na wewe
JF-Expert Member
- Jan 4, 2019
- 231
- 397
Kuna watu wanaamini siasa ni mchezo mchafu,lakini pia wakati huo huo kuna watu wanaamini siasa ni sayansi ya hali ya juu sana..maana pale unapotumia Maneno tu ili mtu akuelewe na afanye maamuzi ya kuacha kazi zote siku hiyo ili akupigie wewe kura na huku anajua kabisa yeye hata pata chochote kwenye mafaniko yako huko mjengoni.. Hapo ndio inathibitika kuwa siasa ni sayansi ya hali ya juu baada ya uchawi. Mshana Jr
Niende kwenye mada.
Kwa sababu ya hali hii ya baadhi ya vyama vya upinzani kujitoa kwenye chaguzi za serikali ya mtaa, naamini Kwa asilimia kubwa kuwa inawezekana kabisa baada ya mda mfupi baadhi ya waliokuwa wagombea kuwabadilikia wale tunaowaita wakubwa na wenye maamuzi ya mwisho ya chama kuwa, maamuzi yao sio sahihi.na hii hatua itaendana na watu kurudi chama cha C.C.M au kujiunga na C.C.M Kwa kasi ya ajabu huku wakituhumu C.C.M iko sahihi kuliko vyama vyao.
Lakini wakati huo huo wengine hawatatoka chamani ila wataunga juhudi wakiwa ndani ya vyama vyao bila kuhama Ikubukwe kuwa mchezo wa siasa ni mchezo kutafuta hisia na huruma Kwa wananchi wakati huo huo mkimchafua mwenzako na kuonesha wewe ndio bora.hivyo basi naamini nguvu iliyotumika kushawishi watu kuunga juhudi tena Kwa level ya wabunge ndio hivyo itatumika kufanya hayo niliyoyaelezea hapo juu