sitasahau hii adhabu. Na wewe hutasahau ipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

sitasahau hii adhabu. Na wewe hutasahau ipi?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Old Moshi, Mar 30, 2012.

 1. O

  Old Moshi Senior Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Habari za mchana. Tukipokua wadogo hatukuruhusiwa kutumia mafuta ya taa. Siku moja kaka yangu aliwasha moto na mafuta ya taa bahati mbaya yakamwagika. Mama alipouliza nani ametumia mafuta, akanisingizia mimi. Nilipigwa sana hiyo siku na niliumia zaidi kwa sababu sio mimi niliyefanya hilo kosa.
  Na wewe mwenzangu ni adhabu gani ambayo hautaisahau
   
 2. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Ya kushika masikio na kupiga push up shule.
   
 3. maziwa ya mgando

  maziwa ya mgando Senior Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 29, 2012
  Messages: 167
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilichapwa siku ya Christmass, tena niko najiandaa kulala kwa kitu ambacho hata sikukielewa.
  Tena nikiwa mkubwa tu, dah nilisikitika sana.
   
 4. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  chuma mboga.
   
 5. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  mi na kaka yangu tulipanga kuiba maziwa nyumba, sasa kaka yangu akawa kachukua lichupa lililokuwa na maziwa( MTINDI) ile kufungua tu du!! kumbe yalikuwa na gas bwana yote yalipanda kwa kas ya ajab yakamwagika.

  Inshu alipokuja mama , kaka akaniambia niseme ni mimi nimeyamwaga na kwa sababu mi ni mdogo atanisamehe!!!!
  tabaaaaaaaaaaaaa usiombe kilichonopata nakijua mimi.
   
 6. O

  Old Moshi Senior Member

  #6
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  izo nimezifanya sana. Hasahasa kama huna namba, hujafagia au hujamwagilia bustani.
   
 7. O

  Old Moshi Senior Member

  #7
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kumbe kaka zetu walikua na akili sawa
   
 8. jchofachogenda

  jchofachogenda JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nilipopigwa kwa kosa la kumtania msichana kosa ambalo sikufanya. Kipindi hicho nilikuwa nasoma Madrasa. Mpaka leo yule Ustadh alienichapa viboko tunaishi nae mtaa mmoja,nikimuangalia ananikumbusha mbali sana.
   
 9. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #9
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Mhmmm!! Mimi ngoja ninyamaze maana ya kwangu ni makubwa kuliko.
   
 10. sister

  sister JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,029
  Likes Received: 3,940
  Trophy Points: 280
  kukaa bila kula siku nzima mana nilikataa kupika na nikaambiwa nioshe vyombo baada ya wenzangu kumaliza kupika.
  adhabu ya kukaa bila kula ni kubwa sana kwangu mana kukaa na njaa siwezi especial kama chakula kipo.
   
 11. sister

  sister JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,029
  Likes Received: 3,940
  Trophy Points: 280
  na kuna siku nilichezea kipigo kutoka kwa baba mpaka nikajikojolea hapo nilikuwa darasa la sita kisa sikuwa kwenye top ten darasani.
   
 12. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Auntie yangu alinisemelea kwa mama baada kunikuta nimepanda tena bila kujishikia ghorofani,tena nacheza nikiwa comfortable..

  Mama yangu hakuwahi kuwa mchapa watoto, ila aliporudi sasa,alinilamba mboko za ajabu na sitasahau maishani.. Maana na ukubwa wangu huu,ile sehemu nikiiangalia(ni maghorofa ya Kariakoo,Dar),naona kizunguzungu..
  Ni Mungu tu,vinginevyo,ninge-RIP kabisa!
   
 13. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Kuokota maganda 250 ya juice aina ya Sunvita!(shule)

  Kulala sakafuni wenzako wakiwa wanaendelea na masomo darasani.

  Kuleta debe 5 za mbolea...na unaambiwa kesho..utajiju pa kuipata,shule yenyewe iko mjini
   
 14. pepim

  pepim JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dah! Kwangu we acha 2, nilipigwa mikanda ya ukweli na kisha nikafungwa mikono + karatasi ili niunguzwe mikono...Mungu c athumani mvua ikaniokoa...Ilikuwa kinyumbani nyumbani miaka ya 90.....
   
 15. Siri Sirini

  Siri Sirini JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 547
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nami nakumbuka kama yako, nilikosa mitihani wakati nipo form1, baba akanipiga na kuniambia ukalale hakuna kula usiku, na kesho yake hakunipa hela ya shule, ila c unajua wamama wana huruma, akanipa hela kisiri, i mic u mum, R.I.P
   
 16. S

  SI unit JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 1,938
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kuruka kichurachura uwanja mzima. Kosa kuchelewa namba PS.
   
 17. O

  Old Moshi Senior Member

  #17
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hii style ukichapwa lazima ukumbuke bibi mzaa bibi, maana yake nyama ya serikali inakua papendikula na bakora.
   
 18. O

  Old Moshi Senior Member

  #18
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hii style ukichapwa lazima ukumbuke bibi mzaa bibi, maana yake nyama ya serikali inakua papendikula na bakora.
   
 19. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Yaweke hadharani kaka
   
 20. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,071
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  nikiwa form six nilikata skirt mikawa kiminiiiiii hadi karibia kwenye k**** na ilikua ni tabia ya wasichana walio wengi pale shule kwasababu tulikua girls tupu, sasa makamu wa shule akanibamba koridoni nimevaa ile skirt looooh nilichimba mashimo sita ya taka na skrti nilinyang'anywa
   
Loading...