Sitaoga wala kunawa mikono sbb nimemshika prince charles mkono

Nilivisikia vile vitoto; nikakisikitikia kizazi kijacho kama ndo kinajengwa na aina ya wanafunzi hawa ; tumekwisha! hata kama ni utani............kuna ujumbe unapatikana hapa kwenye kauli kama hii
 
mimi nilikuwa namfagilia sana Diana
kwa sasa nawakubali watoto wa Diana tu.

na huyo diana ulikuwa unamfagilia kwa lipi? .....................................na hao watoto wake unawakubali kwa lipi?/.................watu wenyewe kwanza wana serikali inayopigia debe ushoga na hawaikemei! ..............................hebu tupunguze haka katabia ka kuwaendekeza hawa wakoloni jamani...........................

ningeongeza mengine ila naogopa ban wakuu.....................
 
nafikiri sasa mtaelewa ni kwa nini al-shabab walipiga marufuku matangazo ya bbc huko somalia...............
 
Huo ni utani msiuchukulie sana, kuna jamaa ninayemfahamu aligusa ziwa la msichana anayemwona kuwa ni mzuri sana, tena juu ya nguo, akasema hatonawa mkono huo kwa mwezi mzima. Ni utani tu, ingawa kwa wasichana na wavulana si jambo la ajabu popote ulimwenguni.
Hamjaona wasichan na wavulana wakiwania angalau kumwona fan wao kama vile waimbaji, wachezaji mpira, wacheza filamu?
Ikiwa haya yanafanyika ulimwenguni kote, kuna ajabu gani yakifanyika Tanzania? Je kama mvulana angesema hivyo kwa kukamata mkono wa JD, au msichana kumata mkono wa Kanumba?
 
hako katoto ni kachafukoga tu, badala ya kufikiria kufauru darasani kenyewe kanafikiria kushikana mkono na binadamu. kweli wazazi wako wana kazi kubwa mno, sijui kama katamaliza form four bila ujauzito - hakana woga hata kwenye media.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom