Sitasahau siku ya jana na leo nilivyolala mahabusu

mkuu hujaambiwa ukaogee...na balozi wa sero, mix kusachiwaa.mwanaume inatakiwa uzoee hali zote. wanasema usipo kujaa ujananii utakujaa uzeeni
 
Wewe jamaa kesi yako iliishaje? Ama upo Jela muda huu? Mbona hujibu wenzako chochote hapa kwa muda mrefu?
 
lock upmkuu, kumradhi nimechanganya, sikujua kama mahabusu na lock up ni tofauti cause sijawahi hata fikiria hivo vitu naonaga tu mitandaoni basi hadi jana...

Sent using Jamii Forums mobile app
Wala usiombe msamaha. Umepatia kabisa na aliyekusahihisha ndiye kakosea. Lockup ni neno la kiingereza na mahabusu ni kiswahili.
 
Dah! Aisee, very sad hope Mungu amguse, kuna moja pia niliona jamaa ni bajaj driver na ana biashara ya chips, sasa kila asubuhi anawahi sokon kununua vitu vya hiyo siku, sasa avokua mwenge wakatokea watu watatu wakamwomba awashushe sayansi akasema poa si mbaya maana anaenda njia iyo iyo tu, sa jamaa avofika science jamaa wakashuka wawili wakasema uyu mwenzetu kalewa ila kuna mtu kituo cha mbele anamsubiri ampeleke home, jamaa akasema poa akasepa, avofika kituo cha mbele kapark bajaj haoni mtu anamfata ikabidi amwamshe jamaa ila wapi mtu haamki, kumtikisa ivi kidogo mtu hasogei duh jamaa akakimbilia polis na maiti kufika apo akadakwa na case akabambikiwa yeye ndio ameua huyo raia ...

Sent using Jamii Forums mobile app
Sitaamini sana hii story. Kubeba mwili wa mtu aliyefariki na kuingia nao kwenye bajaji halafu wakati wa kuteremka unamwambia dereva huyu kalewa anashuka mbele bila dereva kushtuka ni ngumu kidogo. Wakati wale wenzake wanateremka walimlaza? Kma kama walimlaza dereva hakujiuliza wakati wa kuteremka atawezaje mtu ambaye hata kuongea mawasiliano hawezi kufanya?
 
Duh! Wakuu, nilikuwa nasikia tu kwa wengine. Jana nimelala Lock up kwa mara ya kwanza. Kwanza nimedakwa nikatiwa bangili, then nikapandishwa kwenye farasi mweupe then moja kwa moja kituoni (jina la kituo not disclosed) kwa kuwa uchunguzi unaendelea bado, ila in short ni case ya kubambikiwa.

Nilivyofika kwanza unakuwa traumatized na kupanic juu maana huelewi kwanini umekamatwa na pia zile kelele za kule ndani, mixer harufu, mixer matusi ya mapoti, yaani ni experience mbaya sana plus kupigwa pingu mtaani mbele ya watu wanaokuheshimu yani acheni tu Wakuu.

Leo ndio nimetoka kwa neema za Mungu ila bado nitaendelea ku-report. Tujitahidi kuwa waangalifu ndugu zanguni maana nimeamini wengi walio lockup hawana makosa wengi ni kubambikiziwa na pia hakuna uchunguzi uliokamilika hadi unapokamatwa, very disappointing.

Sent using Jamii Forums mobile app


Uliiba nini hapo mtaani kwenu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom