Sitapiga kura tena hadi Katiba ya Uchaguzi ibadirishwe

amba.nkya

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
446
131
WanaJF, nimeamua kutoshiriki kupiga kura kwa chaguzi zijazo hata kama nitapoteza haki yangu ya msingi, unless otherwise, Katiba ya Uchaguzi ibadilishwe ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa Tume huru ya Uchaguzi. Nimeamua hivyo kwa msingi kwamba ninapoteza muda na haki yangu ya kumchagua mgombea nimtakaye lakini NEC wanalazimisha kuwachagua wagombea wao (CCM):sad:.

Nawasilisha kwa majadiliano.
 
If you need change then you must Vote how can you say "change" while you dont utilize your vote???? change begins from you:smile-big:
 
Inaonekana Bongo matokeo ya uchaguzi yanaamuliwa na wale wanohesabu kura (NEC na CCM) na siyo wale wanaopiga kura. Nafikiri ndio maana walijiandikisha milioni ishirini lakini wamepiga milioni nane. La maana piga kura kisha ilinde ihesabiwe kihalali. Watu walihesabu za ubunge wakasahau za urais hivyo ukapatikana mwanya wa kuamuliwa na waliohesabu, siyo waliyopiga. 2015 tusimame kidete, kura za urais zihesabiwe na kutangazwa kwenye kila kituo ili kila mtu aweze kujumlisha.
\
 
Ardhi haikomolewi kwa kuikanyaga,kutopiga kura si suruhisho hata kidogo,piga kura mambo mengine yatajipanga mkuu.
 
WanaJF, nimeamua kutoshiriki kupiga kura kwa chaguzi zijazo hata kama nitapoteza haki yangu ya msingi, unless otherwise, Katiba ya Uchaguzi ibadilishwe ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa Tume huru ya Uchaguzi. Nimeamua hivyo kwa msingi kwamba ninapoteza muda na haki yangu ya kumchagua mgombea nimtakaye lakini NEC wanalazimisha kuwachagua wagombea wao (CCM):sad:.

Nawasilisha kwa majadiliano.

Katiba ya Uchaguzi???, :A S angry: Hakuna kitu kama hicho.Hakuna haja ya kujadili hii kitu wakati aliyetoa hoja haelewi anachoongea
 
WanaJF, nimeamua kutoshiriki kupiga kura kwa chaguzi zijazo hata kama nitapoteza haki yangu ya msingi, unless otherwise, Katiba ya Uchaguzi ibadilishwe ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa Tume huru ya Uchaguzi. Nimeamua hivyo kwa msingi kwamba ninapoteza muda na haki yangu ya kumchagua mgombea nimtakaye lakini NEC wanalazimisha kuwachagua wagombea wao (CCM):sad:.

Nawasilisha kwa majadiliano.

Nadhani ulikuwa unamaanisha mabadiliko ya katiba na tume ya uchaguzi!! umechelewa

watu milioni kumi uchaguzi huu hawakupiga kura na wengi wao sababu ni uliyoitoa-KUMUONA MSHINDI KUPITIA AINA YA TUME YA UCHAGUZI TULIYONAYO

Sasa ukikutana na watanzania wale waliomeza sumu-eti kupiga kura ni haki, inaleta mabadiliko, still KWA TANZANIA HAMNA FAIR GROUND YA KUFANYA KURA YA MPIGA KURA IWE HAKI NA IFANYE KITU, hawa ni wale mbumbumbu ambao ulimwengu huko huku!!!

Hongera kwa kujua hilo mkuu! na pole kwa kupoteza muda!!!! maana tunaosema ni washindi kamwe si washindi wa ubunge, wanatuletea mzgigo mzito wa kuwalipa na kamwe hawatafanya kitu, au kuamua yale maamuzi mazito! still CCM reigns, na njia ya kuwaondoa ni kuweka fair ground ya uchaguzi -Slaa analijua hili ila kwa sababu ya malengo yao ya siri wamemteka kila ambaye hakufikira hili!!!
 
wanajf, nimeamua kutoshiriki kupiga kura kwa chaguzi zijazo hata kama nitapoteza haki yangu ya msingi, unless otherwise, katiba ya uchaguzi ibadilishwe ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi. Nimeamua hivyo kwa msingi kwamba ninapoteza muda na haki yangu ya kumchagua mgombea nimtakaye lakini nec wanalazimisha kuwachagua wagombea wao (ccm):sad:.

Nawasilisha kwa majadiliano.
yaani kwa kufanya hivyo hamna tofauti na kujiunga na ccm. Watawala wengi wanang'ang'ania madarakani kwa hila wanawafahamu wapiga kura watasusa kama wewe nao wataendela kutesa tuu.
 
tufafanulie una maana gani unapodai 'katiba ya uchaguzi?'

Sorry, nilikuwa namaanisha mabadiliko ya katiba na tume ya uchaguzi!! Ingawa tumechelewa kwa uchaguzi huu, je tufanyeje kwa chaguzi zijazo? Naomba tujadili
 
Sasa ndio nitapiga kura sana tena nitaendelea kuhamasisha na wengine. Hakuna kulala. Usipopiga kura unawapa mwanya zaidi. Tuwaamshe walioko vijijini ambako kunabandikwa mabango ya picha za watu, wanagawiwa fulana na vijikofia wanauza kura zao. Hilo likifanikiwa tutakuwa mbali kuliko kususia kabisa. Kuna percent ya wenzetu haijaamka, tuiamshe kwanza na hiyo, halafu kura ziendelee kuibiwa ndio utaona kivumbi chake.
 
WanaJF, nimeamua kutoshiriki kupiga kura kwa chaguzi zijazo hata kama nitapoteza haki yangu ya msingi, unless otherwise, Katiba ya Uchaguzi ibadilishwe ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa Tume huru ya Uchaguzi. Nimeamua hivyo kwa msingi kwamba ninapoteza muda na haki yangu ya kumchagua mgombea nimtakaye lakini NEC wanalazimisha kuwachagua wagombea wao (CCM):sad:.

Nawasilisha kwa majadiliano.

i had the seme idea, nilienda kwa wakubwa wakaniuliza: je kama kila mtu kwenye kundi lako akiamua kufanya hivyo who loses the most?
mind you that maendeleo na mapambano, ccm hawapo kwa dhati kuwasaidia wananchi, wanaangalia manufaa yao sasa basi jua mwanamapinduzi hakati tamaa kwani utapotezaza zaidi unachotakiwa kupambana zaidi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom