Sitasahau nilipofanya mapenzi na mwanamke juu ya kaburi (SIMULIZI)

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
SEHEMU YA 01:

NILIISHI maisha ya starehe. Ujana ulinikamata vilivyo. Pombe na wanawake havikunipita, walionifahamu waliniita ‘popo.’ Nilikuwa popo kweli, popo kasoro mabawa!

Mchana nilifanya kazi ili nipate masurufu ya kwenda kutesa katika viwanja. Japo nilifanya kazi za kijungujiko, fuko langu halikukauka fedha, hata bila aibu ya ule umri wangu wa miaka 33 na sura iliyokomazwa na ulevi, nilipenda kujiita tajiri mtoto!

Jumamosi usiku nilikwishamaliza kuvalia mavazi ya kupendeza. Nilijitazama katika kioo, nikaiona fulana yangu nyeusi na jinsi ya bluu, shingoni nilijaza cheni nyingi hata nikafanana na mbuzi mgeni. Haraka nilivaa viatu vyeupe, nikatoka ndani, nikafunga mlango kisha nikapaza sauti, “nakula ujana nitapumzika nikiwa babuuuu!”

Wapangaji wenzangu waliyazoea makelele yangu. Niliwasikia wakicheka ndani ya vyumba vyao. Kichwa maji mimi, nikapayuka tena, “laleni hamna hela.” Jirani mmoja aliyekerwa na kauli hiyo, akajibu kwa sauti kubwa kuliko yangu, “ungekuwa na hela ungenunua kitanda paka wewe!” Kauli hii ikaamsha vicheko vingi zaidi. Kupunguza hasira na aibu, nikaporomosha tusi kali la nguoni lililozua ukimya. Kisha huyoo, nikaenda kusaka vimwana na vilevi.

Nilifika katika baa moja iliyojaaliwa wahudumu warembo. Nikavuta kiti kwenye meza. Nikaletewa bia bila kuagiza, walinifahamu. Nilipiga mafunda saba, akili ikachangamka. Basi nikawa napiga mafunda kadhaa, huku nasikiliza muziki mororo.

Nilikunywa tani nyingi za bia. Akili yangu ikapumzika kwa muda, pombe ikashika usukani. Kichwani niliwaza kupata mwanamke wa kulala naye. Sikumtaka mwenye maadili, asingekubali kuishi na mlevi kama mimi. Nilitaka ‘kahaba’, tuwe wapenzi kwa sekunde kadhaa, nimpe fedha tuachane kwa amani.

Nilipotoka nje sikupata shida ya kuwaita vimwana, kama mbu, walikuja wenyewe. Wote hawa walikosa cha kuuza, wakaamua kuuza miili yao. Nilipochoka kuwasikiliza wakijinadi, nikaamua kusema, “leo nataka rangi ya kunde! Awe na mzigo, sifa nyama, mzoefu wa kutoa ‘saidoni’ atapewa kipaumbele.”

Nilimpata kimwana mmoja aliyekuwa na sifa nilizotaka. Tukaanza kuelewana:

“Utanifanyia shilingi ngapi leo?” niliuliza kilevi.

“Buku mbili tu… vitu vimepanda bei.”
Sikutaka kuzungumza zaidi, nikakubaliana naye huku tukiongozana kuelekea eneo la kumaliza biashara yetu. Makaburini.
Itaendelea
 
SEHEMU YA 02:

Hatukutembea sana, tukayafikia makaburi. Watu walikuwa wengi siku hiyo, karibia kila kaburi lilikuwa na wazinzi wakifanya mambo yao. Hawakuogopa lolote, mahali walipopumzika wapendwa, paligeuzwa kuwa vitanda vya kufanyia ufusika.

Tulilifikia kaburi moja ambalo halikuwa na watu, nakumbuka liliandikwa, KIMOTA S. SAMIKE. Binti akajilaza, akapandisha juu kidogo kimini, mambo yote yakawa hadharani. Kumbe hakuvaa ‘kufuli’, bila shaka aliipenda kazi yake!

Nilipewa masharti: “Fanya haraka sina muda wa kupoteza , usinishikeshike, hakuna haja ya kuniandaa, hii ni kazi yangu, nimejiandaa toka nyumbani.”

