Sitamsamehe aliyeniambia Education is better than money

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,395
3,897
Elimu ya kikoloni imeua ubunifu na imedumaza akili za watu unalazimishwa kukariri mawazo ya watu katika miongo mitatu ya maisha yako! Unalazimishwa kuyafanyia kazi mawazo ya watu for the rest of your life inakufanya uwe tegemezi kiasi kwamba ukithubutu kusimamishwa kazi kwa mwezi mmoja tu unapata pressure.

Yaani tumetengenezewa mfumo tegemezi wa maisha ambao ukijiingiza kwayo haubanduki hapa ndio unapata risk takers kama akina Bill gates aliyeukataa utumwa wa Fikra akawa huru, akina Steve Job, Mark zukerberg, Thomas Edison.

Kimsingi watu walioamua kuwa huru kimawazo wamefanikiwa sana wana ujasiri sana wa kupambana na maisha yao hawaogopi kukosea ndio matajiri wengi hawakukubali kutumia muda wao kukaririshwa kesho isiyokuwepo, eti unaambiwa education is better than money wazungu siyo watu wazuri, ona mtu kama Diamond ambaye ameamua tu kutumia kipaji chake na kutofungwa mawazo yake alivyofanikiwa
 
Pole sana. Ndiyo hasara ya elimu ya Tanzania. Inakazania kukariri na wahitimu wake wanapomaliza masomo wanajikuta hawajaelimika bali walikariri. Nchi zilizoendelea hali ni tofauti kabisa. Kwa mfano wahitimu wa chuo kikuu ni watu weledi na wanaweza kufanya kazi za maana.
 
Alikuambia ili utumie hiyo elimu kupata pesa.Hao wote uliowatolea mifano walipata Elimu kwanza. Tatizo letu hatu Think ili kutatua matatizo. Hao unaowataja bado huwa wanasoma vitabu kupata maarifa mbali mbali katika kutafuta mapato zaidi.Elimu ni msingi katika kutafuta pesa. Tumia Elimu katika kupata maarifa na kutatua matatizo. Uza solutions zako.
Kina Billgates, Steve, Mark, Jeffrey, Thomason wote hao wamepiga shule.
 
Hahah mkuu usifanishe elimu ya bongo na elimu katika nchi zilizoendelea ,so wewe kama elimu ya tz kama haijakusaidia pole mkuu
 
Kama uliuelewa huo msemo kama ulivyoandika kwenye huu uzi hapa basi unahaki ya kutomsamehe aliye kuambia hivyo,kwa sababu kwa maana hii unakuwa umeidogosha elimu.

Elimu ni pana sana,haiishii kwenye hii ya shuleni tu,na kwa maana hiyo ndio inakuwa ni bora kuliko pesa,hata hao watu uliowataja hawakufanya hayo waliyoyafanya kwa ujinga,waliyafanya kwa elimu swali ni elimu gani?
 
Si kweli hao wote uliowataja wamesoma alafu wakatumia iyo elimu kutafta pesa .
Halafu kusoma pia ni kipaji.

So Kama umeona elimu imekushinda ni bora ukafanya mambo mengine utafanikiwa Ila usikashifu elimu.

Halafu lengo la elimu ni pana sio tu kuwa na mali nyingi bali kuboresha maisha ya mwanadamu.

Kwa mfano bila elimu unafikili wataalam Kama madaktari, ma engineer, wanajimu, n.k wangepatkana wap?

Ni lazima ufikili, lakini pia unaweza kuwa na mali nyingi ila wakafaidi wengine (wasomi)

Mfano mzuri ni nchi za kiafrika na baadhi za Asia zina Mali nyingi ila wanaofaidika ni nchi walio wekeza katika elimu

THINK BIG bro"
 
Elimu ya kikoloni imeua ubunifu na imedumaza akili za watu unalazimishwa kukariri mawazo ya watu katika miongo mitatu ya maisha yako! Unalazimishwa kuyafanyia kazi mawazo ya watu for the rest of your life inakufanya uwe tegemezi kiasi kwamba ukithubutu kusimamishwa kazi kwa mwezi mmoja tu unapata pressure.

Yaani tumetengenezewa mfumo tegemezi wa maisha ambao ukijiingiza kwayo haubanduki hapa ndio unapata risk takers kama akina Bill gates aliyeukataa utumwa wa Fikra akawa huru, akina Steve Job, Mark zukerberg, Thomas Edison.

Kimsingi watu walioamua kuwa huru kimawazo wamefanikiwa sana wana ujasiri sana wa kupambana na maisha yao hawaogopi kukosea ndio matajiri wengi hawakukubali kutumia muda wao kukaririshwa kesho isiyokuwepo, eti unaambiwa education is better than money wazungu siyo watu wazuri, ona mtu kama Diamond ambaye ameamua tu kutumia kipaji chake na kutofungwa mawazo yake alivyofanikiwa
Pole sana. Bado hujachelewa. Maadamu Mungu kakujalia afya na uzima. Chukua hatua sasa. Kama hujasoma kitabu cha Rich Dad, Poor Dad. Kitafute ukisome. Kitakuongezea mwanga wa kuanza maisha mapya ya kujiajiri na kujitegmea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
niliwahi kusoma sehemu ikisema kwamba 90% ya maarifa(knowledge) yote tunayofundishwa shuleni na vyuo vikuu ni batili na useless. ukweli katika maarifa hayo ni 10%. tu.

maarifa mengi ya kidunia na yenye positive impact kwa binadamu yanapatikana nje ya mfumo rasmi wa kishule. ni wewe tu kuweka bidii katika kutafuta maarifa hayo.
 
foundations-of-education-lecturer-i-9-728.jpg
 
Education ni general. Unamaanisha ambaye hajasoma kabisa na kua na utajiri wa kifedha? Kwamba kipi Bora.

Kama ulienda shule ili upate kazi au uwe na maisha mazuri instantly after graduating unajidanganya, na aliyekuambia kua na elimu ndo utajiri naye alikudanganya.

Unapoenda shule unaenda kutafuta knowledge through advancing education level ili ikusaidie katika maisha ila kuna watu hawataki kuhusle kugain knowledge, wanataka kutumia education level kuwin life. It doesn't work in that way.

Through education we gain knowledge and academic certificates.

Sasa Kama wewe unategemea kutoka kimaisha Kwa kujaza mi A kwenye vyeti ndo hapo ukikosa unaanza kuilalamikia elimu.

Education system was not designed for individual, it was designed for masses at least everyone to gain that little knowledge being transferred and hence you should thrive individually what is remained to fulfill your life.
 
mkuu kuna formal ,nonformal na informal.Lakini mwisho wa siku lazima uchague utatumia ipi kwenye maisha yako.Elimu bado ni muhimu inategemea unaidefine vipi elimu?
 
Back
Top Bottom