Sitashangaa "VOTE OF NO CONFIDENCE" ikapigwa kabla ya 2015... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitashangaa "VOTE OF NO CONFIDENCE" ikapigwa kabla ya 2015...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by M'Jr, Aug 24, 2011.

 1. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Kwa mujibu wa mtazamo wangu wa hali ya siasa na bunge katika bunge hili la kumi, nadiriki kusema kwamba sitashangaa sana kama kabla ya mwaka 2015 bunge likaomba kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali hii.

  Serikali watch your back you are running solo and soon you will meet an hungry Lion, believe me it wont leave you
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Haupo TZA wewe, otherwise una kila sababu ya kushangaa sana tu.

  Hii nchi ipo sayari nyingine
   
 3. R

  Rweza Member

  #3
  Aug 24, 2011
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hilo nakuunga mkono maana kwa mwenendo huu nachelea kusema kama mzee wa kaya atamaliza kipindi chake cha miaka mitano.
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Aug 24, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Tz ndiyo ile nchi ya kusadikika, hilo haliwezitokea chini ya wabunge wa serikali hii ya chama tawala
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mh! kwa hii mibunge ya CCM haiwezekani!
   
 6. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Itapigwa vote of confidence na maandamano ya kuiunga mkono serikali .......
   
 7. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Jamani kwa wale ambao wamekuwa wakifuatilia mienendo ya mabunge ya Tanzania hata ukichukulia mfano wa bunge lililopita tu la tisa utagundua kwamba hata hao wabunge wa CCM nao wanasoma alama za nyakati.

  Mtakubaliana na mimi kwamba hivi juzi tu wakati bunge la kumi linaanza hakuna hata mbunge mmoja wa CCM ambaye angemuunga mkono Zitto wakati anatoa hoja ile lakini kwa walioona hii asubuhi watakubaliana na mimi kwamba NOTHING LASTS FOREVER
   
 8. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  kwa Tanzania??? migamba ya ccM???????

  haiwezekani hata kidogo
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Aug 24, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mkuu hapo nakuunga Mkono. Hii mibunge ya ccm ndivyo walivyo. Wanachojali wao ni posho zao si kingine. Hawajali hata kama kanuni zinapindishwa for them is not an issue.

  Hata hili sakata la Jairo ngoja tuone kamati itakayoundwa. Kwa vyovyote watayakubali maamuzi ya Luhanjo, unless mwenyekiti wa kamati atoke chadema ndiyo tutarajie vinginevyo.
   
 10. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wabunge wengi wa magamba hawakupita kihalali, hawewezi kujivika kitanzi kurudi kwenye uchaguzi! Njia pekee inabaki ya MANDAMANO! Serikali imekosa mwelekeo.

  Tunashuhudia video kibao, Alianza Nape vs Magamba (RACHEL), Masaburi Vs Zungu na Mtemvu, Imeingia picha ya Telele na Msekwa na ingizo la sasa ni kali kuliko ni Luhanjo (Jairo, Ngeleja) kwa upande mmoja na Bunge (pinda,sherukindo) kwa upande mwingine. Mwenyekiti naye anaangalia move kama sisi.
   
 11. Paw

  Paw Content Manager Staff Member

  #11
  Aug 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,032
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Inawezekana kuna technical error kwenye report ya CAG ama inawezekana mtoa hoja alitumika ili kupoza joto la hoja za umeme na mafuta zilizokuwa zinaibana serikali kipindi kile...., lakini Watanzania wanajua na wanafuatilia kila kinachojiri.
  Haiitaji mnajimu kutabiri hatima ya haya matukio.
   
 12. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Na hapo ndipo panaponitia shaka zaidi kaka, ni bora wabunge wakafanya maamuzi kabla ya wananchi hawajafanya maamuzi maana ya wananchi yanafika mbali zaidi
   
 13. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Bunge lipi unalotegemea lipige vote of no confidence?? Je ni hili lililojaa wabunge wa magamba wanaofikiri kwa kutumia masaburi yao na linaloongozwa na bikiroboto??? Haitatokea asilani!!
   
 14. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  mkuu sijui kama kwa tanzania hii na wa bunge letu lile kuna mwenye ubavu wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali
  Mlolongo ni mrefu sana na ukisoma katiba ni issue sana kuwa na kura ya aina hiyo
   
 15. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Over my dead body, you guys can continue dreaming of "Vote of no Confidence".
   
 16. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,153
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Tukiendelea na mwendo kama wa asubuhi hakika itawezekana mi sijawahi kuona wala kusikia wabunge wa magamba wanakubaliana na hoja ya upinzani hata kama itakuwa na mantiki ila tu ni leo asubuhi
   
 17. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  TF uko kama mimi hii kitu siamini na haitotokea
  Ngoja niweke hapa kifungu cha katiba uone mlolongo ilivyo mrefu na ambao magamba hawatakubali hata tone


  46A]46A. Bunge laweza kumshtaki Rais Sheria Na. 20 ya 1992 ib. 8; 12 ya 1995 ib. 4
  (1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.
  (2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais–
  (a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au sheria ya maadili ya Viongozi wa Umma;
  (b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba; au
  (c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.
  (3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu kama–
  (a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa aliyoyatenda Rais, na ikipendekeza kuwa Kamati Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze mashtaka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;
  (b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na kama ikiungwa mkono na Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, atatangaza majina ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.
  (4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani–
  (a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;
  (b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar; na
  (c) Wabunge saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa uwakilishi baina ya vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni.
  (5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya ibara 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashtaka yaliyotolewa dhidi yake.
  (6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuundwa, itakaa, ichunguze na kuchambua mashtaka dhidi ya Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
  (7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa yake kwa Spika.
  (8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
  (9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.
  (10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge lilipopitisha azimio hilo.
  (11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na mashtaka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.
   
 18. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  'Vote of No-Confidence' ni nyenzo ya bunge ambalo wakati wake mwafaka kutumika kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu ni HIVI SASA na wala sio kesho, jamani hili ni gunia la misumari ya moto halibebeki tenaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Hakika VOTE OF NO CONFIDENCE isipotoka bungeni kwa kashfa hii nzito basi waheshimiwa mujiandikie mbele ya nyuso zenu kwamba huku uswahilini WALAZWAHOI tayari tumeshaandaaa kura zetu za kutokua na imani na serikali hii na kazi itaanzia kwenye uchaguzi mdogo Igunga!!!!!!!!!!
   
 19. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Unajua hata wabunge wa CCM wameshaona kabisa kwamba KUUNGA MKONO kwa asilimia 100 hata kama kinachoungwa mkono ni upumbavu hakuwasaidii bali kunawabomoa so kwa mtazamo wangu mimi na tungoje tuone maana najua kwa mwenendo huu hata bajeti ya mwakani sijui kama itapita
   
 20. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hahahaha kwa TZ hii ni ndoto aisee
   
Loading...