Sikumjibu, nilitumbukiza mpini kisimani kwa nguvu zote, hakushituka wala kutikisika, ‘lilikuwa gwiji gumegume magumashi lisilo na hisia sababu ya kufanya ile biashara kwa muda mrefu.’

Tukiendelea kushughulika, ghafla nilishikwa mkono wangu kwa nguvu. Nilipogeuka, nilimwona mtu wa kutisha. Alivaa koti, juu alijifunika kofia ya koti lake, uso haukuonekana, kiza kinene kilitanda… sura yake ilikuwa giza!

Mtu yule wa kutisha, alininyanyua akiwa kanishika mkono. Binti kuona vile akapiga kelele akijaribu kujiinua, lakini alichelewa, panga kali lilimshukia shingoni. Akakata roho palepale.

Nilijinasua katika mkono wa yule mtu wa ajabu, nikapandisha suruali nikikimbia, mtu yule akiwa na upanga uliojaa damu ya kahaba, akanikimbiza.

Nilikimbia nikipiga kelele za kuomba msaada. Mtu yule wa kutisha aliendelea kunikimbiza akiwa na panga lake mkononi. Niliyatoka makaburi nikavuka barabara iliyokuwa na magari mengi, ilibaki kidogo nigongwe na magari yale, hata hivyo niliponea chupuchupu.

Nikiwa ng’ambo ya pili ya barabara, niligeuka nyuma kutazama kama yule mtu aliendelea kunifuata. Hakuwepo, pengine wingi wa magari ulimfanya ashindwe kuvuka. Hapo nilipata matumaini, nikakimbia kidogo kisha nikaanza kutembea kuelekea nyumbani.

Pombe ziliisha bila hiyari yangu. Nilitembea kwa ukakamavu kama askari katika gwaride hata usingeweza kuamini kuwa ni mimi niliyekuwa nimelewa ‘chakari’ muda mchache uliopita. Pombe ilimezwa na hofu, hofu ya kumezwa.

Nilifika nyumbani, nikafungua mlango nikiwa siamini kama nilipona katika tukio lile. Niliingia ndani. Nilipowasha taa, sikuamini nilichokiona, yule mtu aliyekuwa akinikimbiza, alikaa juu ya godoro, kashika panga lake mkononi…

Itaendelea
 
SEHEMU YA 03:

Nilifika nyumbani, nikafungua mlango nikiwa siamini kama nilipona katika tukio lile. Niliingia ndani. Nilipowasha taa, sikuamini nilichokiona, yule mtu aliyekuwa akinikimbiza, alikaa juu ya godoro, kashika panga lake mkononi…

ENDELEA KUISOMA…

NILIANZA kukimbia tena kuelekea barabarani. Alinikimbiza. Nilikunja kona ya Sakubimbi, naye akakunja! Alinikimbiza kwa bidii kimyakimya. Nilikimbia mpaka nikaishiwa nguvu, nikaanguka chini. fahamu zikapotea.

Nilishtuka asubuhi, nikajikuta nikiwa nimelala mahali palepale nilipoangukia. Viungo vyote vya mwili viliuma. Watu walikuwa wakinishangaa, wapo waliosikika wakisema: “Mlevi huyo… pombe siyo chai.”

Sikuyajali maneno yao, niliwaza jambo moja tu, ni nani mtu yule aliyenifukuza na kwa namna gani ningeweza kumwepuka.
Nilijizoazoa taratibu, kisha nikaikamata njia ya kuelekea nyumbani, nilikiogopa chumba changu, lakini sikuwa na namna nyingine ila kurejea.

Nilifika, nikakuta mlango uko wazi, wapangaji wenzangu walinishangaa. Nilisoma akilli zao, waliwaza nilifanya vile kwa sababu ya pombe, hawakujua kilichojificha nyuma ya pazia.

Nilipoingia ndani, jambo la kwanza lilikuwa ni kulitupa jicho katika godoro… nilihofu yale mambo ya jana usiku yasije kujirudia. Nilitabasamu, mtu yule wa ajabu hakuwako.

Niliamua kujilaza nikishtukashtuka. Sikula kwa muda mrefu lakini sikuhisi njaa. Akili ilikuwa katika mapambano makali. Sikupata usingizi, badala yake likaja wazo moja. Niende kwa mganga, nisipofanya hivyo, mtu wa ajabu atanitoa roho.

Haraka nilikamata begi lililokuwa juu ya kabati bovu. Nikafungua zipu ndogo nikatoa kiasi cha fedha ambacho niliamini kingetosha.
Nilikuwa ndani ya gari dogo kuelekea kijijini. Mkononi nilibeba maandazi saba makubwa na niliendelea kuyatafuna taratibu. Mtoto mdogo aliyekaa pembeni aliyakodolea macho maandazi yale. Sikumpa.

Haikuwa safari ndefu. Nilifika kijijini, haraka nikaikamata njia kuelekea kwa mtaalamu wa tiba za asili. Nilitembea kwa hofu na woga! Nilihisi muda wowote ningeanza kukimbizwa.

Nillifika kwa mganga nikiwa na matumaini makubwa ya kupata tiba. Sifa za mganga huyu zilitapakaa pande zote nne za dunia, alikuwa fundi asiyeshindwa kitu. Nilimtegemea.

Baada ya kuingia ndani ya chumba cha mganga, nilieleza shida zangu haraka. Sikuacha jambo hata moja. Mganga aliyevalia mavazi mekundu, mkononi akitikisa kibuyu, na shingoni alisheheni hirizi kubwa zilizopumua.

Nilimaliza kuzungumza, ikawa zamu ya mganga kusema: “Nimekusikia mwanangu… kinachokusumbua ni mzimu wa huyo marehemu ambaye hakufurahishwa na kitendo kichafu ulichokifanya mahali alipolala. Hakuna tiba nyingine ila kwenda kuomba radhi katika kaburi lake.”

Itaendelea
 
SEHEMU YA 04:

ILIPOISHIA JANA

Nilimaliza kuzungumza, ikawa zamu ya mganga kusema: “Nimekusikia mwanangu… kinachokusumbua ni mzimu wa huyo marehemu ambaye hakufurahishwa na kitendo kichafu ulichokifanya mahali alipolala. Hakuna tiba nyingine ila kwenda kuomba radhi katika kaburi lake.”

ENDELEA NAYO…

Kwa kuwa lengo langu lilikuwa kupata tiba, nilikubaliana na maneno ya mganga. Alifurahi, akanitaka nilale ili kesho twende katika makaburi yale.

Asubuhi ilifika. niliamshwa na jogoo aliyewika kwa maringo, ‘kokorikoo.’ Msichana mdogo aliingia ndani ya chumba nilicholala bila kubisha hodi. Mkononi alishika kikombe cha uji, alinipatia nikaanza kuunywa taratibu. Uji wenyewe haukuwa na sukari, nilinusa mara tatu nikaachana nao.

“Haya kijana haraka twende!” alisema mganga. Nikatii maagizo yake!

Baada ya kusafiri kwa muda mfupi, hatimaye tulifika mjini Chisanza. Tulishuka karibu na eneo lijaalo vilevi na vimwana ufikapo usiku, ni katika eneo hili ndipo nililizua balaa la kufukuzwa na mtu wa ajabu.

Kwa kuwa ilikuwa asubuhi, tuliwaona walevi wakifunga sherehe ya mvinyo tayari kurudi nyumbani. Wengi walionekana kuwa na majuto baada ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa mambo ya hovyo.

Japo mganga alikuwa mzee, hatua zake zilikuwa kali kama kijana mdogo anayewahi michezoni. Alitembea bila kuchoka. Nilishangaa ukakamavu wake, kwani japokuwa alibeba kapu lililojaa manyanga na kila aina ya ulozi, hakutetereka, alichapa mwendo haraka.

“Kaburi lenyewe liko wapi?” mganga aliuliza mara baada ya kuwa tumeyafikia makaburi yale.

“Ngoja tulitafute… nakumbuka liliandikwaaaa….” nilijiumauma, sikukumbuka jina la kaburi lile na makaburi yalikuwa mengi.

Japo jina nililisahau, niliendelea kutafuta nikiamini kuwa nikiliona nitakumbuka. Tulizunguka kwa muda wa dakika tano, jicho langu likatua katika kaburi lililoandikwa, ‘KIMOTA S. SAMIKE’, nikamwambia mganga, “simama ni hapa.”

Mganga alisimama akashusha vifaa vyake vya kutendea kazi. Alitoa matunguli kutoka katika kikapu kikubwa alichobeba. Akasimama juu ya kaburi huku akisema maneno ambayo sikuyaelewa.

Wakati mganga akiendelea kufanya manyanga yake, yule mtu wa ajabu aliibuka ghafla hata sikujua alipotokea. Mkononi alishika upanga wake, na kama ilivyo siku zote, usoni palikuwa na kiza kinene!

Mganga alikimbia kama swala, niliona rubega yake ikipepea, nilikimbia kuelekea alikoelekea mganga, lakini kasi ya mganga ilikuwa kali na sikuweza kumpata, alikunja kona zake na mi’ nikakunja zangu. Mwisho kila mtu alimpoteza mwenzake, nikabaki nikikimbia peke yangu.

Itaendelea
 
SEHEMU YA 05:


Mganga alikimbia kama swala, niliona rubega yake ikipepea, nilikimbia kuelekea alikoelekea mganga, lakini kasi ya mganga ilikuwa kali na sikuweza kumpata, alikunja kona zake na mi’ nikakunja zangu. Mwisho kila mtu alimpoteza mwenzake, nikabaki nikikimbia peke yangu.

ENDELEA KUISOMA…

Niligeuka nyuma kuhakiki kama nilikuwa salama. Mtu wa ajabu aliendelea kunikimbiza na alianza kunikaribia. Nilijawa na hofu, tumaini pekee la kuiona kesho lilibaki katika miguu yangu.

Nilifika katika nyumba ambayo ilikuwa wazi. Niliingia humo bila hodi kisha nikaufunga mlango kwa nguvu. Waliokuwamo, wakapiga kelele za hofu. “Mwiziiiiih! Tunakufaaaa…”

Sikuyajali makelele yao, nilingoja kuona kama mtu yule wa ajabu angeweza kunifuata katika ficho langu la ghafla. Hakuingia, hapo nikahisi usalama.

Watoto wawili wa kike na bibi mmoja wa makamo waliendelea kupiga kelele za kuhitaji msaada. Akili yangu haikufanya kazi kwa kiwango kilichotakiwa. sikuweza kuwatuliza. Niliwatazama wakazidi kuogopa kwa kuhofu nilikuwa mwizi katili.

Kilio kile nilichokisindikiza kwa macho kilimwamsha mwanamme pekee aliyeishi pale. Aliuliza kwa hasira, “kuna nini huko!” majibu yalikuwa, “Mwizi! Mwizi! Mwizi!”

Mzee akiwa kavaa msuli na baraghashia kichwani, alitoka na panga la familia. Aliponiona akanirukia, nikakwepa nikijitetea: “Mzee mimi si mtu mbaya, nisikilize nina matatizo mjukuu wako!”

Mzee alikuwa mhenga mwema. Alisikia utetezi wangu. Akanitazama usoni kunipima uungwana, hata macho yetu yalipokutana, akanisihi nikakae katika mkeka. Ni katika mkeka huu ndipo alikaa yule bibi mwoga na wajukuu wawili wenye hofu! Wote watatu waliponiona, wakanyanyuka taratibu kisha wakapotelea chumbani kama sisimizi wadogo waingiao katika shimo baada ya saa kadhaa za kuishangaa dunia!

Nilibaki na mzee, hata hivyo nilikuwa na hofu isivyo kawaida. Mwenyeji wangu ambaye niliingia katika makazi yake bila hodi, aligundua.
“Sakina leta vipande vinne vya mihogo. Vitatu vyangu, kimoja cha mgeni,” mzee aliagiza.

Vipande vinne vya mihogo vikiwa katika sahani chakavu, vililetwa. Sakina hakunitazama usoni. Aliniogopa!

Mzee alivikamata vipande vyote vitatu. Nilishangazwa na kitendo kile, nikamuona akitabasamu huku akisema, “Kila mwanadamu ana asili ya ubinafsi. Haiwezekani mihogo nilime mimi kisha tule sawa. Tafuna huo mmoja, usiposhiba kunywa maji mengi!”

Maneno ya mzee hayakuwa kichekesho, lakini yalitosha kuitwa mzaha uliolenga kuniweka sawa kiakili. Alisema maneno yale akitabasamu. Akili yangu iliyochemshwa kwa mawazo, hofu na woga, ikaanza kupoa.

Itaendelea
 
SEHEMU YA 06:


Maneno ya mzee hayakuwa kichekesho, lakini yalitosha kuitwa mzaha uliolenga kuniweka sawa kiakili. Alisema maneno yale akitabasamu. Akili yangu iliyochemshwa kwa mawazo, hofu na woga, ikaanza kupoa.

ENDELEA KUISOMA…

Nilimaliza kula mhogo wangu kama ilivyokuwa kwa mzee.

Babu huyu alikohoa kidogo.

“Haya kijana, tafadhali nieleze kinachokusumbua,” mzee aliomba akiwa kanikazia macho. Sikuwa na sababu ya kuficha maradhi, nikatengeneza sauti yangu vizuri ili nieleze mkasa wote. Lakini kabla sijafungua kinywa, mlango ukagongwa. Wote tukazigeuza shingo kuelekea ilikobishwa hodi!

Nilishtuka, lakini nikajikaza na kutulia mkekani. Aliyebisha hodi akaingia bila ruhusa. Mapigo ya moyo yakarudi katika kasi yake ya kawaida pale nilipomwona mtoto mdogo akijongea taratibu.

Mtoto alitusalimu kisha akaliinamia sikio la mzee na kuanza kunong’ona. Sikuweza kusikia alichozungumza, alikuwa fundi wa kung’ata sikio. Alipomaliza kutoa taarifa, alitoka ndani. Akairudia njia aliyotumia kuja.

“Haya kijana, nieleze kilichokusibu,” mzee alizungumza kwa upole na utulivu.

Nilimsimulia mkasa wangu wote ulionifika. niliposimulia jambo la kusisimua, alitikisa kichwa, wakati mwingine alitoa sauti za mguno kuashiria alinisikiliza.

“Pole sana kijana…” alisema akikunja mguu, “ni lazima ukubali kwamba ulifanya makosa makubwa kulala na mwanamke juu ya kaburi… hakikuwa kitendo cha kiungwana!”

“Najuta mzee wangu, ni ujinga ulinivaa,” nilijitetea.

“Ni bahati kama unakumbuka lilipo kaburi hilo… itarahisisha mambo aliyoyashindwa mganga wako.”

“Nisaidie mzee!” niliomba. Mzee akashika sharubu zake kwa maringo, akarekebisha sauti na kuendelea kuzungumza:
“Unaweza ukakumbuka kaburi limeandikwa jina gani?”

“Ndiyo,” nilijibu nikiua mbu mkubwa aliyetaka kuinyonya damu yangu mchana kweupe, “limeandikwa KIMOTA S. SAMIKE.”

Mzee aliposikia jina hilo alishtuka. Akanitazama usoni kwa huruma, nami nikamtazama kwa jicho lililosema, ‘nisaidie mzee wangu.’
“CHIMOTA S. SAMIKE!” mzee aliendelea kulitaja jina hilo, alishindwa kuficha hisia zake. Alisikitika, akanyong’onyea, macho akayatoa pima, kisha akaagiza aletewe tumbaku, bila shaka alitaka kunena maneno mazito sana juu ya CHIMOTA S. SAMIKE.

Wakati hayo yote yanatokea, nikaishiwa matumaini. Nikajikuta nikitamka maneno bila hiyari yangu. “Nimekwisha.”

Itaendelea Jumatatu…
 
SEHEMU YA 07:


Mzee aliletewa tumbaku aliyoagiza. Ilikuwa tumbaku ya tozo. Akaiweka katika kiko kilichokuwa na kaa dogo la moto, akavuta mikupuo miwili haraka, nikakohoa kwa ule moshi wake.

“Navuta mimi unakohoa wewe! Bwana mdogo acha uchuro,” mzee alisema akinikazia macho. Sikumjibu, niliachia tabasamu jembamba.
“CHIMOTA S. SAMIKE,” mzee alianza kusimulia, “alikuwa mjukuu wa mzee Samike. Samike ni mzee mchawi haijapata kutokea.

