Sitashangaa sana ikiwa siku moja kama RC Paul Makonda atapewa uwaziri

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Naandika maoni yangu ama mada yangu huhusu mtu aliyeitwa majina mengi sana ili kimuharibia sifa zake kielimu na ki social. Kinachonishangaza ni kuwa RC Makonda huziba masikio na kukifanya kile anachoona ni haki.

Siandiki mada hii kwa kujipendekeza, maana kazi yangu inanitosha.

Utabiri wangu ni kuwa sitashangaa sana ikiwa huyu RC wa Dar siku moja atapewa uwaziri kamili ama waziri asiye na wizara maalumu hasa kutokana na utendaji wake kikazi. Hivyo kuingilia kila wizara na kurekebisha mambo.

Maana ukweli ni kuwa RC Makonda ni mchapa kazi na ana maono! Sisemi kuwa makonda ni mtu mkamilifu sana, bali kama binadamu ana mapungifu yake na ameteleza mara nyingi na kujirekebisha.

Uzuri wake ni mwepesi sana /kufanya kitu tunachokiita damage control/kurekebisha uharibifu. Na katika mtazamo wangu ni mwepesi sana kushuka na ku pacify mahasidi wake.Katika hilo ninampongeza sana.

Mengi yalisemwa kuhusu elimu yake nk. Matope mengi na takataka nyingi alitupiwa lakini ningeomba tujifunze toka kwa jirani zetu wa Kenya.

Rais Kenyatta hivi karibuni wakati akibuni baraza lake la mawaziri, aliwaacha wakenya wengi vinywa wazi baada ya kumteua mtu mmoja kuwa waziri wa vijana na michezo ambaye hata hakua amemaliza shule ya msingi.
Sina maana kuwa watu wasisome. Maana elimu ni ufunguo wa maisha.

Kilichomvutia Rais Kenyatta ni CV yake ya utendaji na si masomo na elimu yake. Ukweli jamaa huyu hakuwa amemaliza elimu ya msingi ambayo kwao ni darasa la nane/saba hapa kwetu.

Wazazi wake hawakuweza kumsomesha ila IQ yake ilikuwa juu sana.Kila jukumu katika chama chake cha upinzani alikuwa na ushawishi mkubwa sana.
Kenyatta alipoona hayo akaona huyu mtu ni ni asset.Akamteua awe waziri.

Watu walipiga kelele sana hata wabunge wa chama chake. Hata hivyo Rais alikuwa ameamua bila kujali kiwango cha elimu yake.

Mtu huyo akiwa mbele ya panel ya kumhoji aliweza kujibu kila swali kwa ufasaha mkubwa kwa mshangao wa wana kamati.

Hatimaye wakamwidhinisha kama waziri wa vijana na michezo.Tunavyosikia ameanza magaeuzi makubwa sana kwa mshangao wa kila mtu.

Hii ikiwa ni tofauti na mtangulizi wake aliyekuwa na PhD. Ambaye aliiangusha sana wizara hiyo na kumfanya rais huyo kumwachisha uwaziri.

Na wote wakasema huyu mtu ana akili nyingi sana. Wakampitisha.Kwa hivyo sitashangaa kumwona RC Makonda akipanda kutokana na utendajji wake mzuri.

Maana he has the potential to deliver!
 
Huyo waziri wa Kenya yeye hakufoji vyeti wakati huyu wa kwetu alifoji.Raisi Maghufuli alikuwa kwenye zoezi la kukagua vyeti na wale waliogushi walifukuzwa kazi lakini huyu aliachwa kwa sababu ya uchapa kazi.Je nchi nzima alikuwa mchapa kazi peke yake? Utata ndo ulianzia hapa.
 
Ikiwa hata Juliana Shonza amepata unaibu waziri; seuze dad's son kupewa uwaziri! !

Ndo vile tu Magu alifanya papara kutumia zile nafasi 10 za wabunge wa kuteuliwa!! Matokeo yake, hivi sasa anashindwa kumpa huo uwaziri kwa sababu uwaziri unataka kwanza mtu awe mbunge!
 
Kwa kujenga hoja ni mzuri kweli. Ni mwamasisha mzuri, na kiongozi ambaye akiazimia jambo linafanyika, na anaweza kuiteka hadhira kirahisi na kuishawishi.

ILA huyu mdogo wangu ana kiburi ka dubu, ana dharua ka dume la nyani.

Nahisi laana ya kumpiga kofi Judge na Mh. Waziri mkuu mstaafu Mzee Warioba haijatubiwa.
 
Awe waziri,asiwe waziri mmmmh kwangu sawa tu,tumeishazoe kuishi bila huduma muhimu za kiserikali na hata akiwa waziri hakuna miujiza.Lakini kwa sababu anaweza akasikilzwa na Raisi kuliko mawaziri wengine uteuzi wake utaleta mgawanyiko ndani ya baraza la mawaziri,na labda waziri mkuu Majaliwa ataachia ngazi.
 
Mkuu Chigge, naunga mkono hoja. Wewe hili ndio umelibaini leo?. Angalia sisi wenzio tulimbaini lini na tukashauri nini
Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam

Pia tumeyazungumzia mafanikio yake
Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe Walilolikataa Waashi Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni

Na kumalizia kwa kumtabiria makubwa zaidi
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze...
P
Mkuu naaitwa shige2 na si CHIGE.
Ni kweli anaudhubutu. Ni kama ulivyotaka kusema apunguze... Na aende mdogo mdogo atafika huko kabisa
 
Back
Top Bottom