SITANII; Kodi ya simu za mkononi haiepukiki

Wildlifer

JF-Expert Member
May 12, 2021
1,881
5,180
Hakuna Maendeleo bila Kodi. Kimsingi nchi zetu sisi Afrika kiwango cha walipa kodi ni kidogo sana.

Mfano hapa kwetu Tanzania, kati ya watanzania takribani Milioni 60, walipa kodi ni takribani Mil 5 tu sawa na Asilimia 8. Tazama takwimu hizi za nchi za wenzetu, Sweden 57.19% Japan 55.95%, Austria 55%, Netherlands 51.75%, Belgium 50%, Ireland 48%, Australia 45%, China 45%, USA 43%. Mataifa tunayoyatembezea bakuli watu wake wanaongoza kulipa kodi. Kimsingi kule hadi Barmaid analipa kodi. Sisi nchi zetu tunafanya siasa hata kwenye kodi. Mfano, waendesha bodaboda wengi wao kwa wastani wa mwezi wanaingiza takribani 300,000.

Kiasi hiki kinakaribia kulingana na Take home ya Mwalimu wa Shule ya msingi, ambaye analipa kodi. Hivi mtu huyu akiipa sh 5,000 kodi serikali ni kiasi gani itaingiza kwa mwezi kwa bodaboda wote nchi nzima? "Nothing is certain except death and taxes"- Benjamin Franklin

================

Alhamisi, Aprili 10, 2021 Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, aliwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Kwanza kabla sijaijadili bajeti hii, naomba nimshukuru Mheshimiwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, kwa kulialika Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa mwaliko maalumu kuwapo bungeni wakati bajeti inasomwa. Nasema asante sana, na heshima hii uliyotupa naamini itakuwa endelevu.

Nimefurahia utaratibu uliotumiwa kuwapokea wageni bungeni. Sisi sote ni Watanzania. Zamu hii tumeruhusiwa kuingia bungeni na simu zetu za mkononi, kalamu na viandikishi, kwa maana ya notebook.

Utaratibu huu mzuri ulikamilishwa kwa hotuba ya bajeti kuingizwa kwenye tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango, kisha waalikwa wote tukapewa vitabu vya bajeti tukafuatilia.

Kimsingi utaratibu huu ni mzuri na udumishwe. Hongera Mhe. Spika Ndugai kwa maboresho haya, maana zamani wageni hawakuruhusiwa kuingia hata na kalamu!

Sitanii, ninafahamu watu wengi wamejadili bajeti ya Serikali. Bajeti hiyo Waziri Mwigulu hakupata fursa ya kusoma kila kitu kilichopendekezwa na serikali.

Hakika sisi tumeichapisha yote katika gazeti la Jumanne, Juni 15 – 21, 2021 toleo No. 507 kutokana na umuhimu wake. Hii ni bajeti ya kihistoria. Kwa muda mrefu tumekuwa tukisema tunataka bajeti ya kukuza viwanda, lakini hili limekuwa halitokei.

Bajeti ya mwaka huu imefungua mlango wa kutengeneza vifungashio, magunia, mazao ya kilimo, viwanda vya pikipiki, mabati na chochote kiwacho kutokana na kodi nyingi kufutwa.

Naomba msomaji ujipe muda uisome bajeti hii. Gazeti letu JAMHURI ni la wiki, hivyo hata kama hautamaliza kuisoma ndani ya saa 2 unaweza kuihifadhi baadaye ukipata muda umalizie. Ni muhimu uone mabadiliko makubwa yaliyowasilishwa.

Sitanii, kichwa cha makala hii kinasema: “Kodi ya simu za mkononi haiepukiki.” Nafahamu yapo maeneo matatu ndiyo yanajadiliwa kwa kina katika bajeti ya mwaka huu.

Maeneo haya ni kodi ya Sh 1,000 kwa mita ya umeme kwa nyumba za kawaida na Sh 5,000 kwa nyumba ya ghorofa na zile za biashara. Mimi naona hii imeondoa kero. Ni mfumo unaoondoa hatari ya kuuza nyumba za watu.

Kama haukununua umeme hautadaiwa kodi hii na nyumba yako itabaki salama. Naamini kila Mtanzania ana hamu ya kuishi maisha bora, ambapo umeme ni kichocheo cha maisha bora. Na hakika, kodi hii inalipika. Siasa laini za kudhani mtu atapata huruma ya wapangaji nilizoanza kuziona, tuzipuuze.

Nimeona malalamiko ya watu kadhaa kwenye mitandao, hasa katika eneo la gharama za miamala ya simu ambayo inaanzia Sh 10 hadi 10,000 na kodi ya simu za mkononi ambayo ni kati ya Sh 10 hadi 200 kwa siku.

Pia kuna tozo ya Sh 100 kwa kila lita ya mafuta inaanzishwa. Kodi hizi tatu zimeleta kilio kikubwa mno kwa wananchi.

Sitanii, naziona kodi hizi mpya zikileta wastani wa Sh trilioni 3 kwa mwaka hapa nchini. Najua inauma ukisikia hii kodi mpya imeanzishwa.

Lakini kuna jambo nataka niwaambie Watanzania, tunapaswa kufahamu kuwa nchi yetu haiwezi kuendelea kamwe kwa kutegemea misaada na mikopo. Misaada na mikopo ni sawa na kumwekea mgonjwa ‘drip’. Mgonjwa ataishi, ila ‘drip’ haiwezi kuwa mbadala wa chakula kamwe.

Leo wala sitatumia mifano ya ughaibuni. Mwaka 2006 nilifanya mahojiano na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa. Akaniambia: “Hakuna jinsi tunavyoweza kusambaza umeme bila watumiaji wa umeme kugharamia usambazaji. Ni lazima nitahakikisha serikali inaanzisha chombo cha kusimamia hili na tutaweka utaratibu wa kupata na kuzitumia fedha kutoka kwa watumiaji wa umeme.” Mwaka mmoja baadaye, yaani 2007 ikaanzishwa REA (Wakala wa Umeme Vijijini).

REA tunakatwa asilimia 3 ya gharama ya umeme unaonunuliwa. Fedha hizi tunazitumia kununua nguzo, vifaa kama nyaya na vingine. Leo kila kijiji kinasambaziwa umeme. Nguzo zimemwagwa vijijini pembezoni mwa barabara za miti na zege. Tumeweza kusambaza umeme kwa kutumia fedha zetu za ndani.

Sitanii, uamuzi huu wa kuanzisha kodi ya simu mahususi kwa ajili ya ujenzi wa barabara za vijijini ninauunga mkono asilimia 100.

Hata kodi ya Sh 100 kwa kila lita ya mafuta nayo naiunga mkono asilimia 100. Kama tulivyojenga mfumo wa umeme kupitia asilimia 3 ya ununuzi wa umeme wa REA, naiona kodi hii mpya ya simu ikijenga barabara za nchi hii.

Nawahakikishia sisi Watanzania tunapaswa kusimama kwa miguu yetu. Tukitegemea mikopo, misaada na wafadhili, ukiacha kuwa haiji kwa wakati, kuna mikopo inakuja na masharti.

Wapo wenye hamu ya kutwambia turasimishe ushoga ndipo watupatie mikopo. Binafsi ninasema hapana. Tuepuke kutaka kula vya watu, tutaliwa!

Mwisho, ninalo jambo la mikopo ya elimu ya juu. Niseme kwa ufupi tu kuwa tunahitaji kuanzisha kodi ya huduma ya asilimia 2 kwa kila huduma inayotolewa na hii iende moja kwa moja kwenye elimu. China walianzisha kodi ya elimu asilimia mbili kwa kila huduma inayotolewa mwaka 1980. Leo wanatoa misaada ya kusomesha watoto wa nchi za kigeni, ikiwamo Tanzania kutokana na kukusanya fedha nyingi. Naamini tukiamua tunaliweza hili na tutasomesha kila mtoto wa Tanzania bila kuwapa mikopo.

Tukianzisha hiyo, tutafuta utaratibu wa kuwapa wanafunzi fedha mkononi. Wanafunzi kazi yao ibaki kuwa ni kusoma, kula, kuoga na kulala. Tutapunguza kasi ya watoto wetu kwenda kwenye majumba ya starehe, watapata fursa ya kuishika elimu isiwaponyoke. Vyuo vitakuwa na mabwalo ya kulia chakula, ila tutaweka viwango kuepuka maharage yaliyobunguliwa.

Kwa mfumo wa sasa wa kuwapa fedha mkononi wanafunzi wetu kwa njia ya mkopo, si tu tunawaharibu kwa kuwanyima fursa ya kusoma wakaenda kwenye starehe kwa sababu wana fedha, bali pia wakihitimu hatuna uhakika wataajiriwa wapi, hivyo mkopo wa sasa kulipika kwake ni shaka tupu.

Zimejengwa baa nyingi na nyumba za starehe karibu na vyuo usipime. Leo ukienda kwenye kumbi, kama Dodoma utasikia ma-DJ wanasema: “UDOM piga keleleeeeee,” kisha wanaitikia: “Yooooooooo…” Ma-DJ wanaendelea: “CBE mpooooo?” Wanaitikia: “Yoooooooo”.

Nasema hapana. Muda wa wanafunzi wetu kuwa maktaba wanakuwa kwenye kumbi za starehe. Muda wa kulala, wapo kwenye madangulo. Vyumbani wanashindania simu bora, redio na televisheni.

Ukiingia mabwenini utafikiri umeingia kwenye shamba la wanyama (Animal Farm). Aliyewasha redio haya, wa TV sawa… hakuna utulivu mabwenini siku hizi sawa na ilivyokuwa enzi zetu tuliosoma miaka ya 1980 na 1990.

Watoto wetu kwa kuwapa fedha mkononi kama mkopo tumewaweka katika mazingira hatarishi, halafu tunasema elimu imeshuka!

Nahitimisha safu yangu kwa angalizo. Tunao Mfuko wa Barabara (Road Fund). Unapokea mabilioni kutoka kwenye kila lita ya mafuta. Je, mfuko huu huwa unakaguliwa? Hakuna panya wanaouguguna?

Je, tumejiandaa kuziba matundu kama yapo yasihamie Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA)? Fedha hizi ni nyingi, ikiwa hazitasimamiwa vilivyo, tutawakatisha Watanzania tamaa ya kulipa kodi kwa uadilifu.

Hongera Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukataa kodi za damu. Hongera Dk. Mwigulu Nchemba kwa kuanzisha vyanzo hivi vipya, ila Watanzania wanataka kuhakikishiwa usalama wa fedha hizi zikiisha kulipwa. Mungu ibariki Tanzania.

Deodatus Balile.
Jamhuri; 15-06-2021.
Accessed from Jamhurimedia website.
 
Ulaya na kwingineko katika nchi nyingi zilizofanikiwa kukusanya KODI walitumia mfumo malipo kwa njia ya ELECTRONIC ndio malipo ambayo huweza kupatia serekali kodi STAHILI kwa njia rahisi HAKUNA namna nyingine yoyote ile.

NB: Nchi za ulaya nyingi zina raia wachache sana,sasa hapa kwetu mtaji watu ni mkubwa sana na wote ni lazima watafute mahitaji yao kwa muhimu kwa kila siku.##preciously money making traps to our govt.
 
Wote tumekubaliana hakuna kodi za dhuluma.

Sh100×watu 30,000,000 wanaomiliki simu mathalani= tsh 3,000,000,000 bln per day.

Tunaenda kuwa nchi tajiri duniani. Kwenye hilo mama boresha sheria za kusimamia kodi make akina Dr. Bashiru na Sabaya bado wamekuzingira ofisini.
 
Hakuna Maendeleo bila Kodi. Kimsingi nchi zetu sisi Afrika kiwango cha walipa kodi ni kidogo sana. Mfano hapa kwetu Tanzania, kati ya watanzania takribani Milioni 60, walipa kodi ni takribani Mil 5 tu sawa na Asilimia 8. Tazama takwimu hizi za nchi za wenzetu, Sweden 57.19% Japan 55.95%...
Hatuna pingamizi na huu mfumo wa ulipaji kodi kupitia simu za mkononi, tatizo je hii kodi tunayowakata wananchi wa hali ya chini ambao wengine hawajui hata kesho yao ikoje tunekwenda kuitumia kuwaletea wananchi maendeleo au inakwenda kuwanufaisha wachache?
 
Hatuna pingamizi na huu mfumo wa ulipaji kodi kupitia simu za mkononi, tatizo je hii kodi tunayowakata wananchi wa hali ya chini ambao wengine hawajui hata kesho yao ikoje tunekwenda kuitumia kuwaletea wananchi maendeleo au inakwenda kuwanufaisha wachache?
Kama umeweza kununua simu lets say ya sh ef 15, na umeweza kuweka Vocha ya sh 500, huwezi shindwa lipa sh 10. Mtu huyu huwezi muweka kwenye kundi la asiyejua kesho yake ikoje.
 
Hivi mpaka dakika hii unadhani hulipi Kodi kwenye simu (yaani bundle na kila ukiweka salio) ? Hilo ni ongezeko tu..., na mwaka huu inaanzia mia mwaka kesho buku n.k...

Kama Matumizi ya hizo kodi bado ni ya ajabu ajabu, tunakuwa hatujasaidia kitu... (hivi wabunge tunawalipa kiasi gani ?, Hizo posho ?, Hayo magari ni value for money) kwanza waanze kubana mikanda kabla ya kuendelea kutukamua...
 
Kama umeweza kununua simu lets say ya sh ef 15, na umeweza kuweka Vocha ya sh 500, huwezi shindwa lipa sh 10. Mtu huyu huwezi muweka kwenye kundi la asiyejua kesho yake ikoje.
Hata kama unajua kesho yako ikoje, bado ni lazima mfumo wa haya mapato uwe transparent na wenye kunufaisha wananchi, la sivyo itakua ni sawa na bure

Tumeona huko nyuma matumizi ya pesa za umma yalifanywa kama matumizi ya mtu mmoja na yaliamuliwa na mtu mmoja, mambo yasiyo na maslahi ya umma yalifanyika kwa pesa nyingi huku tukiacha mambo ya msingi na wananchi wakaendelea kuteseka

Lazima tuhakikishiwe usimamizi mzuri wa kodi zetu na matumizi yenye kunufaisha wananchi wote bila kujali ukanda wala ukabila,wala uchama, sio kwenye kutukata mnatukata bila huruma halafu kwenye maendelea mnasema msipochagua ccm hatutawaletea maendeleo
 
Hata kama unajua kesho yako ikoje, bado ni lazima mfumo wa haya mapato uwe transparwnt na wenye kunufaisha wananchi, la sivyo itakua ni sawa na bure...
Sasa hili ni suala la matumizi ya fedha za Umma, ambalo nalo nakubaliana nawe kuwa Uwazi na uwajibikaji ni muhimu.
 
simu sinunui na vocha sinunuie, full stop.
Mkuu sio kosa kujibu hivi na wakati huo unatumia vocha kujibu haya.

Kwa nchi za wenzetu kwa vile urasimu uoo kwa kiwango kidogo watu wanashindana kulipa kodi na huwa jambo la aibu kutolipa kodi. Rejea kesi ya mchezaji messi, huo ni mfano tu.

Naoendekeza mazingira ya upigaji yaanze kushughulikiwa ili watu waone maana na umuhimu wa kulipa kodi.

Tozo hizi mkuu zinaenda kumaliza tatizo la barabara vijijini. Tuliunge mkono mkuu
 
Mnashabikia msichokijua.
Mapato kwa nchi hii ni makubwa sana, tatizo ni kundi la Panya ambao hawana nidhamu, wanatafuna kila karatasi inayopita mbele yao na matokeo yake vipande vya karatasi vinavyobaki vinakuwa havina thamani.

Kupanga ni kuchagua, kama tumekubali kuendelea kufanya biashara ya dagaa ilihali panya wanagombania gharani, ok ndo akili tulizojaliwa wadanganyika walio wengi.
 
Mkuu sio kosa kujibu hivi na wakati huo unatumia vocha kujibu haya.

Kwa nchi za wenzetu kwa vile urasimu uoo kwa kiwango kidogo watu wanashindana kulipa kodi na huwa jambo la aibu kutolipa kodi. Rejea kesi ya mchezaji messi, huo ni mfano tu...
I think tatizo hapa kwetu, partly liko kwenye matumizi ya kodi. Impact ya kodi wananchi wakiiona, nadhani ulipaji wa kodi utakuwa na muitikio mkubwa.
 
Hata kama unajua kesho yako ikoje, bado ni lazima mfumo wa haya mapato uwe transparent na wenye kunufaisha wananchi, la sivyo itakua ni sawa na bure...
Mkuu umenena vema sana, yule dikteta alitaka afaidi peke yake. Sema mama angalau anataka watu wafanye biashara na shughuli zingine kwa uhuru ili hata hizi kodi mpya ziweze kulipika. Usiwe mzigo tena kwa mwananchi.

Huyu mama kama ataboresha sheria za usimamizi wa fedha za umma, amini maisha tunayoyaota kila siku tutauafikia kabla ya 2030.
 
Bado nasema bado sana Afrika kufikia hatua kubwa, sababu sheria zetu hazina nguvu kumkabili jambazi wa mapato ya nchi.

Kiongozi akiwa madarakani anaiba atakavyo anajua sheria inamlinda akiwa na akitoka madarakani, hiyo inafanya hata haya makusanyo kupitia simu hayataweza kuleta matokeo chanya.
 
Ulaya na kwingineko katika nchi nyingi zilizofanikiwa kukusanya KODI walitumia mfumo malipo kwa njia ya ELECTRONIC ndio malipo ambayo huweza kupatia serekali kodi STAHILI kwa njia rahisi HAKUNA namna nyingine yoyote ile.
N.B;-Nchi za ulaya nyingi zina raia wachache sana,sasa hapa kwetu mtaji watu ni mkubwa sana na wote ni lazima watafute mahitaji yao kwa muhimu kwa kila siku.##preciously money making traps to our govt.
Unalinganishaje Sweden, Japan Na Tanzania mkuu?
 
Hatuna pingamizi na huu mfumo wa ulipaji kodi kupitia simu za mkononi, tatizo je hii kodi tunayowakata wananchi wa hali ya chini ambao wengine hawajui hata kesho yao ikoje tunekwenda kuitumia kuwaletea wananchi maendeleo au inakwenda kuwanufaisha wachache?
Hizi kodi za simu zimeelekezwa tarura, na hospital
 
Wote tumekubaliana hakuna kodi za dhuluma.

Sh100×watu 30,000,000 wanaomiliki simu mathalani= tsh 3,000,000,000 bln per day...
Mkuu Uchambuzi mzuri sana. Ishu ta kodi siyo ya kuchezea. Nimejifunza sana umuhimu wa kulipa kodi huku mambele. Kodi ni kama mafuta kwenye maisha yani mafuta kwenye injini ya gari inaendesha maisha.

Utamu wa kodi ni pale baada ya kulipa matumizi yake yanaonekana. Siyo unakuwa hodari wa kukusanya kodi baadaye unajenga international Airport kijijini na kununua wapinzani
 
Back
Top Bottom