Inasemekana alizaliwa na uchawi wake mkononi. Alijaaliwa kuwa na mjukuu mmoja tu, ambaye alipatikana kutoka kwa binti yake wa pekee aliyebahatika kumzaa enzi za ujana wake. Haijulikani hasa baba wa Chimota alikuwa nani kwani mara baada ya binti kupata ujauzito, kichaa cha ghafla kilimvaa akawa haelewi la Kaskazini wala la Magharibi.”

“Kwa nini Samike hakumtibu binti yake? Umesema alikuwa mchawi haijapata kutokea,” niliuliza.

“Acha ujinga. Mchawi si mganga.” Alinikata mdomo. Nikagundua jambo, mzee hakupenda maswali na endapo ningeendeleza udadisi huo, hapana shaka mambo yangeenda segemnege.

Baada ya kimya kifupi, mzee akaendelea kusimulia: “Binti alipojifungua, akakata kamba zake za uzuzu, kisha huyoo akatokomea kusikojulikana. Inasemekana alipigwa ‘kipapai’ na maadui wa mzee Samike, wakamchukua kumuonyesha wao walikuwa walozi waliobobea zaidi. Lilikuwa kasheshe la wachawi wakipambana kuonyeshana umwamba.

Samike akabaki na kitoto kidogo kisichomfahamu mama. Mzee aliishi peke yake katika nyumba ya ukiwa. Pamoja na maisha hayo, alijitahidi kumhudumia Chimota. Chimota akanenepa kwa ule unywaji wa maziwa ya ng’ombe na upendo wa babu.

Hata hivyo, kisicho riziki hakiliki. Wachawi walikuja kumuumiza zaidi mzee Samike. Waliyakatisha maisha ya Chimota akiwa na miezi saba tu. Samike alisikitishwa sana na mkasa huo. Alitegemea mtoto yule ndiye angekuja kuwa mrithi wa mikoba yake ya ulozi.

Mzee Samike kwa sababu ya uchawi wake, alikwishatengwa na jamii. Watu wote walimwogopa na hawakuthubutu kwenda msibani. Japo alisimama juu ya paa la nyumba kutangaza kwa sauti kuwa alifiwa na mjukuu, watu waliziba masikio, msiba wakaupa kisogo.

Itaendelea kesho ili kuweza kufahamu hatma ya Mzee Samike na msiba wa mjukuu wake
 
SEHEMU YA 08:


“Mzee Samike kwa sababu ya uchawi wake, alikwishatengwa na jamii. Watu wote walimwogopa na hawakuthubutu kwenda msibani. Japo alisimama juu ya paa la nyumba kutangaza kwa sauti kuwa alifiwa na mjukuu, watu waliziba masikio, msiba wakaupa kisogo.

ENDELEA KUISOMA…

“Sikitiko likaingia katika moyo wa Mzee Samike. Msiba wote aliufanya peke yake. Alilia, akajibembeleza, akanyamaza na kujifariji. Akabeba maiti ya mjukuu wake kwenda kuizika katika makaburi yaliyokuletea kasheshe. Alipofika kwa sababu hakuwahi kuchimba kaburi maishani mwake, akachanganya mambo, japo ulikuwa msiba wa mtoto mchanga, alichimba kaburi la mtu mzima! Alipomaliza kuchimba, akamzika Chimota akiwa kamshikisha uchawi wa kumlinda. Apumzike kwa amani, asitokee bazazi yeyote akafukua kaburi lile au kufanya ushenzi wowote, hata kama ni kulikanyaga kwa kishindo.”

Mzee alimaliza kusimulia, akaweka kiko chini. Nilikuwa na maswali mengi ya kumuuliza. Nikaitumia nafasi hiyo.

“Nitampata wapi mzee huyu?” niliuliza.

“Swali zuri, ni lazima umpate ili umwombe msamaha. Akuepushe na hilo dubwana linalokukimbiza. Kwa bahati mbaya Samike alihama Chisanza miaka miwili iliyopita.”

“Alihamia wapi?”

“Kigoma!”

