Sitamani tena kuishi Dar, amenifedhehesha sana kuniibia simu yangu

Dar hakuna msamaria mwema wa kukupa fursa ya haraka hivyo zaidi ya wewe kuwa fursa.
 
Kuna Brother nilimwomba anisaidie kunifundisha kunyoa ili nikisha jua nitafute ajira kwenye Saluni hizi za kiume. Juzi bro alikuwa ametoka ameniacha peke yangu Saluni basi kuna kijana akawa amekuja pale kumuulizia Bro nikamwambia Bro ametoka. Jamaa akaniambia kuwa kuna dada mtaa wa pili ana taka kuhama hivyo alikuwa anatafuta mtu wa kusaidiana nae kupakia vyombo kwenye gari kuna Malipo.

Nikaona hili bonge la zali nikamwambia sio shida tunaweza kwenda na mimi nikafunga office tukawa tumeongozana mbaka mtaa wa pili akawa amenionesha nyumba ya huyo dada anae taka kuhama, hivyo akasema nimsubili nje kisha yeye aingie akamwambie kuwa mtu wa kupakia amesha patikana. Akaingia kwenye iyo Nyumba akakaa kama dakika tatu akatoka.

Akaniambia amesha ongea nae hivyo kuna deleva wa kilikuu amempigia simu anakuja yupo njiani, tukasubiri kama dkk 10 huku tukipiga stori nje pale deleva wa kilikuu hajatokea. Jamaa akawa analamika ana mishe nyingi ila deleva wa kilikuu anamwangusha anamchelewesha, akachukua simu yake akawa anampigia simu deleva wa kilikuu anamuuliza uko wapi? deleva anamjibu kama 5 tu nitakuwa hapo, jamaa alikasilika akawa anampigia mara kwa mara mwishoe simu yake ikawa imeisha salio. Jamaa akaniambia inabidi amcheki deleva mwingine wa kilikuu ila simu yake imeisha vocha, Hivyo akaazima simu yangu ampigie deleva mwingine aje chap maana wa mwanzo anazingua.

Ikabidi nimpe simu yangu Tecno Comon 11 basi akawa amempigia uyo deleva mpya wakawa wana ongea, huku anaongea na simu akaniambia anaingia tena ndani mule nimsubili ili amwambie uyo dada aanze kutoa vitu gari inafika sio muda. Wakati naendelea kusubiri kutokana na muda kwenda sana zaidi ya dkk 15 jamaa ajatoka nje na yupo na simu yangu ikabidi niingie ndani kumuizia, nikakuta kuna wadada wawili wanasukana nikawaambia kuna kaka nipo nae ameingia humu ndani kuna dada tunataka kumsaidia kupakia vyombo vyake kwenye gari anahama.

Wote walinishangaa kwa sababu hakuna mpangaji alie kuwa ana hama, wakaniambia ni kweli kuna kaka amekuja hapa anaulizia vyumba vya kupanga kaja mara mbili tukamwambia vyumba vyote vina watu. Na wakaniambia ile nyumba ilikuwa na milango miwili jamaa akawa ametokea mlango wa pili ameenda. Kijasho chembamba nikaanza kukisikia kwa mbali ndipo nikagundua Dar ni shule. Nimehuzunika sana roho kwa sababu toka mim nije Dar sijawai mfanyia mtu ubaya, ila kwanini sasa mim wananifanyia hivi. Nimepoteza mood yote ya kuishi Dar na hapa nikipata nauli narudi Mbeya na sizani kama nitarudi tena Dar.

NB: Tuwe na mioyo ya utu, huu ujanja ujanja unafanya watu turudi nyuma sana kimaendeleo.
Pole sana.
Nadhan bado hujanunua simu na hii article umeandika kabla ya kuibiwa.
So sad
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom