magamba siamini kama wanaweza kufanya hayo
Jamani mi nafikiri wabunge wa CCM sio wajinga kiivyo kwamba hawawezi hata kusoma alama za nyakati i am just trying to see the fast change of this bunge, its not the same even when this budget session started na leo linapoelekea kwisha
 
Kwa mlolongo wa kikatiba ulivyo, ni ngumu sana kuwa na vote of no confidence hasa kwa bunge hili lenye wabunge wengi wa CCm pamoja na wale wa kuteuliwa (CCM)n wauza sura bungeni
 
Kwa mujibu wa mtazamo wangu wa hali ya siasa na bunge katika bunge hili la kumi, nadiriki kusema kwamba sitashangaa sana kama kabla ya mwaka 2015 bunge likaomba kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali hii.

Serikali watch your back you are running solo and soon you will meet an hungry Lion, believe me it wont leave you
Kwa wabunge hawa wa magamba, walioitwa na Jairo kuwa Ze Comedy, SIDHANI..................
Bunge livunjwe wakose posho? THUBUTU.................
 
Jamani kwa wale ambao wamekuwa wakifuatilia mienendo ya mabunge ya Tanzania hata ukichukulia mfano wa bunge lililopita tu la tisa utagundua kwamba hata hao wabunge wa CCM nao wanasoma alama za nyakati.

Mtakubaliana na mimi kwamba hivi juzi tu wakati bunge la kumi linaanza hakuna hata mbunge mmoja wa CCM ambaye angemuunga mkono Zitto wakati anatoa hoja ile lakini kwa walioona hii asubuhi watakubaliana na mimi kwamba NOTHING LASTS FOREVER

Mkuu hiyo rangi inamaabisha sasa wameanza kukomaa na fikra zao zinageuka kuwa pevu!!!!! la vote of no confidence lawezekana!!!!!

VUGUVUGU LA MABADILIKO YA KISIASA NI KAMA MAJI USIPOYANYWA UTAYAOGA, USIPOFULIA UATAPIKIA NK. It is unkwepable!!!!!!
 
Mkuu hiyo rangi inamaabisha sasa wameanza kukomaa na fikra zao zinageuka kuwa pevu!!!!! la vote of no confidence lawezekana!!!!!

VUGUVUGU LA MABADILIKO YA KISIASA NI KAMA MAJI USIPOYANYWA UTAYAOGA, USIPOFULIA UATAPIKIA NK. It is unkwepable!!!!!!
Hiyo ilikuwa inaonyesha msisitizo tu kidogo wala haina maana yoyote
 
Mara ya kwanza suala la Katibu wa wizara ya nishati na madini lilipoibuliwa bungeni, liliibua taharuki na sintofahamu kubwa mpaka kwa wananchi/mitaani.
Waziri mkuu japo hakutoa kauli ya moja kwa moja, lakini alionyesha muelekea wa ni hatua gani angezichukua kama angekuwa na mamlaka juu ya mtuhumiwa, suala lilipofika kwa rais rais alimuagiza waziri mkuu asichukue hatua yoyote mpaka atakaporudi toka safarini (South Africa), lakini akiwa huko South Africa akamuamuru Katibu mkuu Kiongozi kufuatilia kuhusu sakata hilo. Waziri mkuu kiongozi akampa jukumu hilo CAG, na ikatolewa report iliyoibua mshangao na hasira miongoni mwa wana jamii, wananchi na wabunge upande mmoja huku Ikulu, Waziri (wa Madini) na wafanyakazi wa wizara nao wakiwa upande mwingine katika umoja wao.

Katika hali ya kawaida ni vigumu sana kuielezea report ile hata iingie akilini. Pamoja na maelezo mengi ya report lakini kuna eneo katika report ile linasema suala kuchangia ni la kawaida, kama suala hili ni la kawaida mbona waziri husika akiwa bungeni alikana kufahamu lolote kuhusu michango hiyo, na kwa upande wa waziri mkuu japo hakuongelea kuhusu kufahamu au kutofahamu lakini msimamo alioutoa unaonysha kuwa hafahamu chochote kuhusiano na mpango huo au michango hiyo.

Kura ya kutokuwa na Imani ya rais



Suala la kura ya kutokuwa na imani na rais linaibuka na kupata nguvu kila siku kwasababu linarutubishwa na mazingira yafuatayo:
Katibu mkuu kiongozi alifanya uchunguzi kwa maelekezo ya mheshimiwa rais, ni dhahiri kuwa report ile pamoja na kile kinachotafsirika dhahiri kuwa ni dharau kwa bunge, ilipata baraka za rais kabla ya kusomwa, haiwezekana Katibu kiongozi atangaze hadharini report kabla ya kuipeleka kwa aliemtuma, na huo ndiyo utaratibu (Ikumbukwe kuwa hata report ya Mwakyembe japo ilikuwa ni ya Bunge lakini kabla ya kutolewa rasmi, rais alipelekewa ili apate fursa ya kuiona). Hivyo kitendo cha Katibu wa Wizara ya Madini kurejeshwa ofisini lazima kilipata baraka za rais.

Maamuzi tata, yaliyokosa msimamo kwa kukosa makanyagio yanayotolewa na Ikulu yameonyesha yanaonekana kuwadogosha (wanapofananishwa na wanavituko)kuwadhoofisha na kufinya uwezo wa bunge, hili linawalazimisha wabunge wajihoji nafasi yao kikatiba, na kwenda mbali zaidi na kujiuliza kama wao na serikali wapo kwa ajili ya wananchi je jitihada hizi za kuwadhoofisha na kuwadharaulisha mbele ya jamii, zinafanyika kwa maslahi ya nani?

Ni kama vile rais amegoma kuumiza kichwa juu ya mambo ya kimsingi, anapenda kutumia moyo wake katika kufanya maamuzi juu ya mambo magumu badala ya ku-reason, (nilishapata kuongea kuwa ile layer inayomzunguka ina mchango mkubwa sana katika kumfanya aonekane hafai mbele ya jamii, kwa nafasi yake na watu wamzungukao, hatakiwi hata kumuamini mtoto wake).

Jitihada nyingi zimefanyika ili kuikwamua nchi Lakini hilo limeshindikana na kuzidi kuisokomeza nchi katika migogoro na mijadala isiyojenga wala kuashiria masuluhisho yoyote, hapo hapo kuna watu wanaojiona na akili kuliko wote wanajaribu kutupotosha kwa kusema kitendo cha watu kuongea kwa uhuru ni muashirio uhuru tunaopewa na kukomaa kwa democrasia, ni democrasia gani hii ambayo inawapo uhuru the public enemies, na kuzidi kuzorotesha hali za maisha ya wananchi na kufutilia mbali hata matumaini madogo waliokuwa nayo?

Ubabe na hali ya kutojali inayoonyeshwa serikali dhidi ya bunge inazidi kukaribisha wazo hili vichwani mwa wachache japo ni vigumu kulipa uzito kutokana na asili na historia yetu, japo sasa hivi kuna msukumo wa upepo wa kinyakati ambao hautegemei sana au hata kabisa historia wala asili. Sasa sijui kama hatma yetu itaamuliwa na historia na na asili au msukumo utokanao na upepo wa mabadiliko unaovuma hivi sasa...

Kamati ya bunge ipo kwenye mchakato wa kuundwa, naamini katika uchunguzi wao watagundua mambo mengi ambayo yataamsha hasira ambayo haitaishia tu ndani ya bunge bali itasamba na kuenea mpaka huku kwetu miembeni kwa wakina kapuku tusio na cha kupoteza katika maisha haya.....Je katikati ya sakati hili wakati report inajadiliwa akainuka mmoja na kuomba ipigwe vote of no confidence kutakuwa na kurudi nyuma? Sidhani...labda kama hatma yetu inategemea kuamuliwa na historia na asili, na si kama inategemea upepo wa mageuzi unaosambaa kwa kasi duniani kote hivi sasa.......
Je bunge litamsitiri rais??? Tusubiri...tutaona....
 
Wapo wengi wanaotamani iwe kama unavyofikiri mkuu..ila naamini utakubali kwamba hizi ni hisia tu na si rahisi kutokea katika nchi yetu.
 
Back
Top Bottom