“Lazima niende huko. Nikipuuzia mtu wake wa ajabu atanimaliza.”

“Safi! Hakuna namna nyingine ya kupambana, ila kumwomba radhi kwa ufuska ulioufanya.”

“Nitawezaje kumpata nikifika huko Kigoma?”

“Oooh… ni rahisi sana, Mzee Samike ana muonekano wa pekee, waliowahi kupishana naye waligeuza shingo kwa sababu ya ule utofauti alionao. Ana nywele nyeupe isivyo kawaida. Ndevu nyeupe, sharubu nyeupe, kope nyeupe na uso mrefu wenye rangi ya maji ya kunde. Kwa sababu alitumia ujana wake katika kubeba tunguli za kuwangia, ana misuli minene. Samike siyo mzee, ni pande la mzee!”

Niliyaelewa maneno ya mzee. Nikataka kumuuliza jina lake, lakini kabla sijachomoa maneno, mlango ukasukumwa kwa kishindo, mtu wa ajabu akaingia akiwa kashika upanga uleule. Akasimama kama mwalimu anayemtafuta mwanafunzi mpiga kelele.

“Mtu wako kakufuata. Kimbia haraka katokee mlango wa nyuma,” mzee alinishauri.

Nilikimbia kuelekea ushoroba finyu uliozitenganisha kuta mbili ndefu. Sikuvisikia vishindo vya mtu wa ajabu, lakini alinikimbiza. Mlango wa nyuma niliupita kwa mwendo wa farasi wa mashindano. Nikaingia katika barabara ya mwendo kasi. Mwanadamu aendaye mbio, nikakimbia sambamba na magari yaendayo kasi. Abiria wakashika vichwa! Madereva wakaporomosha matusi.

Mtu wa ajabu aliendelea kunikimbiza nami nikakimbia kwa bidii ya kuyaokoa maisha. Kwa kuwa watu waliniangalia na kushangaa jinsi nilivyokuwa nakimbia, nikang’amua kwamba, mtu yule wa ajabu hawakumwona. Ulikuwa mchezo wa mauzauza.

Nini hatma ya mchakamchaka huu?
 
SEHEMU YA 09:


Nilivuka barabara. Gari dogo likakosa kunigonga. Katika harakati za kukwepa kadhia hiyo, nikaparamia mkokoteni wa takataka. Mwenye mkokoteni japo mimi ndiye nilimkosea, akaamua kuwatukana wazazi wangu ambao hawakuwa mahali pale. Sikujali, lengo lilikuwa kujiokoa. Niliendelea kukimbia.

Kila nilipogeuka nyuma, nilimuona mtu wa ajabu akizidi kunikaribia. Nikaongeza mbio ili kujiweka salama. Hata hivyo, kwa sababu ya kukimbia kupita kiasi, mapafu yakashindwa kufanya kazi yake. Nikadondoka kwa kishindo kama furushi, “Puuuh!” fahamu zikapotea.
Nilishtuka asubuhi nikajikuta nikiwa chumbani kwangu. Haya yalikuwa maajabu mengine kwani sikutambua ni nani aliniweka mule ilhali muda uliopita nilikuwa katika tukio la kufukuzwa na yule adui yangu.

Sikutaka kubaki mjini tena, nikaamua liwalo na liwe, lazima niende Kigoma kumtafuta Mzee Samike. Nililisogelea kabati chakavu lililojaa vumbi. Panya mkubwa akakimbia kuelekea juu zaidi ukutani ambako alifahamu nisingeweza kumfikia. Sikupata muda wa kumtafakari, nikafungua zipu ndogo ya begi nikatoa kiasi cha fedha ambacho niliamini kingeweza kunifikisha Kigoma na kunisadia katika gharama ndogondogo.

Nilimaliza kujiandaa. Nikatoka nikiwa na fulana nyeusi, suruali ya jinsi, viatu vikubwa na kiasi cha fedha kufanikisha safari ya kusaka tiba.
Jua halikuonyesha dalili ya kuchomoza, lilipakatwa na mawingu mazito yaliyoifunika dunia. Wingu lile nililiona kama turubai lililoweka matanga. Kama si msiba wangu, ulikuwa msiba wa nani? Sikupata jibu.

Nilitembea kwa hatua za kuruta wa jeshi, ‘chap chap’ mpaka nikafika stendi. Hapo nilipokelewa na wapiga debe wengi ambao kila mmoja alinivutia kwake kama ilivyo kwa mwamba ngoma.

Sikumsikiliza yeyote. Nilikwenda mpaka ndani ya ofisi ya basi nililotaka, nikakata tiketi, kisha nikazama ndani ya chombo cha usafiri.
Nilipokaa juu ya siti, nikapitiwa na usingizi mzito. Kwa muda wa siku kadhaa sikulala vya kutosha. Asili ya maumbile ikanikwapua mzima-mzima. Nikalala kama dume la konokono.

Nilishtuka gari likiwa Dodoma. Nikajinyoosha kinyonge tayari kuendelea na safari. Gari ilikwenda kwa mwendo wa kistaarabu. Dereva alikuwa mzee na alizishika sheria zote za barabarani. Kweli utu uzima dawa!

Nini hatma ya safari hii ya kusaka tiba?
 
SEHEMU YA 10:


Kufumba na kufumbua tulifika Singida. Kupika na kupakua tuliingia Tabora. Taratibu tukauacha mkoa huu wa Wanyamwezi, tukafika Kahama mkoani Shinyanga.

Tulifika wilayani hapo saa nne usiku. Ikabidi tulale kwani sheria hazikuturuhusu kusafiri muda ule. Abiria wachache walishuka, wakaenda kupumzika gesti. Wengi tulibaki ndani ya basi, tukalala tukiwa tumekaa.

Tuliamshwa na mlio wa honi, “boboooooooooh!” wote tulikuwa juu ya viti vyetu. Safari ikaendelea.

Mida ya saa nne asubuhi tuliifikia kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ya Kanembwa. Tuliwaona askari imara wakizungukazunguka kuhakikisha usalama wa kambi na taifa. Wengine walikimbia mchakamchaka wakiimba nyimbo za kuwasahaulisha uchovu:

“Usimseme usimseme shori wangu! Usimseme,

“Usimseme usimseme shori wangu! Usimseme.” Kamanda aliimbisha. Kuruti wakaitika kwa morali.

Tuliiacha kambi, tukaingia eneo kubwa la wilaya ya Kibondo ambalo lilikuwa pori. Kwa muda wote huo, nikagundua uwepo wa binti mrembo pembeni yangu. Nilikaa upande wa kushoto, yeye akakaa dirishani. Nikaamua kumchombeza kujipima uwezo wa kurusha makombora bila fedha.

“Mrembo mamboooh!” nilimsabahi, akageuza shingo kunitazama, akanipandisha na kunishusha. Alipogundua nilikuwa kapuku asiye na bahati, akanipuuza. Hakujibu salamu, nami nikaamua kukaa kimya. Tukasafiri kimyakimya mimi na jirani yangu.

Gari liliendelea kuukata mwendo. Kama kawaida, miti ilirudi nyuma kwa kasi . barabara haikuwa na lami, hivyo vumbi lilitusabahi kwa shangwe. Wachache, walipiga chafya. Akina siye vumbi ni sehemu ya maisha, hatukujali.

Ilinyesha mvua ikakata. Tope kiasi likapunguza mwendo wa basi. Tulizama katika mashimo na vidimbwi, tukaibuka katika tambarare! Safari ikaendelea. Dereva akiendesha, abiria tukiendeshwa!

Tuliingia katika pori nene. Mlio wa risasi ukatushtua. Nilipotazama mbele, niliona magogo yamepangwa katikati ya barabara. Pembeni upande wa kushoto walisimama wanamme watatu walioshiba misuli. Nao upande wa kulia, walisimama wengine wanne wenye vifua vya mazoezi, jumla yao wakawa saba. Na wote kwa pamoja walishika bunduki za kizamani aina ya ‘SAR’.

Ndani ya basi watu walianza kulia hovyo. Dada aliyenipuuza mwanzo akanishika bega kwa woga akinisalimia: “Shikamoo,” nami nikaitika, “Marahaba tumekwisha…”

Nini hatma ya watekaji hawa na safari ya Popo kusaka tiba?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom